Somo la 15
AHADI ZA MUNGU KWA DAUDI
Somo: 2 Samweli 7
Kijana mchunga-kondoo awa mfalme
Utakuwa pengine umesikia juu ya Daudi, kijana aliyekuwa mchungaji wa kondoo, aliyemuua Goliati, mtu wa âmaraba mitatuâ kwa kijiwe kimoja alichomtupia.
Daudi aliishi kama miaka 1000 kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa. Alizaliwa katika eneo moja na Yesu, katika mji mdogo karibu na Yerusalemu uitwao Bethlehemu. Alikuwa mwana wa kiume wa mwisho wa Yese, aliyekuwa mmiliki wa hao kondoo.
Wakati Daudi alipokuwa bado mdogo Mungu alimtuma nabii wake, Samweli, ampake mafuta ya kuwa mfalme juu ya Israeli. Lakini kwa wakati huo, mfalme Sauli, aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Israeli, alikuwa akitawala. Sauli alimuonea sana wivu Daudi, na kwa nyakatii mbalimbali alijaribu kumuua. Matokeo yake yalikuwa Daudi kumkimbia na kuwa mkimbizi.
Sauli hakuwa mfalme mzuri; hakumtii Mungu. Wakati ulifika akauawa katika pambano na Wafilisti. Hapo ndipo njia ilipofunguka kwa Daudi kuwa mfalme.
Baada ya majaribu mengi na harakati, Daudi alijenga Ikulu yake katika Yerusalemu, na ndipo alipoishi na kutawala.
Daudi alipofikiria jinsi Mungu alivyombariki na juu ya sanduku lake ambalo bado lilikuwa likikaa katika hema, alitaka kujenga Hekalu zuri katika Yerusalemu ambalo sanduku hilo lingehifadhiwa ndani yake. Sanduku hilo lilikuwa sanduku ambamo ndani yake kuliwekwa kibao cha Amri-kumi za Mungu, na lilikuwa na kifuniko kilipowekwa juu yake âkiti cha rehemaâ. Juu yake utukufu wa Mungu ulingâaa.
Daudi alimwambia alichotaka kufanya Nathani, nabii wa Mungu. Nathani alimjibu Daudi kwa kumwambia aendelee, lakini usiku huo Mungu alisema na Nathani, na kumpa ujumbe maalum sana kwa Daudi.
Ujumbe wa Mungu kwa Daudi
Fungua tena 2 Samweli, Sura ya 7. Sehemu ya muhimu sana ya ujumbe huo wa Mungu kwa Daudi, upo katika mstari wa 12 mpaka wa 16. Hapa Mungu anamuahidi Daudi kupata mtoto wa kiume. Anasema juu ya âmzaoâ huyo kuwa:
âYeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara mileleâ (ms. 13).
Hili lilikuwa litokee baada ya Daudi kufa, kwa kuwa anaambiwa katika mstari wa 12 kuwa, ni hapo, âSiku zako zitakapotimia, ukalala na baba zakoâ.
Zaidi juu ya huyo Mwana wa Daudi
Sasa Daudi alipata mwana aliyemwita Sulemani, aliyetawala baada yake katika Yerusalemu. Ahadi alizokuwa amepewa Daudi, kwa sehemu zilitimia katika Sulemani, lakini utimilifu wa ahadi hizo ulibidi usubiri ujio wa Bwana Yesu. Sulemani alifanywa mfalme wakati Daudi akiwa bado hai, na kwa vyovyote Sulemani hakutawala milele; alikufa.
Huyo mwana Daudi aliyekuwa ameahidiwa hasa, alikuwa awe mtu wa kipekee sana, kwa kuwa Mungu anasema juu yake kuwa:
âMimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwananguâ (2 Samweli 7:14).
Tugeukie Sura ya kwanza ya Luka. Hapa tunasoma juu ya malaika wa BWANA, aliyemtokea msichana mmoja, mmojawapo wa watu wa ukoo wa mfalme Daudi na kumwambia, atazaa mtoto wa kiume. Huyo alikuwa azaliwe, sio kwa njia ya kawaida ya baba wa kidunia, kama inavyokuwa kwa watoto wote. Alikuwa azaliwe kwa muujiza wa uweza wa Mungu. Mwanamke huyu aliyekuwa bado bikira, aliyeitwa Mariamu, aliambiwa:
âRoho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye-juu zitakufunika kama kivuli, kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Munguâ (Luka 1:35).
Malaika alimwambia tena Mariamu:
âHuyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwishoâ (Luka 1:32,33).
Sasa tunaweza kuona jinsi ahadi Mungu aliyompa Daudi, ilivyotimia alipozaliwa Yesu Kristo:
- Mungu alikuwa ndiye Baba yake.
- Yesu amewekewa atawale milele.
Mfalme wa Wayahudi
Yesu alizaliwa awe Mfalme. Mamajusi walipokuja kumsujudia Yesu, waliuliza, âYuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi?â (Mathayo 2:2).
