256. NUHU- KUHARIBIWA KWA ULIMWENGU AWALI
"Watu wanne waliokolewa na maji"
Sura ya nne ya katika Mwanzo inaeleza yale yaliyotokea wakati Kaini alifukuzwa mbele ya Bwana, na kuanza maisha kwa njia ambayo inalingana na mapenzi ya binadamu. Roho ya Kaini iliendelezwa katika uzao wake. Ilikuwa sifa ya maisha ya mji (v.17), biashara haramu (mst. 20), kuishi bila kumjali Mungu (v.21), vita (v.22). Walikuwa kweli "wana wa wanadamu".
Mwanzo 4 unaeleza kuzaliwa ya Seti. Jina lake lilimaanisha "kuteuliwa", kwa ajili Mungu alimpa Hawa uzao mwingine badala ya Abeli, ambaye Kaini alimuua (v.25). Wakati uzao wa Kaini ilikuwa umejaa wale wanaopenda dunia, na vurugu, uzao wa Sethi ulihifadhi njia za Mungu, na kutambua kwamba maisha yao ya baadaye yalikuwa kwa mikono Yake. Kwa Hivyo walimwita kutimiza ahadi yake ya ukombozi (v.27). Wazao wa Seti wako kwenye kumbukumbu katika Mwanzo 5. Uzao huu unafikia upeo katika Nuhu, wanawe walikua Shemu, Hamu na Yafeti. Uzao huu ukawa "wana wa Mungu".
Lengo la somo hili ni kuonyesha jinsi dhambi na uovu waliwaadhibu wana wa Mungu wakati walijiunga na njia ya dunia.
Mwanzo 6-9
NA MKAJITENGE (Mwanzo 6:1, 2).
Kwa muda mrefu wazao wa Seti walijitenga kabisa na wazao wa Kaini, wanaume wenye ubinafsi ambao hawakujali chochote kuhusu njia ya Mungu. Kaini maana ya "faida", na wazao wake walitafuta furaha katika dunia bila kujali kutoa chochote ili kukidhi hisia. Walikuwa na mafanikio sana katika kutekeleza azma yao ya utajiri na furaha ya mwili; na walikuwa wakatili sana kwa wale wlijaribu kupinga njia zao.
wazao wa Sethi walikuwa tofauti. Walitupilia mbali mambo hayo ya kuridhisha mwili na wakamtumainia Mungu. Waliwapenda wale ambao walikuwa wa haki kama vile Henoko - yeye "alitembea pamoja na Mungu, naye Mungu akamtwaa" (Mwanzo 5:24).
Lakini tofauti kati ya makundi haya mawili ikatoweka. Kulikuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na jinsi wanaume walienea ulimwenguni, "wana wa Mungu" wakaanza kutamani maisha ya raha ya wana wa watu. Na Mwishowe kukawa hakuna tofauti. Baadhi ya "wana wa Mungu" wakawa urafiki na "mabinti wa wanadamu," na kufanya ndoa nao.
Kumbuka kuwa Kaini alikuwa amefukuzwa katika uwepo wa Mungu (ambapo wana wa Mungu walimcha) kwa nchi ya Nodi (yaani uhamishoni). Kwa Hivyo mwana wa Mungu kuoa mmoja wa binti ya watu ilikuwa kuondoka katika njia ya haki, na kukubaliana na yale yatasababisha uhamisho wako kutoka kwa Mungu. Ndoa nje ya ukweli ni mbaya (2 Kor 6:14.), Na hii inaongeza maovu zaidi. Ushirikiano imeonekana kuwa na maafa kwani "wana wa Mungu" walitamani njia za kidunia. Vijana wa leo wanatamani njia za dunia. Wako kwenye hatari ya kiungia katika ndoa iliyo tofauti ya ukweli.
DUNIA YA MABAYA (Mwanzo 6:3-7).
Katika siku hizo, kulikuwa watu wenye ukubwa katika uhalifu. Wao ni kama "mashujaa" - watu wenye sifa - maarufu kwa uovu wao. Tabia yao inaweza kuonekana katika Ayubu 22:15-17 - "ambapo walimwambia Mungu, ondoka na kipi kizuri unaweza kutufanyia".
Uovu ukuja kwa wingi kutoka kila upande. Mioyo ya watu ikajaa ya uasi na uovu (v.5). "Dunia imeharibika mbele ya Mungu na kujazwa na vurugu" (v.11). Rushwa ikawa kubwa na Mungu akaamua kumaliza ustaarabu huu (vv.5-7).
WITO YA NUHU (Mwanzo 6:8-10).
