CSSA 1-2-18 - SAMUEL

Swahili

43. SAMWELI

“Nena, BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikia

Shabaha

Kuonyesha kwamba Mungu hufurahishwa na watoto waaminifu na watiifu, lakini atawaadhibu  wale wanaolidhalilisha Jina lake.

Muhtasari

Kuhani Mkuu wa Israeli, alikuwa na watoto wawili wanaume waovu, Hofni na Finehasi. Wakiwa makuhani walipaswa kushika sheria na kuonyesa mfano bora kwa watu, lakini walijichukulia sehemu ya dhabihu kabla haijatolewa kwa Mungu nao walitenda maovu mengine ambayo yalisababisha watu kutenda dhambi.

 Kwa ajili hiyo Mungu aliamua kuwabadilisha makuhani hawa waovu na mtu yule ambaye angetenda mapenzi yake Mungu (1 Samweli 2:35) 1 samweli 1:21;26;3 na 4

 

KUZALIWA KWA SAMWELI :Samweli 1:9-20

Hana, aliishi na mumewe Elikana katika mji wa Rama, umbali wa maili  chache kutoka Yerusalemu. Kila mwaka walikwenda hekaluni huko Shilo kuabudu na kutoa dhabihu zao kwa Mungu. Hana hakuwa na furaha  kwa sababu hakuwa na watoto ilimfanya Elikana kuhuzunika kwa kumwona mkewe akiwa mwenye majonzi. “Je mimi sio bora kwako kuliko watoto kumi?”Alisema.

 

Hivyo Hana alilipeleka tatizo lake mbele za Mungu kwa sala. Alisali kimya kimya asitambue kuwa Eli, kuhani alikuwa akimchunguza. Aliona midomo yake tu ikinena na baadaye akamwuliza, alimwambia kuhusu huzuni ya moyo wake na kufafanua sala yake. Alikuwa amesali kwa  moyo wa unyenyekevu kwa ajili ya kupata mtoto mwanaume naye akawa amemwahidi Mungu kwamba  kama angempata mtoto angemtoa kwa Mungu ili afanye kazi yake siku zote za uhai wake. Angekuwa Mnadhiri kama Samsoni, mtu aliyewekwa wakfu kwa kazi ya Mungu. Eli aliona kuwa Hana  alikuwa ni mwanamke mcha Mungu, hivyo akasema, Nenda kwa amani na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba (mstari wa 17)

Basi ikatokea kwamba Hana alipata mtoto mwaname. Akamwita jina lake “Samweli” maana yake aliyeombwa kwa BWANA.Akaja kuwa mmojawapo wa watu muhimu sana katika historia ya Waisraeli naye ameorodheshwa katika Waebrania 11:32 kuwa mmoja wa watu wa waaminifu wa Mungu.

 

SAMWELI AENDA  KUISHI NDANI YA HEKALU: 1 Sam. 1:23-28

Hana alimnyonyesha Samweli nyumbani kwa muda, hadi alipokuwa amekua kiasi cha kutosha kumpelekwa Hekaluni. Hapo alikwenda Shilo pamoja na Elikana Mume wake na kumleta mtoto wake kwa Eli.

 Alikuwa tayari amejiandaa  kutimiza ahadi yake ya kumtoa mwanawe awe chini ya uangalizi wa kuhani mkuu  ili amsaidie katika  kumtumikia  Mungu. Alimwambia Eli ,“Ee Bwana wangu, kama iishivyo roho yako, mimi ndiye yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa nikimwomba  BWANA.Naliomba nipewe  mtoto huyu; naye BWANA  amenipa dua yangu niliyomwomba. Kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyo wakati wote wa uhai wake amepewa BWANA”(mstari wa 26-28).

 

KAZI YA SAMWELI :I Sam  3:1-21

Samweli sasa aliishi na Eli kuhani mkuu ambaye alimfundisha mambo ya Mungu. Kila mwaka alivyoendelea kukua, Hana alimletea koti mpya  alipokuja hekaluni pamoja na mumewe kutoa dhabihu. Samweli aliuona mfano mbaya wa watoto wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, lakini alifuata njia ya Mungu na kukua mwenye kupata kibali akimpendeza Mungu na watu (1Sam 2:26). Usiku mmoja, Samweli alipokuwa amelala aliamshwa na sauti, iliyokuwa ikiita Jina Lake. Akifikiri ni Eli, alikimbia kwake ili kujua nini alichotaka lakini Eli hakuwa amemwita.Hili lilipotokea mara tatu ilikuwa wazi kwa Eli kwamba BWANA, Mungu Aliye  juu sana alikuwa amesema na Samweli. Alimwambia kijana kurudi kitandani naye akisikia sauti tena ajibu,“Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikia”

Katika ukimya wa Usiku, Mungu alinena na Samweli na kumpa ujumbe uliomhusu Eli na wanawe.“Nitaihukumu nyumba yake ( Eli) milele kwa uovu anaoujua kwa sababu wanawe walijichafua naye hakuwazuia”(mstari wa 13).

