Somo la 28
MALAIKA
Somo: Waebrania 1
Malaika ni wajumbe wa Mungu. Wanaweza kuuingia âuwepoâ Mtakatifu wa Mungu, kwa hiyo ni sharti wawe viumbe wasio na dhambi. Hatuambiwi malaika wako wangapi, ila tunajua hesabu yao ni kubwa kwa kusoma Waebrania 12:22, na Mathayo 26:53.
Malaika wanafanya nini?
- Wanatoa ujumbe
- Wanaongoza
- Wanafanya ulinzi na kuokoa
- Wanaangamiza
Tutaviangalia vipengere hivi kimoja-kimoja:
- MIFANO YA MALAIKA WAKITOA UJUMBE
|
MAREJEO |
MAELEZO |
|
Mwanzo 1
Mwanzo 19:1-5
Mwanzo 22:11, 15
Kutoka 3:2 |
Ibrahimu aliambiwa kuwa, yeye na Sara wangepata mtoto wa kiume. Malaika hao wanaelezewa kuwa ni âwatuâ; hawakuwa tofauti ni watu wa kawaida. Mara nyingine malaika wanaweza kuonekana tofauti sana, hasa wanapokuwa wanaonesha utukufu wa Mungu. Hapa wawili kati ya malaika hao wanakwenda kumtembelea Lutu na kumtahadharisha kuwa, Mungu alikuwa na mpango wa kuiangamiza Sodoma na watu wa Sodoma. Malaika hao walikuwa ni âwatuâ. Malaika aliita kutoka mbinguni kumzuia Ibrahimu asimchinje mwanawe, Isaka. Baada ya hapo malaika walimbariki Ibrahimu kwa imani na utii wake. Musa alikuwa ameambiwa kuwa, Mungu angemtuma Misri kuwaokoa wana wa Israeli kutoka kwenye utumwa wao. Malaika aliyempa huo ujumbe alikuwa katika moto wa kichaka kinachoungua. |
|
Waamuzi 6:11-24
Luka 1:11 â 19
Luka 1:26
Matendo 8:26 |
Malaika anamwambia Gideoni kuwa, Mungu angemsaidia kuwapiga maadui wa Israeli. Huyo malaika alipotea kwenye moto Gideoni aliowasha. Zakaria anaambiwa na malaika kuwa, yeye na Elisabeti wangepata mtoto wa kiume, ambaye ni Yohana Mbatizaji. Malaika Gabrieli anamwambia Mariamu kuwa, angekuwa mama wa Yesu. Filipo anaagizwa kukutana na mtu wa Kushi. Aliweza baada ya hapo kumfundisha juu ya Yesu na kumbatiza. (Kwenye msitari wa 29 malaika anaitwa ârohoâ) |
2. MIFANO YA MALAIKA WAKIONGOZA WATU
- Ibrahimu alimtaka mtumishi wake amtafutie mke mwanawe, Isaka, lakini alikuwa awe mwanamke wa kumfaa! Ibrahimu anamwambia mfanyakazi wake huyo kuwa, malaika angemsaidia (Mwanzo 24:7). Na kweli alimwongoza.
- Musa alipowaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, nguzo ya wingu ilikwenda pamoja nao. Iliwalinda na kuwaonesha njia. Tunaambiwa kuwa malaika wa Mungu alikuwa pamoja nao katika hiyo nguzo ya wingu (Kutoka 14:19 na Kutoka 23:20, 21).
Ni muhimu kutambua hapa kuwa, ingawa malaika wa Mungu alikuwa na wana wa Israeli wakati wote walipokuwa nyikani, hata hivyo walimwasi Mungu. Malaika hakuwazuia wasiasi.
3. MIFANO YA MALAIKA WAKIWALINDA NA KUWAOKOA WATU WA MUNGU
- Marafiki watatu wa Danieli waliokolewa kwenye tanuru la moto na malaika (Dan. 3:28).
- Danieli mwenyewe aliokolewa kwenye handaki lenye simba. Malaika âaliyafumba makanwa ya simbaâ (Dan. 6:22).
- Malaika alifungua milango ya gereza kwa ajili ya mitume kutoka (Matendo 5:19), na katika Matendo 12 alimfungulia Petro (ms. 7).
