CSSA 3-2-282 - DEFEAT AT AI

Swahili

282. Kushindwa  AI


                                                           "Wamechukua hata kile kitu kiliicho laaniwa"


WaIsraeli walikuwa wametengeneza ukuta wenye nguvu baada ya ushindi wao wa Yeriko. Si vigumu kujua mawazo ya watu wa Israeli wakati huo. Walijaa na furaha  jinsi Yahweh  alivyowapa ushindi dhidi ya ukuta imara wa Yeriko.  Walizidi kutarajia ushindi kama huo lakini hii ikawa kinyume. Hii ilikuwa ili watambue kwamba Mungu alihitaji imani na ujasiri zaidi kutoka kwao.  Pia walihitajika  kuonyesha utiifu, lengo la somo hili ni kuonyesha sheria ya Mungu inastahili kitiwa kabisa.

 

Yoshua 7, 8

MJI WA AI UNAFUNGA NJIA.
Kushindwa kwa Wakanaani katika Nchi ya Ahadi ulikamilishwa na ushambulizi wa kijeshi ambao ulipagwa kwa makini na kutekelezwa kwa nguvu za Mungu. Yoshua alipaga kuteka nchi kwa kutumia kampeni tatu kuu. Kwanza waIsraeli wangeshambulia kuanzia katikati ya nchi, hiyo  kufanya ukuta mkubwa ambao Wakaanani wangeshindwa kuvunja. Baada ya kugawanisha nchi kwa sehemu mbili Wakaanani wakashindwa  kupeleka majeshi kwa upande wa kusini au kaskazini. Hivyo hawangeweza kuondoa upizani wowote katika sehemu hio. Hatimaye, walikutana na jeshi lenye nguvu katika sehemu ya kaskazini mwa nchi.
Baada ya ushindi wa Yeriko, jeshi la Yoshua lilielekea Ai, mji wa kifalme wa Wakanaani, ulioko kilomita 20 kutoka Yeriko, magharibi kidogo kwa upande wa kaskazini. Ai ulikuwa ni mji mkubwa wenye thamani. (Mwa. 12:08).

 

MABADILIKO YA KUSHANGAZA (Yos. 7:1-5).


Yote hayakuwa sawa katika Israeli. Walikuwa " wamekosa " na kuficha makosa yao siku ilipokucha, mwanga wa mchana ulitokea. Israel  walikuwa wajifunze kwamba dhambi zote lazima ziadhibiwe kwa njia sawa ( Zab. . 32:1-5 ).

Kila mmoja katika Israeli alikuwa ameshiriki kwa "Jambo lililokatatazwa" ,  na walikuwa wamekatazwa kabla ya kuanguka kwa ukuta wa Yeriko. ( 6:18). Neno hili linaonyesha " kitu kilicho katazwa "; inapaswa ikumbukwe kwamba kila kitu katika Jericho kilikuwa kiharibiwe kama sadaka ya malimbuko ya ardhi . Isipokuwa tu " fedha , na dhahabu , na vyombo vya shaba na chuma" ambavyo vingetolewa kwa hazina ya Bwana (6:19) - Hii ilikuwa wazi katika malelezo kwamba kila  mtu katika Israeli alitarajiwa kuwa mtiifu. Lakini mtu mmoja alikataa kufuata neno la Mungu , na hivyo "hasira za Bwana zikarejea " ( 7:01 ).


Yoshua alimtuma askari kupeleleza maeneo jirani ya Ai. Ripoti yao ilikuwa na shauku zaidi : " Wanusuruni watu kwani maadui sio wengi. " (Mst. 3 Jerusalem Bible ).

