CSSA 3-2-292 - SAUL: THE PEOPLE'S CHOICE

Swahili

292. SAULO: CHAGUO LA WATU

"Waonyeshe jinsi Mflame atakavyo watawala"

Kwa miaka 450 Israeli ilikuwa ikitawalwa na majaji ambao walikuwa wamechaguliwa na Mungu mara kwa mara ili kuja kuwaokoa wana wa Israeli kutoka kwa aina tofauti ya ukandamizaji. Kipindi hiki  kikahitimisha siku za Samweli ambaye kwa uaminifu alifunza sheria na kuisambaza kwa watu katika njia ya Bwana. Alipozeeka aliwateuwa wana wake kuwa majaji wa Israeli, lakini "hawakufuata njia zake." Badala ya kufuata nyayo za baba yao, upendo wao wa fedha uliwapotosha  na wakawa wala rushwa (1 Samweli 8:1-3).
Tabia ya wana wa Samweli ilisababisha wazee wa Israeli kwenda kwa Samweli na kumsihi ateuwe mfalme ili waweze kutawalwa kama vile mataifa jirani yalivyo kuwa yanatawaliwa. (8:4-5). Walikuwa wamesahau kwamba Bwana ndiye aliyekuwa mfalme wao.

Lengo letu katika somo hili ni kuona umuhimu wa kufuata njia iliyoteuliwa na Mungu badala ya kufanya mambo kwa mapenzi yetu wenyewe.

1 Samweli 8, 9 , 10

 

TAIFA LINATAMANI KUWA NA MFALME (1 Sam. 8:1-5).
Ingawa ni  wazee waliotumwa kwa Samweli ili kumwomba ateue Mflame, ni dhahiri kwamba taifa kwa ujumla lilitaka litawaliwe na mfalme (Mst.19, 20). Sababu yao ya kutaka mfalme ni majaji walikuwa wameguka na kuwa wapenda rushwa hivyo walitaka  kiongozi mmoja atakayekuwa na Mamlaka kamili kwa upande wa utawala na vita, kama ilivyokuwa na Wafalme wa mataifa jirani.
Lakini hapakuwa na uhakika kwamba Mfalme atakaye chaguliwa atakuwa na tofauti yoyote na majaji. Ingawa mwenendo wa wana wa Samweli ulisababisha maombi ya watu, nia yao halisi ilikuwa waliona wivu  na walitamani mienendo watu wa mataifa  na walitaka kuishi kama wao. Utukufu wa kifalme wa kidunia ambao waliuona na macho kuwa mzuri kuliko  "ufalme wa milele na wakudumu" (1 Tim. 1:17) mbali na hayo, wawakilishi hawakuwa na mamlaka zaidi na majaji.

UJINGA WA OMBI LA WAISRAELI ((1 Sam. 8:6-9).

Kwa kuomba mfalme wa ulimwengu, Israeli  walifanya makosa mawili. Kwanza, Samweli alidhani kwamba walikuwa wanamkataa, Lakini Mungu alimwambia wazi kwamba sio Samweli walikuwa wanamkataa, lakini ni Mungu wa mbinguni ambaye aliwaongoza na kuwalinda kuanzia siku ilie walipotoka Misri, licha ya kuasi na kutokosa shukrani kwao ( Mst.7-8).
Msaada ambao Mungu alikuwa amewapa ulisahaulika haraka. Walidhani wakipata mflame wa kidunia wataweza kuepuka matatizo na kuwashinda maaadui zao, hawakuelewa kwamba ilikuwa ni kwa neema ya Mungu waliweza kufanya jambo lolote. Kama mwandishi wa Zaburi alivyosema, jambo ambalo WaIsraeli hawakuwa wametambua, "usiweke imani yako katika wakuu, Wala kwa mwana wa binadamu, kwani kwake hakuna msaada ... atakaye faidi ni yule atakaye mtafuta Mungu wa Yakobo awe msaada wake , na ambaye tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake "(Zab. 146:3, 5).

Ni jambo la hekima kwetu sisi kuweka matumaini yetu katika ushauri wa Mungu badala ya kupokea  ushauri kutoka kwa wale ambao hawana ufahamu njia zake. Tabia za siku za mwisho zitakuwa uasi na ukosefu wa imani (2 Tim. 3:1-5). Ni vyema kufikiri kuhusu baraka na faida ya kuishi kwa Ukweli na hivyo ni muhimu kutoa shukrani kwa Baba yetu wa mbinguni wakati wote.

Pili kwa kutamani kuwa kama mataifa  mengine Israeli walikuwa  wanakataa wito wao wa Kimungu-Watu walionyesha kwamba hawakujua njia za Mungu. Kama Musa hangekumbusha taifa katika mwisho wa kipindi cha miaka Arobaini ya kuzurura kwamba ni Mungu alikuwa amewakomboa na kuwatenganisha na watu wa mataifa. “Nyinyi ni watoto wa Bwana Mungu wenu....aliye mtakatifu na amewachagua kama taifa lake alilojichagulia juu ya mataifa mengine duniani (Kum 14:1-2).

