96. YESU ANASALITIWA NA KUKAMATWA
“Siyo kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatimizwe”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Yesu alivyokamatwa na kuhukumiwa kifo. Mwana wa Mungu alikuwa ni mtiifu kabisa katika kuyatenda mapenzi ya Mungu katika maisha yake yote. Na sasa alikuwa yuko karibu ili kukabiri mtihani wake mkuu na wa mwisho. Alikuwa anafahamu kabisa kuwa hilo ndilo Mungu analotegemea yeye alifanye, kwa maana alikuwa amesoma hayo yote katika vitabu vya manabii.Alikuwa amejitahidi kuandaa kundi dogo la rafiki zake wa karibu kwa wakati huu ambalo alikuwa anakwenda kuondolewa kwao. Alikuwa amewaimarisha na kuwaongoza, na sasa ghafla na kwa ukatili alikuwa auawe. Yesu mwenyewe alifahamu kuwa ni lazima amwombe Baba yake nguvu ili amsaidie kukabili mateso hayo ya mwisho.Kwa hiyo aliwchukua wanafunzi wake kumi na moja hadi bustani ya Gethsemane, juu ya Mlima wa Mizeituni, ambapo mara nyingi alikuwa anakwenda kuomba.
(Yohana18:1-3. pia soma Mathayo 26:36-44, Marko14:32-49; Luka 22:39-53)
KATIKA BUSTANI: Mathayo 26:36-44
Yesu alikuwa amechelewa sana wakati alipoingia pale bustani usiku akiwa na wanafunzi wake. Na sasa ilikuwa ni siku ya Pasaka, siku ambayo mwanakondoo angechinjwa. Aliwaambia wanafunzi wake, “Ketini hapa, hata niende kule nikaombe” (mstari 36). lakini akamchukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye.Baada ya kitambo kidogo akawaambia wamngoje; na wakeshe kwa ajili yake. Maana alijua kuwa muda ni mfupi, na Yuda naye alikuwa mjini akikusanya kikosi cha maaskari ili waje kumkamata.
Kwa hiyo Yesu akaendelea mbele kidogo na akaanguka kifulifuli na akaomba, “Baba yangu ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi,bali kama utakavyo wewe” (mstari 39).
Akiwa ameumimina moyo wake kwa Baba yake wa mbinguni, Yesu akarudi kwa Petro Yohana na Yakobo na akawakuta wamelala. Waliamka aliposema nao. Akamwambia Petro, “Je! hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?”(mstari 40). Petro, kabla alikuwa amesema na hasa kwa kusisitiza ni jinsi gani anavyompenda Yesu na kwamba angeweza kufa kwa ajili yake. Na sasa bado amesinzia bila ya kuwa na tahadhari ya hatari iliyokuwa mbele, tena bado dakika chache tu.
Yesu alifahamu,aliwaamusha na akawahimiza kuomba ili wapate kusitahimili pia. “Kesheni, mwombe msije mkaingia majaribuni” (mstari 41).
Alijua kuwa ingawa wanafunzi walikuwa na nia sana ya kutenda sawasawa, hawakua na nguvu za kutosha za kuweza kuyaweka maneno yao katika vitendo. Yesu alisema, “Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” (mstari 41).
Na hali hii hututokea na sisi mara kwa mara. Njia peke ya kuweza kupata nguvu kwa kuweka nia yetu nzuri katika vitendo, ni kumwomba Mungu, kufuata kielelezo cha Kristo. Yesu akaondoka tena akaenda mbali kidogo katika bustani na akamwomba Mungu mara pili, akiomba apate nguvu na kuomba, mapenzi yako yatimizwe (mstari 42). “Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu” (Luka 22:43). Akarudi tena, akawakuta tena wanafunzi wake wamelala. Akawaacha na akaenda kuomba mara ya tatu, akisema maneno yaleyale.
MAASKARI WANAKUJA KUMKAMATA YESU: Yohana 18:2-6
Wakati alipomaliza kuomba mara tatu, alikuja kuwaamusha wanafunzi wake. Hata akasema nao upole sana pale bustanini, ilikuwa ni usiku wa manane, uliokuwa umefunikwa na kelele za kundi kubwa, wakiwa na mapanga mapya na myenge ya moto. Aliyekuwa akiongoza njia alikuwa ni Yuda Iskarioti, “mmoja wa wale kumi na mbili”. Yuda alikuwa anafahamu kwamba Yesu mara nyingi alikuwa anakwenda kule akiwa na wanafunzi wake kwa ajili ya kupumzika na kutulia.Nyuma yake kilikuwepo kikosi cha maaskari na walinzi wa hekalu, waliokuwa wametumwa na wakuu wa makuhani na Masadukayo. Na ingawaje wanafunzi walihuzunika sana, Yesu alikuwa kimya. Imani yake ilikuwa kwa Mungu. Alipiga hatua mbele na akawauliza askari, “Ni nani mnayemtafuta?”. Wakajibu, “Ni Yesu Mnazareti…” Yesu akawaambia, “Ni mimi”. Maaskari walikuja wakitarajia upinzani mkubwa na hapa alikuwepo waliyekuja kumkamata bila matatizo na kwa upole najikabidhi mwenyewe kwao.Kulikuwa na kitu kilichowapiga hofu ndani ya mioyo yao aliposema, “Ni mimi”, walisukumiwa nyuma “na wakaanguka chini” (Yohana 18:4-6).