Lakini imani Israel ilikuwa ya mda mfupi.  Baada ya  kushambulia mji ,  jeshi la Yoshua liliopunguka  " lilitoroka mbele ya watu wa Ai " (Mst. 4). " Mioyo ya watu ikayeyuka na kuwa maji " - hivyo, wana wa Israeli wakajikuata kwa  hali kama ile Wakanaani walikuwa nayo hapo awali  ( 2:11)

 

YOSHUA AOMBA MWONGOZO (Yos. 7:6-15 ).
Yoshua alikuwa na majonzi makubwa kutokana na matukio yaliyo fanyika  kwa hivyo alitaka kutafuta sababu ya maafa haya yaliyowatokea. (mst. 7-9) .
 
Mungu  naye akajibu ombi la mtumishi wake waaminifu : "Israel wametenda Dhambi " (Mst 11 ). Taifa limepatikan na hatia nne:

1. Walikuwa wamevunja kiapo kikuu;
2. Walikuwa wameiba kisichokuwa chao;
3. Walikuwa wametenda yasiyo ya kweli;
4. Walikuwa wamechukua kile ambacho kilikuwa cha Mungu na kukifanya chao .

Kwa hivyo WaIsraeli wakawa wamejitoa kwa uharibifu; tishio ambalo  lilikuwa tayari limefanyika na kuwauwa watu 36 katika shambulio la Ai;

 


Katika mazingira haya, Yoshua alitakiwa kutenda, na kuchukua  hatua za haraka , ili taifa liweze kuacha kutenda mauovu. Ilibidi “ awatakase watu ", kwa mahitaji ya Mungu. " Kutakasa" maana yake " kufanya safi ". Israeli walikuwa wajifunze kwamba usafi wa nje ni bure bila utakaso wa ndani.

Mataifa walitakiwa kukusanyika na kuwa katika sherehe muhimu zaidi. Walikuwa wakusanyike kulingana na makabila yao, kisha Bwana ataanza kutia alama kila kabila ,kisha ukoo, familia na mwishowe kaya, iliyokuwa na balaa. Basi itakuwa ile hali ya " aliye chukuliwa ..." (mst.15).Sherehe hii ya kutakasa ingekuwa ya maana kwa watu wa Israeli  na wangekubali ubaya wa dhambi na jukumu la kila mtu.
 

 Walio na hatia walikuwa " watekeketezwe kwa moto " – ili iwe kama hukumu ya Jericho ilikuwa imewakwamilia. (Zab. 06:24 na Kum. 4:24; Ebr. 12:29 ; Law 10:02 . . . )

Hii ilikuwa aina ya hukumu ambayo ilikuwa inatekelezwa wakati wa dhambi iliokithiri (Law. 20:14; 21:09 )
 

MWENYE HATIA ATAMBULIWA (YOS. 7:16-21 )

Kabila ya Yuda lilichukuliwa, kutoka ukoo wa Wazera , na jamii ya Zabidi . Na hatimaye, katika jamii ya Akani, ambaye jina lake linamaanisha  " matatizo" . Ni taabu gani ingelikumba  makabila yote. Kimya kimya, walisuburi kuona matukio ambayo yangetendeka. Na hatimaye ukweli ukafunuliwa: hatia ya Akani ikajulikana. Hii ilikuwa onyesho la miujiza wa Mungu anayeona yote na aliye kila mahali.  Hakuna mwenye dhambi anayeweza kuficha dhambi yake kutoka kwa Mungu wa Israeli (Mit. 15:03 ; . Yer. 32:19 ).

Akani mwovu na aliyekata tamaa aliletwa mbele ya Yoshua. Na kwa maagizo ya Yoshua, alikiri.  Alikuwa ameadhirika na tamaa ya macho: "Mimi niliona ... nikatamani..., nikachukua ... " (linganisha hatua ya dhambi ya Hawa katika Mwa. 3:6 na Yak. 1:14-15 ).  Alikaa mbali  na  magofu ya Yeriko, akiwa na shekeli mia mbili za fedha na dhahabu. makosa yake  vifaa hivi viwili alikuwa navyo vilistahili kuwekwa katika hazina ya Mungu.
Kumbuka , alikuwa ameficha vitu vya  kutolewa ardhini, katika hema yake. Hii inatuambia kwamba Akani alikuwa anajua kile alichokuwa akifanya. Hii ilikuwa ni dhambi iliyopangwa, na alikua amepanga pamoja na familia yake. Kwa sababu hiyo pia wao walikuwa na makosa na wakaadhibiwa pamoja na akani.

