- KUTESWA KWA AJILI YA KWELI
“Imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi”
Shabaha
Ni kuonyesha jinsi Paulo na Barnaba walivyohubiri injili kule Listra, Ikonia na Derbe na namna Timotheo alivyofanyika wanafunzi. Ukiangalia ramani ya safari ya kwanza ya Pulo, utaona kwamba yeye na Barnaba walitembelea miji mitatu zaidi kabla ya kuanza kugeukia kuelekea Antiokia nchini Syria ambako walikuwa wametokea mwanzoni. Walikuwa wamefukuzwa kutoka Antiokia nchini Pisidia na Wayahudi wenye hasira ambao waliona wivu kutokana na jinsi watu walivyopenda ujumbe wa wanafunzi. Waliendelea na safari, wakihubiri Injili na kuyaweka maisha yao hatarini, lakini Mungu alikuwa amewatuma nao waliendelea kwa ujasiri kuifanya kazi ambayo Mungu alikuwa amewaitia.
Matendo ya Mitume 14
IKONIO (mistari 1- 7)
Huko Ikonio, waliingia katika Sinagogi siku ya sabato na kuhubiri Injili kwa Wayahudi. Haikuwa shida kamwe kuweza kuwapata watu waliopenda kuipokea habari njema ya wokovu, lakini walikuwapo kila wakati Wayahudi wasioamini ambao walisababisha ghasia itokea. Kwa hiyo ilikuwa ni huko Ikonia ambako “Kundi kubwa la watu wengi wakaamani” (mstari 1), lakini Wayahudi wasioamini pamoja na watawala wao wakakusudia mabaya ili kuwapiga mawe ndugu. Barnaba na Paulo wakapata habari, wakakimbilia Listra, ambayo ilikuwa umbali yapata kama kilometa 30 kutoka huko.
LISTRA (mistri 8 – 12)
“Na huko wakaihubiri Injili” (mstari 7). Wakamkuta huko Listra mtu mmoja dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mama yake ambaye alikuwa hajawahi kutembea. Alikuwa akikimsikiliza sana Paulo kwa makini, ambaye Paulo akatambua kwamba mtu huyo alikuwa na imani ya kuponywa. Mtume akamkazia macho yule kiwete na katamka kwa sauti kuu “Simama sawasawa kwa miguu yako”. Kwa mshangao wa watu wote waliokuwa wamekusanyika siyo kwamba kiwete alisimama tu bali aliruka ruka na kutembea. Aliponywa kabisa. Watu wa Listra wakashangaa sana. Waliona waziwazi kuwa kwamba miujiza ya aina hiyo isingeweza kufanywa na mtu wa kawaida. Hata hivyo, hawakumwamini Mungu wa Israeli, na wala wasingeweza kuelewa kwamba Mungu alikuwa amewapatia Mitume wake nguvu za Roho Mtakatifu ili kuwasaidia watu waweza kuiamini Kweli. Na mkutano wakapaza sauti zao “miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu”. Wakaendelea kupiga kelele kwa lugha yao ya kienyeji. Palikuwa na hekalu la ibada ya sanamu nje ya mji nao walifikiri kwamba Paulo na Barnaba walikuwa ni miungu yao miwili ambao walikuwa wamefika kutembelea hekalu lao. Wakamwita Paulo Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji, na Barnaba wakamwita Zeu ambaye kwa Wayunani alikuwa ni mkuu kati ya miungu.
WATU WANAMWABUDU PAULO NA BARNABA (mistari 13 – 18)
Kila mmoja mjini alifurahi sana, na kuhani wa Zeu akaleta ng’ombe dume na taji za maua malangoni pa mji, akijitayarisha kutoa dhabihu kwa heshima ya Paulo na Barnaba. Paulo na Barnaba wakaanza kutambua yaliyokuwa yakitokea nao wakasikitika sana. Hawangeweza kuruhusu jama kama hilo litokea. Maana Mungu peke yake ndiye aliyestahili kuabudiwa! Wakararua ngua zao na kuingia katika makutano, wakipiga kelele wakisema “Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali mojana nyinyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo” (mstari 15 – 17). Iliwapasa kusema maneno mengi sana kabla watu wa Listra kuweza kuelewa kwamba walikuwa kwa hakika watu wa kwaida na wala siyo kuwa walikuwa miungu.
