Somo la 17
MAISHA YA YESU
SOMO: Luka 2
|
âMalaika akamwambia, usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa mkuu, ataiwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwishoâ (Luka 1:30 â 33). |
Ni ujumbe wa ajabu kiasi gani huu, malaika aliomletea Mariamu! Lakini kuna moja lililomtatiza zaidi. Aliambiwa huyo mtoto atakayemwita Yesu atakuwa awe, âMwana wa Aliye juuâ. Mariamu anamuuliza malaika, âLitakuwaje neno hili?â
Malaika alimjibu kwamba, Mungu angetumia uweza wake kuwezesha mimba ya Mwanawe kutungwa. Hakuna mwanamume ambaye angehusika; ilikuwa Yesu awe mwana halisi wa Mungu.
Soma simulizi juu ya kuzaliwa kwa Yesu katika Mathayo 1 na 2, na katika Luka 2. Utaweza kuona ya kwamba, hakuna mahali katika Sura hizi panaposema Yesu alikuwa mbinguni kabla ya kuzaliwa kwake. Wazo kama hilo lingepingana na maelezo ya Kibiblia, kuhusiana na namna mama yake alivyoshika mimba na Yesu alivyozaliwa.
Ubatizo wa Yesu.
Biblia haisemei mengi kumhusu Yesu akiwa mtoto. Inaruka na tayari anakuwa kwenye ubatizo wake na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Ubatizo huo haukuwa wa kunyunyuzia vimaji kichwani. Ulifanyika katika mto, na baada ya hapo alipanda kutoka majini (Marko 1:10).
Mbingu zilifunguka na Mungu akamshushia Yesu Roho yake âTakatifuâ. Sauti ilitoka mbinguni ikisema: âHuyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa nayeâ (Mathayo 3:17).
Kwa kubatizwa, Yesu ametuonesha jinsi ubatizo ulivyo wa muhimu, na Mungu aliongezea kuthibitisha. Baada ya kubatizwa tunasoma kuwa, Yesu alikwenda nyikani, ambapo alijaribiwa na Ibilisi (Mathayo 4:1).
Lilikuwa ni âduduâ gani lililomjaribu?
Kilichotokea hasa ni nini pale nyikani? Ibilisi ni nini? Hebu tuyachunguze kwa umakini majaribu mawili kati ya yale matatu yaliyompata:
|
â(Ibilisi) akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yakoâ (Luka 4-5-7). |
Hakukuwa na mlima mrefu hapo mahali Yesu alipokuwa (ilikuwa nyikani), na hakuna ulipo popote katika ulimwengu huu, ambapo mtu akisimama, anaweza kuona falme zote za dunia. Kwa hiyo isingeweza kuwa kwamba Yesu kweli alipandishwa mahali pa namna hiyo.
Zaidi ya hapo Biblia inasema kuwa, dunia ni mali ya BWANA; iko mikononi mwa Mungu, sio Ibilisi. Inasema: âAliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yoteâ (Danieli 4:32). Zaburi ya 24:1 inasema: âNchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, dunia na wote wakaao ndani yakeâ.
Kwa hiyo inabidi tufikirie kwa makini maana iliyoko katika jaribu hili.
Sasa hebu tuangalie jaribu lingine lililomkabili:
|
â(Ibilisi) akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kwa maana imeandikwa, atakuagizia malaika zake wakulinde, na ya kwamba mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiweâ (Luka 4:9-11). |
Kwanza tujiulize kama kweli Bwana Yesu angeweza kulifuata hilo âduduâ lililojaa uovu, lisiloonekana, kutoka hapo nyikani, kupanda naye njia yote mpaka Yerusalemu, na kisha kukubali kuwekwa juu kwenye kinara cha hekalu, ili tu ajibu, âImenenwa, usimjaribu Bwana Mungu wakoâ (Luka 4:12). Kwa vyovyote, kama kungekuwa na dudu la namna hiyo, Yesu angelitambua mara moja, na kukataa kuwa na ushirika wowote nalo.
Kama hatuwezi kuelewa kwa namna majaribu haya yalivyotokea kiuhalisia, tutawezaje kuelewa yanachotufundisha?
Yesu alijijua kuwa alikuwa ni Mwana wa Mungu, na kwamba aliwekewa kuwa Mfalme juu ya falme zote za dunia. Katika jaribu la kwanza, aliweza kuzifikiria falme hizi na utukufu wake akilini mwake alipokuwa hapo nyikani. Lakini pia alifahamu kutokana na Agano la Kale kuwa, alipaswa kupata mateso na kufa kwanza msalabani, kabla ya kuyapata mamlaka hayo ya Ufalme wa dunia na utukufu wake.
Kwa jaribu la pili, Yesu atakuwa alifikiri kujitupa chini kutoka kwenye kinara cha hekalu bila kuumia kungekuwa njia nzuri ya kujijengea umaarufu, na kuthibitisha ya kuwa alikuwa ni Mwana wa Mungu. Hili lingeirahisisha kazi ya kuhubiri Injili iliyokuwa mbele yake. Lakini, alitambua haikuwa namna Mungu aliyoitaka.
