SOMO LA 22
DHAMBI NA MATOKEO YAKE (SEHEMU YA 1)
SOMO: Mwanzo 2 na 3
Dunia iko katika hali mbaya: vita, njaa, magonjwa, vurugu, mauaji, mateso n.k. Lakini, Mungu aliiumba dunia ikiwa ânjemaâ. Mwanadamu ameichafua! Hulka ya mwanadamu ya uchoyo, ubinafsi, wivu na kutotii-mamlaka vimeiharibu jamii na dunia hii.
Yalianzia wapi âkwenda mramaâ?
Hapo mwanzo Mungu alimuumba mwanadamu wa kwanza, Adamu. Adamu aliumbwa kutokana na mavumbi ya nchi:
âBwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya nchi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi haiâ (Mwanzo 2:7).
Mungu aliweka bustani nzuri kwa ajili ya Adamu kuishi humo, na baada ya hapo akampatia mke aliyemwita Hawa. Adamu na Hawa hawakuonesha kama wangemtii Mungu au la mpaka walipojaribiwa. Mungu alikuwa amewapa amri moja ndogo:
âMatunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakikaâ (Mwanzo 2:16,17).
Adamu na Hawa walikuwa na uchaguzi
Wangeweza kumtii Mungu, au kutomtii na kula tunda la mti uliokatazwa. Walikuwa huru kuchagua. Mungu hakuwa ametengeneza watu walio kama mashine, wasioweza kuchagua kama watii au wasitii. Mungu alitaka wawe watu wanaoweza kuichagua njia yake kwa sababu ya kumpenda na kumheshimu.
Nyoka alikuja na kuwadanganya. Nyoka aliwaambia kuwa wasingekufa kama wangekula tunda lililokatazwa, na kwamba badala yake wangekuwa kama Mungu, wakijua mema na mabaya. Adamu na Hawa walitaka kuerevuka; kufanana zaidi na malaika. Walichagua kulila hilo tunda, na kwa kufanya hivyo walifanya dhambi kwa kutomtii Mungu.
Adhabu
Mungu alikuwa amewaambia wangekufa kama wasingemtii. Kwa hiyo Adamu na Hawa walihukumiwa kifo, na kutimuliwa watoke katika bustani ya Edeni. Ingawa waliishi maisha marefu baada ya hapo, walibadilika na kuwa viumbe vinavyokufa. Walikuwa sasa wakichoka, wakiugua, wakizeeka na hatimaye kufa, kama ilivyo sasa kwako na kwangu.
Kifo ni nini?
Kifo kilikuwa ni adhabu kwa sababu ya dhambi. Mungu alikuwa amesema:
âU mavumbini wewe, nawe mavumbini utarudiâ (Mwanzo 3:19).
Kwa hiyo mwili wa Adamu ulioza alipokufa na aliyarudia mavumbi, ambayo ndiyo yaliyokuwa yametumika kuufanya huo mwili. Mavumbi ni udongo. Mungu alimuumba Adamu kutokana na udongo wa nchi, na baada ya hapo alimpulizia pumzi ya uhai, kabla hajawa ânafsi haiâ:
VUMBI + PUMZI YA UHAI = NAFSI HAI
Adamu alipokufa, ilikuwa ni:
NAFSI HAI â PUMZI YA UHAI = NAFSI ILIYOKUFA
Kwa hiyo tunaona kuwa:
NAFSI HAI ukitoa PUMZI YA UHAI ni VUMBI (udongo)
Hakuna sehemu ya Adamu iliyokwenda kuishi mbinguni alipokuwa amekufa; kwa hakika hakuna! Mauti yake yalikuwa ni adhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi, na kifo maana yake ilikuwa mwisho wa uhai wote; mwisho wa kuishi. Kifo cha Adamu hakikuwa na utofauti wowote na chetu. Sisi wote tunafanya dhambi, kwa hiyo sote tunakufa:
âKwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambiâ (Warumi 5:12).
Hili halina maana kwamba, watu wote ni wauaji au wazinzi au waongo. Mawazo yasiyo ya wema, yenye ubaya: kiburi, choyo, hasira n.k (ambayo ni udhaifu wetu wote wa kila siku), yote ni dhambi machoni pa Mungu. Hakuna kati yetu atakayekwenda mbinguni tukifa.
Hakuna chochote kinachoitwa ârohoâ kisichokufa
Hakuna mahali ambapo Biblia inataja uwepo wa ârohoâ isiyokufa. Hakuna kitu kinachoendelea kuishi mtu anapokuwa amekufa. Hakuna cheche ya uhai ya kimbingu isiyozimika katika mwanadamu anapokufa.
