Somo la 41
FAMILIA
Somo: 1 Petro 3
Hili somo ni kwa ajili ya wafuasi wa Yesu ambao bado wanaishi katika familia na wazazi wao, au wameoa au kuolewa na sasa wana familia zao wenyewe.
Somo hili linalenga katika kuangalia kwa umakini âfamiliaâ, kwa kutaka kuona mambo yale ambayo ni mazuri juu yake. Tutaangalia pia kuona baadhi ya hasara za kuishi kimakundi. Ni muhimu kutambua kuwa, ingawa jamii zetu zinafofautiana sana tunapoangalia zilivyo sehemu moja ya dunia na sehemu zingine, watu wote walitokana na chanzo kimoja. Wote wana Muumba mmoja ambaye ni Mungu, na ni Mungu aliyeifanya iwepo familia ya kwanza.
Katika masomo ya nyuma tumeiangalia familia ya kwanza ya Adamu na Hawa, na vijana wao Kaini na Habili, na pengine kuona ya kwamba, Adamu hakuwa baba mzuri sana. Hakuwafundisha wanawe tofauti ya mema na mabaya. Hakuona ubaya uliokuwa katika wivu wa Kaini kwa ndugu yake Habili, na ni Mungu, sio Adamu, aliyegundua uuaji uliotokea na kumwadhibu Kaini.
Kama ukimfikiria zaidi Adamu utakumbuka ya kuwa, hakuwa mzuri sana katika kuukataa uovu yeye mwenyewe. Alikula tunda lililokatazwa bila kulihoji. Hili linatuleta katika hoja yetu ya kwanza ya muhimu; wajibu na umuhimu wa baba na mama katika kuiongoza familia. Katika siku za awali katika Biblia, jukumu hilo lilikuwa ni la mwanamume, akiwa ndiye msimamizi au kiongozi.
Mfano mzuri sana ni wa Ibrahimu na kujitoa kwa familia yake na watumishi wake wote, kunaweza kuonekana katika kitabu cha Mwanzo na Waraka wa kwanza wa Petro, Sura ya 3, mstari wa 1-6. Nasaha ya mtume Petro haikuwa ni kwa wanawake tu bali pia kwa wanaume. Anasema, mume na mke ni: âwarithi pamoja na neema ya uzimaâ (1 Petro 3:1-7).
Kitu kimoja cha maana sana katika familia ile ya kwanza ya kibinadamu ilikuwa ni upendo, na tunaona ukizungumziwa katika familia hizi za awali za kwenye Biblia. Katika Mwanzo 22:2 Ibrahimu anaagizwa kitu juu ya Isaka akiambiwa, âmwana wako wa pekee, umpendayeâ, na tunaambiwa juu ya Isaka âkumpendaâ Rebeka katika Mwanzo 24:67.
Kwa hiyo, familia ni kiungo kilichowekwa na Mungu, na kama wazazi wakiwalea watoto wao kumjua Mungu na kuliheshimu Neno lake katika Biblia, watakuwa wameweka msingi mzuri wa maisha ya watoto wao kukulia.
Upendo kati ya watu wa familia moja ni wa muhimu sana, kama familia hiyo inataka kuwa ya furaha. Hekima na mamlaka ya wazazi ni vitu vya muhimu pia kujengwa. Paulo alimwandikia Timotheo juu ya kuvunjika kwa familia ambako kungetokea baadaye (2 Tim. 3:2). Tazama katika Waraka wake wa pili kwa Timotheo, kifungu cha 3, mstari wa 2.
Katika Waraka wa kwanza Paulo anatoa ushauri mzuri kwa wanaume na wanawake walio wafuasi wa Yesu. Kuna mambo ya kina katika maisha ya kila siku muhimu kiibada, ambayo sio tu yale yanayosemwa na mtu katika kuomba, badala yake ni mtindo wa maisha, ambao kwa wenyewe ni namna ya kweli na ya dhati ya kuabudu.
Sura ya tatu ina orodha ya hulka ambazo Timotheo alipaswa aziangalie katika kuchagua wanaume, ambao wangekuwa wazee na viongozi wa eklesia zinazoanzishwa. Kwa ajili ya somo hili hebu angalia sasa mstari wa 4 na wa 5.
Ushauri huu wa Kibiblia unaohusu ânidhamu ndani ya familiaâ unaweza ukawa uliandikwa kwa Timotheo, lakini ni muongozo wa wazi kwa maisha ya kifamilia ya wafuasi wa nyakati zote. Mfumo huu wa kitabia umekataliwa karibu wote na jamii za kisasa katika nchi nyingi. Kuporomoka kwa maadili na kwa uimara wa familia, kumekuwa kukiongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni na kunatisha.
Serikali nyingi zimetambua makosa katika sheria ambazo wameziweka, zikiruhusu talaka kutoka kirahisi na kuchochea na kukubalia wazo la uwepo wa familia za mzazi mmoja. Tatizo kwa sasa ni kwamba, kwa sasa ni vigumu na pengine haiwezekani kuuvunja mwelekeo huu wa hatari.
Utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana wadogo na kuongezeka kunakotisha kwa ugonjwa wa UKIMWI, ni mifano michache tu ya majanga ambayo yatokana na ukosefu wa nidhamu ya kibinafsi. Nidhamu hiyo inaanzia katika familia, na watoto wadogo wanatakiwa wajifunze kwa kuiona kwa wazazi wao.