YUDA ANAMSALITI YESU
Ndipo Yuda akasogea mbele na akasema, “Rabi; rabi na akambusu yeye” (Marko 14:45). Hii ilikuwa ni ishara aliyowaeleza maaskari kuwa ataifanya. Alikuja akijifanya kama rafiki, lakini moyoni mwake alikuwa ni adui mbaya kuliko wote. Baadaye, alipofikiria kitendo alichokifanya-maana alifahamu kuwa Yesu hakuwa na makosa-alijaribu kurudisha vile therathini vya fedha, wala makuhani hawakuvipokea. Kwa hiyo akaondoka na kwenda kujinyonga (Mathayo 27:3-5). Kutokana na ishara ya Yuda, maaskari wakamsogelea Yesu na kumkamata Yesu. Na wanafunzi walipofahamu jambo lililokuwa linatendeka, walimwambia. “Bwana, tuwapige kwa upanga?” (Luka 22:49). Kabla Yesu hajajibu, Petro akashikwa na hasira akachomoa panga lake na kumpiga mmoja wa watumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio lake. Mara moja Yesu akamponya sikio lake, na akamkemea Petro akamwambia “rudisha upanga wako” (Yohana 18:11). Haukuwa wakati wa kupigana vita. Alikuwa ni lazima akabiliane na kifo katika mikono ya watu hawa, kama manabii walikuwa wametabiri. Kisha Yesu akawageukia maaskari na walinzi wa wakuu wa makuhani na wa viongozi waliokuja pamoja nao.Kama tu wangetambua, kulikuwa hakuna haja ya kuwa na mapanga na siraha. Hakuwa mharifu ambaye angejaribu kukimbia. Alijua kuwa saa yake imefika, muda ambao angejikabidhi mikononi mwao, “Kila siku nalikuwa mbele yenu hekaluni nikifundisha, msinikmate; lakini haya yamekuwa ili maandiko yapate kutimia” (Mark 14:49). Kulikuwa na nafasi nyingi kabla, lakini huu ulikiwa ndiyo wakati uliokuwa umepangwa Mungu. Walirudi nyuma wakati aliposema. Kwa hiyo akasema, mara “7 nimewaambia, ni mimi, basi ikiwa mnanitafuta mimi, wachane hawa waende zao” (Yohana 18:8).
Kama Mchungaji Mwema, angeutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake. Kwa hiyo wakamfunga Yesu na wakampeleka kwa Anas; baba mkwe wa Kuhani Mkuu. Lakini wanafunzi wake wote “walimwacha, na kukimbia” (Marko 14:50).
FUNDISHO KWETU
Habari hii ni ya huzuni namna gani, na bado huu ulikuwa ndiyo mwanzo wa mateso mazito ambayo yalikuwa mbele. Kwa kawaida asili yetu ni dhaifu. Hata pamoja na nia nzuri mara nyingi tunasanguka na kushindwa wakati matatizoyanapotukkabiri ili tusimame sawasawa. Yuda alishindwa, lakini alipanga kabla. Hapana rehema juu yake. Petro na mitume wengine walishindwa, lakini walipenda kutenda mema. Katika maisha yao baadaye walijifunza nguvu ya maombi kama Yesu alivyowafundisha. Mara nyingi Mungu aliwaimarisha kwa njia ya maombi ili kwamba waweze kushinda udhaifu wao, na wakaongea kwa ujasiri habari za Kristo na wakageuza wengi wakamwamini. Sisi, pia, ni lazima tuendelea kujaribu kuyafanya mapenzi ya Mungu hata baada ya kushindwa. Mungu atatutia nguvu sisi kwa njia ya Neno lake namaombi, kama tuna nia ya kumtumikia na kuonyesha nia ya kujifunza.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Yesu na wanafuzi wake walikwenda wapi baada ya kuondoka kile chumba cha juu?
2. Yesu alifanya nini katika Bustani?
3. Yesu alipowakuta wanafunzi wamesinzia aliwahimiza wafanye nini?
4. Yesu pale katika busatani alikwenda kuomba mara ngapi?
5. Ni nani aliyemtia nguvu Yesu pale?
6. Ni nani aliyeingia ghafla pale kwenye bustani?
7. Ni nani aliyeongoza njia?
8. Palitokea nini wakati Yesu alipowaambi maaskari, “Ni mimi?”
9. Ni kwanini Yuda alimbusu Yesu?
10. Ilitokea nini wakati Petro alipochomoa upanga?
11. Ni kwanini Yesu alimwambia kuurudisha upanga wake?
12. Yesu alijisalimisha mwenyewe kwa maaskari.Aliwaombea nini wanafunzi Wake?
13. Wanafunzi wote walifanya nini wakati maaskari walipomkamata Yesu?
14. Mwisho Yesu alifanya nini?
15. Yesu na wanafunzi wake walikwenda Bustani ya Gestimani baada ya chakula cha
mwisho cha usiku?
(a). Eleza Yesu alifanya nini pale?
(b). Eleza wanafunzi walikuwa wana fanya nini?
(c). Sema jinsi Yuda alivyomsaliti Yesu?
16. Wakati maaskari wlipotaka kumkamata Yesu.
(a). Wanafunzi wake walitaka wafanye nini?
(b). Petro alifanya nini?
(c). Ni kwa nini Yesu alimkemea Petro?
(d). Wanafunzi wake mwishoni walifanya nini?