4. MIFANO YA MALAIKA WAKIANGAMIZA
- Mji wa Yerusalemu ulipozungukwa na majeshi ya Ashuru wakati wa mfalme Hezekia, Hezekia alimlilia Mungu apate msaada. Malaika aliwaangamiza Waashuru wote waliokuwa wakimdharau Mungu wa Israeli (2 Wafalme 19:35).
- Mfalme Herode, wakati za Agano Jipya, aliuwawa na malaika sababu ya kiburi chake (Matendo 12:23).
Malaika hawatendi dhambi
Katika nyakati za Kutoka, malaika walisababisha uharibifu ulioletwa na tauni. Akielezea hili, mwandika-Zaburi anasema kuwa, Mungu:
âAkawapelekea ukali wa hasira yake (Wamisri), ghadhabu, na uchungu, na taabu, kundi la malaika waletao mabayaâ (Zab. 78:49).
Malaika wenyewe hawakuwa waovu, lakini walitumwa na Mungu kuwafanyia mambo tunaoyaona kuwa mabaya (lakini yalikuwa kwa vyovyote ni ya lazima). Hakuna malaika wanaofanya dhambi. Lakini vipi juu ya 2 Petro 2:4 ambapo tunaambiwa: âIkiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosaâ¦..â
Neno hapa lililotafsiriwa âmalaikaâ linaweza pia kutafsiriwa âwajumbeâ; linaweza kumaanisha wajumbe wa kimbingu (malaika) au wajumbe wa kidunia (watu waliobeba ujumbe). Neno la kiasili lililotumiwa katika Biblia (âaggelosâ katika Kiyunani), halitambulishi kama wajumbe hao walikuwa wa âkimbinguâ au wa âkiduniaâ. Watu waliotafsiri mara nyingine walikosea.
Tunafikiri kuwa, 2 Petro 2:4 inaweza kuwa inaongelea kilichoandikwa katika Hesabu 16.

Malaika wanaonekanaje?
Kwa kawaida, malaika huwa wanafanya kazi zao bila ya kuonekana na watu. Wakati Elisha na mtumishi wake, Gehazi, walipokuwa wakiwindwa na mfalme wa Shamu (Syria), Elisha alijua Mungu angemsaidia lakini mtumishi wake aliogopa sana. Elisha alimwomba Mungu amfumbue mtumishi wake macho. Gehazi alipofumbuliwa ndipo alipoona kuwa:
ââ¦. kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zoteâ (2 Wafalme 6:17).
Jeshi la malaika wa Mungu lilikuwa hapo kuwalinda!
Tumeshaona kuwa malaika waliomtokea Ibrahimu na Lutu walifanana na watu, na kwa hiyo, kwa vyovyote isingewezekana wakawa na mabawa. Lakini tumeshaona pia kwamba, malaika waliweza kuwa katika moto na katika wingu, kama ilivyokuwa katika kichaka kilichokuwa kikiungua, na katika nguzo ya wingu kule nyikani.
Kwa hiyo malaika hawana muonekano wa namna moja, na wanaweza pia kutoweka tu, kama ilivyokuwa kwa yule aliyemtembelea Gideoni.
Yesu na malaika
Malaika waliwaambia Yusufu, Mariamu na wachungaji wa makondeni kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Waliendelea kumwongoza Yusufu kwa kumwambia kumchukua kitoto Yesu kwenda chini Misri, na walimwambia pia lini warudi baada ya hali kuwa shwari.
Zaburi ya 91:11 ilitabiria malaika kumsaidia Yesu. Katika Mathayo 4:11 tunasoma kuwa, baada ya majaribu ya Yesu ya nyikani, walikuja malaika âwakamtumikiaâ. Kutumikia ni âkuhudumuâ, kwa hiyo inaelekea malaika walimhudumia Yesu kwa kumletea chakula, baada ya kufunga kwake kwa muda mrefu.
Katika bustani ya Gethsemane, Yesu alipojua kusulubiwa kwake kumefika, aliomba aweze kufanya lile Mungu alitakalo. Malaika alimtokea, âAkamtia nguvuâ (Luka 22:43). Angeweza kuukwepa msalaba; kukwepa kukamatwa, na kumwomba Mungu atume majeshi kumi na mawili ya malaika kumwokoa. Lakini alijua ilimpasa afe kwa ajili yetu. Ilikuwa ndio njia ya pekee ya sisi kuweza kusaidiwa kuondokana na tatizo letu sugu la dhambi.
