Somo la 16
BABA NA MWANA.
SOMO: Isaya 45
âJe! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu?â (Ayubu 11:7)
Hili swali liliulizwa maelfu ya miaka iliyopita. Jibu lake ni lile lile leo kama lilivyokuwa kwa siku hizo; kwa vyovyote hatuwezi! Hakuna kitu kabisa tunachoweza kujua kumhusu Muumbaji Mkuu wa vitu vyote, nje ya yale Yeye Mwenyewe anayotuambia katika Neno lake; katika Biblia. Hata hivyo hakuna tumaini la uzima wa milele tunaloweza kulipata, bila ya huko kumjua.
Njia pekee ya kuweza kumjua Mungu ni kwa kukisoma kitabu chake, Biblia, au kulisikiliza Neno lake, alilotupa. Mungu mwenyewe amesema:
âMawazo yangu si mawazo yetu, wala njia zenu si njia zangu, asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenuâ (Isaya 55:8,9).
Mungu ni Mmoja
âSikiliza, Ee Israeli, BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zoteâ (Kumb. La Torati 6:4,5).
Musa aliyasema maneno haya kwa Waisraeli wakiwa nyikani. Ujumbe kwamba âMungu ni mmojaâ, umerudiwa-rudiwa mara nyingi katika Maandiko. Katika Isaya 45:5 tunaambiwa:
âMimi ni BWANA, wala hapana mwingine, zaidi yangu mimi hapana Munguâ.
Miaka zaidi ya elfu baada ya hapo, mtume Paulo anasema kitu hicho hicho.
âMungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesuâ (1 Timotheo 2:5). Na tena, katika 1 Timotheo 6:15,16 Paulo anamuongelea Mungu kuwa ni:
âYeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Aminaâ.
Huyu Mungu aliye mtakatifu ni Mungu wa upendo.
Kama Biblia ingetuambia tu juu ya uweza na utakatifu wa Mungu, kwa vyovyote tungemcha, lakini tungeona shida kumpenda. Lakini Mungu ametuonesha kuwa, yeye pia ni mwema na amejaa huruma. Mwandika Zaburi anatuambia kuwa:
âBWANA amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhiliâ¦. Kama vile baba wahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana, Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbiâ (Zaburi 103: 8,13,14).
Ni katika huruma na upendo wake, Mungu ametupa Bwana Yesu Kristo kuzichukua dhambi zetu.
Mwana wa Mungu
Tangu mwanzo Mungu alikuwa amepanga kumtuma Mwanawe kutuokoa. Kuna utabiri mwingi kumhusu Yesu katika Agano la Kale. Katika Isaya 7:14, kwa mfano, tunaambiwa:
âTazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye utamwita jina lake Imanueliâ.
Maana ya Imanueli ni âMungu pamoja nasiâ. Mungu hapa anaahidi kumtuma Mwanawe mwenyewe. Angalia vifungu vingine hivi vinavyoonesha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu:
|
Wagalatia 4:4 âHata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria. |
|
Marko 1:11 âNa sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, nimependezwa naweâ (Mungu alisema hili katika ubatizo wa Yesu). |
|
Yohana 20:31 ââ¦â¦.ili mpate kuamini ya kwamba, Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. |
Yesu hakuwapo kabla
Mtoto anapozaliwa, ndipo maisha mapya yanapoanza. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo hakukuwa na utofauti.
Kuna watu wanaofikiri kuwa, Bwana Yesu Kristo alikuwepo kabla hajazaliwa na Mariamu. Kwa sehemu mtu anaweza kusema hivyo, kama ni kwa kumaanisha kuwa Mungu alishapanga tokea mwanzo kuwa angepata Mwana.
Mungu anapopanga kitu, tunajua kwa uhakika kabisa kuwa kitatokea. Yesu Kristo ni msingi wa kusudi la Mungu; ni mhimili wa mpango wote mkubwa wa wokovu. Kwa hiyo, Mungu alipokuwa akiwaambia waaminifu wa kale katika Agano la Kale kuhusiana na mpango wake huo, aliwaambia juu ya Kristo.
Kwa namna hiyo hiyo Biblia inamwongelea Kristo kuwa ni: âMwana-kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya duniaâ (Ufunuo 13:8). Hili halina maana kuwa Yesu alichinjwa kabla dunia haijaumbwa au wakati ikiumbwa. Tukio hili la kutisha lilitokea mara moja tu kama miaka 2000 iliyopita, Yesu aliposulubiwa (Waebrania 9:25â28).
Kwa kuwa kifo cha Yesu ni cha msingi sana katika kusudi la Mungu, Mwenyezi Mungu amekiongelea kama tukio lililo la muhimu sana linalowagusa watu wa nyakati zote, tangu wakati wa Agano la Kale. Kwa hiyo, ni kifo cha Yesu ambacho kimeyabadili mambo yote, âtangu kuwekwa misingi ya duniaâ.
Biblia inatumia lugha ya kuwepo-kabla katika kumwelezea Bwana Yesu, lakini haina maana kuwa tayari alishakuwepo; akiishi kabla ya kuzaliwa kwake. Alikuwepo, ndiyo, lakini ni katika mawazo ya Mungu. Mungu alipanga kufanya Yesu azaliwe kwa wakati aliouweka, âkatika utimilifu wa nyakatiâ (Waebr. 9:26).
Ni pale Mariamu alipomzaa mtoto wake huyo wa kiume wa kwanza, ndipo Bwana Yesu alipoanza kuwepo; alipoanza kuishi. Ni kama inavyokuwa kwetu.
