CSSA 3-2-289 - RUTH

Swahili

289. RUTH
"Watu wako watakuwa watu wangu , na Mungu wako atakuwa Mungu wangu "


Hadithi ya Ruth inatoa mfano wa mwanamke mwema na mwenye maadili kutoka kwa watu wa mataifa  aliyetamani kuwa na ushirikiano na mama mkwe wake wa Kiyahudi,hadi akapokea urithi katika Israeli, na hatimaye kuwa babu ya Daudi na Kristo. Mungu alimwongoza Ruth kwa Boaz ambaye mtazamo wake kwa mahitaji yake ulionyesha unyenyekevu licha ya utajiri wake.

Lengo la somo hili ni kuonyesha kwamba Mungu  " hana upendeleo " - katika wakati huu wa machafuko katika Israeli, Ruth alionyeshwa neema na Mungu, kwa kuwa Mtu mwaminifu wa mataifa, hii ilikuwa kwa misingi ya imani na matendo yake.


Ruth 1 na 4

HISTORIA YA MACHAFUKO
Hadithi ya Ruth ni ya kuvutia zaidi ikitizamwa katika mazingira ya nyakati. Tabia yake inaonekana bora zaidi ikilinganishwa na machafuko ya kutisha ya mazingira yake - ". Kila mtu alifanya yaliyokuwa ni mema  katika macho yake mwenyewe wakati waamuzi walitawala "ambayo Rekodi ya Ruth imewekwa kati ya rekodi ya kushuka kwa roho ya uasi juu ya Israeli na wakati wa Waamuzi na rekodi ya kutengenezwa tena chini ya Samweli ambaye alitayarisha njia ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu chini ya Daudi. Ni muhimu basi kuelewa kwamba ni watu wachache walikuwa waaminifu wakati ule wenye hali ngumu na hali ya tamaa. Kama ilivyokuwa katika nyakati nyingine. Kwa mfano, watu 7000 walikataa kupiga goti mbele ya Baali katika nyakati za wafalme waovu Ahabu na Yezebeli alitawala (1 kil. 19:18).

Nyakati zetu ni kama kioo cha siku za Waamuzi. Katika hadithi ya Ruth tunaweza tukapata moyo wa kutafuta ufalme wa Mungu kwa unyenyekevu na uaminifu kupitia kukubali tumaini la Israeli na kumtumikia Bwana katika kujitayarisha  kwa ajili ya kushiriki katika Ufalme wa Mungu - licha ya sisi kuishi katika nyakati za kuharibu imani. Mujibu wa Ruth, imani yenye nguvu ya Boaz, na subira ya Naomi, zote zinatofautiana na uovu ulioko leo.

NJAA KATIKA NCHI (RUTH 1:1-2).
Kulikuwa na njaa katika nchi, na hii inaweza kuwa kama dalili ya umaskini wa kiroho wa  WaIsraeli ( Amo. 8:11) , kwani  Mungu aliwatakasa watu wake kwa njia hii (angalia Law 26:18-20 ;  Zab. 105:16 ; . Amo. 4:6-10). Elimeleki (ambaye jina lake lilimaanisha " Mungu wangu ni mfalme" ), katika kipindi cha njaa, aliamua kuondoka Bethlehemu ya Yuda ( "Nyumba ya Mkate na Sifa" ) na kwenda kuishi Moabu, nchi ya Mataifa mbali na nchi yake ya urithi. Haja ya kutafuta riziki ilikuwa ya asili, lakini ukosefu wa imani pia ulikuwa wazi.
Elimeleki aliacha nyumba ya Mkate na Sifa akaelekea nchi ya dhambi na mauti , na hivyo kuonyesha majanga ya kabla uhamisho na majanga  yatakayowakumba  watu wake katika  vizazi vifuatavyo. Elimeleki alikwenda Moabu, akiwa na mke wake Naomi na wanawe wawili Maloni na Kilioni.

UZOEFU WA NAOMI NA FAMILIA  YAKE (RUTH 1:3-22 ).
Huzuni ya Naomi ilianza na kifo cha Elimeleki. Kisha wanawe wawili wakaoa wanawake wa Moabi , Maloni akaoa Ruth (4:10) , na Kilioni kuoa Orpa . katika mstari wa 15 Inaonekana kwamba Orpa, alikuwa mwabudu sanamu, na alitaka kuingiza familia ya Elimeleki katika njia za waMmoabi. Hii ilikuwa ni athari ya kushirikiana na wale wasioamini" (2 Kor. 6:14-18 ;  Kum. 7:1-4) . Maloni (maana yake " mgonjwa, au dhaifu" ) na Kilioni ( kupoteza ") alikufa baada ya miaka kumi. Majina yao labda yalionyesha hali yao ya kimwili.
 Naomi alikumbwa na hali kutisha : alikuwa mjane na mtoto kutoka nchi ya kigeni. Familia yake yote ilikuwa imetoka katika "Nyumba ya Mkate" (Bethlehemu ) na kupata chakula katika Moabu ilikuwa shida kwani watu wa familia yake walikuwa wamekufa.
Hata hivyo, habari ilimfikia kwamba Mungu anatoa mkate katika Yuda, ambapo aliamua kurudi (Mst.6) . Aliwahimiza binti- mkwe wake kubaki Moabu. Baada ya kusitasita, Orpa alikubali, lakini Ruth alikuwa ameamua kuacha historia yake ya Mmoabi na kutafuta njia mpya ya maisha kwa kuandamana na Naomi (Mst.14) .