Peke yake katika ulimwengu wa uovu, "Nuhu alipata neema machoni pa Bwana" (v.8). Tabia yake na mwenendo ni ilivyoelezwa katika aya ya 9: "Nuhu alikuwa mtu wa haki, na kamilifu aliye na haki, bila lawama) katika kizazi chake, na Nuhu alikwenda pamoja na Mungu." Ingawa amezungukwa na uovu kila upande yeye alisisitiza njia ya haki, na Mungu akamtazama na neema na akakubalika kwake: "sijaona mwengine kama wewe aliye na haki mbele zangu katika kizazi hiki" (07:01; linganisha Ebr 11:07..)
HUKUMU YA MUNGU (Mwanzo 6:11-13).
Dunia ilikuwa iwe chini ya utawala wa binadamu (1:26). Lakini wakati Adamu alitenda dhambi, mwanadamu akawa chini ya utawala wa dhambi. Kama vizazi vyote, binadamu wakawa watumwa wa tamaa zao (Ecc. 7:29). Kwa sababu walimtoroka Mungu, Yeye pia akawaacha (linganisha Warumi 1:28.).
Hata hivyo, katika uso wa hukumu, uvumilivu wa Mungu bado upo. Ana nia ya kuwapa wanadamu miaka 100 ya kutubu kwa kutambua dhambi zao, waungame na kumgeukia kwake (v.3;. 1 Pet 3:20). Katika kipindi hiki, Nuhu, baada ya maelekezo kuhusu hukumu ya Mungu inayokuja (v.13), alitangaza neno la Mungu na kuwakaribisha wote waliomsikia kugeuka na kujiunga naye. Hivyo akawa "mhubiri wa haki" (2 Pet 2:05.). Mungu aliamuru Nuhu atengeneze safina ambayo wangeweza kupata malazi kama wangetii onyo lake la mafuriko kuja duniani. Safina lilionyesha imani yake na kutoa ushahidi wazi kwa wote ujumbe aliohubiri.
SAFINA LA USALAMA (Mwanzo 6:14-21)
Jahazi hiyo ilikua mashua kubwa sana, hata kwa viwango vya kisasa. Katika siku hizo, ilionekana kama chombo cha ajabu. Ukubwa wake ingekuwa karibu mita 150 upana wa mita 25 na urefu wa mita 15.
Vipimo vya safina vilikuwa vimetoka kwa Mungu. Ilitumia mti wa mvinje, pamoja na vyumba, wakapanga ndani na nje kwa lami. Wakaweka dirisha na mlango, na ikawa na ghofora tatu.. Nuhu, na vizazi vyake, walikuwa wameelezewa kwamba wokovu utapatikana tu kama maelekezo ya Mungu yangefuatwa.
Kila kiumbe hai duniani kingekufa, isipokuwa wale wangeingia katika safina la Usalama. Ili kulinda maisha, aina mbili ya kila wanyama na ndege, wa kiume na wa kike, wakaongozwa katika safina, na Nuhu na familia yake. Chakula kiliandaliwa na kuhifadhiwa huko kwa muda ambao wangekuwa ndani.
WITO WA WOKOVU (Mwanzo 6:22).
Katika haya maandalizi yote Nuhu alihubiria watu. Aliwaonya kuhusu hukumu inayokuja,akiwaomba kuachana na njia zao za dhambi.(Ebr. 11:07). Na kama aliyohubiri, ndivyo aliendelea kujenga Safina, ilionekana ajabu kwa watu kuona mashua kubwa ikijengwa juu ya nchi kavu, mbali na maji. Ni lazima kuwa Nuhu alionekana wazimu kwa ajili ya kufanya jambo kama hilo. Bila shaka walimcheka na kumdharau. Hakuna aliyeonekana kuitikia wito wake kutubu dhambi.
Miaka ikapita na jahazi akaendelea kuchukua sura. Nuhu alibakia ushujaa katika haya yote. Lakini kama muda ulivoendelea bila hukumu, watu wakapunguza wasiwasi kidogo kidogo kuhusu yale Nuhu alikuwa amesema.Kama vile watu leo ââhupuuza ishara ya kurudi kwa Kristo na kujishughulisha kwa raha za ubinafsi (linganisha Mathayo 24:36-39. ).
Kuna haja kua na subira sasa kama ilivyokua wakati ule. Ingawa ilionekana kuchelewa, Kristo atakuja kwa wakati uliopangwa (Matendo 17:31), kuharibu waovu na kuokoa wateule wake.
GHARIKA (Mwanzo 7).