MATESO ZAIDI KUTOKA KWA WAYAHUDI (mstari 19 – 20)
Wakati huo huo Wayahudi waliotokea Antiokia na Ikonio walikuwa bado wana hasira sana na Paulo na Barnaba nao wakafika Listra kuchochea watu dhidi yoa. Watu wa Listria kwa sasa walikuwa wamefaidhaika juu ya sherehe walizokuwa wametaka kuwafanyia Paulo na Barnaba. Wakati Wayahudi wenye hasira walipofika mjini kwao, kwa upesi wakasahau mwujiza wa ajabu wambao Paulo alikuwa ameutenda katikati yao, nao kwa haraka wakawa adui zake. Hisia zao zilichochewa mno, hata ikawa kwamba wakampiga mawe Paulo na kumburuta nje ya mji, wakidhania kuwa amekwishakufa. Wanafunzi wenye hofu wakamkusanyikia lakini kwa furaha kuu, wafahamu kuwa Paulo hakuwa amekufa. Wakamsaidia kusimama kwa miguu yake wakarejea mjini, bila shaka wakishangilia kwamba Mungu, alikuwa amemwokoa kutoka katika kifo kutoka mikononi mwa hawa watu waovu.
PAULO ANAZIIMARISHA EKLESIA MPYA (mstari 21 – 28)
Siku iliyofuata mitume wakaondoka kwenda Derbe, ambao ulikuwa ndiyo mji wa mwisho katika safari yao. Walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule na “kupata wanafunzi wengi” (mstari 21) wakarejea eklesia mpya walizokuwa wamezianzisha huko Listra, Ikonio na Antiokia. Ujumbe wao maalumu kwa kila eklesia ulikuwa ni “imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi” (mstari 22). Jinsi walivyokuwa mfano mkuu hawa ndugu wawili waliopitia mateso mengi wakati walipokuwa wakiihubiri Injili. Michubuko katika mwili wa Paulo ilikuwa wazi kwa wote na wanafunzi wapaya walifahamu kabisa kwamba michubuko hiyo ilikuwa ni kwa ajili yao Paulo na Barnaba walivumilia mateso mengi. Hivyo wakifanya imara za wanafunzi “kuendelea katika imani” nao ndugu hao wawili wakaendelea na safari yao, wakaenda eklesia moja hadi nyingine mpaka wakafika Antiokia huko Syria. Huko wakawakusanya wanafunzi pamoja na wakawaeleza “mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani” (mstari 27). Ingawaje walikuwa wamepata dhiki nyingi sana, walielewa kuwa Mungu alikuwa pamoja nao na kubariki kazi.
MWANAFUNZI TIMOTHEO (Matendo ya Mitume 16: 1 – 3)
Safari hii ya kwanza ingemwacha Paulo na kumbukumbu nyingi, ambazo ni za aina mbili; za furaha na za kusikitisha. Lakini miongoni mw wanafunzi wote aliowapata, kijana mmoja alimtea Paulo furaha katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia. Kijana huyo alikuwa Timotheo, Aliishi Listra mahali ambapo Paulo alipopigwa mawe na kudhaniwa kuwa alikuwa amekufa. Huenda Timotheo aliliona tukio hili lilipotendeka. Alikuwa amefundishwa Maandiko na mama yake na bibi yake tangu alipokuwa mtoto (2 Tim. 3:15) na alikuwa amebatizwa wakati Paulo alipohubiri pale Listra. Mtume alitokea kumpenda sana Timotheo na akapenda kuwa naye huyu mwanafunzi kijana. Na baadaye Timotheo alikwenda na Paulo katika safari zake. Wakati Paulo alipokuwa gerezani, katika siku za mwisho wa maisha yake alimwandikia Timotheo barua inayopendeza sana akimwimarisha moyo katika imani na kumwambia aende kumwona.
FUNDISHO KWETU
Paulo na Barnaba walikuwa watu wenyenyekevu sana. Wakati watu wa Listra walipotaka kuwaabudu, waliwafundisha wale watu kwamba sifa zote anapaswa kupewa Mungu peke yake. Na sisi tujifunze kwamba yote tunayoyatenda ni lazima iwe ni kwa utukufu Mungu na wala siyo sisi kujipatia sifa wenyewe. Kama tunavyosoma kuhusu mateso ya Paulo, tunatambua kwamba siyo rahisi kufuata njia ya Mungu na kwamba ni “katika njia ya dhiki nyingi” (majaribu au mateso) ili kwamba tuweze kuingia Ufalme wa Mungu. Mungu atatusaidia sisi kuvumilia mateso kama tukimwekea Mungu tumaini kama Paulo alivyofanya.
