CSSA 2-2-06 - THE NEW LEADER

Swahili

156. KIONGOZI MPYA

“Kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja nawe"

Wana wa Israeli walipiga kambi katika nchi tambarare za Moabu na kungojea wakati wa kuingia katika urithi wao. Musa, kiongozi wao mkuu hakukaa bila cha kufanya. Aliandika kitabu cha Kumbukumbu la Torati na kuwataka watu watii ujumbe wake. “Uwe hodari na moyo wa ushujaa,” aliwaambia, “kwa maana hatakupungukia wala kukuacha” (Kumb. 31:6). Mojawapo ya matendo yake ya mwisho ilikuwa kumteua Yoshua kuwa mrithi wake na kumsihi awe hodari na jasiri, “kwa maana, ni lazima uende pamoja na watu hawa hadi kwenye nchi” (Kumb. 31:7-8).

Kumbukumbu la Torati 34; Yoshua 1-4

KIFO CHA MUSA.

Wakati ulikuwa umefika wa kiongozi mkuu kufa. Musa alikuwa bado mtu hodari lakini kazi yake ilikuwa imekamilika (Kumb. 34:7). Alipotoka katika kambi ya Israeli, alipanda Mlima Nebo, na hapo mbele yake palikuwa na nchi ya ahadi. Chini yake kulikuwa na kambi ya Israeliiliyogawanyika katika sehemu nne, ikingojea amri ya kusonga mbele. Upande wa pili wa Yordani ungeweza kuonekana jiji la ngome la Yeriko, ufunguo wa kuingia kwa nchi ya ahadi. Zaidi ya Yeriko ilitandaza milima ya Palestina, vilima pacha vya Ebali na Gerizimu, bonde lenye rutuba la Shekemu. Kulikuwa na vilima vya Yudea na ngome yenye nguvu ya Yebusi ikisimama juu ya kile kilichoitwa baadaye Mlima Sayuni. Musa alipotazama mandhari hii alijua kwamba, ingawa hangewaongoza watu kuingia katika nchi ya ahadi, siku moja angesimama ndani ya mipaka yake. Akiwa na Ibrahimu na wale wengine waliostahili, chini ya uongozi wa Bwana Yesu, ataingia katika urithi wake. Kama wengine wengi, Musa “alikufa katika imani, bila kuipokea ile ahadi, bali ameiona tokea mbali." . ” ( Waebrania 11:13 ). Kifo kilimjia shujaa huyu wa imani upesi, na malaika akamzika bondeni katika nchi ya Moabu, na “hakuna mtu ajuaye kaburi lake hata leo” (Kumb. 34:6).

Musa alikuwa mfano wa Bwana Yesu Kristo. Mungu akamwambia, "Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumb. 18:18). Linganisha maneno haya na Matendo 3:22-23 na 7:37. Tunapomfikiria Musa katika kuwaongoza Waisraeli, kuwajali watu, kuwasihi kwa niaba yao, kubeba dhambi zao, kuwaunga mkono, kuwaongoza jangwani kuelekea Nchi ya Ahadi na kuwafundisha sheria za Mungu, kwa njia hizi na nyinginezo nyingi. ona kazi ya Bwana Yesu Kristo iliyoonyeshwa kimbele.

Lakini mfano huo haukuwa kamili katika Musa, na hivyo mtu mwingine alichaguliwa kuwapa urithi wao, Yoshua. Mungu alipomzika mfanya kazi wake, ndivyo Yoshua alichukua jukumu hilo. Ingawa mafundi hufa na hivyo kuweka chini zana zao, kazi lazima iendelee. Kazi kuu ya kuhifadhi njia ya maisha katika enzi hii ni wajibu wa kila mtu anayetafuta kumfuata Bwana Yesu Kristo “katika roho na Kweli”. Na ni kwa yeye aliye mkuu kuliko Yoshua, Bwana Yesu Kristo, kwamba tutaingia katika urithi wetu, Ufalme wa Mungu.

YOSHUA-KIONGOZI MPYA.

Kulikuwa na wanaume wawili katika kambi ya Israeli waliokuwa wameonyesha imani na ujasiri wa pekee, Yoshua na Kalebu. Kati ya wanaume wote waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 20 walipotoka Misri, ni wao pekee walioingia katika Nchi ya Ahadi. Kati ya hawa wawili, Yoshua alichaguliwa kuwa kiongozi. Alikuwa na sifa hizi muhimu.

  1. Alikuwa na UJASIRI—kwa kuwa hilo lilikuwa limedhihirika alipowaongoza Israeli vitani (Kutoka 17:8-16).
  2. Alikuwa na IMANI—kama alivyothibitisha wakati yeye na Kalebu walipopinga ripoti isiyo na imani ya wale wapelelezi wengine kumi.
  3. Alikuwa na HEKIMA—kwa maana hii alikuwa amepewa (Kumb. 34:9).
  4. Alikuwa na UZOEFU—kwa kuwa mara kwa mara alikuwa kando ya Musa katika majaribu yote ya jangwani.

