281. KUANGUKA KWA YERIKO
"Wakazi wote wa nchi wanaanguka kwa sababu yako"
Yoshua, baada ya kupokea ujumbe wake kutoka kwa Mungu akiwa nchi tambarare za Moabu (Hes. 27:15-23), alijibu kwa kujitolea kabisa kwa huduma ya Bwana na watu wake. Kazi yake ya kwanza kubwa alikuwa kuwatia moyo na kuwahamasisha watu (1:10-15) na kisha kuhakikisha usalama wao wakati wa kuvuka Yorodani - kazi ambayo ingeweza kukamilika kwa miujiza ya Mungu. Sasa nchi yenyewe ikawa mbele yao ikisubiri kunyakuliwa. Ulinzi wake ukiwa ukuta mkubwa wa Yeriko.
Katika somo hili kwanza tunarudi hadi kitabu cha Yoshua sura ya pili ambayo inahusika na kutuma wapelelezi Yeriko - Tukio lililotokea kabla ya kuvuka Yorodani - kabla yakufikia kuanguka halisi kwa ukuta waYeriko katika Yoshua 6.
Lengo la somo hili ni kuona jinsi imani inapata ushindi juu ya nguvu za dhambi.
Yoshua 2; 5:13-15, 6
KUPELELEZWA KWA YERICHO (Yos. 2).
Kwa kutumia ujanja wa kiongozi wa Kijeshi mwerevu, Yoshua alituma watu wawili " kupeleleza kisiri " hali ya kijiografia na ulinzi wa Jericho ( Mst. wa 1) . Watu hawa wawili walikuwa makini hasa kwa hali ya kisaikolojia ya watu wa Yeriko ( 02:11 ); maarifa hayo yalikuwa ya maana katika mipango ya mafanikio ya operesheni ya kijeshi (linganisha Mst. 11 kwa Mst.24 ).
Watu wale wawili walioteuliwa waliondoka Shitimu kimya kimya ( mst.1 , linganisha . 3:01 ), na wakasafiri kuelekea mji wa Yeriko, umbali wa kilomita 20. Katika mji huo, Stanley aliandika: " Jericho inasimama katika lango kuu kutoka bonde la Yorodani hadi sehemu za ndani za Palestina, moja ikielekea kusini - magharibi kuelekea Mizeituni, nyingine kaskazini - magharibi kuelekea Mikmashi , ambayo alitizamia upande wa Ai na Betheli. Kwa hivyo ikawa ni muhimu kwa mvamizi yeyote wa Palestina kujua haya"(" Sinai na Palestina " , p. 305) . Jericho ilikuwa umbali wa 11 kilomita kaskazini mwa Bahari ya Chumvi , na 8 kilomita magharibi mwa Yordani na mita 270 chini ya usawa wa bahari. Hiyo inaitwa " mji wa mitende " (Kum. 34:3 , 2 ââNya. 28:15 ; . . Amu 1:16).
Kwa mbinu za kujificha, na kwa uangalifu, wapelelezi hawa wawili walingia ndani ya Mji lakini walitambuliwa. ( mst. 2). Habari ya kuweko kwa wapepelezi katika nyumba ya Rahab yule kahaba ilimfikia Mfalme wa Yeriko, na hivyo yeye iliamuriwa kuwatoa . Akionyesha kiwango cha kushangaza cha imani, na roho ya kutokuwa na ubinafsi , alikubali kuwaficha wapelelezi katika paa la nyumba yake ( mst. 4-6) , na hii iliwasaidia kutoroka Mji kupitia dirisha ya nyumba yake. (mst. 15) .
Rahabu aliamini Mungu - kwamba alikuwa Mungu mkubwa juu mbinguni, ambaye alikuwa na wana wa Israeli katika kuwaleta kupitia Bahari ya Shamu miaka arobaini na kwa hakika alikuwa nao wakati walikuwa wanajitayarisha kupambana na wenyeji wa Kanaani (mst. 9-10). Yeye alionyesha imani yake , na hofu ya watu , wakati aliambia wapelelezi, "tuliposikia kuwahusu , mioyo yetu iliyeyuka, na hatukuwa na ujasiri wowote, kwa sababu ya Bwana, Mungu wenu, Yeye ni Mungu aliye juu mbinguni, na pia huku duniani."( Mst. 11).