Asili ya Yesu
Kwa kuwa Yesu alizaliwa na mwanamke, alikuwa na hulka kama ya kwetu. Katika Waebrania 2:17 tunaambiwa:
âKwa hiyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yoteâ.
Wakati wa uhai wake hapa duniani, alijaribiwa kwa namna nyingi, lakini hakuwahi kuanguka dhambini. Hebu vitazame vifungu hivi, vyote vikiwa vimechukuliwa kutoka katika kitabu kwa Waebrania, kuona kuwa Yesu alikuwa na hulka kama yetu, alipokuwa akiishi hapa duniani:
|
Waebrania 4:15 âKwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu, bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambiâ. |
Waebrania 2:14 âBasi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu ya mauti, yaani, Ibilisiâ. |
|
Waebrania 2:9 âIla twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtuâ. |
Waebrania 5:7,8 âYeye, siku hizo ya mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu, na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompataâ. |
Kwa vyovyote, Yesu alikuwa hivi kabla ya kufa na kufufuka kwake tu. Baada ya kufufuka alipewa hulka tofauti ya utukufu na nguvu; hulka ya kutoweza kufa tena.
Wazo potofu
Watu wengi wameyapuuzia mafundisho ya Biblia yanayomhusu Mungu, na kuja kuamini kitu wanachokiita, âUtatu Mtakatifuâ. Wanasema kuwa Mungu anazo nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, na wote wako sawa. Hakuna ukweli juu ya dhana hii. Tutatafakari kuhusu Roho Mtakatifu mbeleni kidogo, kwenye Somo la 20.
Maneno âUtatu-Mtakatifuâ na âMungu-Mwanaâ hayapo kabisa katika Biblia. Tumekwishaona mafundisho ya moja kwa moja ya Biblia kuwa Mungu ni mmoja, na kwamba Yesu ni Mwanawe. Kama vile mwana aliye mwema anavyokuwa chini ya baba yake, ndivyo Yesu alivyokuwa chini ya Mungu.
Yesu hakuwahi kudai kuwa yuko sawa na Mungu, bali alimtegemea Baba yake kwa mambo yote. Alisema, âMwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitendaâ (Yohana 5:19).
Ni kweli kwamba Yesu aliwahi kusema: âMimi na Baba tu umojaâ (Yohana 10:30). Alikuwa na maana kuwa, yeye na Baba yake walikuwa wamoja kidhamira na kimalengo, na aliomba umoja huo uwepo pia kati Yao na wafuasi (Yohana 17:21). Tunaambiwa:
âBasi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake(Yesu), ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika woteâ (1 Wakorintho 15:28).
Mstari huu unatuambia kuwa, hata baada ya utawala wa Yesu wa miaka 1000 katika dunia, ambao ni kipindi cha Ufalme wa Mungu katika dunia, Yesu ataendelea kuwa chini ya Baba yake, na Mungu atakuwa yote katika wote.
Imani ya âUtatuâ ilitoka wapi?
Wakristo wa awali hawakuamini âUtatuâ. Waliamini kile Biblia inachofundisha, kuwa: âMungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesuâ (1 Tim 2:5).
Sasa, mambo haya potofu ya âutatuâ yalitoka wapi?
Ilikuwa imepita miaka zaidi ya 300 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, âWakristoâ walipoanza kuamini katika âutatuâ. Wazo hilo halikuwa na msingi katika Biblia, badala yake lilitokana na imani za kale za Wayunani, ambao hawakuwa wakijua lolote kumhusu Mungu mmoja pekee Aliye wa Kweli. Pole pole, kanisa lililichukua wazo hilo la âMungu mmoja katika nafsi tatuâ, na kuukana ukweli wa Biblia unaomhusu Mungu.
âImani ya Mitumeâ iliyotungwa kama miaka 100 baada ya Kristo kupaa kwenda mbinguni, inaonesha imani waliyokuwa nayo Wakristo wa awali, Wakristo wa kwanza. Inasomeka hivi:
âNamwamini Mungu Baba, Mwenye uweza wote, Muumba wa mbingu na nchi. Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu. Aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na mwanamwali Mariamuâ¦â¦â¦â
Hiki ndicho hasa Biblia inachofundisha (tofauti na imani zingine). Ukuu na uweza wa Mungu ni vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu wa kufikiri. Tunajikuta tukishindwa kuelewa hasa-hasa jinsi Mungu huyu wa milele alivyoweza kupata mtoto na msichana huyu wa kimwili na damu, lakini yeye Mungu anatuambia ndivyo ilivyokuwa. Tunajua Neno lake ni kweli; wajibu wetu ni kulipokea hivyo kwa imani.
Kama tunahitaji kumpendeza Mungu, ni lazima tulipokee lile analotuambia bila kuongezea mawazo ya kibinadamu yasiyo kwenye Biblia.
|
Muhtasari
|
Vifungu vingine vya kupitia.
|
Yesu alianza kuishi alipozaliwa. |
1 Petro 1:20, Waebrania 9:26 |
|
Yesu alikuwa ni mtu. |
Matendo 2:22, Wafilipi 2:8, Waebrania 2: 9, 14 â 18. |
|
Mungu ni Mkuu kuliko Yesu |
Waefeso 4: 6, 1 Wakorintho 11:3, Yohana 14: 28, Yohana 10: 29. |
Vifungu vya kusoma: Kumb. la Torati 6, Mathayo 1:18â25.
Jifunze kwa moyo: 1 Timotheo 2:5
âMungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja; mwanadamu Kristo Yesuâ.