6. KUITWA KWA ABRAMU
“Na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”
Shabaha
Kujifunza ahadi za Mungu kwa Abramu na maana yake. Watu wakasahau haraka sana fundisho kuhusuiana na gharika na uovu uliongezeka tena kwa kuwa waligeuka wakaabudu sanamu. Abram aliishi katika Uru ya Ukaldayo,karibu na mji wa Baberi.Uru ulikuwa ni miongoni mwa miji mashuhuri ya Ukaldayo,ukiwa na hekalu maridadi lililoitwa Ziggurat- ambapo walimwabudu mungu mwezi.Katika nchi yote ile watu waliabudu miungu mingi– jua mwezi na nyota na miungu mingine –Viongozi wao katika ibada hizi za uongo walikuwa wachawi na wanajimu kama wale alionenwa katika Kitabu cha Danieli 4:7Mwanzo 11:31-12-10
JAMAA YAABRAMU WANAONDOKA URU: Mwanzo 11: 31, 12:1
Abram hukufundishwa Kweli katika utoto wake,kwa sababu wazazi wake waliabudu sanamu kama ilivyo kuwa desturi ya wengine waliowazunguka.“Baba zako waliishi upande wa pili wa mto (hasa ule wa mto na Frati) hapo zamani,maana Tera baba yake Abramu naye ni baba yake Nahorii wakaitumikia miungu mingin”(Yosh 24:2-4). Hata hivyo baadaye“Tera alimchukuwa mwanae Abramu, Lutu… na Sarai…wakaenda moja kwa moja kutoka Uru ya Wakaldayo mpaka nchi ya Kanaani na kuweka makazi yao katika Harani”(Mwanzo 11:31)
Katika Kitabu cha Matendo 7:2-4 tunaambiwa kwa nini waliondoka Uru na kusafiri kuelekea kaskazini hadi Harani. Wakiwa Uru , Mungu alikuwa amemwambia Abram kuondoka sehemu ile na kwenda katika nchi atakayo mwonyesha.Tera,baba yake,na jamaa yake waliosalia ni dhahiri kuwa walipenda kwenda paomoja naye pia.Lakini walipofika Harani hawakuweza kuendelea na safari.Wote walingoja hapo mpaka Tera alipofariki.
Ndipo Abramu katika kutii maagizo ya Mungu- “Toka wewe katika nchi yako na jamaa zako na nyumba ya baba zako uende mpaka nchi nitakayo kuonyesha”(Mwanzo12:1) -akamchukua Sarai,mkewe na Lutu mwana ndugu yake na kondoo zao,na mifugo na mali walizo kuwa nazo,wakauvuka mto.Ni kwa kufanya hivyo ndipo akajulikana kuwa ni “Abramu Mwebrania”,lilikuwa kuwa na maana ya “kuuvuka” (Kutoka 14:13). Na hivyo akaanza maisha mapya.
ABRAMU ANAITWA MARA YA PILI NA AHADI NZURI SANA ZA MUNGU:Kutoka12:2-4
Mungu akamwambia tena Abramu pale Harani. Alimpatia Abramu ahadi kuu za kwanza na nzuri sana ambazo zimeandikwa katika Kitabu cha Mwanzo 12;2-3.Mungu alimwahidi Abramu kuwa:
(a)Atakuwa taifa kubwa.
(b)Jina lake litakuwa kuu na atakuwa baraka.
(c)Mungu atawabariki wale wanaombariki na kuwalaani wale wanaomlaani.
(d)Katika Abram jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Hakika hii ilikuwa ahadi kubwa. Abram, akiwa na imani kubwa na ujasiri, akiwa na umri wa miaka 75, aliichukua jamaa yake- Sarai mke wake(ambaye baadaye alijulikana kama Sara) mototo wa ndugu yake,wachungaji wa mifugo na watumishi wake na akauvuka mto Frati akaingia katika nchi ya Kanaani (Mwanzo 12:4)
Mtume Paulo anazungumzia imani kubwa aliyokuwa nayo Abram katika Waebrania 11:8“Kwa imani,Abrahamu,alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi,akatoka asijue aendako”
ABRAMU KATIKA NCHI YA AHADI: Mwanzo 12:5-10
Abramu na jamaa yake waliingia katika nchi ya Kanaani na wakasafiri hadi wakafika Shekemu(mstari 6),mahali alipogenga madhabahu na kumwabudu Mungu,bila shaka kumshukuru kwa kufika safari salama. Huko Mungu alimpatia ahadi nyingine“Uzao wako nitawapa nchi hii”(mstari 7).Kutoka hapo Shekemu,walisafiri kuelekea kusini hadi Betheli, akamjengea BWANA madhabahu nyingine huko. Aliendelea kusafiri katika nchi hiyo lakini kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya Kanaani aliingia katika nchi ya Misri na kuishi huko kwa muda.
Ilikuwa safari ndefu kutoka Uru ya Wakaldayo na bado kulikuwa na kilometa nyingi ili kurudi tena Kanaani.Mungu alikuwa amesema “Uzao wako nitawapa nchi hii”. Hadi leo Abramu na uzao wake bado hawajaipata nchi ile.Lakini kile alichoahidi Mungu, Yeye hakika atatimiza (Soma Matendo 7:5). Abramu atafufuliwa kutoka katika wafu baada ya Bwana Yesu Kristo kurudi na ndipo ataipata nchi aliyoahidiwa na uzao wake miaka mingi iliyopita.
