287. GIDEON AIKOMBOA ISRAELI
" Kwa nini basi haya yote yametupata? iko wapi miujiza yake yote"
Katika Isa. 09:04 na 10:26 ushindi wa ajabu wa Gideon umeelezwa kama mfano wa ushindi wa Kristo juu ya majeshi ya watu, kwa ushindi wake sio kwa nguvu za kijeshi, lakini kwa nguvu za Mungu. Jeshi la Gideoni lilikuwa na watu wachache waliokosa imani, walio waoga na wenye upele walikuwa washaondolewa. Walioobaki walikuwa watu 300 wenye imani, waliangamiza majeshi ya muungano wa Wamidiani na Waamaleki na kusababisha wao kupigana wenyewe kwa wenyewe.
Lengo la somo hili ni kuonyesha kwamba Mungu anaweza kutoakoa kutoka kwa hatari kubwa, cha muhimu ni kumgeukia kwa ukweili na uaminifu kamili.
Waamuzi 6 , 7 , 8
DHAMBI HULETA MATESO (AMU. 6:1-10) .
Wana wa Israeli walitenda dhambi tena mbele ya macho ya Bwana (Mst.1) na akawaaachilia kwa Wamidiani , Waamaleki na " wana wa mashariki. " Watu hawa walivuka mipaka ya waIsraeli wakiwa juu ya ngamia na kutawala Israeli kwa ukatili, waliwaweka katika hali ya hofu na woga. Wakatawaliwa na wafalme wawili , Zeba na Salmuna, wakishirikiana na wakuu wawili - Orebu na Zeebu (maana yake " Mwewe" na " Mbwa mwitu" )
Vita vilipiganiwa katika Mlima. Tabori ambapo WaIsraeli walishindwa na ndugu za Gideoni wakauawa (8:18), ili kwamba mkono wa Midiani ukapata ushindi (6:02). Na sasa Israeli wakakabiliwa na ukandamizaji wenye uchungu. Moto na upanga ulieneza hofu kila mahali. Uporaji na mauaji ulifanya WaIsraeli kukimbilia mapango na ngome zilizokuwa juu ya vichwa vya vilima. Mazao yao yalikuliwa na wavamizi na nyumba zao kuharibiwa.
Kwa nini waliteseka? Kwa sababu ya dhambi. Na mateso yote katika dunia yanatokana na dhambi. Huu ni urithi ambao binadamu amejiletea yeye mwenyewe na jambo la kipekee kufanya katika hali hii ni kama walivyofanya waIsraeli.
Walipokabiliwa na njaa na kukata tamaa, WaIsrael walimgeukia Mungu. Alimtuma nabii ambaye aliwakumbusha watu jinsi wame-asi dhidi ya Mungu na kukosa kutii sauti yake. Hivyo akawaonyesha sababu ya mateso yao yote. Pamoja na tabia ya udhaifu ya binadamu pengine walimlaumu kila kitu na kila kitu ila wao wenyewe.
WITO WA GIDEONI (Amu. 6:11-24 ).
Mungu alimtuma malaika kwa Gideon, mwana wa Yoashi. Alikuwa akipepeta ngano kwa siri kwa hofu ya WaMidiani. Malaika alimpa changamoto na kumwambia , " Bwana yu pamoja nawe, wewe mtu shujaa ". Gideoni alikuwa na haraka ya kutii yale aliyoyasikia kwani yale aliyoyaona yalikuwa ya madhubuti. Alihoji huduma ya Mungu kwa Israeli kwani aliona wakiwa kwenye uonevu. Lakini swali lake lilifutiliwa mbali na akaamuriwa kwenda kuwakomboa wana wa Israeli kutoka kwa Wamidiani. Ni vikwazo gani vingekuwepo kama Mungu alikuwa pamoja naye ?