MAELEZO YA NYONGEZA
Tunaweza kuona mambo yote ambayo Bwana Yesu alimtabiria Paulo yakitimia katika maisha yake “Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu” (mstari 9:16). Baada ya kuongoka kwa kuiamini Injili, Paulo ni lazima sasa apate mateso kwa ajili ya Jina la Yesu Kristo, kama alivyowafanya wengine kuteseka mno siku za nyuma (Matendo ya Mitume 8:3). Paulo baadaye alimwandikia Timotheo, “wewe umeyajua ... adha, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, katika na Listra kila aina ya adha niliyoistahimili; naye Bwana aliniokoa katika hayo yote” (2 Timotheo 3:10 – 11). Siyo mara nyingi wanafunzi kukabiliana na kitendo cha kupigwa mawe au mateso ya nguvu siku hizi, kama mitume walivyofanyiwa. Shida zinazotukabili leo mara kwa mara kutokana na ushawishi kutoka kwa wanafunzi tunaosoma nao ili tuweze kufanya yale wanayoyafanya-tuvae kama wanavyopenda kuvaa, tutembee sehemu wanazozipenda kutembelea, tusikilize aina ya “muziki” wanaoupenda kuusikiliza, tusoma vitabu na magazeti wanayoyapenda wao, kutazama televisheni, tufuatane na wao katika michezo wanayoipenda wao. Hayo ni aina ya mateso au ushawishi ambao unakuwa ni vigumu kwetu kuweza kuyavumilia. Paulo alimtia moyo yule kijana Timotheo kushiriki mateso, kama askari mwema Yesu Kristo (1 Timotheo 2:3). Akamwambia Timotheo kuhusu “nyakati za hatari” ambazo zingekuja, na hizi ndizo nyakati zetu hizi ambazo tunaishi; kabla ya kurudi kwa Kristo. “Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kutukana, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi ... wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu”. Onyo la Paulo kwa Timotheo ni onyo kwetu sisi sote na ushauri wake wa busara ulikuwa: “hao nao ujiepushe nao” (2 Timotheo 3:1- 5). “Maandiko Matakatifu” ambayo Timotheo alijifunza kutoka kwa mama yake na bibi yake yanaweza: “kutuhekimisha hata kupata wokovu” (2 Timotheo 3:15 -17). Na tumchukue Timotheo kuwa mfano wetu, ili tuwezekushiriki furaha ile atakayokuwa nayo katika Ufalme wa Mungu.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Wayahudi wasioamini waliwatendaje Paulo na Barnaba kule Ikonio?
2. Je, Paulo alifanya mwujiza gani kule Listra?
3. Watu walitaka kufanya nini walipouona mwujiza huu?
- Watu walifikiri Paulo na Barnaba kuwa walikuwa ni nini?
- Nini kilimtokea Paulo kule Listra?
- Ni kijana gani mwanafunzi aliyekuwa mwelewa,kutoka Listra?
- Ni ujumbe gani maalumu wa Paulo kwa eklesia mpya baada ya matatizo yake huko Listra?
Majibu ya Kina
- Kule Listra Paulo alimponya mtu aliyekuwa kiwete.Eleza nini kilitokea baadaye?
- Mwanafunzi mmoja wa Listra aliyekukuwa rafiki wa Paulo katika maisha yake yote yaliyobakia. Eleza yote
unayoyafahamu kuhusu mwanafunzi huyo.
Majibu ya Nyongeza
- Paulo alimwambia Timotheo kwamba “nyakati za hatari” zitakuja.
- Alisema watu wangekuwa wanamna gani?
- Ni ushauri gani wa busara aliutoa Paulo?
- Timotheo alijifunza nini kilichomsaidia kuvumilia?
- a) Eleza ni jinsi gani Paulo alivyoteseka kule Listra.
b) Ni aina gani ya mateso unayoyaona kuwa ni magumu kwako? Eleza mifano miwili
c) Ni kipi tunaweza kusoma ili kitusaidia kutenda kwa hekima wakati tunamgonjea kurudi kwa
Kristo?