Kwa hiyo, tunafikiri, majaribu haya yalikuwa ni fikra zilizomjea Yesu akilini akiwa nyikani. Alikuwa muda mfupi uliopita amejazwa Roho kutoka juu baada ya kubatizwa. Alikuwa sasa amepata nguvu sana zinazomvuta azijaribu, hata kama ni kwa kuyafanya mawe yawe chakula ili ale kutokana na njaa aliyokuwa nayo.
Lakini Yesu alijua kuwa, uweza unaotoka kwa Mungu ni lazima utumike kwa namna inayofaa. Kuongelea âIbilisiâ ni namna tu ya Ki-maandiko ya kusemea kwa kuficha, msukumo katika hulka zetu wanadamu unaotujia akilini mwetu sisi wote, kutuvuta tufanye yasiyokubalika. Kuutambua ni muhimu sana. Yesu alipatwa na majaribu haya kama na sisi yanavyotupata, lakini hakuwahi kujiachia ashindwe.
Yesu alikuwa na hulka gani?
Baba yake Yesu alikuwa Mungu, lakini mama yake Mariamu alikuwa mwanadamu. Je, Yesu alikuwa wa kimbingu, au alikuwa mwanadamu kama sisi?
|
Hulka ya kibinadamu (kama sisi) |
Hulka ya kimbingu (kama Mungu) |
|
Tunazaliwa.
Tunaweza kujaribiwa na tunafanya dhambi.
Tunakufa. |
Mungu amekuwepo nyakati zote (Zaburi 90:2).
Mungu hawezi kujaribiwa na hawezi kukosea.
Mungu hawezi kufa. Yeye ni wa milele. |
Ingawa Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu na alikuwa na Roho yake, alikuwa bado ni mwanadamu. Kama tulivyoona katika somo letu lililopita, rejea zifuatazo zinaonesha hili wazi: Waebrania 2:9, 14- 18; 1 Timotheo 2:5; Matendo 2:22.
Hatuwezi kuelewa sana jinsi Yesu alivyokuwa na baba wa kimbingu na mama wa kidunia. Tunapaswa tu kupokea kile Biblia inachosema juu yake. Biblia inatuambia pia jinsi Yesu alivyokuzwa (alivyo âadhimishwaâ) na kupewa utukufu (Wafilipi 2:9-11). Ni lazima tulipokee hili nalo.
Huduma ya Yesu
Baada ya ubatizo wake na majaribu katika nyika tunasoma kuwa, Yesu alisafiri katika miji yote na vijiji, akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, akiwa na wanafunzi wake kumi na wawili.
Sasa hebu tuyafikirie mafundisho yake, na miujiza aliyofanya. Tutatazama pia namna alivyoishi na jinsi alivyokikabili kifo chake:
1. Mafundisho ya namna tunavyopaswa kuishi.
Katika Mathayo, Sura ya 5, 6 na 7 yamejaa mafundisho ya hekima ya Yesu, aliyoyatoa katika hotuba yake maarufu inayojulikana kama, Hotuba ya Mlimani. Kitu cha kwanza anachokisema Yesu ni: âHeri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni waoâ (Mathayo 5:3).
Kwa kuwa Yesu aliongelea Ufalme wa Mbinguni, ni wengi sana wanaofikiri Ufalme huo uko mbinguni. Lakini hebu uangalie mstari wa tano wa kifungu hiki. Anasema: âHeri wenye upole, maana hao watairithi nchi.â
Ufalme wa mbinguni- maana yake ni Ufalme wa âkimbinguâ. Hebu yaangalie maneno yaliyo katika Sala ya Bwana, katika Mathayo 6:10, Yesu anapowafundisha wanafunzi wake kuomba. Anawaambia waombee Ufalme wa Mungu uje, ili mapenzi ya Mungu: âYatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguniâ. Kwa hiyo, Ufalme wa mbinguni utakuwa ni hapa katika nchi, katika dunia.
Hapa kuna baadhi ya mambo mengine Yesu aliyofundisha kwenye Hotuba ya Mlimani. Anawaambia watu kuwa:
- Wawapende adui zao.
- Wasiwahukumu wengine.
- Kumtazama mwanamke kwa kumtamani (kwa nia ya ngono), ni kubaya sawasawa na kuzini.
- Waziachie taa zao ziwake (yaani, waoneshe imani yao katika maisha yao).
- Wanapotoa kitu au msaada, wafanye kwa siri (wasijitangaze).
- Wasihofie mambo ya maisha haya; wamtumainie Mungu kuwapatia mahitaji yao.
- Wautafute kwanza Ufalme wa Mungu.
Yesu aliwaonya wafuasi pia katika Mathayo 7:13â23, kuwa:
- Wasifuate-mkumbo: Ni wachache wangeiona njia iendayo uzimani.