FUNDISHO KWETU
Katika safari zake, Abramu alijenga madhabahu ili kumwabudu Mungu, akimsifu na kumshukuru kwa kuwa na ufahamu wa Kweli ya Mungu, na kumwomba Mungu kutimiza mapenzi yake. Siku hizi tunafanya hayo hayo tunapoomba Ufalme wa Mungu uje, na kwa kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo katika nchi. Abramu aliamini ahadi za Mungu na tunapaswa kufanya hivyo hivyo. Ni mfano wa ajabu kwetu sisi,wa imani (kumwamini Mungu) na utiifu.
Abramu alipoondoka Uru, alieachana na maisha yake ya kale. Hakuishi tena katika nyumba ya anasa iliyokuwaimezungukwa na maisha ya kifahari.Wakati huo sasa alikuwa mtu wa kuishi katika hema “mgeni na msafiri katika nchi” (Waebramia 11:13) Mungu alikuwa amemwahidi nchi ya Kanaani kuwa miliki yake milele, lakini alijua kuwa hili halitatimizwa mpaka baada ya kufufuka kwake.Hivyo aliridhika kuzurura kama mgeni katika nchi ile, akiishi katika hema katika maisha yake yote mpaka hapo Mungu atakapo mwezesha kuimiliki nchi hiyo milele.
Ingawa Mungu hategemei sisi kuyaacha makazi yetu na kwenda kuishi katika mahema, anatutaka sisi tuonyeshe imani kama ile ya Abram. Anatutuka tusiyathamini maisha ya raha na anasa bali tutarajie maisha ya furaha na raha wakati tutakopoishi katika nchi ile na Abramu na watu wote waaminifu, waume na wanawake wa zamani.
Ni lazima tujiepushe na mambo ya dunia, kama Abramu alivyoijitenga kutoka katika mienendo ya Wakanaani na kutumikia Mungu aliye hai kwa uaminifu wa utiifu.
MAELEZO YA ZIADA
Kuuvuka Mto Frati kulikuwa na maana ya kuyaacha nyuma matendo maovu na kuabudu sanamu katika Babeli na kuanza kuishi maisha mapya.Jambo hili hututokea sisi tunapobabatizwa katika Kristo“vivyo hivyo na sisi tuenede katika upya wa uzima”(Warumi6:4).Tunaachana na mambo ya kidunia ili kuanza maisha mapya.Ingawaje Abramu alikuwa“nimrithi wa nchi” (Warumi4:13), lakini lakini “hakupata sehemu yeyote ya urithi” wakati wa uhai wake(Matendo 7:5) bali alikuwa mgeni na mpitaji pale(Waebrania11:8-9). Imani yake ilikuwa ndiyo mwongozo kwa watu wote wa Mungu(Warumi 4:23-24).Ingawaje wao pia ni “warithi wa nchi” wasitake kujihusisha na vivutio vinavyopatikana katika ulimwengu huu wa sasa bali tungonjee bila kukata tamaa kurudi kwake Bwana kutoka Mbinguni.
Ahadi ambayo Mungu alimpa Abramu katika Mwanzo 12:3 (“Katika weweMataifa yote yatabarikiwa”) ilikuwa ni injili(Wagalatia3:8).Injili maana yake ni “habari njema”au “Ujumbe mwema”habari njema ni kwamba kupitia mzao wa Abramu (Yesu Kristo) hata sisi ambao ni watu wa mataifa tunapata kuwa na uhusiano na Abramu kupitia ubatizo.Tunapobatizwa tunakuwa jamaa kubwa ya Mungu ambayo Abramu na yeye yumo humo na kwa hiyo na sisi tunakuwa warithi wa ahadi za Mungu alizomwahidia.
Wayahudi,ambao sasa wamezagaa kwa sababu ya dhambi zao watakuwa taifa kubwa (Mwanzo 12:2), wakati mkombozi (Yesu Kristo) atakapokuja katika Sayuni na “atamtenga Yakobo na maasi yake” (warumi 11:26, Isaya 59:20).
Kwa hiyo Wayahudi na watu wa mataifa watabarikiwa pamoja na Abramu aliyemtii wakati Ufalme wa Mungu utakaposimikwa na Yesu kristo kutawala akiwa mfalme katika nchi. Kitakuwa ni kipindi cha utukufu,amani na furaha kwa mataifa yote.
“Jina lake,na lidumu milele.Jina lake lidumu milele pindi ling`aapo jua, Watu wote watabarikiwa katika yeye.Mataifa yote watamwita mbarikiwa” (Zaburi 72:17)
MASWALI
Majibu Mafupi
- Abramu na jamaa yake waliishi wapi?
- Je Abramu na jamaa yake walimwabudu Mungu wa Kweli kule?
- Kwa nini Abram aliuhama mji wa kwao?
- Mungu alitaka Abramu aende wapi?
- Ni nani waliovuka mto wa Frati pamoja na Abram?
- Kwa nini Abramu aliishi katika hema katika nchi ya Kanaani?
- Kwa nini Abramu aliondoka kuelekea Misri?
Majibu ya Ziada
- Eleza safari ya Abramu kutoka Uru kwenda nchi ya ahadi.
- Mungu alitoa ahadi gani kwa Abrahamu katika Harani?
Majibu ya Nyongeza
- Ahadi kwa Abramu itatimizwa lini?
- Ni habari njema ipi iliyohubiriwa kwa Abramu?