Hata hivyo hii ilikuwa ni kazi kubwa ambayo Gideoni alikuwa amepewa. Nchi ilikuwa imejaa na maadui mbalimbali na wenye nguvu. WaIsrael wakajawa na hofu kubwa kwani hawakuwa na nguvu zozote za kivita. Si ajabu Gideon ali omba ishara. Nayo ikatolewa. Gideoni alikuwa ametayarisha chakula kwa ajili ya malaika na kukiweka juu ya jiwe. Malaika alipogusa chakula hiko na fimbo yake papo hapo moto ukawaka naye Gideoni akatambua kwamba alikuwa " amemkaribisha malaika pasipo kujua" na akashikwa na hofu (Ebr. 13:2) . Mtazamo wake wenye shaka na kukata tamaa ukageuka na kuwa wa uamuzi na hatua. Akawa na moyo na uhakika na imani ya Bwana, ambapo alijenga madhabahu na kuyaita Bwana - shalom ( Bwana ni amani ).
IBADA YA BAALI KUANGUSHWA (AMU. 6:25-32).
Lakini kabla ya Israeli kukombolewa kutoka kwa maadui wao, lazima ibada ya Baali ingeharibiwa. Ili kufuata utii na maelekezo ya Mungu (Mst.25-26), Gideoni alichukua watumishi kumi jasiri na kuangusha madhabahu ya Baali yaliyokuwa ya baba yake. Aliikata sanamu ya mbao iliyokuwa imeshikilia ile sanamu na hapo akajenga madhabahu ya bwana, akitumia mbao zile za sanamu kama kuni alimtayarishia Mungu sadaka.
Alifanya hayo yote usiku kwa sababu watu wa kijiji kile walikuwa wacha Baali. Asubuhi ilipowadia walitaka kumuua Gideoni lakini Yoashi, baba yake, akawaambia, "Kama Baali ni mungu kweli, wacha ajitetee mwenyewe." Imani Yoashi katika Mungu ilikuwa imerejeshwa na ujasiri na imani ya mwanawe, kama vile imani ya taifa.
WAISRAELI WANAKUSANYIKA (AMU. 6:33-40).
Haya yote hakwenda bila kutambuliwa na Wamidiani. Waliweza kuona vitendo vya Gideoni na jinsi alivyowatia WaIsraeli msisimko wa roho kwa kupanda mbegu ya uasi. Wakakusanya jeshi kubwa kukabiliana na uasi. Wakati huo Gideoni naye alikuwa ameshatuma wajumbe kwa makabila mbalimbali ili wakusanyike. (angalia ms. 34-35) . Ukilinganisha idadi ya wavamizi, na idadi ya WaIsraeli waliounganika chini ya Gideoni walikuwa wachache sana. Kuona hivi Gideoni akaomba ishara nyingine kutoka kwa Mungu ili kuonyesha yu pamoja naye. Ishara ilitolewa. Kama alivyoomba, Wakati Gideoni aliweka ngozi ya kondoo nje usiku mmoja, aliamka na kupata ngozi ile imejaa umande,ilhali ardhi ilikuwa kavu kabisa. Ishara hii iligeuzwa usiku uliofuatia na Gideoni akajua kwamba Mungu alikuwa pamoja naye.
JESHI LA GIDEON LAPUNGUZWA HADI WATU 300 ( Amu. 7:1-8 ).
WaIsraeli elfu thelathini na mbili waliitikia mwito wa Gideon ( Mst.3). Walikusanyika katika bonde la Yezreeli karibu na kisima ambacho kiliitwa Harod (" tetemeko'') Kwa sababu ya hofu yao.
Waliona jeshi la Wamidiani waliojihami kwa silaha, idadi yao ikifikia watu 135,000 ( 8:10) . Walikuwa na vifaa vikali vya vita na walifahamu nguvu za adui. Lakini Mungu alisema kuwa jeshi la Israeli lilikuwa kubwa mno. Hivyo ingekuwa rahisi kwa waIsraeli kujipa sifa ya ushindi wao ( 07:02 ) Mungu Alitoa mwito kwa Gideon kuwaondoa wale waliokuwa waoga na wenye hofu (ona Kum. 20:08 ). Na 10,000 waliobaki.
Hata hivyo, bado walikuwa wengi. Nguvu za Mungu " zingedhihirika kwa udhaifu." Gideoni aliambiwa kuwapeleka mtoni na kuwatizama jinsi wanavyokunywa maji. Wale waliotumbikuza vichwa vyao mtoni waliambia wasimame upande, wale waliochota ,maji kwa mikono macho yao yakiangalia uwepo wa adui, waliwekwa upande wa pili. Waliotumbukiza vichwa ndani ya maji waliondolewa, sasa jeshi la Gideoni likabaki watu 300 tu.
