Correspondance Course - Lesson 53

Swahili

SOMO LA 53

KUJAMIIANA, Zawadi kutoka kwa Mungu

SOMO: Mwanzo 19

Kama unaamini kwamba Mungu alimuumba mwanadamu awe kiumbe aliye bora zaidi kati ya wanyama wengine, utaamini pia kwamba ndiye aliyeubuni mwonekano wa miili yetu ya ajabu; ndiye aliyetupa miguu na mikono na viungio vyake na misuli. Alitupa akili yetu na uwezo wa kufikiri na kupanga, kutii au kutotii.

Katika Mwanzo 2:7 tunaambiwa jinsi alivyomuumba mwanamume kutokana na mavumbi ya udongo, na katika mstari wa 21 na 22 alivyomuumba mwanamke. Hakuna taarifa popote kwamba Mungu aliwabadilisha kimwili Adamu na Hawa baadaye, alipowafukuza watoke katika bustani ya Edeni kwa sababu ya kutomtii.

Kwa hiyo katika wakati wa kuumbwa, Adamu na Hawa ni lazima waliwekewa uwezo wa kupata watoto. Walikuwa wamewekewa via vinavyotofautiana vya uzazi kwa ajili ya kujamiiana, kufanya suala la watoto liwezekane. Sasa ni nini kingetokea, kama Adamu na mke wake wangekuwa wamejizuia wasiangukie katika kula tunda la mti uliokatazwa?

Kwa hakika hatujui, lakini kuna mambo mawili ya kusisimua ya kutafakari hapa. La kwanza lipo katika Mwanzo 1:28 ambapo amri ya “Zaeni, mkaongezeke”, inakuja kabla laana ya ‘kufa’ haijaja juu yao. La pili lipo katika Mwanzo 2:25 ambapo tunasoma kuwa: “Walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona  haya”. Walikuwa wameumbwa na via vya uzazi, walikusudiwa wazae watoto, lakini hawakuoneana haya kwa kuwa uchi.

Lakini pamoja na kupewa uwezo huo, hawakuutumia mpaka baada ya kufukuzwa kutoka katika bustani hiyo. Ni mpaka tunapofika katika Mwanzo 4:1 ndipo tunaposoma juu ya wao kufanya ngono, na Hawa kupata mimba ya mwanawe wa kwanza.

Ningependa nirudi nyuma kidogo na kuangalia kwa undani zaidi juu ya kitendo cha uasi kilichoubadili mwelekeo na historia ya mwanadamu, na kuleta shida na maumivu, na mchakato wa kuzeeka unaoishia kwenye mauti.

Kumbuka kuwa mti waliokatazwa kuugusa ulikuwa ni, “mti wa ujuzi wa mema na mabaya”. Ulikuwa na matunda yaliyoonekana kuvutia kuliwa (Mwanzo 3:6).

Sasa, katika nchi karibu zote duniani, kuna miti yenye matunda ambayo watu wanaweza kuyala bila wasiwasi wowote, lakini ipo pia miti michache ambayo inazaa matunda yenye sumu; matunda yanayoweza kuwauwa wale wanaoyachuma na kuyala.

Tunda alilochuma Hawa na kuliwa na wote wawili, mume na mke, lilionekana zuri kwa kuliwa, lakini lilikuwa hasa na sumu. Lilikuwa na uwezo wa kuibadili miili ya wanadamu na pia akili zao (Mwanzo 3:7). Adamu na Hawa waliona kila kitu kimebadilika; walipatwa na hisia tofauti za kuwasitua, na ghafla kuona mambo mengine mengi kwa wakati huo huo.

Hawakuwa na hofu kabla ya kulionja tunda, bali walianza kuogopa baada ya hapo (ms. 10). Utambuzi wao wa jinsi jambo walilofanya lilivyokuwa la hatari na la kutisha kwao, uliwavunja-vunja kimwili na kiakili. Hawakuwa na la kufanya isipokuwa kujificha, kwa kuwa walijitambua wako uchi. Tunaambiwa walitengeneza vizibao vya majani (Mwanzo 3:7). Walifanya hilo wenyewe kwa kuwa walijisikia iliwapasa wafunike sehemu zao za siri.

