CSSA 1-4-23 - THE CRUCIFIXION

Swahili

98. KUSULUBIWA MSALABANI

“Baba, uwasamehe;kwa kuwa hawajui walitendalo”.

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi Yesu alivyosulibiwa na kuzikwa. Mara tu baada ya Pilato kukubali Yesu asurubiwe, ndipo maaskari walipomtendea Yesu kama vile mharifu wa kawaida kabisa. Ndipo wakamtendea jeuri au kwa ukatiri na wakamdhihaki. Wakamvalisha nguo ya zambarau na pia wakamvalisha taji ya miiba kichwani pake na ndipo wakamfanyia dhihaka kana kwamba wanamheshimu wakiinamisha vichwa na kusema, “Salamu Mfalme wa Wayahudi”. Pilato mwenyewe hakuwa na raha, lakini alipojaribu kwa mara ya mwisho kufafuta nafasi ya kumwachilia Yesu, Wayahudi alimwita tena na kumwambia, “kama wewe ukimwachilia mtu huyu basi ujue kuwa wewe siyo rafiki wa Kaisari”. Pilato akapima uzito atapoteza nini ikiwa atawakasirisha Wayahudi, akawakubalia. (Yohana 19:16-42; Mathayo 27:31-60; Marko 15:20-27; Luka 23:26-53

 

WAKAMPELEKA GOLGOTA

Waliandaa mti mkubwa sana ambao Yesu alilazimishwa kubeba na akapita mitaani na kuelekea upande wa kaskazini ya mji, kwenda mlima wa Golgota. Na wafungwa wengine nao ilikuwa ni lazima wasurubiwe siku hiyo hiyo. Na sasa Yesu akawa amechoka sana. Hakuna amelala usiku mzima na kwa zamu akawa akihojiwa na watu hao waovu, maaskari wakimdhihaki na pia wakimpiga kumsukuma kwa nguvu. Alikuwa na nguvu kidogo za kuweza kuubeba msalaba wake. Wakamkuta mtu mmoja njiani, aliyeitwa Simoni, Mkirene, wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu. Nyuma yao baadhi ya wanawake walikuwa wakiwafuata, wakilia na kuomboleza. Yesu akageuka na akawaambia: “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi; bali jililieni nafsi zenu, na watoto wenu” (Luka 23:28). Alifahamu hakika taabu iliyokuwa inakuja kwa Yerusalemu, kwa sababu walikuwa wamemkataa na kumwua Masiya wao.

 

YESU ANASULUBIWA

Ilikuwa yapata kama saa 3 za asubuhi, Yesu kwa ukatili wakampigilia misumari mikononi na miguuni kwenye ule mti.Na maaskari wakauinuia na kuweka mti ule ndani ya shimo na kuusimamisha juu na wakamwacha Yesu afe juu ya mti huo. Wezi wawili wakasurubiwa pamoja naye, mmoja alikuwa upande wa mkono wa kulia na mwingine upande wa kushoto wa Yesu. Juu ya msalaba Pilato aliandika maandishi, yaliyoyandikwa kwa Kiebrania, Kiyunani na Kirumi, ili kwamba kila anayepita hapo aweze kusoma: “YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”, na wakuu wa makuhani waliposoma anwani hiyo, walitaka Pilato abadilishe. Wakamwambia, “Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema kwamba, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi”. Lakini hakukubali. Akajibu, “niliyoandika, nimeyaandika”(Yohana 19:19-22).

 

BABA, UWASAMEHE

Hata alipokuwa katika uchungu mkubwa mno wa mateso na maumivu sana,Yesu alikuwa kimya na mwenye mawazo mazuri. Alimfikiria Baba yake Mbinguni na akakumbuka aliyoandikiwa katika Zaburi na manabii kuhusu mateso yatakampata. Hatimaye kwa upole na akasamehe, akawatazama watu ovu waliokuwa wamemzunguka akaomba: “Baba, uwasame, kwa kuwa hawajui watendalo” (Luka 23:34). Na hivi ndivyo, alikuwa amefundisha wanafunzi wake, aliposema, “wapendeni maadui zenu, wabrikini wanaowalaani... nawaombeeni wanaowaudhi na kuwatesa” (Mathayo 5:44).

 

ALIDHIHAKIWA NA WATU

Watu watatu walisulibiwa hadharani,ili kwamba waliokuwa wanapita njiani wawaone na wengine wakasimama kutazama.Wengine walimtukana,na kumdhihaki.“Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu shuka msalabani” (Mathayo 27:40). Wakuu wa makuhani na waandishi na wazee wakamdhihaki. “Aliwaokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni mfalme wa Israeli na ashuke msalani, nasi tutamwamini” (Mathayo 27:42). Maaskari wanne waliokuwa wamewekwa pale kulinda wakagawana nguo zake kuwa “zawadi” zao. Na walipofikia kanzu yake, ambayo ilikuwa imefumwa tangu juu, ilikuwa haikushonwa, wakaipigia kura (Yohana 19:23-24).

