CSSA 3-2-293 - SAUL'S FAILURE

Swahili

293. KUANGUKA KWA SAULI

"Kutii ni bora kuliko dhabihu, na kisikiza ni bora kuliko mafuta ya kondoo"

Mwanzo wa utawala wa Sauli ulijaa matumaini, kama angezidi kuwa mnyenyekevu na azidi kuweka matumaini yake kwa nguvu za Yawheh basi mafanikio yangemfuata. Kazi ya Sauli ya kwanza ilikuwa kuwaangamiza Waamoni ambao walikuwa wanatishia wakaazi wa Yabesh-Gileadi (1 Sam. 11:01). Uongozi wake katika kuwashinda Waamoni ulikuwa wa kutia moyo lakini jambo la kufurahisha zaidi lilikuwa jinsi alivyo mpa Mungu shukrani kwa ushindi huo kwani ndiye aliyekuwa amewapa WaIsraeli ushindi ule. “Leo Yahweh amewapa wokovu wana wa Israeli.”(mst.13) ilionekana kwamba tamaa ya watu ya kupata uongozi mzuri ilikuwa na Sauli. Lakini hadithi ya kuanguka kwake na kukataliwa kama Mfalme ndio mojawapo ya hadithi za kutisha katika kumbukumbu.

Lengo letu katika somo hili ni kutoa muhstasari wa sababu zilizofanya Sauli kukataliwa na kuelewa kanunu zinazokubalika na Mungu.

WAFILIPI WANATISHA WAISRAELI (1 Sam. 13:1-7)

Tunasoma katika 1 Sam. 7:13 kwamba “ Mkono wa Yahweh ulikuwa dhidi ya Wafilisti katika siku zote za Samweli, ilikuwa ni katika siku za kwanza za utawala wa Sauli wafilisti walianza kuingilia mipaka ya WaIsraeli. Ilionekana kana kwamba Mungu amekubalia haya kutokea ili aweze kuijaribu imani ya Sauli. Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Sauli, mwanawe Jonathan alikuwa tayari kuchukua hatua dhidi ya Wafilipi. Kwa ujasiri alipiga ngome ya wafilisti iliyokuwa kilomita 15 kaskazini mwa Yerusalem, Sauli alifurahishwa na ushindi huu, alitangaza mafanikio hayo kwa mataifa ya mbali na kwa watu wengi. (Mst.1-4).

Kupigwa kwa ngome hii kulikuwa ishara kwa Wafilipi kupanga mashambulizi mengine makali, watu wote waliitwa pamoja kule Gilgal ili kupanga hatua za siku zijazo.

Lakini WaIsraeli sio pekee waliokuwa wakijitayarisha kwa vita, Wafilipi baada ya kushindwa wakiwa Geba walikuwa wanajitayarisha kwenda vitani. (Mst.5)  Walikusanya Jeshi kubwa ikiwa ni pamoja na magari ya farasi na wakakusanyika Mikamashi umbali wa kilomita 25 mashariki mwa Gilgal.

Jambo hili lilitia shaka Imani ya Sauli hasa pale ilipochanganyisha uwonga wa watu wake, alishindwa. Badala ya kuweka imani yake kwa Mungu watu walichanganyikiwa. Wengine wao walijificha mapangoni, kwenye vichaka na mahali popote walipopata. Kuna wale waliotorokea kupitia mto Yorodani hadi nchi ya Gileadi. Tunaweza fikiria jinsi jambo hili lilivyomwathiri Sauli, kama ilivyo andikwa kwa kumbukumbu “ kwa ajili ya Sauli, aliyebaki Gilgal na wote waliomfuata walitetemeka” (Mst.7)

IMANI NA UTII WA SAULI UNAJARIBIWA (1 Sam. 13:8)

Hapa ndipo palikuwa na mtihani mkubwa wa imani ya Sauli, aliamriwa kusubiri Gilgal kwa siku saba mpaka Samweli afike atoe sadaka ya kuteketezwa kama toleo la imani kwa Mungu kabla kufanya mashambulizi dhidi ya watu wa Wifilisti.Hali iliyomzunguka Sauli haikuwa ya kutia moyo. Jeshi la kutisha lilikuwa umbali wa kilomita 25 kwa upande wa mashariki na alikuwa amezungukwa na watu wenye uoga na hofu kila upande.