RAHABU ANABADILI TABIA.
Rahabu alikuwa kahaba -hakukuwa na njia nyingine ya kumwelezea tofauti. (taz.Ebr. 11:31; Jas 2:25 ..). Itakumbukwa kwamba kwa Rahabu na rika lake hawakutambua kitu kibaya katika njia za maisha, (tazama Kum. 09:05 ). Lakini ujuzi wa kweli ulibadilisha haya yote kwa Rahabu . Tazama kwa makini maneno ya Bwana Yesu juu ya somo hili katika Mat. . 21:28-31 . Alifundisha kwamba " " viongozi walioheshimiwa wa dini wa siku zake watakuja kukataliwa- Kwa sababu ukweli hauko ndani ya Mioyo yao - lakini wale waliodharauliwa, " watoza ushuru na makahaba " watakubalika. Hawakujifanya kama wanafiki kwani walijua ni wenye dhambi (Lu. 18:9-14 ). Unyenyekevu ulionyesha kubadilika kwa tabia ya Rahabu. Linganisha 1 Kor. 6:9-11. Vile tulivyo sio Muhimu mbali ni jinsi tunavyokuwa, baada ya neno la Mungu kutubadilisha.
UHAKIKISHO WA IMANI NA MATENDO
Rahabu alikuwa Haki kwa imani na kwa matendo. Mwandishi wa Waebrania anaorodhesha Rahabu katika orodha yake ya waamini (Ebr. 11:31) ,Yakobo anamchukua Rahabu kama mfano wa kanuni: " kwa matendo ya imani kukamilishwa " ( Yak. 2:22, 25). Yeye aliamini (au alikuwa na imani kwa ) Mungu na yeye alionyesha imani yake katika hatua ya kupokea wapelelezi na kuwatorosha kutumia njia nyingine.
Baadaye, Rahabu alifunga ndoa na Salmoni, mwana wa Nashoni, mkuu wa kabila la Yuda, kwa hivyo akawa babu wa mfalme Daudi kupitia Boaz na Ruth. Bwana Yesu Kristo mwenyewe alikuwa wa ukoo wa moja kwa moja kupitia wanawake hawa wawili wa ajabu na wa imani kutoka kwa watu wa mataifa ya nje ( Mat. 1:05 ambapo " Rachab " = Rahabu) , na kusisitiza kwamba sio tu uhusiano wa kimwili, bali uhusiano wa kiroho na imani ndani ya Mungu .
Imani ya Rahabu ilionyeshwa kwa vitendo wakati aliuliza wapelelezi kwamba familia yake iweze kuhifadhiwa na akauliza ishara kwamba hii itafanyika( 2:12-13). Kwa kuonyesha shukurani wapelelezi hawa wawili, walikubali hili kwani waliona imani yake, na walitoa masharti yafuatayo:
1. Asimwelezee yeyote makubaliano haya" (m. 14, Biblia ya Yerusalem).
2. Lazima "angefunga uzi mwekundu katika dirisha" wakati Israel watarejea katika nchi. Hii itaonyesha wazi nyumba yake nayo haitashambuliwa. (mst. 18).
3. Yeye na familia yake wangabaki ndani ya nyumba (Mst..19;. linganisha Kut.12 22).
Wapelelezi walirudi kwa Yoshua wakiwa na furaha. Mioyo ya Wakanaani ikijaa na mshtuko, walimwambia Yoshua. Nchi tayari imekuwa yao, kwani wakazi wake tayari walikuwa wameshindwa kisaikolojia (mst.24).
NAHODHA WA JESHI LA YAHWEH (YOS. 5:13-15)
Kisha Yoshua akatoka, kimya kimya peke yake, akaenda kutafakari juu ya mgogoro uliokuwa mbele yake na Yeriko - ngome ya mwili ,iliyozuia wana wa Israeli kuingia katika nchi, kikwazo ambacho kilihitajika kuharibiwa. Ghafla, akatokea "Mtu akiwa na upanga mkononi mwake. " Yoshua alimjibu mara moja: "Je, wewe upo kwa ajili yetu, au kwa wapinzani wetu ?" Somo hili ni wazi. Katika vita ya imani hakuna maelewano. Kuna vikundi viwili tu : "wao" na "sisi" . kwa Yoshua, hakungekuwa na msimamo wa wastani . Lakini hakutarajia utambulisho wa mgeni wake , wala jibu lake : " Bali mimi , kama mkuu wa jeshi la Bwana, Nimekuja" (m. 14 Roth. ).