 

MTAZAME, MAMA YAKO

Kati yao waliokuwa wakitazama lilikuwepo kundi dogo la waliompenda sana. Alikuwepo Yohana, mwanafunzi wake mpendwa, na Maria mama yake na baadhi ya wanawake waliokuwa wamemwamini. Maria mwanzo alikuwa ni mwenye furaha kwa miaka thelathini tatu na nusu, wakati Mwokozi-Mwana alipozaliwa, na sasa alitakiwa ashinde huzuni kubwa. Kwa ajili ya kuwatunza wengine kama alivyokuwa akifanya Yesu akamwambia Yohana amtunze Maria, ambaye naye kuanzia saa hiyo akampeleka nyumbani kwake (Yohana 19:25-27).

 

IMEKWISHA

Ilikuwa yapata kama muda wa mchana, ambapo kwa kawaida jua linakuwa lina angaza sana, giza nene likaifunika nchi yote. Kukatokea ukimya wa ajabu kwa muda. Giza lilidumu kwa muda masaa matatu, ndipo Yesu akasema maneno yake ya mwisho, “Imekwisha”, na akainamisha kichwa chake, akakata roho (Yohana 19:30). Ghafla tetemeko la ardhi likaitetemesha nchi. Miamba ikapasuka na mawe ambayo yaliyokuwa yamefunika baadhi ya makaburi yakafumuka, makaburi yakabaki wazi. Mwisho miili ya watakatifu ikafufuka (baada ya Yesu kufufuka) na wakauingia mji wakawatokea wengi. Ilikuwa ni wakati huo huo Yesu alipokufa, makuhani waliomsulubisha Masiya wao walikuwa karibu kumchinja mwanakondoo wa Pasaka katika ua wa nje wa hekalu, pazia la hekalu, lililokuwa katikati ya chumba cha Patakatifu na Patakatifu pa Pataktifu lilichanika kutoka juu mpaka chini. Hakuna mkono wa mtu ambao ungeichana hivyo (Mathayo 27:51-53). Nje ya mji, pale Golgota, akida, Mrumi, aliyekuwa akimlinda Yesu alishangazwa na mambo aliyoyaona na yaliyofanyika na kwa jinsi Yesu alivyokuwa kimya akiyavumilia yote. Wakati Yesu alipolia kwa kupaza sauti kwa Mungu na ghafla kufa, akida alijua kwamba ameona mambo ya ajabu ambayo yalimfanya aogope sana. Aasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu” (Marko 15:39).

 

MAZISHI

Saa 12 usiku huo, ingeanza siku maalumu ya sabato. Sasa, Wayahudi wakiwa wamefanikiwa kile walichokitaka, wakamwambia Pilato ili waishushe miili chini.Kwa hiyo maaskari walikwenda kuivunja miguu ili kuharakisha kifo, lakini walipokwenda kwa Yesu, walishangaa walimkuta amekwisha kufa tayari, basi hawakumvunja miguu. Sawa na mwanakondoo wa Pasaka usiku ule wana wa Israeli walipoondoka Misri, wala hakuna mfupa uwao wote utakao vunjwa (Kutoka 12:46). Mmoja kati ya maaskari akachukua mkuki na kumchoma ubavuni mwake, na mara ikatoka damu na maji, lakini Mungu alikuwa ni wa rehema kwa Mwana wake maana tayari alikuwa amekwisha kufa (Yohana 19:31-34). Akaja mzee wa baraza mwingine wakati huo kwa Pilato. Alikuwa Yusufu wa Arimathayo. Alikuja kuomba apewe mwili wa Yesu, aushushe na kumzika. Pilato akakubari, na Yusufu akiwa na Nikodemu wakauweka mwili ndani ya sanda ya kitani pamoja na yale manukato. Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani, na ndani ya bustani mna kaburi jipya wakamzika ndani ya “kaburi jipya ambalo mtu yeyote hajazikwa ndani yake” (Yohana 19:38-42). Kwa hiyo Yusufu na Nikodemu, wote sasa wakiwa wanafunzi wa Yesu, wakimheshimu kutokana na kifo chake. Na baadhi ya wanawake wakiwa katika kundi dogo waliwafuata kuona mahali mwili wake ulipozikwa, wakikusudia kurudi wakiwa na manukato na marhamu ya kumpaka baada ya siku ya sikukuu kuisha.

