32. WATU WAWILI YERIKO
Shabaha:
Ni kuonyesha jinsi Mungu anavyowalinda wale wanaomtii na kumwamini.
Muhtasari:
Yeriko ulikuwa Mji wa kwanza ambao ungechukuliwa na wana wa Waisraeli walipovamia Kaanani. Haukuwa mkubwa, lakini ulikuwa umejengwa boma imara ,ukiwa na kuta mbili, mmoja ukiwa 1/6 unene na wa ndani ukiwa futi 1/12 unene. Wataalam wa mambo ya Kale waliogundua mabaki ya mji huo wanasema kuta hizo yamkini zilikuwa futi 30 urefu wake. Watu wengi walifanya shughuli zao mashambani na waliishi nje ya mjii, lakini walikusanyikia ndani wakati wa hatari, kwa ajili ya usalama walitegemea kuta hizo ndefu na nene. Yoshua 2.
Wapelelezi walitumwa kwenda Yeriko. Joshua 2:1-3
Kutoka Shitimu, Yoshua alituma watu wawili kuipeleleza Yeriko. Huu ulikuwa Mji muhimu sana kwa upande / sehemu nyingine ya Yordani. Waisraeli ilikuwa ni lazima kuuteka Yeriko kabla ya kuingia Nchi ya Ahadi kwa usalama. Kwa hiyo Yoshua aliwatuma watu kuangalia namna ya kuutwaa na kuwashinda wakazi wake. Yeriko ulizungukwa na kuta mbili nene sana zenye nafasi katikati na nyumba zilijengwa kutoka upande mmoja hadi upande wa pili juu ya kuta. Katikati ya ukuta wa nje kulikuwa na mlango mkuu uliofunguliwa wakati wa mchana kutwa na usiku ulifungwa, kiasi kwamba adui asingeweza kufanya shambulio linaloweza kufanikiwa. Wapelelezi waliungia Miji ,kwa siri kupeleleza na walipewa hifadhi na Mwanamke aliyeitwa Rahabu, ambaye nyumba yake ni kati ya zile zilizokuwazimejengwa juu ya kuta. Mtu mmoja aliwaona wale watu na akafikiria kuwa watakuwa wapelelezi wa kutoka Israeli, ambao walikuwa na kambi yao ng’ambo ya Yordani. Mfalme wa Yeriko aliambiwa kuwa walikuwa ndani ya nyumba ya Rahabu na mara hiyo akatuma watu ili wawakamate.
RAHABU ANAWASAIDIA WAPELELEZI: Joshua 2:4-7
Rahabu alikuwa ameshasikia maajabu mengi sana yaliyokuwa yametendwa na Mungu wa Israeli - jinsi Mungu alivyowaokoa Waisraeli kutoka Misri kwa kuifuma Bahari ya Shamu na kuwashinda maadui wa Waisraeli katika njia yao. Sasa Waisraeli walikuwa wamepiga kambi kuikabili Yeriko upande mwingine wa Yordani na Rahabu alijua hakika kuwa Yeriko itatwaliwa na Waisraeli pia. Haraka sana Rahabu akijua kuwa watu waliotumwa na Mfalme walikuwa wanatafuta wageni wawili waliokuwa ndani ya nyumba yake; aliwapandisha juu ya dari ,aliwaficha kule kwa mabua ya kitani.
Wakati wajumbe waliotumwa na mfalme walipomwendea aliwaambia kuwa hao watu walikuja kwake lakini yeye hakujua walikotoka. Kulipokuwa giza waliondoka wakati wa kufunga lango kuu. Kama watu wa Mfalme wakiwafuatia haraka watawapata. Wale watumishi wa Mfalme wakafanya haraka kuwafuatia wapelelezi kwa njia iendayo Yordani kuelekea vivukoni (sehemu za kuvukia kwa kuwa na majiyalikuwa machache) Mto ulikuwa umefurika hivyo walitegemea kuwa wale wapelelezi wangerudi Kambini kwa kupitia sehemu hii ya vivuko vya mto. Lakini bila shaka hawakuona dalili zozote za kuwaona.
WAPELELEZI WANAOKOKA: Yoshua 2:8-24
Wakati huo huo, Rahabu aliwafuata darini wapelelezi; "Mimi ninajua yakuwa BWANA amewapa ninyi nchi hii", na akasema ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu; (mst 10) Maana tumesikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu na ushindi mlioupata kwa wale wafalme wa Waamuzi yalisababisha watu wa Yeriko kuhofia yatakayowapata na mioyo yao imeyeyuka (mst 11).
Rahabu aliamini ukuu wa Mungu wa Israeli kuwa ndiye Mkuu kuliko wote.