Malaika labda malaika wa uwepo wa Mungu na ambaye alichukua jina lake alionekana na Musa katika kichaka (mst. 15 na Kut. 03:05 , 23:20-23 , Isa.63:9 . ). Malaika wa Israel au "mkuu" alikuja kutambuliwa baadae kama Michael na Yuda anatuambia kwamba yeye ni malaika mkuu (Dan. 10:13 , 21; Yuda 9) .
Yoshua akasujudu na kisha akakubaliana na maelekezo ya malaika kwanza kutoa viatu vyake kwani mahali ambapo alikuwa amesimama ni mahali takatifu ( mst. 14-15). Yoshua kisha akajua kwamba vita vinavyo kuja sio vita yake mwenyewe , wala sio vita vya Israel . hivi vilikuwa vita vya Bwana - vita dhidi ya dhambi, ambavyo Bwana bila ya shaka angeibuka mshindi ( 6:02 , 6:16 linganisha . )
MPANGO WA MASHAMBULIZI (YOS. 6:1-7).
Mji wa Yeriko ulikuwa takriban hekta 2 au 3 ukizungukwa na ukuta wa mita 2 mita, na ukuta wa ndani â wa mita 4 hadi 5 kwa nyuma - ambayo ilikuwa mita nne kwa upana na mita 9 kwa urefu. Mji ulikuwa " umefungwa kabisa " (Mst. 1) , kuonyesha kwamba ulikuwa umefungwa kutoka ndani. Wenyeji walikuwa katika hali ya woga na wasi wasi, wanasubiri mashambulizi kutoka kwa wana wa Israeli.
Utaratibu ambao WaIsraeli walifuata haukuwa ule wa Kijeshi - ilikuwa ni kwa zoezi la kidini, onyesho la imani katika Bwana, na si onyesho la nguvu za kimwili (mst. 2-5).
Kwa muda wa siku sita watu wa Israeli walikuwa wafanye maandamano kuzunguka mji wa Yeriko - kimya kimya, na bila majigambo yoyote. Kisha siku ya saba walikuwa wafanye maandamano kuzunguka mji mara saba. Utaratibu wa maandamano ilikuwa sawa kila siku : Kwanza, watu wenye silaha wangetangulia makuhani saba wakibeba na kupuliza tarumbeta saba, kisha wakifuatwa na sanduku la agano ; hatimaye " walizi nyuma " (mst. 9 , Rot. ). kwa siku sita za kwanza hawangepiga ââ kelele (Met. 13:3). Lakini siku ya saba, katika mwisho wa mzunguko wa saba, wote wangepiga kelele na makuhani wangepiga tarumbeta â ambapo nguvu za Bwana zingeonekana na kuta za mji zingeanguka.
KUANGUKA WA YERIKO ( Yos. 6:8-25 ).
Kwa uzoefu wa kijeshi , hatua hii ya mashambulizi ilionekana kukosa msingi. Lakini Yoshua alikuwa mtu wa imani. Jinsi alivyokuwa Kapteni wa jeshi la Bwana aliwahimiza Israel kufanya hivyo hivyo. Tafakari imani aliyokuwa nayo ya kushikilia usukani kwa siku 6 , siku baada ya siku. Imani ilikuwa muhimu kwa kupata ushindi na hapo tunapata somo: "Kwa imani kuta za Yeriko , ziliaanguka chini, baada ya kuzunguka ukuta kwa siku 7 " (Ebr. 11:30).
Kila kitu katika mji huu kilikuwa kitolewe (mst. 17. ) , Kwa Yeriko ilikuwa aina ya " matunda ya kwanza ya Israeli na " mlango wa Israeli katika nchi . fedha, dhahabu, shaba na chuma tu ndio zingebaki na kuwekwa katika hazina ya Bwana. Vingine vyote vilikuwa viharibiwe kabisa. (Kum. 7:1-2 ; . 9:3-5 ).
