CSSA 3-1-251 - MUNGU, MWANDISHI WA BIBLIA

Swahili

251. MUNGU, MWANDISHI WA BIBLIA

                            “kila andiko limeandikwa kwa upako wa Mungu

Kama mtu anaweza kuangalia ukubwa wa bingu ama ulimwegu kupitia ungo wa viumbe , atashangazwa na ubunifu na muundo msingi wa uumbaji.  Kila upande  wa jinsi dunia ilivyoumbwa ni ushahidi kimya kuwa yupo Muumbaji. Mbali na kitabu tunachojua kama Biblia, Binadamu atazidi kubaki mjinga na ashindwe kuelewa asili na hatima ya dunia. Biblia ndio ufunia wa Mungu kwa binadamu. Inaonyesha ukweli dhahiri kuhusu Mungu na binadamu. Inaonyesha kusudi kuu la uumbaji, asili ya dhambi na kifo, kuendelea na hatima ya mataifa na kisha ufalme wa Mungu unaokuja. Lakini Biblia pia ina dhamani ya kibinafsi. Na huwapa vijana na wazee matumaini. Inatuonyesha sababu halisi ya kuishi na pia kufunua ujinga ufuatao wa dunia ambayo imejitenga na Mungu na Uumbaji wake. Kwa kifupi,biblia inaweza kubadilisha maisha yetu.

Lengo la hili somo ni kuonyesha kwamba kuna Muumbaji mmoja mkuu ambaye aliongoza kuandikwa kwa biblia ili kuonyesha tabia zake na kusudio lake kwa mwanadamu.

 

                   2Tim: 3:14-17; 2 Pet 1: 19-21

BIBLIA: UFUNUO WA MUNGU KWA BINADAMU

Ijapokuwa Biblia imegawanywa katika sehemu sitini na sita ina ujumbe mmoja dhabiti. Inadai kuwa Neno la Mungu. Kwa vitabu vitano vya kwanza imetajwa mara zaidi ya mia tano “Bwana akasema” au “Bwana akanena” tena kwa mara 300 inarudia maneno hayo kutoka kwa kitabu cha Yoshua hadi Wimbo wa Solomon. Vitabu za manabii zinarudia maneno hayo kwa mara 1200.

Waandishi wa Biblia walikua wanatimiza jukumu kama waalimu wa sheria wa Mungu aliyekua mwandishi Mkuu. Alionyesha mafunzo yake kupitia kwa wanadamu. Waliandika kutokana na upako wake (Heb :1:1-2; Neh 9:20) Aliwaelekeza jinsi watakavyosema ijapokua lugha waliotumia ilikua yao.  Kwa kusudi hili Mungu aliwachagua wanaume kutoka kila tabaka la jamii. Wafalme, viongozi, makuhani, wasomi, wachungaji na pia wavuvi walikua kati ya waliochaguliwa. Aliwagawanya kulingana na hadhi, watkat na mahali walikotoka. Mwandishi mmoja akiwa Syria wa pili alikua Uarabuni, wa tatu Italia, wa nne Ugiriki, wa tano Babelli na wasita palestina. Hii inaaanisha walikumua na masasiliano machache sana. Musa ndiye aliyekua mwandishi wa kwanza na aliandika vitabu vitano nya kwanza vya BIblia miaka 1600 kable ya Yohana kuandika kumbukumbu ya ufunuo.

Licha ya tofauti hizi kubwa kuna uwiiano wa ajabu kwa yale yalionadikwa yanavyounganisha vitabu hivi vyote 66 na kuwa moja ili kufanya Biblia kitabu cha kipekee katika ulimwengu wa fasihi. Mungu amempa mwanadamu kitabu hiki ili kumpa matumaini (Warumi 15.4) Biblia pekee ndio inaweza onyesha njia ya wokovu (2Tim 3:15). Kukataa ujumbe huu ni kumaanisha kifo. (Kumb 30:17-20, Mithali 14:12.)

Kwa kawaida Biblia imegawanya katika sehemu mbili; Agano la kale (vitabu 39) na Agano jipya (vitabu 27). Mgao huu umefanywa na mwanadamu kwa sababu Biblia inastahili kuchukuliwa kama kitabu kimoja cha ufunuo wa Mungu kwa binadamu. Agano la kale lilikua limeandikwa kwa kiebrania na Agano jipya na Kigiriki.  Mfumo wa kuandika Biblia na Kiingereza ulioidhinishwa na hutumika leo ulichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1611. Pia ilitafsiriwa na Kiswahili kama Biblia Muungano. Ilijulikana kama mfumo ulioidhinishwa kwa sababu mamlaka ya kutasfri kwa kizungu ilipewa Mfalme James wa Uingereza. Kutoka wakati huo tafsiri nyingi zimetolewa zingine zina manufaa na zingine zina manufaa kidogo sana. Nakala rasmi haina makosa lakini hakuna toleo lisilo na makosa. Kwa miaka iliyopita kumekua na  makosa ya kutafsiri kwa waandishi kuiga nakala rasmi na kutafsiri kutoka kwa lugha asili kwa lugha nyingine. Lakini makosa haya ni kidoga na hayana umuhimu mkubwa kwa sababu kila toleo lina mafunzo muhimu ya Biblia yanayoeleweka.