Jina "Yoshua" lilionyesha utume wake, kwa maana "Yahwe ni wokovu." Jina la Kiyunani "Yesu" katika Agano Jipya linamaanisha sawa na "Yoshua" ya Kiebrania katika Agano la Kale (tazama Matendo 7:45; Waebrania 4:8 - pambizo). Yoshua alikuwa kweli, Mwokozi wa Israeli, na mfano wa Bwana Yesu ambaye ni Mwokozi wetu, na "mkuu wa wokovu wetu."

Mungu alimwambia Yoshua kwamba yeye na watu wote walipaswa kuvuka Yordani hadi nchi ya urithi wao, nchi iliyoahidiwa kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo (Yoshua 1:6), alimhakikishia Yoshua msaada wake (m. 5). Alimpa msingi wa mafanikio: “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; NJIA YAKO IMEFANIKIWA, NDIPO UTAPATA MAFANIKIO MEMA." Na hiyo ni kanuni ya msingi kwa mafanikio yetu pia.

Yoshua aliagiza maofisa waone kwamba Israeli wana chakula kwa siku tatu wakiwa tayari (Yoshua 1:10-18).. Makabila ya Rubeni, Gadi, na nusu ya Manase yalikumbushwa agano lililofanywa siku za Musa. Walikuwa wameomba nchi ya Gileadi, mashariki mwa Yordani, kwa urithi wao, na waliahidiwa kwa sharti kwamba kwanza wasaidie ndugu zao kupigana na Wakanaani (Hesabu 32:1-5; 5:29-30). Makabila haya yalikubali kwa urahisi kusaidia katika ushindi huo.

MAJASUSI KATIKA YERIKO (Yoshua 2).

Kabla ya kuvuka Mto Yordani, Yoshua akawatuma wapelelezi wawili kutoka kambini huko Shitimu. Walikuwa wamejificha katika nyumba ya Rahabu ambaye nyumba yake ilikuwa imejengwa juu ya kuta za jiji, na alikuwa amewalinda wakati Mfalme wa Yeriko alipotaka kuwateka. Rahabu alikuwa amesikia habari za maajabu ambayo Mungu alikuwa amefanya, na akakiri imani yake kwa Mungu (Yoshua 2:9-11; Waebrania 11:31). Kama thawabu kwa ajili ya fadhili na imani yake wapelelezi waliahidi kwamba yeye na familia yake wangeokolewa. Wapelelezi walirudi katika kambi ya Israeli wakiwa na maneno ya kutia moyo, “Hakika BWANA ameitia nchi yote mikononi mwetu; maana hata wenyeji wa nchi wamezimia kwa ajili yetu” (Yoshua 2:23-24).

FUNGU LA YORDAN (Yoshua 3).

Kwa siku tatu Israeli walipiga kambi karibu na kingo za Mto Yordani. Siku ya tatu waliamriwa wajitakase kwa sababu kesho Mungu alikuwa anaenda kufanya maajabu kati yao. Walipaswa kutafakari umaana wa kiroho wa kile ambacho kilikuwa karibu kutokia.

Sanduku lilikuwa ni ishara inayoonekana ya uwepo wa Mungu, na lilipovushwa Yordani, Israeli walielewa kwamba Mungu alikuwa akiongoza safari yao na angewapa ushindi juu ya mataifa saba ya Kanaani (Yoshua 3:10).

Wakati miguu ya makuhani waliokuwa wamebeba Sanduku ilipogusa maji, maji ya mkono wa kuume “yalirudishwa nyuma” kimiujiza ( Zaburi 114:3-5 ), na kuimarishwa ( Yoshua 3:16 ). Maji yale ya chini yalitoweka. Muujiza huo ulikuwa wa kushangaza zaidi kwa sababu wakati huo mto ulikuwa umefurika.

Lakini, muujiza huo una ulinganifu fulani wa kuvutia. Neno Yordani linamaanisha "Kushuka." Mto unashuka polepole kutoka bahari ya Galilaya (bahari ya maji safi) chini kupitia jiji, Adamu hadi Bahari ya Chumvi (Yoshua 3:16). Ni kama mfano wa maisha na kufa, unaoanza na uhai (ziwa la maji safi) na kupita kwa Adamu na hatimaye kupita kwenye kifo (Bahari ya Chumvi). Lakini, Sanduku la Agano (lililowakilisha Bwana Yesu) liliposimama katikati ya maji haya yanayoshuka, walirudishwa nyuma mpaka mji wa Adamu, kuelekea Bahari ya Uzima (tazama Yoshua 3:16; Zaburi 114:3). Maneno "mbali na mji wa Adamu" yanaweza kutafsiriwa "mbali katika Adamu" (R.S.V.). Kuvuka huku kwa maana sana kuingia katika Nchi ya Ahadi ni kielelezo cha ufufuko wa Kristo, kikihakikishia ufufuo wa kibinafsi wa watu wengi sana ambao wamekufa kwa imani na kuwahakikishia kuingia katika "Nchi ya Ahadi", yaani, Ufalme wa Mungu.