 

 

UAMUZI DHIDI YA DHAMBI (YOS. 7:22-26 ).
 Uamuzi  huu wa kutisha ulipitishwa na hukumu kutolewa. Akani na familia yake, pamoja na mali zao zote , walichukuliwa hadi bonde la Akori . Hukumu iliyotolewa ilisimamia kukanusha kwa dhambi kwa taifa. Walipigwa na mawe hadi kufa na kisha kuteketezwa moto. " Bwana atakuwa shida yako" , yalikuwa maneno ambayo alinena akiongoza utekelezaji wa hukumu, kuonyesha kwamba Mungu ni mmoja ambaye anaweza kuharibu dhambi.

Bonde lilipewa jina Akori ( neno sawa na Akani ) , hivyo kuonyesha kwamba Bwana ataendelea kuadhibu dhambi mpaka pale itakapo shindwa kabisa. Lakini katika ufalme Umri bonde hili litakuwa linajulikana kama Pethach Tiqvah maana yake ( mlango wa tumaini), hivyo kufundisha binaadamu ambao  watapitia njia hiyo katika safari yao ya kwenda Hekaluni, Bwana atazidi kupambana na kuharibu dhambi - na kama wangejisalimisha wenyewe kwa mapenzi yake, Angewafungulia mlango " mlango wa tumaini " ambapo hatimaye wangepata uzima wa milele. ( Hos. 2:15; . Isa. 65:10 ).

 

KURUDI AI (YOS. 8:1-14).

Baada ya neno lake kuzingatiwa, Mungu aliahidi Israeli ushindi (mst. 1-2). Yoshua alielekea Ai tena. Kwa kutumia ujuzi wake wa kijeshi  alipeleka jeshi lake usiku. Aligawanya  jeshi lake  and kuwaweka tayari  kushambulia. Akaliambia jeshi lake kwamba: "tutakimbia mbele yao, wao watatufuata" (mst. 5-6). Yoshua alielewa asili ya binadamu. Alijua kwamba watu wa Ai watakuwa wamejiamini  kwa sababu ya ushindi wao wa awali dhidi ya Israeli na watakuwa tayari kuwashinda kwa kutoka nje ya mji. Watu wa Ai waliona jeshi la Israeli na walikuwa tayari kabisa kupigana. Wao "wakaondoka mapema" kufanya maandalizi kwa wakati uliopangwa na mfalme wa Ai, wakaenda katika vita bila kujua kuhusu mpango wa shambulizi uliokuwa nyuma ya mji (mst. 14).

 

 

USHINDI WA IMANI NA UTII (YOS. 8:15-29 ).
 Wakanaani walitoka nje ya ngome yao wamejaa ujasiri, nao waIsraeli "walijifanya kushindwa " (Mst. 15). Wakakimbia " , na kuwafanya watu wa Ai kuwafuata wakielekea mbali na mji – Jinsi WaIsraeli walivyo toroka ndivyo ujasiri wa adui zao ulizidi. Hakika ya ushindi wao waliwaita wanaume wote wenye nguvu waliobaki mjini kuungana nao kuwafuata WaIsraeli na kuhakikisha ushindi kabisa. Lakini katika kufanya hivyo, " wakauacha mji ". Yoshua alitoa ishara kwa watu waliojificha kushambulia mji . Waliondoka kwa kasi na kuingia mjini na kutwaa (mst. 19) .
Jeshi la Ai, wakiwafuata jeshi la Israeli walianza kuhisi kuna jambo ambalo sio sahihi, waligeuka na kwa mshangao waliuona mji wao ukiwaka moto. Hofu iliwaingia na ghafla wakahisi kuishiwa na nguvu. ( mst. 20). Jeshi lililokuwa linatoroka la Israeli likawageukia watu wa Ai waliokubwa na mshutuko. Kuungana kwa wenzao. Jeshi la Ai likazingirwa na jeshi la Yoshua kutoka pande zote mbili. Matokeo yake yakawa dhahiri. " Hawakuacha hata mmoja wao aponee” (mst. 22), hivyo wakatimiza matakwa ya Sheria (Kum.7:1-2 ).
Kwa kukamilisha ushindi, Mfalme wa Ai aliuawa na kutundikwa juu ya mti ( Mst. 29). Ai maana yake ni " uharibifu " na Mfalme huyu alikuwa mfano wa  “mfalme wa dhambi” ambaye alitamani kututawala (War. 6:12). Lakini katika vita vyetu vya imani , ni lazima auawe na " kuharibiwa " badala ya kumwacha atuharibu sisi”. Ukweli ni kwamba Mfalme wa Ai ilikuwa  â€œametundikwa juu ya mti" ni ishara ya kuonyesha kusubishwa kwa mwili, njia ambayo dhambi inashindwa na hatimaye kuharibiwa kabisa  kwa huruma ya Mungu (Gal. 5:24).