Yesu alipokamatwa na kupelekwa kwa Pilato ahukumiwe, Pilato alimuuliza: âWewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?â Yesu alimjibu kwa kusema, âWewe wasemaâ (Marko 15:2). Hii ni namna ya Kiyahudi ya kusema: âNdiyo, kwa hakika ndiyeâ. Kama ambavyo tumekwisha kuona, Yesu atarudi katika dunia hii na kuwa Mfalme wa Wayahudi; na kutawala katika kiti cha enzi cha Daudi.
Ufalme wa dunia yote
Yesu hatakuwa Mfalme wa Wayahudi tu atakaporudi. Atakuwa Mfalme wa dunia nzima. Mungu alisema hivi juu yake: âNi neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu, ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya duniaâ (Isaya 49:6). âMataifaâ maana yake ni, âWatu wasio Wayahudiâ.
Daudi Je?
Ingawa Daudi alitambua kuwa ahadi hiyo ya Mungu isingetimizwa kwa kipindi kirefu sana, alikuwa na shukrani sana kwa Mungu. Tunaweza kusoma maombi yake ya kushukuru katika 2 Samweli 7:18-29. Mungu alimwambia:
âNa nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yakoâ (2 Samweli 7:16). Maana yake ni akiwepo.
- âNyumbaâ inaweza kuwa na maana ya jengo. Hekalu liliitwa, âNyumba ya Munguâ. Lakini ânyumbaâ inaweza kuwa na maana pia ya familia au ukoo, na hiki ndicho kinachomaanishwa katika ahadi hizi kwa Daudi.
Kwa hiyo Daudi mara nyingi aliifikiria hiyo ahadi, au agano, ambalo Mungu alikuwa amempa na analiongelea katika Zaburi. Kwa mfano, katika Zaburi 89: 2-4 analikumbuka likisema:
âMaana nimesema, Fadhili zitajengwa milele, katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. Nimefanya agano na mteule wangu, nimemuapia Daudi, mtumishi wangu. Wazao wako nitawafanya imara milele, nitakijenga kiti chako cha enzi hata mileleâ.
|
AHADI ZA MUNGU KWA DAUDI (2 Samweli 7) |
|
|
Andiko Ms. 12: âSiku zako zitakapotimia ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitafanya imara ufalme wakeâ. |
Muhtasari Maisha ya Daudi yalipokwisha, alikufa. Mungu angemwinua mmoja kati ya wazaliwa wake, na Mungu angeusimamisha tena Ufalme wake. |
|
Ms. 13: âYeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, |
Huyo âmzaoâ atamjengea Mungu nyumba. Sulemani alimjengea Mungu nyumba. Yesu Kristo anamjengea Mungu nyumba hata sasa (Soma Waefeso 2:19-22). |
|
â¦nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara mileleâ. |
Mungu atafanya ufalme wake imara milele. Sulemani hakutawala milele, wala Ufalme wa Israeli haukudumu milele. Yesu ndiye atakayetawala milele. |
|
Ms. 14: âMimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu, nitamwadhibuâ¦â |
Mungu atakuwa ndiye baba kwa mzaliwa huyu wa Daudi, naye atakuwa Mwana wa Mungu. Yesu ni mwana wa Mungu. Yesu hakutenda dhambi, hivyo Mungu hakulazimika kumwadhibu. |
|
Ms. 16: âNa nyumba yako, na ufalme wake, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara mileleâ. |
Nyumba ya Daudi na ufalme vitasimamishwa, na Daudi atakuwa yupo hapo. Hili litatokea hapo Yesu atakaporudi. Daudi atafufuliwa kutoka kwa wafu na kuwa katika Ufalme huo. Yesu kwa wakati huo atakuwa akitawala kutoka katika kiti cha enzi cha Daudi (Yerusalemu). Ufalme wake utakuwa hauna mwisho. |
Kitu cha kutazamiwa
Paulo anatuambia kwenye Waebrania 11:39,40 kuwa:
âNa watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi, kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisiâ.
Sasa, Ibrahimu na Daudi na waaminifu wengine wengi, walikufa wakijua kuwa, katika siku ya kuja kwa Yesu Kristo, watafufuliwa tena na âkukamilishwaâ. Watapewa uzima wa milele na wote wale walio wa Kristo. Lakini kama kifungu hicho kinavyoonesha, uzima wa milele hautakuwa kwa ajili ya watu hao waaminifu tu, unaweza ukawa wetu pia.
Msitari wa msingi
Tumeona kwamba Yesu Kristo ni mzao wa Ibrahimu, na mzao wa Daudi. Msitari wa kwanza kabisa wa Agano Jipya, unaanza na:
âKitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimuâ (Mathayo 1:1).
Kwa hiyo tunaweza tu kulielewa Agano Jipya, kama tumelisoma na kulielewa Agano la Kale.
|
Muhtasari
|
Vifungu vya Kusoma: 2 Samweli 7, 1 Nyakati 17.
Jifunze kwa moyo: 1 Nyakati 17 : 11, 12
âNa itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake mileleâ.