 Mungu hakuruhusu wana wa Eli kuwa wachungaji nyumbani mwake kwa ajili ya maovu yao.Lilikuwa  ni tatizo gumu  na la kuhuzunisha lililomfika Samweli kuweza kumwambia mwalimu wake aliyempenda ujumbe wa Mungu.

Kuanzia hatua hii na kuendelea mabadiliko makuu yalitokea katika maisha ya kijana huyu aliyetolewa kwa Mungu Samweli alikua, na Mungu alikuwa pamoja naye, naye hakuachia maneno yake kuanguka chini  nao Waisreli wote kutoka Dani hadi mpaka Beersheba wlitambua  kwamba huyo  Samweli amewekwa  kuwa  Nabii wa BWANA(mstari wa 19-20).

 

KIFO CHA ELI : 1 Samweli 14

Eli sasa alikuwa ni mzee sana mwenye umri wa miaka 98. kwa mara ningine tena, kulikuwa na vita dhidi ya wafilisti lakini safari hii maelfu ya waisraeli waliuawa.Kati ya wale waliouawa walikuwamo Hofni na Finehasi ambao walitoa sanduku nje ya Hekalu hadi katikati ya mapigano wakitumaini kwamba hili litamfanya Mungu kuwasaidia lakini Mungu asingewasaidia kwani hawakumtii Yeye, nalo sanduku lenyewe lilitekwa na Wafilisti. Mtu mmoja alipoleta habari hizi kwa Eli naye aliposikia kwamba sanduku lilikuwa limetekwa na wafilisti, Eli alishtuka mno hata ikiwa alianguka  chali kutoka kwenye kiti,“na shingo yake iliivunjika naye akafariki .

Samweli sasa akawa kiongozi na Nabii katika Israeli. Karne nyingi baadaye kazi  yake ilifananishwa na ile ya Musa. (Yeremia 15:1) alileta utaratibu katika kumwabudu Mungu katika Israeli, na wema alioutenda ulidumu miaka mingi.Alikuwa mwaminifu na mwenyekuheshimiwa ,naye;alitenda kwa ajili ya Waisraeli katika matoleo na dhabihu zao.

FUNDISHO KWETU

Watu  ambao ni waovu hawana sehemu katika mpango wa Mungu na kusudi lake juu ya dunia. Biblia inatueleza jinsi tunavyoweza kumpendeza Mungu. (Waebrania 6:1-4) Tukiwa watoto tunarekebishwa na kuonyeshwa njia sahihi na wazazi wetu.Mara nyingi hili huonekana  kuwa  gumu;na wazazi hawapendi kuwaumiza watoto wao, lakini mtu mwenye hekima Selemani alisema:“Yeye ampendaye mtoto wake humrudi”(Mithali13:24) lakini alikuwa mpole mno kwa wanae wenye vichwa vigumu.  Eli alikuwa baba mpendwa lakini alikuwa mpole mno kwa wanawe wenye vichwa vigumu.

Kwa ajili hii, Mungu alimkasirikia Eli. Na kuwa kataa Hofni na Finehasi. Lazima wote tuzifunze tunapokuwa watotoi ni lazima  tuwasikilize wazazi wetu na kuwatii ili kwamba tuongozwe katika njia ya Mungu.

MASWALI:

Majibu   Mafupi

1.Kwa nini Hana alisali Hekaluni

2.Nani alisema naye Hekaluni

3. Ni ahadi gani Hana aliyoitoa  kwa Mungu kuhusu mwanaye?

4. ”Samweli maana yake nini?”

5.Samweli alikwenda kuishi na Eli. Nani alisema naye usiku mmoja ?

6. Ni jibu gani alilitoa Samweli wakati Mungu aliposema naye usiku?

7. Ni majina gani waliitwa wana waovu wa Eli kuhani?

8. Kwa nini Mungu alikuwa na hasira juu ya Hofni na Finehasi?

9. Ni habari gani za kutisha zililetwa kwa Eli kutoka vitani?

10.  Nani alikuw kiongozi katika Israeli baada ya  Eli kufariki ?

Majibu ya Kina.

1.(a) Eleza  Hana alikiomba  nini na jinsi gani  Mungu alivyojibu sala yake ?

    (b) Je alitimiza vipi ahadi yake ?

 2.  (a) Kwa nini Mungu alikuwa na hasira juu ya Eli na wanaye?

      (b) Eleza walivyofariki

      Majibu ya Nyongeza

3. Ni ujumbe gani Mungu alimpatia Samweli usiku ?

 

Swahili Title
043 SAMWELI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type