Ungefanya nini kama ungekuwa katika mazingira haya? Tunajua vile Sauli alifanya, lakini ni heri tukumbuke kwamba matukio haya yameandikwa ili tuweze kujifunza na kupata mawaidha. Kutakuwa na nyakati katika maisha yetu wakati tunapokumbana na mambo yanayohitaji imani yetu. Kumbuka kwamba Mungu hatupatii majaribio ambayo hatuwezi yashinda.

Alipowekwa katika nafasi hii ngumu, Sauli alipaswa kukumbuka maneno ya kutia moyo yaliyo semwa na Samweli wakati  alipokuwa anamteua kama Mfalme: Fanya  kama vile unavyoona inapasa kwani Mungu yu pamoja nawe” (1 Sam. 10:07.) je kama Mungu hangekuwa naye? Sauli alitambua haya wakati aliwaangamiza Waamoni (1 Sam. 11:13). Na si miaka mingi iliyopita Mungu alikuwa ameaahidi kupitia kwa kinywa cha Musa kwamba “ Nita wafukuza maadui zenu na wataanguka  mbele yenu kwa upanga. Watano kati yenu watawafukuza mamia yao na mamia yenu watawafanya maelfu yao kutoroka. Na maadui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.

Kama Sauli angetafakari kuhusu haya, matatizo yaliyomkumba yangeweza epukika. Lakini badala yake alishindwa kwa kukosa imani.

KUTOTII NA KUKATALIWA KWA SAULI KAMA MFALME (1 Sam. 13:9-22)

Kama vile siku zilivyozidi kusonga ndivyo Sauli alizidi kuingiwa na woga. Mwishowe siku ya saba ilipofika bila ya Samweli kutokea, Sauli kwa kukata tamaa aliamua kutoa sadaka ya kuteketeza yeye mwenyewe. Alidhani kwamba Mungu atasahau kwamba alikuwa ameondoka kwa njia maalum ya ibada. Kitendo hiki kilikuwa cha ujinga. Angetambua kwamba wale tu walioteuliwa na Mungu ndio walipaswa kutoa sadaka na njia nyingine yeyote ilikuwa bure. Baadae katika Historia ya Israeli, mfalme mwingine, Uzia alipuuza Sheria ya Mungu na kutoa madhabahu. Kwa sababu hii alipigwa na ugonjwa wa ukoma kwenye kipaji cha uso (2 Nya. 26:16-21) Hii ni adhabu ya Mungu kwa makadirio hayo.

Punde tu Sauli alimaliza kutoa sadaka, samweli akafika na kuuliza nini kilichokuwa kimetendeka. Sauli alimjibu bila kuogopa kwamba alikuwa ametoa sadaka yeye mwenyewe kwa sababu alikuwa mwoga. Hakuwa akitarajia maneno makali yaliyofuata kutoka kwa Samweli. Kwa fikra zake hakuona kana kwamba alikuwa amevunja amri, Samweli alipaswa amsamehe kosa na kila kitu kingekuwa sawa.

Jibu kutoka kwa Samweli lilikuwa ufunua wa jinsi Mungu anavyochukulia uasi wa amri zake; “umefanya ujinga” na matokea yake ni kwamba “Ufalme hautaanzishwa” (Roth) ingawa Sauli hakuwa amekataliwa kabisa ( 1 Sam. 15:26) Uridhi wa kizazi chake katika ufalme ulikuwa umeisha. Mungu alikuwa anatafuta “Mtu atakaye upendeza moyo wake” kwani yeye huangalia roho ya mtu na wala sio kimo. (1 Sam. 13:13-14;. 16:07;. Zab. 89:20).

Tunaweza pata taswira ya kutisha pale Samweli alipogeuka na kurudi Gibea huku akimwacha Sauli akiwa amevunjika moyo huku amezungukwa na kundi ndogo la watu walikuwa na hofu.

Sauli  angepata ushindi mkubwa juu ya Wafilipi kama angetii, lakini WaIsraeli waliabishwa na Wafilisti walipoingia katika makao yao. (Mst.17-22)

SAULI NA WAMELEKI—FURSA YA KUTUBU (1 Sam. 15:1-3)

Imani ya Sauli ilikuwa ijaribiwe tena. Fursa hii ilikuwa ya kuonyesha kama alikuwa amejifunza somo kule Gilgal. Kutoka kwa nafasi ya udhaifu, Sauli aliweza kujiiunua na kupata ushindi wa mataifa yaliyo mzunguka (1 Sam. 14) Ndipo Samweli alikuja akiwa na maagizo kuhusu Waamaleki (Mst.1-3) ni muhimu kutambua kwamba maneno ya kwanza ya Samweli yalikuwa “sikia sasa...