Ni vizuri sasa kuelezea kwa umakini kanuni ya kiimani ya ânidhamu katika familiaâ, kwa kuwa hii ni rahisi sana kutumiwa vibaya. Fungua sasa Waebrania 12 na utazame mstari wa I mpaka wa II. Mababa wanaokuwa na watoto jeuri au wenye tabia mbaya, wanaweza kuwa wakali mno au wapole mno. Busara na haki vinaweza kutumika, na mwongozo wa msingi upo katika amri za Yesu kwa ajili ya wafuasi wake.
Baadhi ya nchi za kimagharibi kwa sasa zina sheria zinazokataza wazazi wasiwaadhibu watoto wao. Katika kifungu hiki uhusiano kati ya Mungu na Mwanawe, Bwana Yesu Kristo, umetolewa kama kielelezo. Mungu alikuwa tayari kwamba Mwanawe wa pekee apate mateso kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.
Yesu akiwa ni Mwanawe aliyempenda na mwenye kuwajibika, alikuwa tayari kuyapokea mateso hayo. Tunaweza kamwe katika familia zetu tusiweze kufikia kiwango hicho cha udhibiti na utii wa kujitoa, lakini ni vizuri tuyatafakari maneno ya Paulo kwa undani.
Angalia mstari wa 7 kwanza na ulinganishe na mstari wa 9 na 10. Biblia inachofundisha hapa ni kwamba, wazazi wadhibiti nidhamu ya watoto wao; ikibidi wawaadhibu. Hawatakiwi wafanye hivyo kunguza au kuondoa hasira zao, bali kwa upendo kwa ajili ya kumfundisha mtoto kwa faida yake.
Tutaangalia mada ya mateso katika somo la 47, lakini kwa sasa ushauri wa mstari wa 11 ni kuwa, mtoto atanufaika kwa kuwa sehemu ya familia yenye sheria. Zaidi ya hapo, sheria au kanuni hizo ni sharti ziwe zimetoka kwenye Biblia.
Hii pengine ni sehemu ya somo yenye uchungu, lakini ni ya muhimu. Tunaweza sasa kuyaangalia maisha ya familia kuona ni wapi mwongozo na uzito ulipo. Kusoma Biblia kunapaswa kuwe mahali pa kuanzia. Kama hatujui mafundisho na miongozo ya Mungu na ile ya Yesu na mitume wake, tutawezaje kuileta katika maisha yetu? Kuna uheri na usalama pia katika kuwa karibu na Neno la Mungu, na usomaji wa Biblia wa pamoja unaweza kuwa kitu cha kutuelimisha na kutuburudisha.
Ni muhimu watoto watiwe moyo kujiunga na hili, na wasaidiwe wanapoyakuta maneno magumu. Wazazi wanaweza kuufanya muda huu wa kusoma Biblia pamoja kuwa wa kusisimua sana, kama mambo yale wanayoyakuta yanaelezewa, na muhimu zaidi yanajadiliwa ili wote wapate fursa ya kuchangia mawazo yao.
Nyaraka za Paulo hazikuandikwa kwa kundi dogo la waumini tu, bali zilikusudiwa kwa eklesia zingine pia (unaweza kuliona hili katika Wakolosai 4:16). Jukumu kubwa la kuleta Agano la Kale la Wayahudi na Injili, pamoja na maandishi ya mitume na kitabu cha Ufunuo lilifanywa ili wafuasi, wa nyakati zote waweze pia kunufaika kutoka katika Neno la Mungu. Mtume Petro, akiandika katika wakati ambao wafuasi wa Yesu walikuwa na Agano la Kale tu kama kiongozi chao, alitoa maoni yenye nguvu. Unaweza kuyasoma hayo katika 1 Petro 1:19-21.
Anasema Neno lenye pumzi ya Mungu linaaminika kwa kuwa, Mungu alikusudia tulipate. Limeandikwa na wanadamu wa kawaida, wasiodumu, lakini waliandika kile Mungu alichowakusudia waandike. Paulo anasema kitu kama hicho katika 2 Timotheo 3:14-17. Anatuambia hata na sababu ya kulitumia hili Neno la Mungu; ni kwa âkuonya na kuongozaâ, na manufaa yake yapo kwenye mstari wa 17. Utatambua hapa ya kuwa, Timotheo alikuwa akisoma na kujifunza Biblia yake tangu utotoni.
Pamoja na ushauri na muongozo huu mzuri, wazazi ni wanadamu na wanakosea. Mara nyingine wanafanya makosa makubwa yasiyoweza kusahaulika. Kwa mfano: wanajiachia mara nyingine hasira na kuchukia kujionesha, na kutumika dhidi ya watoto wao.
Katika hili maneno ya busara ya Paulo kwa Waefeso yanapaswa kutufundisha (Waef. 2:1-4). Maneno makali na vitendo vya kikatili vimefanya familia nyingi zisambaratike. Sheria ya upendo kwa jirani yetu ni lazima ianzie nyumbani kwetu wenyewe, kwa kuwa na upendo kati ya wanandugu, na inapaswa iendelee wakati wa hali mbaya na nzuri, katika kujielekeza kuushinda ubaya.
Endapo wafuasi wanaona shida kutumia upendo na kusamehe nyumbani katika ya familia zao, watawezaje kwa furaha kufanya kazi pamoja katika familia pana zaidi, ya undugu wa Kikristadelfia duniani? Kanuni zile zile za nidhamu kibinafsi na moyo wa Yesu katika Eklesia, ni vitu vinavyotakiwa kuanzia nyumbani kwenye mioyo yetu wote.