"Kwa kuwa BWANA, Mungu wenu,yeye ndiye Mungu katika mbingu juu na katika nchi chini" (mst 11)
Rahabu akishawatendea wema mkuu wale wapelelezi hatimaye aliwaomba wamwokoe yeye na familia yake wakati watakapoutwaa, maana aliamini kabisa kuwa Mungu wa Israeli kuwa "amewapa ninyi nchi hii" (mst 9). Wale wapelelezi walimwahidi kuwa watamwokoa ikiwa mtu yeyote asipoelewa kuwa walikuwapo pale. Aliwasaidia kuokoka kwa kuwashusha kwa kamba nyembamba (kamba) kupitia dirishani. Aliwaonya wasifuate moja kwa moja njia inayoenda kwenye kambi ya Waisraeli, kwa sababu kama wangevukia njia ya tambarare inayoenda mto Yordani watu wa Yeriko wangeweza kuwaona wazi wazi. Rahabu aliwashauri waende mlimani upande wa Magharibi wa Mji wa Yeriko wajifiche huko kwa muda siku tatu mpaka wale watu wa mfalme watakapokuwa wamerudi. Na hivyo wangerudi salama katika kambi ya Waisraeli.
Wale wapelelezi walimshukuru sana Rahabu kwa msaada wake na wakamwahidi zawadi kwa ajili ya wema wake. Walimweleza afunge kamba nyekundu katika dirisha lile alilowatelemshia, na Waisraeli watakapoipiga Yeriko awe tayari ameshakusanya familia yake yote katika nyumba yake na wawe ndani. Kama atafanya hivi basi wote walio ndani watapona.
Baada ya siku tatu za kujificha, wapelelezi walirudi kwa Joshua wakamwambia habari za mambo yote yaliyowapata "Hakika BWANA ameitia nchi yote katika mikono yetu, tena zaidi ya hayo wenyeji wa nchi wameyayuka mbele yetu". (mst 24)
Fundisho Kwetu:
Rahabu alikuwa amesikia kwa masikio yake habari za kweli kuhusu BWANA mwenye uwezo mkuu alioudhihirisha kwa watu wa Israeli. Aliamini na akaweka tumaini kwa BWANA. Yeye aliamini na atapewa zawadi ya uzima wa milele katika ufalme wa Mungu; kwa maana jina lake limeorodheshwa pamoja na watakatifu wengine wanaume na wanawake wa zamani. Waebrania 11.
Tazama jinsi Rahabu alivyo mfano wa muhimu kwetu. Hata sisi pia, lazima tuamini mambo yale tunayosikia ,Neno la Mungu. Kama tukiliamini neno lake, sisi pia tutapewa thawabu sawa sawa na Rahabu mwaminifu.
Bado kitambo kidogo, Mungu atadhihirisha uwezo wake Mkuu tena duniani na watu wake Israeli wataishi katika Nchi milele.
KWA UKUMBUSHO ZAIDI:
Kama Musa na Joshua, hata Rahabu aliyekuwa wa Mataifa (si Myahudi) alionyesha imani kubwa. Imani ya Rahabu ilimpatia heshima kubwa ya kuwa mzazi wa Bwana Yesu Kristo. Baada ya Waisraeli kuuteka kuimiliki Yeriko Rahabu alipokelewa katika Kambi ya Waisraeli na baadaye aliolewa na Salmoni wa kabila ya Juda, kabila alilotokea Daudi; mamia ya miaka baadaye, alizaliwa Bwana Yesu Kristo (Math 1:5; Ruth 4:4-22) .Sisi pia tunaweza kuunganika na Yesu Kristo kwa imani; Yaani, kwa kuiamini Injili na kubatizwa katika Jina lake. Tunafanyika wana wa Mungu na warithi wa ahadi za Mungu alizoomwahidi Abrahamu (Galatia 3:26-29; angalia Mwanzo 12:1-3).
MASWALI:
MAJIBU MAFUPI.
- Jina la Mji wa kwanza wa Kaanani kutekwa na kumilikiwa na Waisraeli ni?.
- Ni watu wangapi wlitumwa Yeriko na Musa?.
- Ni nani aliyewaficha wapelelezi kule Yeriko?.
- Nyumba ya Rahabu ilijengwa sehemu ipi ya Mji?
- Ni jinsi gani Rahabu aliwaficha wapelelezi?.
- Ni kwa nini Rahabu aliwaficha wapelelezi?.
- Rahabu aliwasaidiaje wapelelezi kuokoka?.
- Ni kwa jinsi gani Rahabu angepewa thawabu?.
MAJIBU YA UFAHAMU:
- a) Eleza ni jinsi gani Rahabu aliwaficha wapelelezi wale wawili waliokuwa wameingia Yeriko.
b) Ni kwa jinsi gani Rahabu angepewa thawabu kwa ajili ya kuwa msaada aliowapa wapelelezi?.