NDOTO YA USHINDI (Amu. 7:9-15 ).
Mungu Aliamwamuru Gideoni kufanya mwendo wa usiku akiwa na Mtumishi wake Phura aliyembebea silaha ili akaone jeshi la Midiani. Wakitambaa kichini chini, walikwenda hadi nje kidogo ya kambi. Wakiwa hapa nguvu kamili ya adui zingekuwa dhahiri kwa Gideoni. Kwa wingi wao Walionekana kama mkusanyiko wa nzige." Huu ulikuwa mfano wa nguvu za kimwili. Kwa maagizo ya Mungu, Gideon na mtumishi wake walikwenda karibu na kambi ya adui wakati wa usiku, hapa walisikia askari wawili wakizungumza katika hema zao. Moja alielezea ndoto yake. Aliona keki ya mkate wa shayiri imetupwa katika kambi ya Wamidiani na ilipongonga hema ikapinduka juu. Rafiki yake akamjibu: " Hili si jambo lingine ila upanga wa Gideoni mwana wa Yoashi , mtu wa Israeli : kwani katika mikono yake Mungu ameweweka Wamidiani na jeshi lote " (Mst.14).
Mkate wa shayiri ilikuwa kitu kidogo kugeuza hema ya WaMidiani, Aidha shayiri ilikuwa chakula cha maskini. Somo liilikuwa wazi. Mbele ya macho ya binadamu, Jeshi la Israeli lilikuwa dogo lakini nguvu za Mungu zingedhihirika wakati wa udhaifu wa binadamu. Tafsiri ya ndoto pia ilionyesha jinsi Gideoni alikuwa ameogopwa - Tayari alikuwa ameshapata ushindi wa kisaikolojia. Alitiwa Moyo na hili, na akaamua kufanya mashambulizi ya ghafla.
USHINDI (Amu. 7:16-25 , 8:1-23 ).
Gideon aliwagawanywa watu wake 300 katika makundi matatu. Alimpa kila mtu tarumbeta na mwenge uliofunikwa na mtungi. Kwa kuenea waliweza kuwazingira majeshi yote ya Midiani. Usiku wa manane â wakati wa kubadilishwa kwa walinzi wa Midiani waIsraeli wakashambulia (Mst.19) . Wamidiani waliamshwa kwa ghafla na sauti za tarumbeta, kutoka kwa watu 300 na mwangaza wa mienge 300 na kupiga kelele, "Upanga wa Bwana na wa Gideoni ." Wakiwa tayari wamejazwa na wasiwasi, adui waliamka kwa hofu. Katika machafuko ya giza ,hali ya kuchanganyikiwa ilizuka na wakaanza kukimbia kiholela wakielekea chini ya bonde kila mtu akiwa na upanga dhidi ya mwenzake . Wakati huo wana wa Israeli 300 "walisimama kila mtu katika sehemu yake pande zote kambi" (Mst.21) . Kweli Mungu alikuwa amewaweka WaMidiani katika mikono ya Gideoni" (Mst.15) .
Gideon alikuwa amewaomba kabila la Efraim msaada, sasa Waefraimu walikusanyika kwenye vivuko vya mto Yorodani kuwazuia Wamidiani waliokuwa wakitoroka. Wakuu wawili Orebu na Zeebu Wakakamatwa (Mst.24-25).
Wamidiani Elfu kumi na tano walitoroka chini ya wakuu wao Zeba na Salmuna, na wakajificha mbali mahali penye usalama ( 8:10-11) . Walifikiria wametorokea upanga wa Gideoni, lakini Gideoni na watu wake 300 waliokuwa wamechoka waliwafuata. Walipowapata waliwaangamiza wote pamoja na wakuu wao Zeba na Salmuna.
Kisha alirudi na kuwaadhibu wale WaIsraeli ambao walikataa kumsaidia katika vita vyake na Wamidiani. Kabila kubwa ya WaEphraim lilionyesha wivu kwa mafanikio ya Gideon, lakini alitumia maneno matulivu yaliyogeuza hasira zao. (8:1-2;. Met 15:1). Lakini miji ya Sukothi na Penueli ilikuwa imekataa kumsaidia Gideoni na jeshi lake kwani walikuwa na shaka kama wangefaulu na pia waliogopa kuadhibiwa na WaMidiani (Mst.5-9), kwa hivyo waliadhibiwa pia(Mst.13-17;. Linganisha Hes. 33:55-56).