Kilichotokea katika miili yao wakati tunda la ‘mti wa ujuzi wa mema na mabaya’ liliposagwa miilini mwao, kiliwabadilisha kimaumbile kwenye mfumo wao wa chembechembe za kiurithi (‘kijenetiki’). Matokeo yake yakawa kwamba, laana iliyowapata ilikuja pia kwa watoto wao, na juu ya vizazi vyote vya wanadamu. Watu wote wakawa viumbe ambavyo vinakua na kuzeeka, na hatimaye kufa.

Na sisi tunao pia ujuzi huo wa mema na mabaya na, ingawa mema yanaweza kutuongoza kwenye matendo ya maana na mazuri sana, ubaya upo pamoja nasi wakati wote. Mitume wa Yesu walilazimika kulionya kanisa jipya la Yesu (waumini) kujichunga sana na huo. Maneno ya mtume Paulo kwa Warumi katika Warumi 3:9-12, ni maneno anayonukulu Zaburi 14:1-3. Paulo anachosema hapa hasa ni kwamba, katika wakati wake huo, hali ilikuwa ni ile ile kama ilivyokuwa katika enzi za Daudi, mfalme wa Israeli, aliyeiandika hiyo Zaburi miaka 1000 nyuma. Ni hali inayoendelea.

Tazama pamoja nami sasa katika waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wakorintho kifungu cha 6 mstari wa 9 mpaka wa 11. Paulo analosema hapa ni habari njema kwa wote wanaojisikia kuwa, uovu katika maisha yao ya awali unamaanisha kuwa mtu hawezi kamwe kusamehewa; hawezi kubatizwa. Hivi kwa hakika sivyo. Toba ya kweli na ubatizo vinayaosha yote ya kale, na kuwapa waumini wote mwanzo mpya wa kuwa wafuasi wa Yesu.

Yesu ametupa msaada mkubwa katika mada hii ya kujamiiana. Alieleza kuwa, Mungu alikusudia mume na mke waungane kwa maisha yote. Alieleza kwamba katika Sheria Mungu aliyowapa watu wake Israeli kupitia kwa Musa, uzinzi ulipigiwa marufuku; uzinzi ni kumchukua mume au mke wa mwingine (Marko 10:2-12).

Uzinzi katika sheria ya asili, ulikuwa hukumu yake ni kifo, kwa hiyo kwa hao wafuasi wa awali, uaminifu katika ndoa ulikuwa ni kitu kilichoheshimiwa sana. Ili ndoa ivunjike, ilikuwa ni lazima kuwe na sababu nzito sana, na ikitokea ikavunjika, mume na mke hawakuwa huru kuondoka tu na kuoa au kuolewa tena. Hakuna hasa mahali katika Agano la Kale ambapo mume alikuwa na ruhusa ya wake zaidi ya mmoja, kwa sababu tu ya kuwapenda na kuwa na uwezo wa kuwatunza. Matala ni namna isiyo ya kinidhamu ya matumizi ya fursa ya kujamiiana Mungu aliyoikataza.

Hebu turudi nyuma kwenye mafundisho ya Yesu katika Mathayo 5:27,28. Hapa aliirudia kwa uzingativu amri ya kale kuhusu uzinzi, lakini kwa ajili ya wafuasi wake aliielezea kwa umakini zaidi. Alionesha kuwa uovu wote unaanzia kwenye fikra. La muhimu kukumbuka juu ya hili ni kwamba, Mungu anayatambua yote tunayofikiri, kama ambavyo Yesu alivyowashangaza Mafarisayo waliokuwa wakimkosoa wakati wote, kwa kuyajibu mawazo yao zaidi kuliko maswali waliyouliza.

Kama ukiangalia maneno yake katika Mathayo 5:29,30 utaona yakisemea kitu cha kufanywa, ambacho tungeona vigumu kukielewa: “Jicho lako ling’oe/mkono wako ukate”. Hata hivyo anachoongelea hasa ni kuyakatilia mbali nasi mawazo mabaya na nia mbaya; sio kujitia ulemavu. Vinginevyo, kungekuwa na idadi kubwa na wafuasi ambao ni chongo au wenye mikono vigutu kama maneno ya Yesu yangekuwa ni ya kuchukuliwa tu alivyosema.

Anachokitaka Yesu tufanye ni kuondoa katika maisha yetu mambo yale yanayotuweka katika majaribu zaidi. Hiki sio kitu kirahisi kufanya, lakini tunategemewa tukifanyie kazi.

