Somo la 19
UFUFUO NA KUPAA KWA YESU KRISTO.
SOMO: Yohana 20

Kwa huzuni wanawake walikwenda kwenye sehemu mwili wa Yesu ulipolazwa. Walibeba marashi kwa ajili ya kuupaka mwili wake. Hawakujua namna gani wangeliondoa jiwe kubwa lililowekwa mlangoni pa kaburi, lakini walijisikia kwenda kuupaka mwili wa Bwana wao. Walipolifikia kaburi karibu walikuta:
- Jiwe limeondolewa!
- Kaburi liko tupu!
- Malaika walikuwa hapo!
Wanaambiwa: âKwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufukaâ (Luka 24:5,6).
Wanawake hao walirudi na kuwaambia wanafunzi wa Yesu kuwa Yesu amefufuka, lakini hakuna hasa aliyewaamini. Petro na Yohana wanakwenda mbio kaburini kujionea wenyewe. Ni hakika wanakuta kaburi lipo wazi na sanda aliyovikwa Yesu imejiviringa pembeni.
Mariamu Magdalena, aliyekuwa mmojawao wanawake wale, anarudi kaburini na hapo analia. Alifikiri mtu ameuiba mwili wa Yesu, ingawa malaika walikuwa wamesema amefufuka katika wafu. Yesu anakuja na kusema naye, lakini Mariamu anafikiri ni mtunza-bustani (Yohana 20:14 â 18).
Kisha Yesu anasema, âMariamu!â Anamtaja jina lake, na ghafla Mariamu anamtambua kuwa ni Yesu. Alikuwa kweli hai! Alikuwa amefufuka!
Ni kweli Yesu alifufuka kutoka wafu?
Wapo watu ambao hawaamini maelezo ya Biblia kuhusu kufufuka kwa Yesu. Zifuatazo ni baadhi ya sababu wanazotoa kwa kutokuamini kwao:
1. Wanasema: âYesu hakufa msalabani; ilionekana tu kama amekufa. Alizinduka baadaye kutokana na ubaridi wa kwenye kaburiâ.
Lakini Biblia inasema wazi kuwa, Yesu alikuwa amekufa msalabani (Yoh. 19:33). Katika Marko 15:42â45 tunasoma vile Pilato alivyotaka kuona kama Yesu alikuwa kweli amekufa. Alimtuma akida wa Kirumi kuthibitisha, na akida huyu alimletea habari kuwa ni kweli alikuwa amekufa. Akida hakuwa mtu wa kuamini, bali kuthibitisha kama alikuwa amekufa au yuko hai.
2. Wanasema: âwanafunzi waliuiba mwiliâ!
Lakini, hili haliwezi kuwa kweli. Kuhani-mkuu na wazee hawakutaka watu wajue kuwa kaburi lilikuwa tupu, na kwamba Yesu alikuwa hai tena. Waliwahonga watu waliokuwa wakililinda kaburi ili waseme wanafunzi wake wameuiba mwili. Soma Mathayo 28:11-15, na utaona uongo huu ulivyotungwa.
Hakuna kitu katika maelezo ya Biblia kinachodokeza kuwa wanafunzi wa Yesu waliuiba mwili. Wanafunzi hawakuamini kwanza kuwa Yesu alikuwa hai tena, mpaka walipomwona. Baada ya kufa kwake walikuwa wameogopa na kuhuzunika sana, wakiwa hawaamini kilichotokea. Tena hawakuwa katika hali ya kuweza kuwafanyia ujanja wakubwa wa Kiyahudi.
Baadaye, walipothibitisha kuwa Yesu amefufuka, walikuwa watu waliobadilika sana. Walihatarisha maisha yao wakihubiri kuhusu ufufuo huo, na wapo hata waliokufa kwa imani yao. Kama wangekuwa kweli wameuiba mwili na kufanya ujanja, wasingeweza kufanya mambo hayo.
3. Wanasema: âaliuacha mwili wake nyuma, na kurudi kama mzima au rohoâ.
Lakini, Biblia inatuambia waziwazi katika Marko 16:6 kuwa, wale wanawake walikwenda kaburini mwili ulipolazwa, na malaika walisema nao pale. Kama kweli Yesu aliwatokea wanafunzi wake na kuwaonesha makovu katika mikono yake, miguu na mbavu, basi ni lazima awe amerudi kutoka kwa wafu, na kaburini alipokuwa amelazwa lazima kuonekane kutupu. Kwa vyovyote, viongozi wa Kiyahudi wangependa waoneshe kwamba alikuwa bado amekufa, lakini hawakuweza kwa kuwa alikuwa hai.
Imani ilihitajika ili kukubali kuwa Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Hata Tomaso, aliyekuwa mfuasi wa Yesu, mwanzoni hakuamini. Hakuwa ameshawishika kuamini mpaka alipomwona Yesu kwa macho yake. Yesu alimwambia: âHeri wale wasioona, wakasadikiâ (Yoh. 20:29).
Wakati wa Ufalme wa Mungu ulikuwa umefika?
