CSSA 2-4-07 - TEACHING HIS DISCIPLES:2

Swahili

207. KUFUNDISHA WANFUNZI WAKE

i) Uanafunzi “Mmesikia ilisemwa hapozamani… lakini mimi nawaambia” Yesu amesgaeleza tabia ya mtu mkamilifu, sasa nafafanua matendo ya adili (uadilifu) ambayo tabia aina hiyo hudhihirisha, akitumia mfano ya nguvu Yesu anaonyesha kwetu njia sahihi ya kufikiri, kusema, na kutenda katika aina mbalimbali za mazingira. Tabia zilizotajwa katika heir zinaonyeshwa kimatendo katika mambo ya maisha ya siku kwa siku. Wanafunzi wote wa Kristo wana wajibu wa kuonyesha bila kikomo tabia hizi kwa marafiki zao na jirani zao dunia.

 

Mathayo 5-6 Kristo na Musa – Mfanano wao

Sheria ya Musa ilihukumu matendo ya nje, lakini Yesu alihusika na mawazo yasiyoonekana ambako kutokea matendo hayo. Ni katika akili, basi, ambamo utii inapasa uanze. Kuhusu dhambi, Yesu alifundisha ya kwamba mawazo ni muhimu vile vile kama matendo. Yesu alitimiza sheria ya Musa kwa nje na kwa muhimu zaidi, kwa ndani.

 

  1. Hasira isiyo ya haki imekatazwa (5:21-26)

Kutoka 20:13 ilisema “usiue”Yesu aliona katika hasira chanzo cha mauaji zaidi ya hayo alifundisha ya kwamba yoyote anayemchukia kwa uchungu nduguye au yeyote aliye na dharau kwa ndugu yake, au yeyote anayemwita nduguye mpumbavu wa adili anakuwa katika hatari kuu ya hukumu juu yake. Kabla Mungu kupokea ibada (sala) yoyote kutoka kwa mtu asiyepatana na nduguye huyo mtu inamapasa atafute njia ya kurejesha umoja kati yao.

            Yesu anamaliza sehemu hii kw akuonyesha jinsi ya kutenda kuhusiana na wapinzani, ni bora kabisa kuw akatika uelewano mema nao upesi kabla matatizo hayajaongezeka na kuelekeza kwenye matatizo mabaya zaidi. Unyenyekevu (upole) na kujidhili (kujishusha) ni vigezo vya lazima kupata hili (linganisha na sehemu ya 4)

 

  1. Wazo la uzinzi limekatazwa (5:27-32)

Sheria ya Munga ilisema “usizini” yaani uhusiano haramu na mke wa mtu mwingine. Walakini Kristo anashutumu mtu yule anayemtazama tu mwanamke kw amawazo maovu akilini mwake. Mawazo aina hii ni mabaya vile vile kama matendo yoyote ya nje mbele ya Mungu.

Yesu anaendelea kusema ya kwamba iwapo jicho la mtu au mkono unamsababisha kutenda dhambi ni bira zaidi kwake kuviangamiza kuliko kupoteza uzima w amilele kw asababu yake. Hakuwa akipendekeza ya kwamba watu hasa hasa wavikate mikono yao  wanyofoe macho yao. Hapa Yesu anatumia jicho kuwakilisha tamaa na mkono kuwakilisha vitendo. Tamaa mbaya zizuiwe (zikatwe) zisije zikamsababisha mtu kuanguka. Kushindwa mtu inampasa ajaze akili na mawazo mema, akijaribu kuyaondoa,  mawazo maovu na hivyo kuweza kufanya matendo mazuri.

 

  1. Kuapa kumekatazwa (5:33-37)

Linganisha Hesabu 30:2 wakati wa Kristo Wayahudi walikuwa na mazoea ya kuapa viapo 9siyo kuapa kwa maana ya kutamka lugha m,baya). Kwao kiapo chochote kikichanganyika na jina la Mungu kilikuw athabiti sana, lakini hivyo kingine chochote kisichomtaja Mungu kilikuwa siyo thabiti sana. Hili lilileta kwa waapaji wa viapo mara nyingi kuapa ili kufunika kweli, kuwawezesha kusema kama walivyosema hawakumaanisha hivyo, na bila kutenda kama walivyosema wanafanya. Hii ilikuwa tofauti (kinyume) na roho ya sheria ya Musa na Yesu alimrisha wafuasi wake kutofanya (kutotoa) viapo kabisa, ila kusema “ndiyo’ au “siyo” na kusimama hapo.

 

  1. Kupigana (kujihami) na uovu kunakatazwa (5:38-42)

Utaratibu wa haki chini ya sheria ya Musa uliruhusu mwamuzi kutekeleza adhabu ile ile ya dhambi, kama “jicho kwa jicho”(Kutoka 21:23-25). Katika kushughulikia tabia za watu binafsi mmoja kw amwingine, Yesu anaamrisha kutokupigana na dhambi, pasiwepo na kurejesha mapigo au kuhisi chuki katika mashauri ya kuumizwa binafsi (mst39) na amri kali (mst40). Patakuwepo utiifu kw amamlaka zilizowekwa (mst41) vitu vitatu visivyoweza kutendwa na mwanafunzi wa kweli ni hivi.