 

FUNDISHO KWETU

Wakti Yesu alipokufa msalabani, alitimiza maisha ya utii wa ukamilifu kwa Baba yake, na kwa sababu hii, Mungu akamfufua kutoka kwa wafu na kumpatia uzima wa milele. Utii ndiyo ambao Mungu anautegemea kwa watoto wake wote.Yesu alisema; “Mtu akinipenda atalishika neno langu, na Bab yangu atampenda” (Yohana 14:23). Kwa dhabihu yake, Yesu akawa amefungua njia ya uzima wa milele kwa ajili yetu. Ndiye peke yake aliyestahili kuupata, na Mungu atawapatia thawabu ya aina moja yaani uzima wa milele kwa wote wanaomfuata mpaka mwisho. Kama tutamwamini na kumtii yeye uwezo wetu wote, Mungu atatusamehe dhambi zetu na kutuwezesha tuweze kuyakabili mateso yatakayokuja mbele yetu. Jinsi Mungu alivyotuonyesha pendo lake kwa kutupatia Mwana wake wa ampendaye kuwa dhabihu kwa ajili yetu, ili tuweze kuokoka. Yesu alimwambia upendo mkuu wa Mungu kwa ajili yetu: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Yesu alifahamu sana mambo mengi kuhusu kusulubiwa kwake kutoka katika maandiko ya Agano la Kale.Yalinganishe maandiko na yale yaliyotoke

 

1.

“Wote wanionao hunicheka sana, hunidhihaki...   wakisema, Umtegemee BWANA; naamponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye”.

 

Zaburi 22:7-8

“Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki, pamoja na waandishi na wazee, akisema... Amemtegemea Mungu na amwokoe kama anamtaka kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu”

Mathayo 27:41-43.

2.

“Wamenizuia mikono yangu na miguu yangu”

 

Zaburi 22:16

Walimsulibisha, na kwa kufanya hivyo wakampigilia mikononi na miguuni

 

Mathayo 27:35.

3.

“Wanagawana nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura.

 

Zaburi 22:18

Maaskari wakagawana nguo kati yao na vazi lake wakalipigia kura.

 

Yohana 19:23-24.

4.

“Alidharauliwa na kukataliwa na watu”

 

Isaya 53:3

Walimkataa kuwa siyo mfalme wao

 

Yohana 19:15

 

5.

“Alionewa, nakuteswa wala hakufunua kinywa chake”

 

Isaya 53:7

Pilato alipomwuliza Yesu, “Yesu hakumjibu lolote”, ingawaje Pilato alikuwa amemtesa kwa kumdhihaki.

 

Yohana 19:1-106.

6.

Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya, na pamoja na matajiri katika kufa kwake

 

Isaya 53:9

Yesu alisulibiwa katikati ya wahalifu (Luka23:32)

Na akazikwa katika kaburi la mtu tajiri, Yusufu wa Arimataya.

Yohana 19:38-41

Mathayo 27:57-60

 

Kutokana na vifungu hivi vya Agano la Kale tunaweza kuona uhakika wa unabii ulivyotabiri sawasawa na jinsi kusulibiwa kwa Yesu kulivyokuwa. Wana wa Israeli walimkataa Masiya wao, lakini watamtambua atakaporudi kwao. “Watamtazama yeye ambaye walimchoma” na watauliza, “Je! jeraha hizi ulizonazo kati ya mikono yako ni nini?”. Na ingawa alimkataa Yesu, watampokea kumweka kuwa Masiya na Mfalmewao. Ni wakati mzuri ulioje wa kuutazamia kuuona (Soma Zekaria12:10; 13:6).

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Yesu alisulibiwa wapi

2. Ni kwa nini Yesu aliwaambia walilie nafsi zao wenyewe

3. Ni nani waliosulibiwa kila upande wa Yesu

4. Juu ya msalaba wake yaliandikwa maneno gani

5. Ni maneno gani ya ajabu aliyosema Yesu alipokuwa msalabani kuhusu wale waliomwua

6. Je, wapita njia walimwambia nini

7. Jinsi gani wakuu wa makuhani walivyomdhihaki Yesu

8. Ilitokea nini kwenye vazi la Yesu

9. Ni yupi ambaye Yesu alimwambia amtunze mama yake

10. Ni mambo ya ajabu yaliyotokea ilipokaribia kuwa mchana

11. Maneno ya mwisho ya Yesu ni yapi

12. Ni jambo gani la ajabu lililotokea katika hekalu Yesu alipokufa

13. Ni nani waliomzika Yesu

14. Katikati ya mateso yake  msalabani, Yesu aliwakumbuka wengine. Ni jinsi gani alivyoonyesha

       upendo wake kwa:

a. Maadui zake

b. Mama yake

c. Baba yake wa mbinguni

 

Majibu ya Kina

15   a. Fafanua mambo mapya yaliyotokea wakati Yesu alipokuwa juu ya msalaba

      b. Akida yule wa Rumi aliyeona mambo hayo mapya aliserma nini?

16. Wayahudi walitaka miili ya waliokufa kwa kusulibiwa ishushwe na kabla ya ya kuwa   

      usiku.Eleza ilivyotokea na jinsi Yesu alivyozikwa.

 

Majibu ya Nyongeza

17. Eleza unabii tatu katika Agano la Kale zilizotimizwa wakati kifo cha Yesu.

 

Swahili Title
098 KUSULUBIWA MSALABANI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type