Somo la 9
UFALME WAKO UJE
SOMO : 1 Nyakati 29
âUfalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama mbinguniâ.
Ni mara ngapi umeyasema maneneo haya, au kuyasikia yakitamkwa na wengine? Yapo yakiwa ni sehemu ya maombi, ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake. Unaweza kuyasoma katika Luka 11:2-4. Tunayafahamu maneno haya vizuri, lakini unajua yanachokimaanisha?
Yaangalie tena. Ni maombi kwamba Ufalme wa Mungu uweze kuja ili mapenzi yake Mungu yaweze kutendeka katika dunia hii, kama yanavyofanywa wakati wote huko mbinguni. Kwa hiyo tunaona moja kwa moja kuwa, Ufalme ambao tunauombea ni wa kuwa hapa duniani, na kwamba, Ufalme huo wa Mungu ukija, ndipo watu watakapoyatimiza anayoyapenda Mungu, katika dunia hii.

Nchi kwa ajili ya Ufalme
Ufalme ni lazima uwe na mahali, na miaka elfu kadhaa iliyopita Mungu aliichagua nchi ambayo itakuwa Makao-Makuu ya Ufalme wake; ni nchi ya Israeli.
Yerusalemu ni Mji-Mkuu wa Israeli, na ndio utakaokuwa âkitovuâ cha utawala wa dunia, wakati Yesu Kristo akiwa Mfalme. Yesu mwenyewe alisema:
âUsiape kabisa, hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kitu cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuuâ (Mathayo 5:34,35).
Yesu aliyapata maneno haya kwenye Zaburi ya 48; kitu kinachotudokezea kwamba, tunapaswa kulisoma Agano la Kale nalo vizuri. Msitari wa pili wa Zaburi hiyo unasema hivi juu ya mlima Sayuni, mahali Yerusalemu ilipo:
âKuinuka kwake ni mzuri sana, ni furaha ya dunia yote, mlima Sayuni pande za kaskazini; mji wa Mfalme mkuuâ (Zab.48:2).
Mlima Sayuni ni sehemu ya Yerusalemu na hapa unaelezewa kuwa, âNi furaha ya dunia yoteâ. Zaburi ya pili nayo inasema: âNami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifuâ. (Zab.2:6).
Zaburi hii ni unabii unaohusu wakati Yesu atakapokuwa akitawala kutoka katika mlima Sayuni. Mungu alichagua âkuliweka Jina lakeâ katika jiji la Yerusalemu miaka mingi nyuma. Katika 2 Nyakati 6:5;6 alishasema: ââ¦Lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humoâ.
Hapa kuna vifungu vingine viwili kwa ajili yako kuvisoma kiuangalifu:
- Isaya 62:1-7: Tunatakiwa kumwomba Mungu aifanye Yerusalemu kuwa mahali pa sifa duniani (âtaji ya uzuriâ).
- Isaya 65:l7-25: Mungu anaweka mpango wake juu ya Yerusalemu, na anatutaka tuufurahie.
Kuliwahi kuwa na Ufalme wa Mungu katika dunia hii miaka mingi iliyopita, katika Agano la Kale. Je, unalifahamu hilo?. Fungua sasa 1 Nyakati 29, na soma msitari wa kwanza, na wa 10 mpaka wa l3. Msitari wa 11, unasema:
âUfalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyoteâ (1 Nyakati 29:11).
Ufalme unaoongelewa, kama utakavyoona unavyoendelea kukisoma kifungu hiki, ni Ufalme wa Israeli, katika nchi ya Israeli, kwani tunasoma:
âNdipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babayeâ (1 Nyakati 29:23).
Kiti cha enzi alichokikalia Daudi na ambacho mwanawe Sulemani alikikalia baada yake, kilikuwa ni mamlaka katika Yerusalemu, mji uliokuwa mkuu katika nchi ya Israeli. Ufalme ambao aliutawala akiwa mfalme ulikuwa Ufalme wa Israeli.
Ni kwa nini Ufalme wa Israeli uliitwa Ufalme wa Mungu, na âkiti chake cha enziâ kiliitwa, âKiti cha Enzi cha BWANA?â Sababu ni kwamba:
|
Ufalme wa Mungu ulipinduliwa
Mamia ya miaka yalipita. Wafalme mmoja baada ya mwingine waliitawala Israeli katika Yerusalemu. Baadhi yao walikuwa wafalme wazuri waliowaongoza watu wao kwa kumcha Mungu, na wafalme wengine walikuwa waovu; wasiozizingatia Sheria za Mungu.
Mwisho ulifika wakati ambao Taifa la Israeli liliziacha mno njia za Mungu na mfalme katika Yerusalemu alikuwa mwovu mno. Mwenyezi Mungu aliamua kuuvunjilia mbali Ufalme huo.
Soma Ezekieli 21:25 â 27, na hasa msitari wa 27 unaosema: âNitakipindua, nitakipindua, nitakipindua (kiti cha enzi cha Israeli katika Yuda); hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake, nami nitampaâ.