    1. Kutukanwa na kuwa na chuki kwa sabbu ya matendo yaw engine
    2. Kulazimisha (kuomba) haki yake , na
    3. Kulakikisha kufanya zaidi kuliko alichotakiwa afanye lengo la hali hii ya kutofurahia kutopigana na roho ya kuwapa wengine ni kuwapata watuhumiwa kwa ajili ya Kristo

 

  1. Upendo umeamrishwa (5:43-48)

Hii ni sehemu muhimu san asana ya mahubiri ya mlimani mila ya Wayahudi iliruhusu (ilitia moyo) Wayahudi kuchukia adui zao. Kinyume chake Yesu alisema “wapendeni adui zenu” neno panda linamaanisha “kumtakia Fulani mema kabisa” hisia hii idumishwe hata mtu yeyote afanyaye kwa muamini pendo namna hii hmshinsa *humteka) mtu, ambapo kupigana huongeza tatizo zaidi.

Wale wanaowapenda adui zao watakuwa “wana wa baba” wako kama yeye. Mungu anawapenda anaonyesha pendo kwa watu wote kila wakti angalao wanamkosea (Linganisha Yohana 3:16). Hufanya juu ya wenye haki na wasio na haki, anatutaka nasi kuonyesha tabia hiyo hiyo kama tutawapenda tu wale wanaotupenda hatuana jema lolote kuwazidi watu waovu wa kupindikua, ambao watawatawatunza watoto wao kw avyovyote vile.

 

DHAMBI YA UNAFIKI ( 6:1-8; 16-18)

Yesu alichagua hali aina tatu ambamo unafiki (kujifanya) ulionyeshwa na Waandishi na Mafarishayo, hali hizo ni

  1. Kutoa sadaka au kufanya matendo ya haki, hususani kutoa fedha kwa masikini
  2. Kusali hadharani
  3. Kufunga

Wale walio chini ya sheria ya Kristo ni budi wafanye matendo 9kazi) zao za haki kwa siri, wasali kwa siri na wafunge faraghani (wajikane na kujiheshmu / kujidhili) faraghani, zikiwa kazi za kumpendeza Mungu, siyo kwa ajili ya sifa yaw engine, ndipo Mungu atatuzawadia waziwazi. (6:6)

 

HAZINA YA KWELI (6:19-34)

Kisha Yesu anaweka mbele ya wasikilizaji wake changamoto kwa uaminifu wao kwake. Watu hupenda kuweka imani zao katika mali walizonazo kama vile fedha na nyumba ambavyo havidumu, walikini Yesu anawasisistizia wanfunzi wake kuona upumbavu wa utaratibu hu wa vitendo, nao wajiwekee hazina kwa Mungu, yaani tabia inayokubalika kwa Mungu (linganisha Malaki 3:16-17)

Neno “tumikia” Katika 6:24 inamaanisha “uwe mtumwa” mtu mmoja anaweza kuajiriwa na watu wawili lakini anaweza tu “kuwa mali” ya mmmoja. Kwa kuwa Mungu anahitaji mtu kumpenda yeye kw amoyo wake wote na roho yake yote na nguvu, anaweza vipi kuw amtumwa na Mungu na pia awe hivyo kwa vitu bua kutumia (ona Warumi 6:16)

Basi ikiwa Mungu ndiye Bwana anaweza kutegemewa kutoa mahitaji yote. Kwa vile Mungu amatoa uhai na kuumba mwili atavitunza. Kwa nini basi tuwe na wasiwasi? Iwapo baba yetu wa mbinguni anawapatia chakula kwa ndege na kuwavika uzuri maua, je, anaweza akasahau mahitaji ya watakatifu wake wanaotaka ufalme wake? Ni hakika kabisa watasikiwa na kutuzwa.

 

Somo kwetu

Yesu ametuonyesha sisi amali ambazo wanfunzi yawapasa kuwa nazo iwapo watakubaliwa na mwamuzi wa ulimwengu wote. Amali hizo zimeandikwa kifupi na Mathayo 22:36-40”umpende Bwna Mungu wako kwa moyo wako.. roho, …na akili, nawe umpende jirani yako kama nafsi yako.”

            Kumpenda jirani yetu kama nafsi yetu litakuwa tokeo lisilo kikwzo (la wazi) la upendo wetu kwa Mungu. Inatupasa kuwafikiria wengine kw ayaliyo sasa nay a ubora wao wa milele, tuukiwaza kufanya mema siku kwa siku. Changamoto ya uanafunzi ni kuw amtiifu mwaminifu, na wenye msimamo imara katika kumwuabudu Mungu, anamsisitizia kila mmoja wetu, kufnaya auamuzi binafsi ambao utaongoza kwneye uanafunzii wa kweli

 

Maktba ya rejea

“The TEACHING OF THE MASTER” (L.G.Sargent) part II

“ The life of Jesus” (M.Purkis) pages 138-148

“The story of the bible”(H.PMansfield) vol 8, pages 152 – 159

 

Maswali ya fungu

  1. Ni kwa vipi mafunzo ya Yesu ni tofauti na sheria ya Musa?
  2. Yesu anasema nini kuhusu kujizuia katika mahubiri ya mlimani?
  3. Kutokana na mahubiri ya mlimani onyesha jinsi Yesu anavyotuahidi sisi ya kwamba Mungu atawatunza watoto wake.

 

Maswali ya insha

  1. Yesu anasema nini klhusu kujihusisha na upendo tunapokabiliana na wapinzani katika mahubiri yake ya mlimani?
  2. Onyesha jinsi Yesu akatika mahubiri yake mlimani aliwahamasisha waafunzi wake kuweka imani (tegemeo) na tamama yao kwa usalama katika nana wa mbinguni mwenye upendo.

 

Swahili Title
207. KUFUNDISHA WANFUNZI WAKE
English files
Literature type
Sub type
Sub sub type