SOMO LA 55
HUKUMU
SOMO: 1 Wakorintho 15
Mojawapo ya njia zilizotumiwa huko nyuma kuwashawishi watu wajiunge na Ukristo, ilikuwa kuwatisha juu ya Kiti cha Hukumu cha Kristo. Kusudi la masomo haya ni kukuelezea faida na haja ya wewe kubatizwa katika Jina la Yesu. Kwa hiyo, ni muhimu tuangalie mada hii ya hukumu, kwa kuipitia mistari inayosemea jambo hili katika Biblia.
Mada ya hukumu ni mada inayotisha, lakini ni vizuri itazamwe kwa pamoja na ahadi alizotoa Mungu, za msamaha na rehema yake kwa wale wanaomtafuta.
Kwa kuwa tutakuwa tukiangalia jambo hili linalokuja, rejea zilizo nyingi tutazichukua kutoka kwenye unabii. Unaweza ukazitegemea zitoke kwenye Agano la Kale; lakini nyingi zipo pia kwenye maneno ya Yesu na mitume wake, na zingine katika kitabu cha Ufunuo.
Kwa yeyote ambaye, kwa bahati mbaya, ametakiwa kukabiliana na mashtaka katika mahakama ya kisheria, mara nyingi atataka kujua hakimu atakayeendesha kesi yake ni nani. Sababu ni kuwa, hata kama hakimu amesoma kiasi gani na ana uzoefu kiasi gani, ni binadamu, na hivyo anakuwa na mtizamo ambao ni wake kibinafsi, juu ya kile kilicho haki au kosa mbele ya sheria.
Tunapotaka kuangalia mada hii ya hukumu kama ilivyo katika Biblia, tutataka nasi kufahamu kitu juu ya mwamuzi. Hebu ifungue Biblia yako kwenye Zaburi ya 72. Hapo tunaambiwa: âAtawaamua watu wako kwa haki, na watu wako walioonewa kwa hukumuâ¦Siku zake yeye mtu mwenye haki atasitawi, na wingi wa amani hata mwezi utakapokomaâ (ms. 2-7).
Kumbuka ya kwamba haya ni maneno ya Mungu, yanayoongelea haki iliyo ya kweli kama ilivyokusudiwa na Mungu, kwa ajili ya wanadamu, tangu mwanzo kwenye bustani ya Edeni. Maelezo mengine kumhusu huyu âhakimu wa kweliâ yapo kwenye unabii wa Isaya, Sura ya 11, ambapo utangulizi wake ni: âBasi litatoka chipukizi katika shina la Yeseâ, na maelezo kuhusu âTawiâ yanapolinganishwa na rejea kama hiyo yanaonesha kuwa, mwamuzi huyo mkamilifu atakuwa Bwana Yesu, Mwana wa Mungu.
Paulo aliondoa mashaka yoyote juu ya hili alipowaandikia, kwa uweza wa Roho ya Mungu, Warumi, na kuonesha wazi kuwa, ni Yesu atakayekuwa Mfalme wa dunia yote atakaporudi (War. 14:7-13). Katika maneno yake ya kumalizia kwa Timotheo, Paulo aliongelea juu ya tumaini lake kibinafsi na imani aliyokuwa nayo juu ya huyu mwamuzi wa kipekee sana (2 Tim. 4:6-8).
Gundua hapa ya kuwa hakuwa na hofu hapo; kutamani tu kwamba hiyo siku ingekuja mapema. Hili linaweza kuwa hivyo hata kwetu kama tunayaishi maisha yetu kwa kuzingatia miongozo ya Yesu na kufuata mfano wake.
Petro alipokuwa akimfafanulia Injili akida wa Kirumi, Kornelio, alionesha pia kuwa, Yesu ndiye atakayekuwa Hakimu (Matendo 10:38-43). Kuna taarifa zaidi hapa juu ya hukumu hiyo, kwa kuwa Petro anasema kuwa, Yesu, âNdiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafuâ (ms. 42).
Yakobo katika waraka wake, Sura ya 5 mstari wa 8 na wa 9 anaandika akiwa na tumaini kuwa, kurudi kwa Yesu kungekuwa wakati wa uhai wake. Haikuwa hivyo, lakini, kwa kuwa maisha yetu ni mafupi sana, na wakati wa kufa inakuwa, utambuzi unaofuata ni wakati wa kufufuliwa kwetu, hatuwi mbali na siku hiyo ya hukumu; hata iwe mamia ya miaka yamepita.
Mengi zaidi juu ya hili yapo katika kitabu cha Ufunuo, na tutaangalia kwanza Ufunuo 11:18. Hebu yaangalie maneno hayo kwa makini na utaona kuwa, kusudi la Mungu kwanza ni kuwazawadia wale waliomtumikia, na kuonesha imani kwake na kupenda kulitukuza Jina lake. Adhabu kwa wale wanaomkataa Yesu ni kitu ambacho sitaki kukijadili katika somo hili.
Tunapofungua mbele kwenye Ufunuo 20:11-13 tunaona kinachosemwa kinavyovutia, na ni lazima kivutie, na hasa tukilinganisha na mambo madogo madogo yanayohusu maisha yetu, ujanja-janja wote wa mwanadamu katika yote anayofanya. Mwanadamu aliumbwa katika uso wa dunia ili hatimaye alete hali ya utulivu, haki na upendo ambao utampendeza Mungu daima.