Tungeweza kutegemea Mungu amfanye Mwanawe awe kama malaika, lakini haikuwa hivyo; alikuwa mtu. Ni katika kuwa katika hali yetu wanadamu, ndivyo ambavyo angeweza kujaribiwa; kuvutwa na dhambi. Aliteseka na hatimaye kufa. Malaika hawawezi kufa (Luka 20:36).
Katika Waebrania 2:9 tunaambiwa kuwa, Yesu, alifanywa mdogo punde kuliko malaika, âkwa sababu ya maumivu ya mautiâ. Tunaambiwa tena: âHatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimuâ (ms. 16).
Alipofufuka kutoka kwa wafu, malaika walikuwapo. Hebu fikiri walivyofurahi! Akiwa ameishinda dhambi na mauti, Yesu alipewa hadhi ya juu zaidi ya malaika. Hana tena hulka ya kiasili ya binadamu wengine:
â(Yesu) akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; amefanyika bora kupita malaikaâ¦.â (Waebr. 1:3,4).
Heshima ya kukaa katika mkono wa kuume wa Mungu ni ya Bwana Yesu Kristo peke yake. Hakuna malaika aliyewahi kupewa fursa ya namna hiyo (Waebr. 1:13). Katika Sura hiyo malaika wanaelezewa kuwa ni: âPepo na watumishi wake kwa miali ya motoâ (ms. 7). Anasema malaika: âWote si roho watumikao wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?â (ms. 14). (Neno âwoteâ hapo ni la muhimu. Hakuna malaika anayeweza kumwasi Mungu).
Malaika wanafanya kazi kwa ajili ya wale watakaourithi wokovu. Tuliona katika kisa cha towashi wa Kikushi (Matendo 8:27-39) jinsi malaika alivyomuweka towashi huyo katika mazingira yaliyomwezesha kujifunza ukweli wa Injili, na kubatizwa. Tuliona mitume wakiwa wanasaidiwa watoke gerezani. Lakini malaika hawamsaidii kila mtu! Wanatumika kwa ajili ya wale tu watakaourithi wokovu (Waebr. 1:14).
Kazi ya malaika leo
Ingawa hatuwaoni, malaika wanaweza kutusaidia hata leo, lakini ni kama tunaishi kwa kujaribu kumpendeza Mungu. Zaburi ya 34:7 inasema kuwa, malaika wa Mungu wapo kuwazungukia âwamchao na kuwaokoaâ. Wanaweza kutusaidia, lakini haina maana kwamba waumini hawatapatwa na wakati mgumu.
Shida katika maisha zipo ili kutufundisha mambo fulani-fulani, na kutuweka karibu na Mungu. Wala malaika hawatawazuia waumini wasifanye dhambi. Kumbuka, malaika hakuwazuia wana wa Israeli kuasi wakiwa nyikani!
Kazi ya baadaye ya malaika
Bwana Yesu Kristo hivi karibuni atarudi hapa duniani, lakini hakuna anayejua ni lini. Hata malaika wa Mungu mbinguni hawajui (Marko 13:32). Atakapokuwa anarudi, malaika wataongozana naye. Katika 2 Wathesalonike 1:7,8 tunaambiwa, Bwana Yesu atafunuliwa kutoka mbinguni:
âPamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto, huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesuâ.
Malaika watahusika katika kuwakusanya watu kwa hukumu. Katika wakati huo, waumini wa kweli watafanywa wawe kama malaika. Hawataoa au kuolewa tena, au kuweza kufanya dhambi, au kufa (Mathayo 22:30, Luka 20:36). Ndio maana kunakuwa na shangwe mbinguni (kati ya malaika), kila mdhambi mmoja anapotubu!
|
Muhtasari
|
Vifungu vya kusoma: Tafadhali zipitie tena rejea zilizoko kwenye somo hili. Zisome zote na utapata ufahamu juu ya malaika na kazi wanazofanya kwa niaba ya Mungu.
Msitari wa kushika: Waebrania 1:14
âJe! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?â