- Kuna kujuta: Wengi wanaojihesabia haki wenyewe watahuzunika sana, baada ya kuona hawakupata nafasi katika Ufalme wa Mungu.
2. Kufundisha kwa mifano.
Katika Mathayo 13 kumejaa mifano. Utagundua iliyo mingi inavyouhusu Ufalme. Mifano katika Luka 15 inatuonesha jinsi Mungu anavyotutaka tuikatae dunia, na kuifuata kweli yake.
3. Mafundisho kwa unabii.
Mathayo 24 ni unabii Yesu alioutoa, kwa kuwa wanafunzi wake walitaka kujua ni lini hekalu katika Yerusalemu lingebomolewa kulingana na Yesu alivyosema. Hili lilitokea katika mwaka wa 70 B.K. (Baada ya kuzaliwa Kristo). Walitaka pia wafahamu kungetokea ishara gani kuonesha kuwa Yesu anarudi na dunia imefikia mwisho wake.
Hili lilijadiliwa katika Somo la 8 (ni vizuri ulisome tena). Mafundisho ya Yesu yaliyo mengi yalikuwa juu ya Ufalme wa Mungu unaokuja.
Miujiza ya Yesu
- Miujiza ya Uponyaji: Injili zimejaa miujiza mingi ya kuponya aliyofanya Yesu. Alikuwa akiwahurumia watu na alipenda kuwasaidia. Uweza wake ulikuwa mkubwa; aliweza hata kufufua waliokufa.
- Miujiza mingine: Yesu aliyageuza maji kuwa divai, alitembea juu ya maji, alilisha maelfu ya watu n.k. Alitumia wakati wote uweza aliokuwa nao kusaidia, na kamwe haikuwa kuwavutia watu au kuringishia. Miujiza aliyoifanya ilikuwa ni ishara ya uweza aliokuwa nao na mamlaka, na ilitoa fursa kwa watu kujifunza kitu. Ilionesha wema na huruma aliyokuwa nayo.
- Yesu alivyoishi:
Mwana wa Mungu alizaliwa katika hori la kulia ngâombe. Mara nyingi hakuwa na makao, aliweza hata kusema: âMbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chakeâ (Luka 9:58).
Kabla ya kufa, Yesu aliwaosha wanafunzi wake miguu yao. Hii ni kazi iliyokuwa ikifanywa kwa kawaida na watu wa chini sana; watumwa. Ingawa alikuwa Mwana wa Muumba Mkuu wa ulimwengu wote, Yesu hakuishi maisha ya kifahari. Hili linatufundisha kuwa wanyeyekevu, na kuwatumikia wengine.
Bwana Yesu aliutumia muda wake mwingi katika maombi kwa Baba yake wa mbinguni. Kabla hajawachagua wanafunzi wake kumi na wawili, alikesha usiku mzima akiomba. Hakuomba kwenye hadhara kuonesha watu alivyokuwa akijua kuomba; aliwakosoa viongozi wa kidini kwa kufanya hivyo. Aliwakosoa kwa unafiki wao kwa kuwaambia hivyo. Kamwe hakujali kudharauliwa!
Maandalizi ya kifo
Kuna siku Yesu aliwachukua watatu kati ya wanafunzi wake, akapanda nao mlimani. Alipokuwa akisali hapo âsura ya uso wake ikageukaâ, Musa na Eliya wakaonekana wakiwa naye wakizungumzia habari za kufa kwake katika Yerusalemu. Maono haya ya Yesu akiwa katika hali ya ufukufu, yalikuwa ni picha yake ya mbele wakati wa Ufalme. Yatakuwa yalimpa nguvu kuutazamia huo Ufalme, wakati akikabiliana na mauti yake.
Alifahamu kutokana na unabii katika Agano la Kale kuwa, angekufa kifo cha kikatili. Zaburi ya 22, 69 na Isaya 53 ni sehemu ya utabiri uliohusu kifo chake. Yesu alianza sasa kuwatahadharisha wanafunzi wake kuwa angeteswa na kufa, lakini aliwaambia pia kuwa angefufuka kutoka kwa wafu (Luka 9:22).
Viongozi wa kidini walikuwa wakati wote wakitaka kumnasa, na Yesu alijua walimchukia. Walijaribu kumuua kwa kumpiga mawe mara mbili, lakini âsaa yake ilikuwa haijaja ya kufaâ.
âIkawa, siku za kufa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemuâ
Hakuwa na woga wa kufa. Alijua ilikuwa ndio njia pekee ya kuweza kuwasaidia wanadamu wadhambi. Alijua angeweza tu kuwasaidia kwa namna hiyo, kama yeye mwenyewe hakuwa na dhambi. Alipambana kila siku na dhambi, na akashinda. Ametuachia kielelezo cha ajabu. Aliwaambia wafuasi wake kuwa hawana budi kumfuata:
âMtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuateâ (Luka 9:23).
Vifungu vya kusoma: Mathayo 5, 6 na 7; Luka 9.
Kujifunza kwa moyo: Luka 1:32
âHuyo atakuwa Mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yakeâ.