Gideon aliombwa na wana wa Israeli awe mfalme wao, lakini alikataa na kusema, "Bwana atatawala juu yenu." Hivyo Israeli wakaishi na amani siku zote za Gideon.
MFANO WA BWANA YESU.
Gideon alitoa mfano mzuri wa kazi ya ajabu ya Bwana Yesu (Isa. 09:04 , 10:26 ). Hizi ni baadhi ya kazi hizo;
1. Nyumba ya baba yake ilikuwa imeziacha njia za Mungu âvivyo hivyo WaIsrael walikuwa katika siku za Bwana Yesu Kristo.
2. Jina lake lilimaanisha, "Shujaa mkuu "- Bwana Yesu pia alikuwa " Shujaa Mkuu zaidi " (Isa. 09:06 ).
3 . Aliangusha ibada ya Baali kama vile Bwana Yesu ataangusha dhambi zote. (Ufu. 18).
4. Alianzisha tena ibada ya Bwana - Bwana Yesu atafanya vivyo hivyo (Zek. 14:16).
5 . Aliondoa shaka na uoga kwa wafuasi wake - Bwana Yesu naye atafanya vivyo hivyo akiwa kwenye kiti cha hukumu ( Rum.14 : 10).
6. Pamoja na wafuasi wake aliwashinda adui wa Israeli bila kutumia silaha âBwana Yesu atafanya hivyo wakati atakaporudi kwa mara ya pili (Eze. 38:19-22 ).
7. Baada ya ushindi, aliwaadhibu WaIsraeli ambao walikataa mwito wake, Itakuwa hivyo wakati Bwana Yesu atarudi kwa mara ya pili. (Zek. 12:10).
8. Akawa mtawala ( Jaji ) katika Israel- pia Bwana Yesu atakavyokuwa wakati atakapokuja kwa mara ya pili. (Mat.17:31 , Mic 05:02 . ).
MAFUNZO KWETU:
⢠Nguvu za Mungu hudhihirika katika udhaifu. "Kama vile Mungu alipunguza jeshi la Gideon kutoka 32,000 hadi 300, ili Gideon aweze kutegemea zaidi nguvu ya Mungu ili kuepuka maadui wa Israeli.
⢠Uzoefu wa maisha yetu unatufundisha kwamba tukitegemea nguvu za kibinadamu, basi kazi zetu hazitaambulia popote. Lakini kama tukitafuta msaada wa Mungu na kuweka imani kwake, tunaweza kushinda matatizo ya maisha.
⢠Kama ukombozi wa awali, Mungu alimhitaji Gideoni kuharibu madhabahu ya Baali, kama ibada ya sanamu ni lazima iwekwe kando na wale ambao wanatafuta msaada wa Mungu.
⢠Kushindwa kwa WaMidiani katika mikono ya Gideoni imetumiwa na nabii Isaya kama aina ya kazi ya baadaye ya Yesu Kristo.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Visible Hand of God" (R. Roberts)âsura 21
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)âTol.3, NaM. 1, 2
"The Judges" (C.S.S.S. Study Notes)
MASWALI YA AYA:
1. Nini dalili gani Mungu alimpa Gideoni ili kuonyesha kwamba angewaokoa WaIsraeli kwa mkono wake?
2. Ni somo Mungu alikuwa anafundisha wakati alipunguza ukubwa wa jeshi la Gideoni?
3. Jinsi gani jeshi la Gideon la watu 300 liliweza kushinda majeshi ya Wamidiani na Waamaleki?
MASWALI YA INSHA :
1. Ni somo gani kubwa tunalopata kutokana na maandalizi ya Gideoni na jeshi lake?
2. Elezea jinsi jeshi Gideoni lilivyopuguzwa kwa ukubwa. Je, hii inatufunza nini?
3. Jinsi gani kazi ya Gideoni inafanana ile ya Bwana Yesu Kristo?