Yeye ambaye âni haki yakeâ
Tunaweza kuona kutoka katika mistari hiyo ya Ezekiel kuwa, kulikuwa na mtu âwa kujaâ ambaye Kiti hicho cha Enzi cha Ufalme wa Mungu kilikuwa ni âhaki yakeâ. Huyu alikuwa awe ndiye mrithi wa kukifaa, na Mungu alikuwa amepanga kukimpa.
Tokea wakati huo wa mfalme huyo wa mwisho aliyengâolewa kutoka katika kiti hicho cha enzi, mpaka sasa, hakujawa na mfalme wa Kiyahudi aliyetawala katika Yerusalemu tena. Lakini fungua Biblia yako kwenye Luka 1:31 â 33 na usome maneno yaliyosemwa na malaika kwa Mariamu, mama yake Yesu. Akisemea malaika juu ya jina la Yesu, alisema:
|
Huyo atakuwa Mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye Juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yakeâ (Luka 1:32). |
Ni nani aliyekuwa na âhakiâ ya Kiti cha Enzi cha Ufalme wa Mungu? Hakika ni Yesu, Mwana wa Mungu. Haki yake ina sura mbili:
- Alikuwa ni Mwana wa Mungu.
- Mama yake Mariamu alikuwa wa uzao wa Daudi.
Kuna kutokuelewa kwingi kunakohusu utawala wa Yesu katika Ufalme wa Mungu. La muhimu kutambua ni kwamba:
|
Hii ndio sababu ya Yesu kurudi duniani. Kusudi la Mungu linawahusu wanadamu katika dunia na atalitimiza, ndio maana Mwenyewe anasema: âDunia hii nzima itajawa na utukufu wa BWANAâ (Hesabu 14:21).
Kufikiri kwamba mtu anakwenda mbinguni anapokufa, hakwendani na Maandiko; hakukubaliani na kile Maandiko yanachofundisha. Ufalme unaoanzishwa ni wa hapa katika dunia. Mungu anaongoza kutoka katika mbingu, lakini mpango wake ni kumtuma Yesu kuitawala dunia. Wafuasi wake walio waaminifu wa enzi zote watakuwa watu wa kumsaidia katika jukumu hili kubwa.
Yesu alidai kuwa ni Mfalme. Kwenye kesi yake wakati Pilato alipomuuliza, âWewe u Mfalme basi?â, yeye alijibu, akisema: âWewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalmeâ (Yohana 18:37). Hii ni namna ya Kiyahudi ya kusema, âNdiyo!â
Juu ya msalaba Yesu aliosulubiwa, iliandikwa, âHUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDIâ (Mathayo 27:37). Maadui zake walidhani wanamdhihaki; hawakujua kuwa wanachosema ni KWELI.
Injili aliyoihubiri Yesu ilikuwa ni Habari Njema ya huo Ufalme wa Mungu. Katika Luka 8:1, tunasoma kuwa: âAlikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji, akihubiri na kuitangaza habari njema ya Ufalme wa Munguâ.
Sasa unajua sababu ya kurudi kwake Yesu. Anarudi kuusimamisha tena Ufalme wa Mungu katika dunia.
|
KITI CHA ENZI CHA DAUDI KATIKA YERUSALEMU |
||
|
UFALME WA ISRAELI Wafalme katika Kiti cha Enzi Daudi, Sulemaniâ¦â¦â¦â¦ VITABU:Samweli na Wafalme; kama 1000 K.K. |
KITI CHA ENZI KITUPU Hakuna Wafalmeâ¦..
KITABU: EZEKIELI 21:27 600 K.K. Leo(tulipo) |
YESU: Kurudi kutoka mbinguni; kuusimamisha Ufalme wa Mungu duniani. KITABU: LUKA 1:32 Mbeleni â¦â¦â¦â¦. |
Ufalme huo na sisi
Pengine unaweza kufikiri, kwa nini, basi, tuombe âUfalme wako ujeâ, wakati Ufalme wenyewe ni wa Kiisraeli? Unatuhusu nini sisi?
Unavyoendelea kujifunza utagundua kuwa, Ufalme huo ambao Yesu atauongoza, utapanuka sana na kuenea maeneo ya mbali, kuliko ilivyokuwa kwa ule Ufalme wa Mungu wa kwanza. Utaenea dunia yote, na kuleta amani kwa watu wote.
Kwa hiyo tunauombea Ufalme wake uje, na tunaomba pia kwamba, Yesu atakaporudi aweze kutuambia: âNjoni mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwenguâ (Mathayo 25:34).
|
Muhtasari- Ona vile kila sehemu ya Biblia inavyosaidia kuelezea sehemu nyingine. Sasa tumejifunza kuwa:
|
Vifungu vya kusoma: Mwanzo 22, Wagalatia 3
Jifunze kwa moyo: Ufunuo 11:15
âMalaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na mileleâ.