BIBLIA: UPAKO NA UKWELI

Petro aliweka kanuni za msingi kwamba Biblia imechaguliwa (2 Pet. 1:20-21). Alitangaza kwamba “ hakuna nabii wa andiko  alikuwa na tafsiri ya kibinafsi; kwa sababu unabii wa kale  haukuletwa na mapenzi ya binadamu bali ni wanaume watakatifu  walioteuliwa na Mungu kuongeo kama wananvyoongozwa na Roho Mtakatifu.

Kwa hivyo ukweli unaweza patikana kwenya biblia na hakuna yeyyote anaweza kuonyasha uwongo kwenye matokeo ya kihistoria. Wanaopiga Bibliawamelazimika kukubali kwamba kuna ukweli ndani yake. Mashahidi  wa manabii wanaonyesha kwamba kuna ukweli dhahiri kwamba Mungu ndiye Mwandishi kwani yeye pekee ndiye anaweza  kutabiri siku zijazo. Utabiri wa kushangaza katika Biblia umetimia jinsi ulivyo tabiriwa. Mfano:

  • Ukuta wa Babelli bado ni vifusi (Isa. 13:19-21, Yer. 51:37).
  • Ninevehe bado ni tupu na imejaa taka ((Nahumu 2:10).
  • Misri ni moja kati ya mataifa duni (Eze. 29:15).
  • Tiro iliyokua bandari imemezwa na bahari (Eze. 26:5).
  • Taifa la Israel limesambaa katika mataifa yote (Kum. 28:64) na sasa wanakusanywa tena Yer. 30:11; Eze. 37:21-22)
  • Nguvu za Kaskazini zina uadui na taifa la Israel kama Urusi iliyoendelea.
  •  

MUNGU KATIKA BIBLIA

Biblia inaaza kwa kuongelelea mtu mmoja ambaye ni Mungu (Mwa. 1:1). Na ufunuo unamalizia kwa kuonyesha jinsi Mtu huyu mmoja atakavyo wekwa wazi kwa viumba vyote. “Mungu awe yote katika wote” (1 Wakor. 15:28). Inatuonyesha jinsi kila mmoja wetu anaweza kushiriki katika kukamilisha utukufu wa Mungu. Injili inatuita kila mmoja wetu tujitenge kutokana na wanaume na wanawake ambao wanajitengenezea njia ya kuelekea kuzimu milele. Mungu anachukua watu wake kutoka kwa Gentiles (Matendo. 15).

Jambo la kwanza muhimu ni kuelewa kwa usahihi Mungu ni nani (Yoh 17:3; Waebr. 11:6) lazima tukubali umoja wa Mungu an kwamba kuna Mungu mmoja pekee amabye ni Baba yetu sote. Pia inatubidi tukataane na wazo  la wengi kwamba Mungu ni Utatu(Angalia 1 Tim. 2:5; Kumbu. 6:4; Isa. 45:5; 1 Wakor. 8:6; 2 Wakor. 1:3). Ni bora kukumbuka kwamba Yesu Christo alisema yeye ni mtumishi wa babake (Yoh. 12:28; 1 Wakor. 15:24-28) na roho mtakatifu ni nguvu za Mungu (Lk. 1:35; Matendo 3:12).

TABIA ZA MUNGU

Kuna pande mbili katika tabia za Mungu tunapaswa kufikiria. Paulo alisema “ fikirieni kuhusu wema na ukali wa Mungu (Warum. 11:22. Pande hizi mbili za tabia ya mungu zilidhihirishwa na Musa katika Mlima Sinai(Kumb. 34:6-7) n azote zilidhihirika katika uhusiano wake na mwanadamu. Kwa mfano kipindi kile Mungu alimtuma Musa kuwokomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Aliwaokoa kutoka kwa bahari ya Shamu lalini aliangamiza majeshi ya Faraoh. Yesu Bwana anakuja kuhukumu dunia kwa haki. Hii inammanisha kutakuwa na huruma na ukombozi wa wateule wake na pia kifo na uharibifu kwa wale waovu.

Sababu ya haya ni uasi wa binadamu”  hata neema ionyeshwe walio waovu hawatajifunza haki (Isa. 26:10-11) Mungu anafunza binadamu kwa wema wake na wokovu wa milele.