Mungu atawafanyaje upya waliokufa katika kuwafufua, hatukuoneshwa; lakini kwake yeye mwenye hekima na maarifa makuu, aliyeviumba vitu vyote, itakuwa hakika ni kitu kirahisi tu. Ni muhimu pia kuyaona maneno yaliyopo kwenye mstari wa 12: âHao wafu wakahukumiwa katika mambo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yaoâ (Ufun. 20:12).
Uthibitisho huu wa mambo tuliyojifunza katika masomo ya awali ni wa maana. Uhusiano uliopo kati ya imani kwa Mungu na kuiweka imani katika matendo katika maisha yetu, ni kitu anachokichunguza Yesu kila siku, akiwa ni mpatanishi wetu na Mwamuzi ajaye. Hakuna kinachompita pembeni.
Nataka sasa kuiacha picha hii ya hukumu, tuweze kuangalia tena Ufalme wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tumekwisha soma undani wa Ufalme unaokuja, utakaokuja na Mhukumu wa Haki ambaye atakuwa Mfalme Mkuu sana. Siku za mwanzo za enzi yake zitakuwa, kwa vyovyote zimejaa umwagikaji wa damu na kipigo kwa mataifa ya dunia yanayompinga na kutaka kumwangamiza.
Lugha ya manabii sio rahisi kuielewa sana, na kuna mifano mingi ya kuchagua, lakini angalia kwanza Isaya 24:21-23 ambapo tunaoneshwa picha ya adhabu. Sasa twende kwenye Zekaria 14. Kisome kifungu chote. Vita na uharibifu unaosemewa ni vitu visivyokwepeka, lakini ni lazima tutegemee hili kutokea kwa kuwa ujio wa Yesu utakuwa ni ujio kwa dunia iliyojaa uovu.
Kitu kinachosisimua katika unabii huu ni jinsi Yerusalemu inavyosemewa mara kwa mara na Wayahudi. Hili kwa hakika lina jambo la muhimu katika kusudi la Mungu, na migogoro ya mara kwa mara katika Taifa la Israeli ni lazima inaashiria jinsi kurudi kwa Yesu kulivyo karibu. Kuna picha ya mibaraka Mungu aliyoiahidi kwa wale wote watakaokubaliwa katika Ufalme wake katika Isaya 25:8 na 9, inayosemewa pia kwa kuelekezwa kwa watu wake.
Wafuasi wa Yesu ni wale wanaosemewa katika Ufunuo 20, kama watu walioandikwa katika âkitabu cha uzimaâ. Ni watu maalumu na ni pamoja na Wayahudi kati ya mataifa yote, waliokusanywa katika nchi yao wenyewe na kubarikiwa na Mungu. Ni picha nzuri sana ya Mungu akiwa anawafuta machozi watu wake katika Ufalme huo unaokuja. Picha hiyo imerudiwa tena kwenye Ufunuo 21:3-5.
Mibaraka ya wakati wa Ufalme ni mingi, na imetajwa katika sehemu nyingi za Biblia kama tulivyokwishaona. Kwa sehemu kubwa undani wa haya upo katika maeneo ya unabii yanayosemea vita na uharibifu, adhabu itakayokuja juu ya wale wanaoitwa maadui wa Mungu na maadui wa watu wake, Wayahudi. Mfano wa hili upo katika Isaya 35 ambapo manufaa watakayoyapata watu wa kawaida (wanaokufa) wakati wa Ufalme yameoneshwa.
Kwa hiyo kutakuwa kuna watu wa kawaida (wanaokufa) katika kipindi cha Ufalme wa Yesu, na watakuwapo wale ambao wamepewa uzima wa milele, wasioweza kufa. Katika Isaya 35: 5 wanaongelewa vipofu na viziwi, na katika mstari wa 6 vilema na walio bubu. Huu ni ulemavu unaohusiana na baadhi watu wa kawaida (sio watakatifu wa Mungu wasiokufa). Urefu wa muda Ufalme utakaochukua umeoneshwa kuwa ni miaka 1000 katika Ufunuo 20:4-6.
Yanayosemewa mengine juu ya ibilisi na shetani katika mstari wa 2 na âwafu waliosaliaâ katika mstari wa 5 yatakuwa katika somo la mbeleni; hatutayasemea hapa.
Habari zinazohusu Ufalme zimeenea katika Biblia yote, na utakuwa kwa sasa umepata mawazo ya jinsi itakavyokuwa. Paulo, katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho, Sura ya 15 anatoa taarifa ya mchakato wa ufufuo, lakini pia analo la kusema kuhusiana na kazi ya Yesu akiwa sasa ni Mfalme wa dunia. Ni vizuri kukisoma kifungu hicho chochote, lakini kwa sasa tuangalie mstari wa 20 mpaka wa 28.
Hapa tunaona ya kuwa, Ufalme wa Mungu ni wakati wa maandalizi ambayo dunia yote na watu wake, wakiongozwa na wale ambao wamekwisha pata uzima usio na mwisho, itaifikia hali ya amani, utulivu na ufanisi. Ndipo Yesu, Mfalme Mkuu, atakapoikabidhi dunia kwa Baba yake, Mungu, tayari kwa kipindi kinachofuata katika mpango wake, akiwa ni âYote katika Woteâ.
Hatujui mpango huo ukoje, hakuna taarifa iliyotolewa zaidi ya kwamba, kutakuwa na ufufuo mwingine (wa pili) kabla ya hapo na hukumu nyingine, na kutokomezwa kwa mauti duniani. Hili lina maana kuwa watu watakuwa hawafi tena, kwa maana, adui wa mwisho atakayekuwa amebatilishwa ni mauti (1 Wakor. 15:26).