Safina ilikamilika na maelekezo yote ya Mungu yakafuatwa, Nuhu aliamriwa kuingia na familia yake (v.1). Nuhu alitolewa duniani kabla ya gharika kutokea (v.4), na kwa njia hiyo hiyo, rafiki wa Bwana Yesu watakusanyika kutoka mataifa kabla Mungu kuadhibu dunia (Isa 26:20; 1 Wathesalonike . 4:16-17; Mathayo 24:31)..
kulingana na maelekezo ya Mungu, Nuhu alichukua aina saba (kiume na klike)katika safina ya kila nyama safi na ndege, na aina mbili za wanyama na ndege wachafu (v.2;. Linganisha kiasi). Basi, "Bwana akamfungia " (v.16), na kwa kufanya hivyo, akawafungia wengine wote nje.
Siku saba zikapita. Dhoruba-mawingu yakakusanyika, na yakawa meusi na ya kutishia. Kisha dhoruba ikaanza kwa hasira kubwa, na maji kutoka angani yakajiunga na maji kutoka chini ya kinana kama chemchemi yakaanza kujaa ulimwenguni.
Mvua Ilinyesha bila kukoma kwa siku arobaini mchana na usiku, hivyo kwamba hata milima ya juu walikuwa imefunikwa. Safina alichukuliwa juu ya maji, ambayo pale ilipokaa kwa muda wa siku 150, na kila kilichokuwa hai kiliharibiwa kuanzia, mwanadamu na wanyama, vitambaavyo, ndege wa mbinguni; waliangamia; Nuhu ndiye aliponea na wale waliokuwa pamoja naye katika safina "(v.23).
KUTOKA KWENYE GHARIKA
Mungu ikasimamisha mvua na chemchemi za kina, na kusababisha upepo kupita juu ya ardhi ili maji yapunguke. Polepole maji yalipungua na katika siku ya 17 ya mwezi wa saba safina ikatua juu ya milima ya Ararati. Siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima viliweza kuonekana. Siku ya arobaini baadaye, Nuhu alifungua dirisha la safina na alimtuma kunguru na njiwa ili kuona kama maji yamepunguka. Kunguru hakurudi, lakini njiwa alirudi, baada ya kupata "hakuna pahali pa kutua wayo wa mguu wake" (mst 9). Siku saba baadaye, njiwa alitumwa tena, na akarudi na "jani la mzeituni alilo ng'oa", ambapo Nuhu alijua kuwa maji yalikuwa yameisha (v.1 RSV). Baada ya siku saba zaidi, njiwa alitumwa nje mara ya tatu, lakini hakurudi.
Nuhu alikuwa katika safina kwa zaidi ya mwaka (linganisha 7:11 na 8:13-14). Kisha Mungu amemwagiza kuchukua familia yake na wanyama wote na ndege wote, na kuondoka safina, ili kuanza mwanzo mpya duniani. Nuhu akatoka kama ilivyoamriwa, na tendo lake la kwanza lilikuwa kujenga madhabahu na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu katika shukrani kwa ajili ya ukombozi wake.
ISHARA YA AGANO LA MUNGU (Mwanzo 8:21-22; 9:8-16).
Mungu alikubali sadaka ya Nuhu. Aliweka ahadi na kutangaza kwamba tena hatalaani duniani kama alivyokuwa amefanya, kuharibu viumbe hai wote. Laana ya Edeni juu ya ardhi, na ambayo ilizaa 'miiba na michongoma', lakini Mungu hatatuma tena mafuriko kwa ulimwengu wote (linganisha Isa 54:9.).
Kama ishara ya agano hili, Mungu aliweka upinde wake katika wingu. Upinde wa mvua hutokea wakati jua limeng'aa na mvua inanyesha kwa wakati mmoja. Kuna rangi saba katika upinde - saba ni namba ya agano - na wakati rangi hizi saba zimeunganishwa, huunda mwanga safi wa jua. Katika Biblia , jua husimamia Yesu, "jua la haki" (Malaki 4:02); wingu husimamia watu wa Mungu (Ebr. 12:01); mvua husimamia mafundisho ya Mungu akishuka kwa ajili ya ardhi (Kum. 32:2). Hivyo, ishara ya upinde wakati watu wote watajua Bwana. Utukufu wa Bwana Yesu Kristo kuonekana kwa njia ya watakatifu, kwa njia mbalimbali, wote wakichanganywa kuonyesha utukufu kamili wa utawala wake.
Yohane, katika Ufunuo 4, anatupa picha ya kuanzishwa kwa Ufalme, na Kristo (v.2) ameketi juu ya kiti cha enzi, akizungukwa na watakatifu wake (vv.4, 6), na upinde wa mvua ukiwazunguka.