Lakini sasa hawakutamani kujitenga bali walitaka kufanana na mataifa mengine na utawala wao. Israeli ilikuwa imeitwa Taifa lilikuwa juu ya mataifa mengine lakini baada ya muda usio kuwa mrefu wangejipata chini.

Hisia za taifa zinaweza fupishwa na maneno kutoka kwa kitabu cha 'The Man David' Kuanzia marejesho ya taifa na Mungu kupitia Samweli, kulitokea hali ya  umoja katiak taifa hali ambayo haijawahi onekana kwa vizazi vingi. Makabila kumi na mawili kutoka Dani mpaka Beer-sheba walielezewa kuhusu ushirikiano na nguvu. Tunashangaa kuona kwamba hali hii ya umoja na kushikamana kwa taifa kulileta tamaa ya kutaka kuwa na mflame wa kidunia. Samweli alisikitishwa na haya, kwani maisha yake yote alifanya kazi ya kujitolea. Ukosefu huu wa shukrani na heshima ulimtia machungu  hasa wakati huu alikuwa amezeeka. Matarajio haya mpya ya taifa yalitokana na sababu kubwa zaidi kuliko kumkosea heshima mtu  huyu mkubwa;. imani ya taifa ilishindwa kuona Mungu katika mnara. Walitaka kubadili utukufu wa Mungu usio kuwa na ufisadi na kuchukua uongozi wa binadamu uliojaa ufisadi. Hii ilikuwa njia ya maafa kwa taifa la Israeli, nasi hatupaswi kuanguka kwa mtego huo kama watu binafsi. "
Tukumbuke kwamba Mungu anatamani sisi tujitenge na desturi na mitazamo ya dunia ambayo tunaishi sasa ili tuwe watu wa kipekee na  "kumpa sifa yeye ambaye ametuita kutoka kwenye giza an kutuleta kwa nuru yake ya ajabu "(1 Pet. 2:09). Hamu ya Israel kuwa kama mataifa  mengine iliwaongoza kwa maafa- hebu tizingatie somo hili.

MZIGO WA MFALME WA KIDUNIA (1 Sam. 8:10-22)

Akifuata maagizo ya Mungu Samweli aliwaelezea watu matatizo na gharama ya kudumisha mfalme wa kidunia. Aliwafafanulia kwamba wengi wao wataajiriwa kama watumishi na watatozwa kodi  na Mazao yao yatachukuliwa kulisha wafalme(Mst.12-18). Lakini maneno ya Samweli hayakusikizwa kwani walikuwa washaamua: "Tunataka kuwa Mfalme wetu” walimjibu",(Mst.19).

Watu wa Israeli walikuwa wakaidi na katika siku za Samweli haikuwa tofauti. Nyoyo zao zikawa ngumu kwani hawakusikia maneno ya ushauri. Kuna hatari kwetu sisi, kwani tunaweza kuwa na mioyo migumu na kufuata mipango yetu bila kujali. Kwa upole na hekima ni vyema tutambue kwamba sio kila mara tutajua kile kilicho bora nasi na tunapaswa kuwa tayari kukubali sauti ya maandiko na maaelekezo kwa ajili ya faida yetu wenyewe.

MFALME ALIYECHANGULIWA (1 Sam. 9)

Mtu aliyechanguliwa na Bwana awe mfalme wa Israeli alilingana na matakwa yao. Walitaka kiongozi atakaye waongoza katika vita kama tunavyosoma katika 1 Samweli 9:02 kwamba Sauli alikuwa " kijana mzuri  na wa Kimungu...  na jukumu la taifa lilikuwa juu ya mabega yake, na alikuwa mrefu kuliko watu wote. " Kwa mtu huyu Israel waliweka imani yao lakini walikuja kutambua kwamba kimo na nguvu za kimwili sio mambo muhimu katika suala la utawala wa taifa (linganisha 2 Sam. 23:03). Baadaye Zaburi ilisema kuwa , "Hakuna mfalme anayeokoloewa na wingi wa jeshi lake: mtu hodari hawezi okolewa na  nguvu zake" (Zab. 33:16).
Ni dhahiri kwamba katika kitabu cha 1 Sam. 2:10 kumbukumbu inatolewa na mamake Samweli akiiashiria mfalme ambaye atakuwa ameteuliwa na Mungu. Sheria ambayo Mungu aliwapa zamani ilionyesha kwamba wakati utafika na watapata mfalme atakaye weka masharti na sheria katika kuteuliwa kwake. (Kum. 17:14-20, Linganisha. Pia Mwa 49:10 na 28:36 Kum -. "hautaweka kitu juu yako" – huu ilikuwa utabiri wa kifalme ulionzishwa na watu utaongoza watu kwa njia ya dhambi na utumwa. Dhambi ya watu ilikuwa kwa mtazamo wao – walikuwa na suala hilo kwa hamu, badala ya kumsubiria Mungu. Ilikuwa wazi, hata hivyo, kwamba Samweli ndiye angekuwa kuhani wa mwisho na nabii wa kwanza ambaye ataadhiri mabadiliko ya kifalme (1 Sam. 2:35). Kwa hiyo, licha ya kusita kwake, aliitwa ili "kuisikiliza sauti ya watu" (1 Sam 08:09, 22;.. Linganisha 9:16).