Wanafunzi wa Yesu, hatimaye, walipohakikisha kuwa Yesu alikuwa hai tena, walitegemea kwamba angeusimamisha Ufalme wa Mungu moja kwa moja. Kwa siku 40 Bwana alikuwa nao, akiwafundisha juu ya Ufalme huo (Matendo 1:3). Wakamuuliza:
âJe, Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?â (Matendo 1:6).
Yesu aliwajibu:
âSi kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyeweâ (Matendo 1:7)
Kulikuwa na kazi ya kufanywa kabla Ufalme huo haujasimamishwa. Wanafunzi ilibidi waende ulimwenguni, wakiihubiri Injili ya huo Ufalme. Yote haya yalitokea miaka 2,000 iliyopita, lakini kazi hiyo ya kuhubiri bado inaendelea hata sasa.
Kupaa
Wakati Yesu alipokuwa akiwazungumzia wanafunzi wake mambo haya katika Mlima wa Mizeituni, nje kidogo ya Yerusalemu, alinyakuliwa kutoka kwao kwenda mbinguni. Walipokuwa wakimtazama anavyopaa, malaika wawili waliwasemesha. Maneno ya hao malaika yanatuambia kwa uhakika kuwa Yesu atarudi. Tunaambiwa:
|
âWalipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguniâ (Matendo 1:10,11). |
Hebu ona jinsi mstari huu unavyokazia mambo. Hausemi tu kuwa, âYesu atarudiâ. Unasema, âHuyu Yesuâ¦â na kama vile kuondoa mashaka yoyote wanayoweza kuwa nayo, anasema, âAliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguniâ¦â
Walimwona Yesu akienda kimwili juu (kumbuka, hakuwa roho).
Atakuwa ni Yesu huyo huyo, na atarudi kwa namna hiyo hiyo kama alivyokwenda. Ulikuwa ni ujumbe mzuri sana wa matumaini, malaika hao waliowapa hao wanafunzi. Atakuja tena, kimwili, sio kwa kufa tena, bali kutawala kama Mfalme juu ya dunia yote. Hapo ndipo atakapourudishia upya Ufalme wa Israeli (Matendo 1:6).
Ufufuo wa Yesu, na Ufufuo wetu.
Katika 1Wakorintho 15, mtume Paulo anaongelea ufufuo wa Yesu Kristo. Anasema, kama Yesu hakufufuliwa kutoka kwa wafu, basi imani yetu ni bure, na dhambi zetu hazijasamehewa. Wale ambao wamekufa âwameishiaâ, hakuna matumaini juu yao (1 Wakor 15:17-19). Ni picha mbaya ilioje!
Lakini anasema katika 1 Wakorintho 15:20 â 23 kuwa:
|
âLakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala (waliokufa). |
Kristo amefufuliwa katika wafu. Yeye ni wa kwanza; wengine watafuata. |
|
Maana mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu (ufufuo) uliletwa na mtu. |
Mauti ililetwa na Adamu, ufufuo kutoka kwa wafu umeweza kuja tu kwa sababu ya Yesu. |
|
Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwaâ. |
Kila mtu anakufa kwa kuwa kila mtu yuko âkatika Adamuâ. Wale wote walio âkatika Kristoâ (walio Wakristo), watawekwa hai Kristo atakaporudi. duniani. |
Hili linamaanisha kuwa, kama tutakufa kabla Yesu hajarudi, sisi nasi tunaweza kufufuliwa kutoka kwa wafu. Lakini tutaweza tu kupewa nafasi katika Ufalme wa Mungu duniani kama tupo âkatika Kristoâ. Tunaweza tu kuwa Wakristo kama tukibatizwa katika mauti yake (Tazama Wagalatia 3:27-29).
Wafu wanafufuliwaje, na wanakuja na mwili gani?
Hili ni swali ambalo watu walikuwa wakijiuliza katika siku za Paulo (1 Wakorintho 15:35). Yesu alikuwa na mwili alipofufuka kutoka kwa wafu, kwa hiyo hao watakaofufuliwa kutoka kwa wafu atakaporudi, watakuwa na miili; hawatakuwa roho. Yesu anaishi sasa; amepewa mwili ambao hauwezi tena kufa.
Inakuwa wazi kama unavyoona unaposoma 1 Wakor. 15 kuwa, wale wanaopewa uzima usio na mwisho, watapewa miili iliyobadilishwa.
Miili yetu ya sasa ni ya kufa; inakufa. Tunapata maumivu, na kuna wakati tunaugua. Hao wanaopewa nafasi katika Ufalme wa Mungu, watakuwa na miili mipya, isiyokufa. Watafanywa wasiwe âwa kufaâ tena, kama tunavyosoma katika 1 Wakor 15:50 â 57. Ni tumaini zuri la ajabu kiasi gani hili Mungu ametupa!
|
Ndio maana mtume Paulo anasema:
âLakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristoâ (1 Wakor 15:57).
Ni ujumbe wa maana sana wa wokovu. Yesu aliwaambia wanafunzi wake wamhubiri kwa watu wote. Sisi nasi tutahitaji kuufikisha kwa watu wengine.
|
Muhtasari
|
Vifungu vya kusoma: Matendo 1
Soma pia habari zinazohusu ufufuo katika Mathayo 28 na Luka 24.
Mstari wa kushika : Matendo 2:24.
ââ¦ambaye Mungu alimfufua (Yesu), akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe naoâ.