Mji ukawekwa mikononi mwa wana wa Israeli , kwa sababu walifuata kwa makini maelekezo ya Bwana. Ushindi alikuja siku ya saba. Hivi inawakilishwa miaka elfu sita ya vita dhidi ya dhambi. Siku ya saba, wakati wa mwanzo wa milenia - Bwana atawapa ushindi Wale ambao wamethibitisha uaminifu. Katika kampeni dhidi ya Yeriko, WaIsraeli walikuwa wamsubirie Mungu Ambaye angeangusha kuta za Yeriko, kuonyesha kwamba mwili hauna nguvu katika vita dhidi ya dhambi. Ni Bwana pekee anaweza, kutoa ushindi. Sisi pia lazima kujisalimisha wenyewe kwa Mungu ili aweze kufanya kazi kupitia kwetu (Efe. 2:10 , Gal. 4:19. ).
Ni lazima kushiriki katika vita dhidi ya dhambi Mtume Paulo anasema, "Maana silaha zetu za vita ni za mwili, lakini zina uwezo katika Mungu kiasi cha kuangusha ngome " (2 Kor. 10:04 ). Katika vifungo vinavyofuata tunaelezewa jinsi ya kushida dhambi katika maisha yetu.: " tukiondoa mawazo na hoja, zinazo tuondoa katika elimu ya Mungu , na tukiteka fikra zote kwa utii wa Kristo"(2 Kor. 10:05 ).
MAFUNZO KWETU:
⢠Ingawa alikuwa wa jamii ya waovu, Rahabu aliamini Mungu : aliamini kwamba siku moja Mungu bila ya shaka ataingilia kati jamii , kuitoa kwa uharibifu. Imani yetu ya neno la Mungu pia inatupa imani kwamba Mungu hivi karibuni atafanya vivyo hivyo katika jamii yetu ya kisasa.
⢠Ingawa maisha yake ya zamani yalikuwa maovu, kuwasiliana kwake na Mungu wa Israeli kulisababisha yeye kuwa na imani katika Mungu na kisha akaonyesha imani hio kwa matendo. Kwa sababu Rahabu alitii na kuheshimu maneno ambayo wapelelezi walimwambia nao walikumbali na kumhakikishia usalama. Sisi pia, lazima tutende kulingana na mapenzi ya Mungu na maisha yetu yataokolewa.
⢠kama vile malaika wa uwepo wa Mungu alikuwa karibu na mkono wa Yoshua, hivyo Mungu anatumia malaika wake kuwalinda waumini wa leo .
⢠Imani ya WaIsraeli ilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu kama isiyo na maana kwa maandamano karibu na Jericho kabla ya mji kuanguka "kwa imani ". Ni lazima kuonyesha imani yetu katika mkono wa kuokoa wa Mungu kwa kubatizwa - tukio lingine ambayo linaonekana la ujinga duniani ni la ubatizo lakini ndio njia pekee ya wokovu.
⢠Vita vyetu " ni vita dhidi ya mwili na damu , " kuondoa " nguvu na hoja za binadamu na kutafuta njia ya elimu ya Mungu .
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Ways of Providence" (R. Roberts)âSura 12
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)âTol. 2, Nam. 9
"Joshua" (J. Ullman)âSura 2, 6
MASWALI YA AYA
1. Somo gani Yakobo anaonyesha katika maisha Rahabu?
2. Ni ripoti gani nzuri ambavyo wapelelezi wawili walitoa Yeriko na kumletea Yoshua?
3. Elezea mkutano kati ya Yoshua na nahodha wa jeshi la Bwana.
4. Kama Yoshua, tuna "vita" mbele yetu. Eleza vita vyetu vya leo. Jinsi gani kitabu cha Yoshua kutusaidia katika maisha yetu ya "vita"?
MASWALI YA INSHA:
1. Elezea jinsi Rahabu alibadilika kwa imani na kisha kwa matendo.
2. Elezea kuanguka kwa Yeriko. Ni somo gani tunalojifunza kutokana na tukio hili?
3. "Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka," (Ebr. 11:30). Elezea maana ya maneno hayo na uyahusishe katika hali yetu wenyewe.