Lakini wakati Bwana alipomteua Sauli kama watu walivyotaka, alikuwa tayari kuwaongoza na kumsaidia mfalme ili aweze kutoa taifa kutoka kwa ukandamizaji. Kwa kweli hii ilikuwa inahusiana na Samweli (9:16). Huruma na uvumilivu wa Mungu ulionekana katika tukio hilo katika historia ya Israeli. Watu walikua wamemkataa Mungu, lakini Mungu alikuwa tayari kuwasaidia. Sauli angeweza kufanikiwa kama Mtawala, kama angefuata maagizo na kuelekeza akili yake kwa neno la Mungu na akumbuke maneno ya kutia moyo wa Samweli, "Mungu yu pamoja nawe" (10:07)

KUCHANGULIWA RASMI KWA SAULI (1 Sam. 10)

 Sauli alikuwa wa kabila la Benyamini, maarufu kwa kurusha  kwa mkono wa kushoto. Tunasoma katika mstari wa 1 kwamba alikuwa ametauliwa na Samweli kabla ya kuwasilishwa kwa watu. Kisha kuka kuwa na uchanguzi rasmi. Samweli aliwakusanya  watu kule Mispa.Akawakumbusha tena yale yote Bwana alikuwa amewafanyia kuanzia siku ile waliotoka Misri. Lengo la Samweli lilikuwa kuwaonyesha wti kuwa halikuwa jambo rahisi kuomba mfalme kwani hii ilionyesha kumkataa Mungu wao (Mst.17-19). Bila shaka kuna wakati katika maisha yetu tunapomkataa Mungu na tunafuata mambo ya kidunia yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Tunawezakuchukulia mambo hayo kwa njia ya wepesi, lakini maneno ya Samweli kwa WaIsraeli ni kwetu pia ili tuweze kuchukulia hii kama onyo kutoka kwa Mungu wakati kunapotoka kwa njia zake.

Sauli aliletwa mbele ya watu na  maneno haya kutamkwa, "Angalieni yule Bwana amemchagua, hakuna aliye kama yeye miongoni mwa watu wote" (Mst.24).
Sifa za kiroho za Sauli hazijatajwa ila tu umbo lake- ambalo lilikuwa la kupendeza mbele ya taifa ambalo lilikuwa limeacha njia za Mungu (Mst.23). "Mungu kuokoa mfalme" au "Wacha Mfalme aishi", watu wamlilia huku wakipiga kelele kwani walijarajia mabadiliko kwa siku za usoni. Lakini mfalme ambaye alikuwa mkuu na hivi karibuni angewacha uongozi wa Mungu na kuangusha taifa.

MAFUNZO KWETU

  •  Uamuzi unapotoka wakati imani inakosekana na watu wanashindwa kutambua njia za Mungu
  • Kamwe tusiwe kama waIsraeli kwa kumtumainia Mfalme wa duaniani kwa ulinzi wetu
  • Ni lazima tutambue kwamba majaribio tunayojipatia hatuwezi pata msaada kwa binadamu kwani yatatuelekeza kwa maovu.
  • Ingawa Mungu haonekani mbele ya macho yetu, ni yeye tunapaswa kumwamini kwani  ndiye msaidizi na ngao yetu.

MAKTABA YA KUREJELEA

"The Man David" (H. Tennant) — kurasa 15-16

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 14

"The Visible Hand of God" (R. Roberts) — Sura 22

MASWALI YA AYA

  1. Ni makosa gani WaIsraeli walifanya kwa kutaka mfalme? Ni mafunzo gani ya kibinafsi tunaweza kujifunza kutokana na ombi la Waisralei la mfalme.
  2. Ni onyo gani ambalo Samweli aliwapa WaIsraeli kuhusu chaguo lao la kutaka Mflame.
  3. Ni sifa gani ambazo wana wa Israeli walikuwa wanatafuta kwa mfalme ambaye walitaka awatawale? Ubaya wake ulikuwa upi?

    MASWALI YA INSHA
    1. Kwa nini waIsrael walitamani kuwa na mfalme na nini ilikuwa ubaya wa tabia zao?
    2. Andika insha juu ya hamu ya WaIsraeli kutaka mfalme wa kidunia. Katika jibu lako onyesha yafuatayo:
    a. Kwa nini hamu yao ilikuwa na makosa.
    b. MaJibu ya Samweli na majibu ya Mungu.
    c. Masomo ya kibinafsi tunayoweza kujifunza kutoka kwa matukio haya.

 

 

Swahili Title
292. SAULO: CHAGUO LA WATU
English files
Sub type
Sub sub type