Kwa kawaida tunao uhuru katika maisha yetu, kama tuna Luninga, kuona kipindi tunachokitaka, kuona gazeti gani tusome, tuwe na ushirika na nani au kuwa rafiki wa nani. Hii ni baadhi tu ya mifano ya maeneo tunayopaswa kuwa waangalifu; unaweza kuyafikiria mengine. Ni rahisi sana kuvutwa kwenye dhambi kama tunakuwa ‘limbukeni’ wa kila kitu.

Somo kutoka kwa Yesu kwa wafuasi wake na wale wanaotaka kubatizwa, wanaotaka kumpendeza Mungu, ni kwamba, ni lazima wadhibiti tamaa zao za kufanya mapenzi. Ni lazima wakwepe mazingira ambayo wanajua yanaweza kuwavuta kwenda ovyo. Maneno hayo ya Yesu ya kungoa jicho na kukata mkono, yamekusudiwa yawe kama kengele inayolia akilini mwao majaribuni. Inapotokea wakajikuta wamejaribiwa vikali zaidi, basi ni muhimu watafute msaada kutoka kwa Mungu kwa haraka kwa kuomba.

Katika maandishi ya Paulo, kuna ushauri mzuri mwingi unaohusu maisha ya kila siku, ingawa barua zake ziliandikwa kwa ajili ya Wakristo karibu miaka 2000 iliyopita. Mfano mzuri sana upo katika Warumi 1:26, 27. Madai na kelele zinazoendelea kukua za makundi ya watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, wanaodai haki zao, ni tatizo kubwa katika dunia ya sasa.

Wakiwa wanaungwa mkono na serikali na sheria za haki-sawa, wanachosema wakati wote ni kuwa, uhuru wa kufanya hivyo ni haki ya kawaida, na wale ambao hawajiingizi katika mambo hayo ni wenye ukasoro fulani au wenye kupitwa na wakati.

Wanaposomewa Biblia inachosema, kunakuwa na michomo ya hasira na kukana, na hili ni kwa kuwa mafundisho ya Biblia yanasema wazi kuwa, huu ni uovu (ms. 28-32). Unaweza kuona hata zaidi umuhimu wa mstari wa 32. Kama unavyoona, Paulo anatuonya kuyaepuka mapenzi ya jinsia moja akionesha kuwa, ni kutokumuamini Mungu kunakowafanya wanaume na wanawake wafuate namna ya kuishi, inayoabudu tamaa.

Katika Walawi 18 kuna Sheria za Mungu kwa watu wake Israeli. Kwenye mstari wa 22 mpaka wa 24 kuna muongozo unaokataza kukiuka ngono-halali. Mapenzi ya jinsia moja yanaelezewa kuwa ni ‘machukizo’ kwa Mungu. Kitu cha kukumbuka kutokana ni hili ni katika mstari wa 24 ambapo tunaambiwa, mataifa yaliyokuwa yakiishi katika nchi ya Kanaani yalikuwa yakiyafanya machukizo hayo, na Mungu alikuwa amepanga kuyaadhibu vikali kwa hili.

Ni muhimu kwa wote wanaokuwa wafuasi wa Yesu kukumbuka wakati wote kuwa, ngono huria ni uovu mkubwa mbele ya Mungu. Mfano mmoja ambao ni rahisi kuukumbuka upo katika Mwanzo 18:20 na pia Mwanzo 19:-1-29.

Tangu wakati huo mpaka leo, neno Sodoma limekuwa likitumiwa kusemea mapenzi ya mwanamume kwa mwanamume wenzake, na Sodoma na Gomora imetumiwa kuwakumbusha Waisraeli juu ya hukumu ya Mungu ya kutisha, inayowaonya wasiufuate mtindo wa kimaisha kama huo unaoikiuka Sheria ya Mungu.

Imekuwa ni muhimu katika somo hili kutafakari matumizi mabaya ya kujamiiana, ambako ni zawadi kutoka kwa Mungu. Sababu ni kwamba, ngono ni kitu chenye msukumo mkubwa katika maisha yetu, na ni rahisi sana kutumiwa vibaya. Tutaona katika somo linalofuata, uzuri wa kitu hicho.

Swahili Title
Kujamiiana, Zawadi kutoka kwa Mungu
English files
Swahili file
PDF file
African text
Christadelphian Bible Mission