 

Uamizi wake ( Mst.16, 17)  ulionyesha hali ya usafi na kujitolea kwa kwa hali ya juu kwa Naomi na matumaini Naomi yake. Pia kwa watu na Mungu . kwa hivyo alihitambulisha kama Ecclesia wa Mataifa alipojitambulisha na matumaini ya Israeli na kuacha kazi zake za zamani za giza. Kwa vile Musa alichagua " kuteseka pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia raha ya dhambi ambayo ni ya muda " (Ebr. 11:25; tizama Phil 3:13; . Mat. 11:23).
Wawili hawa walirudi Bethlehemu, ikawa msisimko mkubwa wa mji . Naomi hakutaka kujulikana kama  Naomi (" maana yake kupendeza sana, neema, utamu "), lakini kwa sababu ya huzuni yake alitaka kujulikana kama Mara ( " chungu "). Walipofika "katika mwanzo wa mavuno ya shayiri " (Mst.22) ambayo ni wakati sawa na sikukuu ya Pasaka, sikukuu ambayo inazungumzia ukombozi. Huu ulikuwa wakati mzuri kwa Naomi na Ruth kurudi wakati matumaini ya Mungu na ukombozi yalikuwa yameanza kukumbukwa tena Israeli.


MKONO WA UKOMBOZI ( RUTH 2 NA 3) .
jukumu la Ruth kujisaidia yeye na kumsaidia Naomi lilikuwa kuokota masalio ya mavuno bila kujua kwamba wanaongozwa katika shamba la Boazi. Sheria ilikuwa imeruhusu maskini kuokota mabaki ya mavuno (angalia Law. 19:9-10 ; . 23:22 ; . Kum. 24:19) , ingawa wamiliki wengine wa ardhi walikuwa na neema kuliko wengine kwani waliwagawia maskini chakula.

 Alibarikiwa kwa kufika katika shamba la Boazi ambaye alionyesha huruma na hali ya kuwajali watumishi wake. Aliwamkua kwa salamu, " Bwana awe pamoja nawe", na walijibu, " Bwana akubariki " ( 2:04 ). Hivyo uongozi wa Boazi na kuwalisha watumishi wake, uliongozwa na hofu  ya Mungu (Efe. 6:5-9 ). Ingawa uovu ulijaa duniani, kulikuwa na haki katika shamba la Boazi (ambaye jina lake lilimaanisha " ndani yake ni nguvu ").
Ruth alijitoa kwa bidii katika kazi yake (Mst.7) , na wakati Boazi alimwona , aliongea naye kwa ukarimu  alimwahidi ulinzi kama angekaa karibu na wavunaji wake (aya 14 , 21). Kazi yake ilibarikiwa na Bwana " ambaye  alikuwa amemweka chini ya bawa zake" (Mst.11, 12) . Boaz aliwaambia wavunaji wake kubakisha mazao mengi ili Ruth aweze kuokota. Sisi pia tuna  uhakika wa baraka kama tutafanya kazi kwa bidii katika mashamba ya Bwana Yesu Kristo (Lu. 11:9-13) , ingawa tuko kama Ruth , " wageni kutoka jamii ya Israeli na wageni katika maagano ya ahadi " (Efe. 2:12 , 13; . 1 Pet. 2:09 , 10).

Baada ya kurudi kwa Naomi na malipo tele ya kazi kwa sababu ya bidii  yake , Ruth alitambua kwamba kwamba Boazi alikuwa  jamaa wa karibu. Kwa hivyo alitiwa moyo na Naomi azidi kubaki katika mashamba yake, karibu na wajakazi wake wa kike, kwani katika nyakati za Waamuzi, zilijaa hatari.
Baada ya muda, Naomi aliimpa Ruth maelekezo ende kwa njia ya unyenyekevu mbele Boaz na kumwomba amkomboe, ili apate ulinzi na usalama wa mwanamume (3:1-5).

 

SHERIA YA  UKOMBOZI.
Sheria ya Ukombozi ilishirikisha  mambo yafuatayo:
• Kama mtu amekuwa maskini, na alihitaji kuuza ardhi yake, ilikuwa ni wajibu wa jamaa wa karibu  kuikomboa kwa ajili yake, kwa kuinunua ile ardhi, au kulipa lile deni (Law. 25: 25).
• Kama mtu amekuwa maskini, na kuamua kujiuza yeye mwenyewe kama mtumwa kwa mgeni, basi yule aliye na uhusiano wa karibu angeweza kulipa  ili awekwe huru (Law. 25:47-48).
• Kama mtu amekufa bila kuacha mrithi, ilikuwa ni wajibu wa jamaa wa karibu kuoa mjane wake na kulea watoto katika jina la mtu aliyekufa ili jina lake pia lisisahaulike katika Israeli (Kum. 25:5 - 10; Lu. 20:28).

