161. YAKOBO, HAKI YA MZAWA WA KWANZA NA BARAKA
Somo hili linaonyesha namna Mungu alivyompenda Yakobo kuliko Esau; na jinsi Mungu alivyoongoza maisha ya wote katika kutekeleza kusudi lake.
Mwanzo 25
ESAU NA YAKOBO
Wana wawili mapacha walizaliwa na Rebeka na Isaka baada ya unabii wa ajabu kuletwa kwao na Mungu (Mwanzo 25:23). Unabii ulifunua:-
- Mataifa mawili yangeanzishwa na hao wavulana wawili.
- Wangekuwa aina mbili za watu- mmoja mkali na mpenda vita atakayetafuta kumtawala mdogo wake, lakini hatimaye mkubwa angemtumikia mdogo.
Katika unabii huu, Mungu alionyesha maarifa yake juu ya namna hawa wavulana wangekuwa. Mungu alitambua kuwa Esau angekuwa asiye mcha Mungu, mtu apendaye mambo ya mwilini na asiye mheshimu Mungu, ambapo Yakobo angekuwa kinyume chake. Basi Mungu akapanga inavyopasa na kumchagua Yakobo kuwa ndiye ambaye kupitia kwake ahadi za Ibrahinu zingekua kwake (Warumi 9:10-13).
Angalia jinsi Sura 25:24-34 inavyothibitisha wa tendo la Mungu kuwa ni sahihi. Esau alikuwa mwekundu (kama udongo) na mwenye malaika nyingi mwilini (sura yake ilionekana hovyo) alipozaliwa (mstari 25). Yakobo alipozaliwa, alikamata kisigino cha Esau kama kwamba angempita na kuchukua nafasi ya kwanza (mistari 26). Hili lilisababisha aitwe Yakobo ikimaanisha “anayembadili” au “anayeshika kisigino” (kwa kusudi la kwenda kutaka kutangulia mbele). Hii hamu ya kuwa wa kwanza kushiriki baraka za Mungu ilibakia ndani ya Yakobo katika maisha yake yote. Esau alikuza kazi za ufundi wa mambo ya dunia (mstari 27) lakini Yakobo alikuwa mtu wa “kawaida” au “mcha Mungu”. Hili linatuonyesha ya kwamba alipendelea kutumia muda mwingi katika kukuza ufahamu ili kuzijua njia za Mungu. Lakini hakuwa mtu dhaifu. Maisha yake yanamwonyesha kuwa alikuwa mtu mwenye bidii na mwenye kukusudia ili kufikia lengo lake.
Kwa kweli alitaka urithi wa ahadi! Mstari 28 unaeleza kwa kina habari mbaya ya kwamba Isaka aliruhusu upendo wake kiasili kama mzazi kwa Esau ili kubatilisha ufahamu wake juu ya mapenzi ya Mungu. Rebeka alikuwa na ufahamu mkubwa sana na kuona ndani ya Yakobo mbegu ya kumcha Mungu. Isaka alijua kusudi la Mungu ya kwamba Yakobo alikuwa ndiye wa kupata zile ahadi. Hilo linaweza kuonekana wakati maana ya Mwanzo 27:33 inapozingatiwa (soma sehemu Baraka kwa Yakobo).
ESAU ANAUZA HAKI YAKE YA MZALIWA WA KWANZA (Mwanzo 25:29-34)
Chakula aina ya dengu hutengenezwa kwa kuchemsha mbegu nyekundu ( kama maharagwe) ndani ya maji. Esau alirudi akitokea mawindoni bila kupata mawindo na akiwa amechoka mno na akiwa na njaa akifiri kuwa angekufa.
Akataka apewe chakula hicho na Yakobo, ambaye aliiona nafasi hiyo akahitaji kununua haki ya kuzaliwa ya Esau kwa chakula cha dengu. Kwa kuwa Esau alikubaliana na hili, inadhihirisha mambo mengi kuhusu Esau:-
-
- Alijifikiria yeye mwenyewe kuliko kumfikiria Mungu.
- Hakujali sana heshima ya kuwa mzaliwa wa kwanza, ambayo ilimpatia “haki” ya kupata sehemu mara mbili ya urithi.
- Hakufikiria lolote kuhusu wajibu alionao mwana mkubwa kwa ndugu zake wadogo katika familia.
Paulo anasema Esau alikuwa mtu asiye mcha (Waebrania 12:16-17), inayomaanisha mwasherati au asiye mcha Mungu. Alikuwa mtu aliyetawaliwa na nia ya mwili, na ambaye alikuja kujulikana kama “Edomu” maana yake “Mwekundu” rangi ya dhambi ( pia rangi ya chakula cha dengu .mstari 30)
HAKI YA MZALIWA WA KWANZA: (Kumbukumbu la Torati 21:15-17)
Katika ukoo nyakati za Biblia ndugu wengine wote wa familia walimheshimu mwana mkubwa kuzaliwa . Alikuwa mzaliwa wa kwanza, alikuwa ni kichwa cha ndugu zake . Angechukua madaraka ya kuheshimiwa yampasayo baba, alikuwa na haki maalumu ya baraka za baba yake, na kupokea sehemu “mara mbili” ya mali za baba yake kwa maana ya urithi. Haki ya mzaliwa wa kwanza, baba angeweza kumpatia mwana yeyote na kwa sababu ya nia njema. Esau aliiachilia haki yake ya thamani kubwa mno kwa ajili ya mlo mmoja mdogo.
YAKOBO ANABARIKIWA (Mwanzo 27)
Baba yake Yakobo,Isaka alikuwa na umri wa miaka 117 na macho yake yalikuwa yamepofuka,asione. Alifikiri kuwa alikuwa anakabiliana kufariki na akaamua kumpa baraka mzaliwa wake wa kwanza.
Inasikitisha kuona Isaka akikataa kukubali mapenzi ya Mungu kuhusu Yakobo na kukaza nia yake ya kumbariki Esau. Angalia namna wana wanavyoelezewa, “mwanawe” (mstari 5) na “mwanawe” (mstari 6). Huu ni upinzani mkubwa zaidi kutokana na upendeleo wa Isaka na kushindwa kwake kumkemea Esau aliyekuwa akifuata njia zake za dunia.
Rebeka alifanya haraka ili mwanawe mdogo abarikiwe . Akamsisitiza Yakobo mwenye mashaka atii sauti yake na kumdanganya Isaka. Yakobo akaja mbele ya Isaka, akatimiza sehemu yake na kumdanganya baba yake (mstari 18-26). Isaka alichanganyikiwa kwa namna ambayo chakula kilivyoandaliwa haraka na sauti ya mwana ambayo haikuwa kama ya Esau kabisa. Akiwa bado haelewi, aliendelea kula na kumbariki mwana aliyeamini kuwa ndiye Esau. Akatamka baraka za mafanikio ya mali, mamlaka juu ya watu na mataifa na baraka juu ya marafiki na laana juu ya maadui. Baraka hii inafanana na baraka ya Mungu aliyompa Ibrahimu. Lakini katika tamko la kushangaza Isaka akasema “Uwe bwana wa ndugu zako na wana wa mama yako wakusujudie” (mstari 29). Hapa ndipo yalipotimia maneno ambayo Mungu alimwambia Rebeka kabla wavulana hao hawajazaliwa .Mkubwa atamtumikia mdogo. Lakini Isaka alidhani alikuwa akizungumza na Esau! Ndipo alipotambua kwamba alikuwa amejaribu kupinga kusudi la Mungu wakati Esau m aliwenyewe alipotokea na kutaka baraka (mstari 30-33).
Akiwa ameshtuka sana kwa jambo hilo la kinyume, Isaka “alitetemeka kwa tetemeko kuu sana”. Imani yake haikushindwa. Katika onyesho la kusisimua la kujinyenyekeza kwa kutii mapenzi ya Mungu, alisema, “Ndiyo, naye atabarikiwa”. Kitabu cha Waebrania kinatueleza kwamba kwa imani Isaka alimbariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yatakayokuja (Waeb. 11:20). Esau “akapaza sauti yake akalia” (mst. 38). Haya yalikuwa machozi ya hasira na kukata tamaa. Tafakari shinikizo lililomfikia Isaka kwa maombi yenye machozi ya mwana aliyempendelea. Hata hivyo, imani ya Isaka, ilikuwa imetikiswa sana, ilisimama imara chini ya shinikizo lile. Akiwa ameshindwa kubadilisha mawazo ya Isaka, Esau akaonyesha tabia yake halisi kwa kupanga kumwua nduguye (soma Waebrania 12:16-17).
Isaka hatimaye alimbariki Yakobo kwa ukamilifu wote wa agano la Ibrahimu, (28:3-4), na wakati huo huo akathibitisha sehemu ya Esau ya kumtumikia nduguye (Mwanzo 27:38-40).
Inatubidi tuzingatie kwamba Isaka aliishi miak 63 zaidi baada ya matukio haya, ambayo ilimfunulia haraka yake ya kung`ang`ania kutaka kumbariki Esau.
FUNDISHO KWETU
- Kabla wavulana hawa wawili hawajazaliwa Mungu alimchagua Yakobo kwa sababu aliwaona kabla tabia watazokuwa nazo. Lakini mwana alipendelewa na Isaka alikuwa ni Esau aliyekua hadi akawa mtu wa tabia za dunia. Ni budi tupinge ushawishi wowote wa dunia na kupendelea tabia ya ukimya na kumcha Mungu iliyoonyeshwa na Yakobo.
- Esau alionyesha kutothamini kwake alipouza haki ya mzaliwa wa kwanza kwa “ chakula kimoja”. Kamwe tusizifanyie mzaha ahadi za Mungu kwa kuyaacha mambo yanayofaa. Tumepewa tumaini la thamani sana la uzima wa milele. Tulithamini hili zaidi kuliko faida yoyote ya muda mfupi leo.
- Imani ya Isaka ilikua hadi kuongezeka alipojinyenyekeza chini ya mapenzi ya Mungu. Alinyenyekezwa kwa mkono wa nguvu wa Mungu. Katika maisha yetu inatubidi “ tupate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema na kumpendeza, na ukamilifu” (Warumi 12:2) na kuyatii. Tunaweza kuona kutoka na somo hili ya kwamba “tusitegeme akili zetu wenyewe” bali “tumtumaini Mungu katika njia zetu zote” kwani hapo ndipo Mungu ataongoza hatua zetu (soma Mithali 3:5-7). Tukitenda hivyo, Mungu atatuongoza kuelekea kwenye Ufalme na urithi wa zile ahadi kubwa na za thamani alizoahidiwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
MAKTABA YA REJEA
“Historia ya Biblia” (H.P. Mansfield) Ukurasa 141-150
“Njia za Mungu za kutoshereza mahitaji” (R. Roberts) – Sura 5,6
“Tumaini la Israeli” (J. Thomas) – Ukurasa 264-272
“ Mkufunzi Kristo” Ukurasa 87-89
MASWALI YA FUNGU
- Ni ujumbe gani Mungu alimpa Rebeka kuhusu wanawe wawili?
- Ni njia gani Esau alidharau haki ya mzaliwa wa kwanza?
- Ni jinsi gani Isaka alionyesha imani katika kuwabariki wanawe?
- Eleza maana ya “haki ya mzaliwa wa kwanza” (au “mzaliwa wa kwanza”)
MASWALI YA INSHA
- Andika maelezo ya tabia ya Esau na Yakobo
- Onyesha jinsi nia ya Isaka ya kumbariki Esau ilivyoshindwa kwa vitendo vya Yakobo na Rebeka.