âRohoâ ni uhai; kiumbe hai, au mtu, au nafsi
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya vifungu vilivyopo katika Biblia inayoonesha sehemu neno hili ârohoâ linapotumika. Hebu uvitazame mwenyewe uone kama utakubaliana na maoni yaliyotolewa:
|
REJEA |
MAONI |
|
Mwanzo 46:15
Mwanzo 46:26
Walawi 5:2
Walawi 17:12
Yoshua 10:28, 30,32, 35, 37
Yoshua 11:11
Matendo 27:37 |
Wana wa Yakobo (wanaoishi) wanaitwa ânafsiâ (kwa Kingereza-souls); lenye maana ya ârohoâ. âNafsi zoteâ (all souls) hapa kwa hakika inamaanisha âwatu woteâ. âKama mtu akigusa kitu kilicho najisi â¦..â -neno ârohoâ (soul) hapa ndilo lililotafsiriwa âmtuâ. âKama mtu akifanya dhambi, na â¦..â (ms. 17): Neno ârohoâ (soul) hapa ndilo lililotafsiriwa âmtuâ. Maana ya roho ni mtu. Roho (souls) zinaweza kufanya dhambi, kwa maneno mengine watu wanaweza kufanya dhambi. ââ¦â¦.Hapana mtu mingoni mwenu aliye na ruhusa kula damuâ¦..â (ms. 12). Neno ârohoâ (soul) hapa ndilo lililotafsiriwa âmtuâ. Hapana mtu (ârohoâ yaani mtu) kati yao aliyekuwa akiruhusiwa kula damu. Neno wote katika mistari hiyo limekaa badala ya âroho wote piaâ (All the souls). âRoho woteâ (yaani, watu wote) waliangamizwa kabisa. (âRohoâ wanaweza kuangamizwa, kuuwawa!) Neno âwoteâ tena ni neno ârohoâ. âWao wakawapiga wote pia waliokuwamoâ¦.â (And they smote all the souls that wereâ¦..) Waliwaua roho wote (watu wote); hakuna aliyebaki akipumua. âNa sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu 276â Neno âwatuâ hapa ni neno ârohoâ. Roho 276 ni watu 276. (âAnd we were in all in the ship 276 soulsâ) Roho hapa ni wazi ni hao abiria. |
Kuna mifano mingi zaidi tungeweza kutoa kuonesha kuwa neno ârohoâ maana yake ni mtu (au kiumbe hai). Ni neno pia linalotumika kuwahusu wanyama katika lugha ya asili (lugha ya Kiebrania). Kwenye Mwanzo 1:21, 24, 2:19, 3:10 ni neno lililotafsiriwa âkiumbe haiâ kwenye Kiswahili. Kwenye Kingereza ni âliving creatureâ. Yote haya yanathibitisha kile kinachosemwa katika Mhubiri:
âKwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama, jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu, naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Wote huenda mahali pamoja, wote hutoka katika mavumbi, na hata mavumbini hurudi tenaâ (Mhu. 3:19, 20).
Hakuna utofauti wowote kati ya mtu na mnyama katika mauti. Mnyama hana sehemu inayokwenda mbinguni anapokufa, na mwanadamu ni hivyo hivyo. Wote wanakuwa ni miili isiyokuwa na uhai wanapoacha kupumua; ni udongo:
|
âRohoâ maana yake ni uhai, mtu, kiumbe kilicho hai |
Vifungu hivi vinatuonesha kinachotokea tunapokufa:
|
Zaburi 146:4
Mhubiri 9:5 Zaburi 6:5
Zaburi 39:13 Zaburi 115:17 |
âPumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake yapoteaâ âWafu hawajui neno loloteâ¦â¦â¦.â âMautini hapana kumbukumbu lako, katika kuzimu (kaburi) ni nani atakayekushukuru?â âUniachilie nikunjuke uso, kabla sijaondoka nisiwepo tenaâ. âSio wafu wamsifuo BWANA, wala wowote washukao kwenye kimyaâ (kaburini). |
Vifungu hivi vyote vinaonesha kuwa, watu waliokufa hawana utambuzi wowote; hawawezi kufikiri.
Mfalme Hezekia alipoambiwa kuwa alikuwa afe, alisononeka sana. Alitaka aendelee kuishi kwa kuwa alijua kwenye mauti hakukuwa na kitu. Alimwomba Mungu aishi, ili aweze kuendelea kumsifu:
âKwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yakoâ (Isaya 38:18).
Badala yake, anamwambia: âAliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leoâ (ms.19).
Je, mfalme Daudi? Tunaambiwa wazi mfalme Daudi hakwenda mbinguni, ingawa anaitwa mtu aliyekuwa na moyo uliompendeza sana Mungu (Matendo 2:34, 13:22)
Watu wote wapo kwenye hukumu ya kifo kwa sababu ya dhambi. Hawaendelei kuishi kwa namna yoyote nyingine baada ya kufa.
Kama hatulielewi hili vizuri, hatuwezi kamwe kutambua jinsi ambavyo Bwana Yesu alivyoteseka na kufa ili kutuweka huru na matokeo ya dhambi.
Kama tungekuwa na âroho zisizokufaâ, kusingekuwa na haja ya Yesu kutufia. Biblia inatuambia, hakuna tumaini la uzima kama sio katika Kristo.
|
Muhtasari
|
Kifungu cha kusoma: Mhubiri 9
Mstari wa kujifunza: Zaburi 146:4
âPumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake yapoteaâ.