Biblia Inatufundisha kwamba Mungu ni asiyebadilika kwa lengo lake (Mal. 3:6) Yeye ni mwenya kujua yote (Zab. 139:1-6) Yupo kila mahali (vv.7-12); na ni mwenya nguvu (vv. 13-18).

Ni ukweli kwamba Mungu anayajua yote (Wahebr. 4:13; Jer. 23:24) na anaweza kutelekeza mapenzi yake ili kutuonyesha jinsi tunavyostahili kuishi mbele zake. Hata hivyo yeye hutawala kwa maenzi na wala sio woga. Madhumuni ya ufunuo wake ni kubadili tabia zetu ili tupate kuendana na njia zake, na tuwe tunafaa kiakili na kimaadili ili tuweze kupewa uzima wa milele na  Kristo anarudi tena( Wafilipi 3:20-21.).

KUSUDI LA MUNGU

Kusudi kuu la Mungu imeelezwa kwa kimsingi katika Numbers 14:21- kama kweli ninavyoishi dunian yote itajazaa utukufu wa bwana.” Hii inamaanisha nini? Dunia nzima itangaa kwa nguvu an utukufu wa mungu lakini utukufu wa mungi ni zaidi ya haya. Inagusia tabia zake. Wakati Musa alimwomba Mungu amwonyeshe utukufu wake, Kwa kumjibu Mungu alimwonyesha tabia zake, mwenye  huruma, neema na mwingi wa rehema na ukweli. Kutok. 33:18; 34:6-7)

Utukufu wa Mungu utadhihirika kwa wote himu duniani wakati wanaume na wanawake watakoa uonyesha katika maisha na tabia zao. Yesu alituonyesha maisha yake ya "utukufu wa Baba yake" kwa kuwa alikuwa "amejaa neema na kweli" (Yoh. 1:14). Yeye ni mzaliwa wa kwanza wa ndugu wengi na tunaweza kuwa miongoni mwa wale ambao watakuwa kukombolewa tukifuata mfano wake (1 Petr 2:21;. Warum 8:29-30.).

Mungu anawaita wanaume na wanawake kwa lengo hili.kama tunaweza kuelewa madhumuni ya Mungu na kuonyesha tabia ya Mungu katika maisha yetu, wakati Kristo atakaporudi, tutapewa asili ya Mungu (1 Petr 1:04.), Na kuonyesha tabia za Mungu katika ukamilifu wa uzima wa milele.

Wacha tuangalie Masomo yetu ya Biblia ili tuweze kupata “hekima na hata kupata wokovu” na ili tustahili kuingia katika ufalme wa mbiguni wakati Yesu ataporudi.

MASOMO KWETU

  • Ni kwa kusoma Biblia tu ndio tunaweza kujua hatima ya mwisho ya dunia na mwanadamu
  • Mungu anataka tujue Ukweli Kumhusu
  • Kusoma Biblia kunaweza kubadili maisha yetu
  • Jinsi gani kijana kubali njia zake na kutii na kulifuata neon lako? (Zab. 119:9).
  • Msimkatae yeyote anayeongea (Ebr. 12:25)
  • Hakikisheni kila jambo huku mkizingatia yaliyo mema. (1 Wathesalonike 5:21.).

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"Christadelphian Instructor" (R. Roberts)—Nos. 6-15

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 1 & 2

"Elpis Israel"—Sehemu ya kwanza, Sura 1

"Christendom Astray" (R. Roberts)—Sura 1 & 6

"First Principles Bible Marking Course" (C.S.S.S.) — Kurasa 1-8

"God's Way" (J. Carter)—Sura 1 & 2

 

MASWALI YA AYA

  1. kwa nini Mungu alitaka Bibilia kuandikwa?
  2. Elezea Matukio mawili ambayo yametokea kwa mataifa katika karne ya ishirini yanayoonyesha kwamba Biblia ni ya ukweli?
  3. Uthibitisho gani unaweza kutoa kutoka katika Biblia kuonyesha kuwa Mungu ni mmoja?
  4. Ni mambo gani mawili kuhusu tabia ya Mungu? Toa mfano unaoonyesha jinsi tabia za Mungu zilivyoonyeshwa zamani na siku zijazo.

MASWALI YA INSHA

  1. Ni msingi gani tunao wa kuamini Biblia iliandikwa kwa upako?
  2. Nini kusudi la Mungu huku duniani na litatimizwa aje?
  3. Kwa ujumla Biblia inatufunza nini kuhusu;

    a) Mungu
    b) Kusudi lake
     
Swahili Title
MUNGU, MWANDISHI WA BIBLIA
English files
Sub type
Sub sub type