Ruth alikuwa katika hali ya kuhitaji mkombozi.

BOAZ ANAKUWA MKOBOZI WA RUTH (RUTH 4).
Boaz aliguswa na ukataji wa rufaa wa dhati wa Ruth. Alijua yeye ni mtu wa tabia nzuri - "kwani watu wote ndani ya mji wangu wanajua kwamba wewe ni mwanamke mwema", alisema (3:11). Alitaka kumsaidia lakini kulikuwa na jamaa wa karibu ambaye lazima angepewa nafasi kwanza ya kumkomboa. Boaz alichukua haja ya Ruth kwa jamaa wa karibu ambaye alikataa kumkomboa (4:6), na hivyo akamruhusu Boaz kumchukua Ruth kama mkewe.


Baada ya muda Ruth akajifungua Obedi, na kuleta furaha kubwa kwa Naomi kwani sasa mbegu ilikuwa imeanza kukua katika nyumba ya Elimeleki. Obedi baadaye akakuwa  babake Yese, baba ya Daudi (4:17). Hivyo  Ruth akawa babu wa Bwana Yesu Kristo (Mat. 01:05), ukweli ambao unaeleza kwamba ni imani na sio ukoo wa kimwili ambao unafanya mtu kukubalika na Mungu.
 

KRISTO MKOMBOZI WETU.
Tabia Nzuri ya Boaz  inaashiria Kristo mkombozi wetu ambaye yuko tayari kutukomboa sisi kama  tutanyesha haja yetu kwa dhati na kwa vitendo vyetu.Kwa upande mwingine, jamaa aliyekataa kumkomboa anaashiria sheria iliyo katikati ya njia ya ukombozi ambayo tunaambiwa haiwezi kutukomboa. Pet. 1:18; . . Gal. 3:17-19).

Kumbuka mambo yafuatayo:
• Mkombozi lazima awe jamaa wa karibu (Law. 25:48-49 ). Kristo ni wa mbari yetu kwa sababu alikuwa wa asili yetu (Ebr. 2:14-15).
• Mkombozi lazima awe na uwezo wa kutukomboa (Rut. 4:6). Kristo alikuwa na uwezo wa kujitoa mwenyewe kama sadaka kamili kwa ajili ya ukombozi wetu (Rum 3:24-25 , Ufu. 5:9-10).
• Mkombozi alinunua mtu na urithi ( Rut. 04:05 ; . Law. 25:25 , 47, 48 ). Hivyo  Kristo  aliwakomboa wale ambao ni watumwa wa sheria ya dhambi na kifo, na kutoa urithi katika ufalme wa Mungu. Hivyo sisi " tumekombolewa kwa damu tukufu ya Kristo , kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala doa" (1 Pet. 1:18-19; . . Isa 61:1-3) .

Somo la Ruth ni somo la ukombozi. Wokovu utapewa wale watakao jitenga na mambo ya dunia na kumtumikia yesu kwa uaminifu Kristo. Wale ambao watatafuta ukombozi kwa unyenyekevu wataupata katika Kristo.

MAFUNZO KWETU

  • Katika nyakati za Waamuzi, watu walimwogopa Mungu na waliishi kwa imani, sisi pia tunaweza simama mbali na uovu wa dunia na kujifunza mambo ambayo ni safi mbele ya Mungu.
  • Hakuna matumaini kwa kuacha njia ya Ukweli kama vile Elimelech alifanya kwa kutoka Israeli. Ushirika na wengine katika ukweli  utatatusaidia kumfuata Mungu.
  • Uzoefu wa Maisha ulimfunza Naomi somo na akamsihi Ruth kukaa karibu na mashamba ya Boaz na karibu na watumishi wake. Kwa Msingi Ruth aliambiwa akae karibu na ecclesai akifanya kazi kwa karibu na ndugu zake.
  • Hadithi hii inaonyesha Ruth kama eccelesia wa Mataifa na Boaz kama Yesu Kristo anayetoa ukombozi.

 

MAKTABA YA KUREJELEA

 

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield) — Tol. 3, Nam. 5

"The Christadelphian Expositor" (H. P. Mansfield)—Kitabu cha Ruth

MASWALI YA AYA

  1. Ruth alijibu nini wakati Naomi alimwambia abaki Moab?
  2. Ni kwa nini Naomi alitaka kubadili jina aitwe “Mara”
  3. Imani ya Ruth kwa Mungu ilitukuzwa  kwa njia gani?

 

MASWALI YA INSHA

  1. Ni mafunzo gani tunajifunza kutoka safari ya Elimeleki hadi Moab na kuishi huko
  2. Andika kuhusu utafiti wa tabia ya Ruth na Wamoabi
  3. Elezea jinsi Boaz anaashiria kazi ya ukombozi iliyofanywa na Kristo.
  4. Kama watu wa mataifa, ni masoma gani tunaweza jifunza kutoka kuongezewa kwa Ruth katika ukoo wa Israeli hadi kuzaliwa kwa yesu.

 

 

 

Swahili Title
289. RUTH
English files
Swahili file
Sub type
Sub sub type