Kadhalika, Ufunuo 10 inatoa picha ya malaika mwenye nguvu (anayewakilisha Kristo na watakatifu wake wa milele), amevaa upinde, akitekeleza hukumu ya Mungu juu ya mataifa.
MAELEZO YA UBATIZO.
Petro (1 Petro 3:20 .) anailinganisha wokovu wa Nuhu katika jahazi kama ubatizo na Kristo na ubatizo katika maji dhambi zetu huoshwa. Hivyo, katika siku za Nuhu, maji ya gharika yalisafisha dhambi za dunia ya zamani, ili ulimwengu mpya uweze kuanza. Ubatizo ni ishara ya mwanzo wa maisha mapya (linganisha Mdo 2:38;. Rum 6:04). Kwa ubatizo tunaingia ndani ya Kristo (Gal. 3:27), ambaye ni safina ya usalama wetu.
Kwa sababu sisi tuko "katika Kristo", sisi tutaokoka wakati hukumu ya Mungu itatolewa kwa dunia ya waovu - dunia ambayo Yesu alisema itakuwa sawa "kama ilivyokuwa siku za Nuhu". Neno "Nuhu" ina maana ya "pumzika", na katika siku ya hukumu, wakati Mungu ataweka utaratibu mpya duniani, kutakuwa na "mapumuziko" kwa waumini (Ebr. 4:09).
MAFUNZO KWETU
• Wakati wazao wa Seti walioa "mabinti wa watu", Ukweli ukaoza: na haikuwahi kuwa ya manufaa .
• Mungu kuamua kuhukumu dunia kwa gharika, lakini alionyesha uvumilivu na rehema zake kwa kuwapa miaka 120 ili kuendana na haki na mahitaji Yake.
• Nuhu, ingawa alikua peke yake, alitangaza uaminifu na haki ya Mungu.
• Kwa kukubali njia ya Mungu, Nuhu alikuwa na uwezo wa kuokoa yeye na familia yake.
• dunia ya leo ni "kama ilivyokuwa siku za Nuhu" - kipindi cha "kula na kunywa, kuoa na kuolewa"; kutojali umri (Luka 17:26-27).
• Kama Nuhu aliokolewa na maji, hivyo basi sisis pia tunaweza kuokolewa kwa njia ya ubatizo katika Kristo.
MAKTABA YA KUREJELEA:
" The Visible Hand of God" (R. Roberts)—sura ya tano
"Elpis Israel" (J. Thomas)—Uk. 118-120
"Noah—Preacher of Righteousness" (J. Martin)—C.S.S.S. Study Notes
"The Genesis Flood" (Henry M. Morris & John C. Whitcomb Jnr.)
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Vol. 1, UK. 61-74
MASWALI YA AYA:
1. Eleza jinsi uasi ulisababisha mafuriko katika siku za Nuhu?
2. Ni jinsi gani Mungu alionyesha mateso yake ya muda mrefu katika siku za Nuhu? Taja kazi ya Nuhu kwa watu.
3. Jinsi gani ulimwengu wa leo unalinganishwa na siku za Nuhu? Tunapaswa kufanya nini ili kuepuka hukumu ya Mungu inayokuja?
MASWALI YA INSHA
1. Andika Unachoelewa kuhusu kazi ya Nuhu?.
2. Masomo gani tunayojifunza kutokana na mafuriko katika siku za Nuhu?
3. Kwa kifupi eleza hadithi ya mafuriko na masomo yake.
sehemu ya pili
INJILI ILIYOHUBIRIWA IBRAHAMU
Wito wa Ibramu ( aliyeitwa Ibrahamu hapo mbeleni) ulikuwa mwanzo wa enzi mpya katika shughuli za Mungu na watu. miaka ilikuwa imepita tangu Gharika kukomesha dunia. Ilifuatiwa na mnara wa Babeli, na hukumu ya Mungu ambayo ilileta mchanganyo wa lugha na ufanisi ukawagawanya kuwa mataifa.
Lakini si Gharika wala machafuko ya lugha iliweza kuzuia wimbi la mauovu, kwa ajili ya tamaa ilibakia kama kanuni ya uovu ndani ya asili ya binadamu, ambao wako tayari kukaidi amri za Mungu.
Tunaweza fanya nini ili sauti ya ukweli wa Mungu kuendelea katika nchi? Jibu litapatikana katika wito wa Ibrahimu, na maendeleo kutoka kwake kwa taifa la Israeli. Kutoka mwanzo, ilikuwa wazi nia ya Mungu na kutengeneza Mwanga ili wengine, wavutiwe na uzuri wake,ili waje waokolewa. Mafunzo yanayo fuata yana zungumzia kwa kifupi jinsi haya yalifanyika.