Maagizo hayo yalikuwa kamili. Sauli alipaswa awaangamize Waamaleki wote na vyote walivyokuwa navyo- kila mme na mke, watoto, mbuzi, ngombe, ngamia na punda”

Hapakuwa na shaka ya maagizo kuhusu maafa yaliyopaswa kutimizwa, na juu ya hayo maneno ya Samweli yalisisitiza kwamba kuendelezwa Ufalme wa Sauli kulitegemea kutii kwake. Sababu ya kuharibiwa kwao inaweza  kuonekana kama kali. Wamaleki ndio walikuwa taifa la kwanza kuwashambulia wana wa Israeli baada ya kuondoka Misri na kufanya safari yao ya kuelekea nchi ya ahadi kuwa ngumu.(Hes. 24:20). Kwa nguvu za Yahweh Yoshua aliweza kuwaangamiza na baada ya Ushindi huo Mungu akamuamuru Musa kuandika kumbukumbu katika kitabu  kwamba ataweka ukumbuka wa Amaleki chini ya mbigu. (Kut. 17:14)

Baadae, wakiwa katika kikomo cha miaka Arobaini ya kuzunguka jagwani, Musa anakumbuka tukio hili and kuwakumbusha watu jinsi taifa hili lenye woga lilivyo wapiga na kuwaangamiza wana wa Israeli waliokuwa hafifu na dhaifu(Kum. 25:17-18). Kisha akawakumbusha kwa mara nyingine azimio la Mungu kuliangamiza taifa hili. Waameleki wakakuwa ishara ya kufaa ya kuonyesha dhambi ambayo ni vita tunavyopaswa kupigana katika safari ya kuelekea nchi ya ahadi.

SAULI ANACHUKULIA KWA WEPESI AMRI YA MUNGU (1 Sam. 15:4-9)

Kama Sauli angetambua jinsi Mungu alivyowachukulia Waamaleki basi angetekeleza amri ya Mungu kwa kikamilifu. Lakini kutoka kwa tukio la Gilgal tunaelewa jinsi Sauli alivyofikiria na kutenda. Hakuwa mtu wa kiroho na hakutambua kanuni za kiroho. Alifikiria kwamba Mungu angeridhika na mambo madogo. Alikuwa ameelekeza na hangeshughulika na mambo madogo. Lakini tunapata kwamba badala ya kuharibu kila kitu kama alivyoamriwa alimnusuru Agagi pamoja na wanyama walio bora kwa kisingizio kwamba angewatoa kama sadaka kwa Mungu baadaye. Hili lilikuwa lengo nzuri kwa maoni yake ingawa hakuwa ametenda kama alivyoamriwa na Mungu. Ni kwa nini Mungu hakufurahishwa naye?

Lakini Sauli alikosa lengo kuu la maagizo. Haikujalisha uzuri wa  nia zake kwani zilikuwa bure kama hakufanya alivyoamriwa.

KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU (1 Sam. 15:10-26)

Mungu aichunguzaye fikra na nia za nyoyo zetu aliona yote yaliokuwa yamefanyika and kutofanyika. Baada ya kuelezewa Samweli ambaye bila shaka alikuwa anatumai Saul atakuwa na tabia tofauti alihuzunika sana na kumlilia Mungu usiku kucha.(mst.11)

Kesho yake alienda kumwona Saul kule Gilgal akiwa na moyo mzito. Sauli alimtokea akiwa na ujasiri na furaha ya ushindi wake, alimwambia Samweli “Baraka ziwe kwa Mungu, nimetenda amri ya Bwana” (Mst.13)

Lakini Samweli hakufurahishwa na onyesho hili la utakatifu. Kwa sauti ya kejeli alijibu “ nini maana ya makelele ya kondoo kwa masikio yangu na sauti za ngombe ninazosikia” (Mst.14)  sauti za wanyama zikawa ushahidi dhidi ya Sauli kuonyesha kwamba hakuwa ametimiza amri ya Mungu.

Sauli alijitetea bila mafanikio na kusema kwamba alikuwa na sababu ya kuweka wanyama wale. