202 - YESU AKUTANA NA NIKODEMU MFARISAYO
“Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme na Mungu” baada ya harusi ya Kana Yesu alikwenda kapernaumu na kukaa kwa muda mfupi pamoja na nduguze na wanafunzi. Kapernaumu ulikuwa mji katika barabara kuu ya serikali upatayo safari ya siku mbili au tatu kutokea Yerusalemu. Alikuwa sasa tayri kuanza kazi yake kati ya watu. Walikuwa waanze kusikia maneno mengi ya ajabu zamani yakifafanuliwa kwa njia mpya. Watu wa Israeli, sasa wakijulikana kama Wayahudi, kwa muda mrefu walikuwa wameishi chini ya sheria Mungu aliyompa Musa (Kutoka 19). Miaka mingi ilikuuwa imepita kutokea hapo, na watu walikuwa waweongezea katika sheria magizo (amri) zao wenywe, hadi maana halisi ikawa imepotea.
Hekali zuri la kupendeza lilikuwa limejengwa Yerusalemu ambamo Wayahudi walijaribu kudumisha kafara na kutunza sherehe za maana za Mungu. Kwa njia kadha wa kadha hizi pia zilikuwa zimebadilika. Ilikuwa wakati wa pasaka ambapo yesu alisafiri kwenda Yerusalemu kwa ajili ya kile sasa kilichoitwa “pasaka ya Wayahudi”(Yohana 3:13)
Yohana 2:12-13;3:1-8 Wakati wa Pasaka kwenye hekalu (Yohana 2:13-23)
Wakati wa Yesu alipofika hekaluni mitaa ya Yerusalemu ilikuwa imejaa watu naye aliona kwa sikitiko /husuni na hasira watu walipoendelea mpaka ukumbi wa nje kununua wanyama na ndege kw aajili ya dhabihu (kafara). Hapa watu walikaa na kubadilishana fedha za kigeni na wali waliouza wanyama kwa ajili ya kafara wakawa wanachukluwa, viwango vya juu kuliko bei sahihi ya thamni ya wanyama wao(Yohana 2:14). Hii haikuwa njia ya Mungu aliyoikusudia kuwa wamwabudu. Kelele na sauti za wafanyabiashara wachoyo zilimkasirisha Yesu. Nyumba ya baba yake ilikuwa inachafuliwa kwa sabubu ya matendo maovu ya matajiri waliowaibia maskini.
Akisokota kamba kadhaa kuw akiboko, Yesu akakimbia kati ya wafanya biashara, akitawanya wanyama wenye nao, akipindua meza za fedha na kuwaamrisha hao watu wenye njiwa (hua) kuondoka (mst10). Wakakimbia mbele yake wakijua ya kwamba hawakutunza heshima ya nyumba ya Mungu. Sauti yake iliwafuata “msifanye nyumba ya baba yangu kuw anyumba ya biashara” hakuna yoyote amabye angeweza kubioshana na ukweli wa tuhuma hiyo kali. Alikuwa sahihi na wakaogopa umakini wake wa kuheshimi (kudumisha) utukufu wa Mungu, kuwa wakti utakuja ambapo dini ya kwlei itajaa ulimwenguni mwiote (Mika 4:2; Zakartia 14:20-21), na ndipo hekalu la Mungu litakuwa nyumba ya ibada (maombi) kwa ajili ya watu wote (linganisha Isaya 56:7). Leo sasa hivi tunaona dini ya uwongo kila upande wanaofundisha makosa na kupata fedha kupitia huduma zao za dini, lakini katika siku ambapo yesu atarudi watu watafundishwa kweli na kumwabudu Mungu kama aliivyoagiza.
Nikodemu aja kwa Yesu usiku (Yohana 3:1-10)
Watawala wa Israeli hawakuchanganyikana na watu wa kawaida ila hasa walikaa katika vikundi vyao na kuchungulia kwa mbali. Walakini, palikuwepo mmoja kati ya watawala Mfarisayo aliyeitwa nikodemu aliyeona vitendo na akawaza juu ya fundi seremala wa Nazareti. “Huyu alikuja kwa Yesu usiku, na kusema naye, mwali (Bwana), tunajua ya kuwa wewe ni mwalimu utokaye kwa mUngu, kwani hakuna awezaye kufanya miujiza unayofanya Mungu asipokuwa naye” Yohana 3:2. yesu akajibu “mtu asipozaliwa mara ya pili au (kutoka juu) hawezi kuona ufalme wa Mungu”
Watu wote huzaliwa mara ya kwanza kama vifaranga lakini ni uzaliwa mara ya pili wakati anapokuja kulifahamu neno la Mungu na kutaka ktenda kama anavyoagiza, ambaondiyo wenye maana zaidi katika macho ya Mungu. Ni neno lake Mungu “litokalo juu” linalomfanya mtu “azaliwe mara ya pili” (1Petro 1:23). Ni kuzaliwa tena kimaadili (badiliko la msimamo na masilahi ya maisha) nao waliozaliwa upya kwa njia hiii wansemekana “kuzaliwa kwa maji” (mst 5) wanapobatizwa. Katika tendo la ubatizo wanaonyesha kwamba wanakufa kwa njia ya maisha ya zamani kama viile walivyokuwa wamefuata dhambi, nao wananza masisha mapya ya utiifu kwa Mungu.
Nikodemu hakujua hili. Alifikiri yesu alimaanisha kuzaliwa tena kwa njia yaasili. Lakini Yesu alikuwa akisemea juu ya badiliko la akili na moyo. Halafu Yesu akaongezea ya kwamba kwa mtu kupata ufalme, inampasa pia “azaliwe kwa roho”
Kwa kuwa watu wana hali ya kufa na ufalme utadumu milele itawabidi kupewa uzima wa milele (kubadilika kuwa na hali ya kiroho) ili kurithi ufalme. Ni Mungu pekee anayeweza kuleta badiliko la ajabu hivyo katika hali ya mtu.
Kama vile Musa alivyomwinua nyoka (Yohana 3:11-21)
Yesu alisema kuhusu vitu vingi kwa Nikodemu. Alimkumbusha wakati jangwani watu waliponungunika na M<ungu aliwaadhibu kw anyoka wakali ambao kuuma kwao kulileta kifo (Hesabu 21:4-9). Ndipo basi, walipotubu, na Yahwe akamwagiza Musa kutengeneza nyoka wa shaba, na kumwinua juu ya mti. Yeyote aliyemtazama kwa imani angaliponywa. Wengi waliofanya hivyo walipona kutokana na kile ambacho kingalikuwa kifo cha hakika. Palikuwa na mdanano kati ya kile kilichotokea wakati ule na kile kingalichotokea kupitia kwa Kristo. “Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, hivyo hivyo mwana wa Adamu inampasa kuinuliwa”(Yohana 3:14). Kw anjia hiii Yesu alieleza jinsi yeye mwenyewe atakavyosulubishwa, lakini baada ya kufufuka kwake njia ingalfunguliwa kuelekea uzima wa milele kupitia ima kwake (mst 15). Wakati huo huo, Yesu akieleza kwa Nikodemu, ahadi ya uhai wa milele haikuwa kwa Israeli peke yao tu, ila ingaliwekwa tayari kwa wote kwa msingi wa imani (mst 16,17)
Nikodemu anarudi
Nikodemu alipomwacha Yesu alifikiri juu ya vitu ambavyo walikuwa wameviongelea, na katika Yohana 7:50-51 tunasoma ya kuwa alizungumza kinyume na wengien ambao walitaka kumtesa Yesu. Hata baadaye tena, Nikodemu alikuja kufahamu kwa ukamilifu kuwa yote ambayo Bwana alikuwa anayasema yalikuwa kweli. Ni yeye aliyemsaidia Yusufu wa Arimatayo kwa upole kuchukuwa mwili wa Yesu msulubiwa kutoka msalabani na kuutia ndani ya kaburi (Yohana 19:39,42)
Somo kwetu
Yesu alianza kuonyesha utukufu wake kuwa mwana wa Mungu katika matukio ya kuheshimika mawili, lile la kugeuza maji kuwa mvinyo kule Kana na lile la kuwafukuza kutoka hekaluni wle waliotenda utovu wa heshima, lile kama ni pango la wezi. Katika matukio yote mawili nguvu zake zinadhihirika. Moja kuonyesha shangwe na furaha ya kwamba yeye peke yake anaweza na hasa atatoa, na katika lile lingine kuonyesha umahiri wake katika kuiheshimu nyumba ya Mungu. Tunapolichukua neno la Mungu ndani ya mioyo yetu ndipo tutakapopata shangwe ya kweli na furaha, pamoja na hilo patakuwa na tamaa yak um,heshimu Mungu katika njia zetui zote (Mithali 3:5-6). Hatua ya kwanza kumheshimu Mungu ni kuzaliwa mara ya pili kwanza kwa ubatizo ndani yake, na baada ya maisha yote., kumheshimu Mungu, kupokea uzaliwa” wa kushangaza wa badiliko kuelekea hali (asili) ya kiroho kupata shangwe ya milele na furaha katika ufalme wa Mungu.
Maktaba ya rejea
“A life of Jsus” (M. Purkis) book 3, chapter 1, 2
“The Gospel of John” (J.Carter) pages 39 -63
“Nazareti Revisited” .Roberts) chapter 12, 13
Maswali ya fungu
- Kwa nini Yesu alikasirika alipokuja hekaluni wakati wa pasaka?
- Yesu alimfundisha Nikodemu kuhusu uzaliwa aina m,bili. Vilikuwa vitu gani na vina maana gani?
- Kwa nini Yesu alirejea kwa nyoka kuinuliwa jangwani wakati wa maongezi yake na Nikodemu?
Maswali ya insha
- Fafanua tukio wakati Yesu alipolitakasa hekalu wakti wa pasaka
- Andika insha juu ya mazungumzo yaliyofanyika wakati Nikodemu alipomtembelea Yesu usiku.