KUMBUKUMBU MBILI (Yoshua 4).

Yoshua aliamuru mtu aliyechaguliwa kutoka kila kabila kuchukua jiwe kutoka katika mto Yordani. Mawe hayo 12 yaliwekwa huko Gilgali, kambi mpya ya Israeli, kwenye ukingo wa magharibi mwa Mto. Ukumbusho wa pili wa mawe 12 uliwekwa katikati ya Yordani, moja kwa kila kabila (mst. 9).

Kumbukumbu hizi zilipaswa kuwafundisha watoto wa vizazi vilivyofuata hadithi kuu ya kupita Yordani ili daima waweze kuthamini uwezo mkuu wa Yeye aliyeipigania Israeli. 23, 24).

Makuhani walibaki wakiwa wameshikilia Sanduku la Agano juu, katikati ya Mto Yordani, mpaka “watu wote walipovuka” (Yoshua 3:17). Kisha wakabeba Sanduku juu kutoka kwenye mto, na Mto Yordani ukaanza tena mwendo wake wa kawaida, ukitiririka hadi Bahari ya Chumvi.

SOMO KWETU:

Baada ya kuvuka Yordani, Israeli walianza maisha mapya kama watu maalum wa Mungu katika nchi ya ahadi. Misri, nyika na maisha yao ya zamani, sasa walikuwa nyuma yao. Chini ya uongozi wa Yoshua katika Kanaani walikuwa na vita vya muda mrefu na vya mfululizo dhidi ya adui zao. Lakini, walishinda huku wakitii amri za Mungu. Kutokana na uzoefu wa Israeli tunaweza kuchukua somo.

Kristo akiwa Kiongozi wetu tunaanza maisha mapya. Tunavita ndefu ya kupigana dhidi ya tamaa ya asili na mambo ya kidunia, kwa kuwa wao ni adui zetu. Mungu atatusaidia kushinda mradi tunampenda na kumtii. Kama vile Israeli walivyopaswa kujitakasa, vivyo hivyo lazima sisi pia "tuwekwe wakfu", ili kujifunza kusudi Lake, na kutii amri zake. Kuvuka kwa kimuujiza kwa Mto Yordani uliofurika, kulionyesha umuhimu wa Kristo ambaye alirudisha nyuma wimbi la hali ya kufa na kuwawezesha wale ambao watapita katika maji ya ubatizo kupokea, kwa neema ya Mungu, urithi wa milele katika nchi ya ahadi - Ufalme wa Mungu.

 

MAKTABA YA MAREJEO:

"Hadithi ya Biblia" (H. P. Mansfield)—Kitabu. 2, nambari 9

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura ya 12, 13

"Mkono wa Mungu Unaoonekana" (R. Roberts)—Sura ya 21

"Joshua" (J. Ullman)

 

MASWALI YA AYA:

  1. Nini maana ya Kristo anapoelezewa kuwa nabii kama Musa?
  2. “Hawa wote walikufa katika imani, bila kuzipokea zile ahadi, bali wakaziona kwa mbali, na kuzishangilia. Onyesha jinsi Musa anavyolingana na maelezo haya.
  3. Ni sifa gani za tabia ambazo Yoshua alikuwa nazo ambazo zilimfaa kuwa kiongozi mpya wa Israeli?
  4. Yoshua alipewa maagizo gani alipowekwa rasmi kuwa kiongozi mpya wa Israeli?
  5. Jinsi gani na kwa nini Rahabu aliwasaidia wapelelezi wawili waliokuja Yeriko?
  6. Eleza matayarisho ambayo Yoshua alifanya kabla ya Waisraeli kuvuka mto Yordani.

MASWALI YA INSHA:

  1. Yoshua alishikilia sifa zinazohitajika kwa uongozi wa Israeli wakati wa kifo cha Musa. Eleza sifa hizo na maagizo ambayo Mungu alimpa Yoshua kwa ajili ya mafanikio yake.
  2. Eleza jinsi taifa la Israeli lilivyovuka kimuujiza Mto Yordani na uonyeshe maana wa tukio hilo kuwa mfano wa ufufuo.

 

Swahili Title
156 KIONGOZI MPYA
English files
African text
CSSA
Translator 1
Carl Hinton
Translator 2
Jacob Haule
Literature type
Sub type
Sub sub type