24. Mada ya Habari: Sheria ya Musa na Mkristo leo

Mada ya Habari: Sheria ya Musa na Mkristo leo

Israeli walipokuwa watu wa Mungu, Mungu alifanya agano nao. Mungu angewatunza kama wangetii amri zake (Kutoka 19:4-8). Pia alitoa maagizo ya jinsi ya kutengeneza hema la kukutania, jinsi ya kuweka kazi za makuhani na jinsi ya kutekeleza dhabihu mbalimbali. Kwa pamoja sheria hizi zinajulikana kama "Sheria ya Musa". Ni mapatano ya agano kati ya Mungu na Waisraeli.

23 - 14. Mwanafunzi wa Yesu

14. Mwanafunzi wa Yesu

Wale wanaotaka kufaidika na kazi ya kuokoa ya Yesu wanatakiwa kumfuata Yesu na kuishi kama wanafunzi wake. Hii ni pamoja na kile kinachofafanuliwa katika Matendo 2:42 , ambapo tunasoma kwamba wanafunzi waliendelea katika “mafundisho ya mitume na ushirika, na kuumega mkate, na kwa kusali."

22 - 13. Kurudi Kwa Yesus

13. Kurudi Kwa Yesu

Yesu sasa yuko mbinguni lakini atarudi duniani (Matendo 1:10,11; 3:20-21; Yohana 14:2,3). Atakapokuja, atawatuza waumini kulingana na maisha waliyoishi (Mathayo 16:27, Ufunuo 22:12). Jambo la kwanza atakalofanya ni kuwafufua wafu na kuwahukumu (1 Wathesalonike 4:16; 2 Timotheo 4:1).