 

MAFUNZO KWETU:
• Dhambi ya Akani ilikuwa ni tamaa ya vitu vya kimwili - nguo, fedha na dhahabu - pengine alifikiria vitu hivi vingeweza mpa  usalama wa maisha. Amri ya Yesu ilikuwa kwanza "kutafuta ufalme wa Mungu" (Mat. 6:19-21, 31-34).
• Akani alificha dhambi yake kutoka kwa ndugu zake, lakini hakuweza kuificha kutoka kwa Mungu. Ukweli ni kwamba Mungu anayajua mawazo na matendo yetu na tunapaswa kujishawishi jinsi tunavyo fikiria na kutenda. (Ebr. 4:13).
• Dhambi inaweza kuonekana nzuri kwa muda, lakini mwishowe huleta "matatizo" (Akani) na itasababisha uharibifu wetu, kama Akani ilivyotambua pale alipelekwa katika bonde la Akori ("shida") na kupigwa mawe.
• Wito wa kwenda kinyume na Ai na mfalme wake (aina ya Mfalme wa dhambi) ilielezwa kwa maneno, "Usiogope, wala usifadhaike; ... inukeni, mwende" (Yos. 8:01). Maneno haya yanatuhimiza tuendelee na vita dhidi ya dhambi kwa msaada ambao Mungu ametupa.

 

 

MAKTABA YA KUREJELEA

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 2, Nam. 9, 10

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)— Sura 21

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 12

"Joshua" (J. Ullman)—Sura 7-8

MASWALI YA AYA
1. Nini maana ya neno "kitu haramu" Yeriko na kwa nini wana wa Israeli walikatazwa kushiriki?
2. Dhambi ya Akani ilikuwa gani? Kwa jibu lako elezea sehemu tatu za dhambi yake na ulinganishe dhambi hii na ile ya Hawa.
3. Katika Ufalme wa Umri, binadamu watafikia Hekalu kupitia bonde la Akori. Watajifunza nini?
4. Mfalme wa Ai aliuawa na kutundikwa juu ya mti. Elezea umuhimu ishara ya hii.

MASWALI YA INSHA
1. Elezea jinsi Akani alitia wasiwasi watu wa Israel na jinsi dhambi yake iliwekwa wazi. Ni masomo gani  tunajifunza kutokana na hili?
2. Kwa nini Mungu kuondoa msaada wake kwa waIsrael katika jaribio lao la kwanza kushinda Ai, na tunapaswa kujifunza nini  kutoka na kushindwa kwao?
3. Elezea kwa kifupi jinsi mji wa Ai ulichukulia na jinsi mfalme wao aliharibiwa. Katika jibu lako elezea  masomo tunayo jifunza kutokana na tukio hii.

 

 

 

Swahili Title
282. Kushindwa AI
English files
Swahili file
Sub type
Sub sub type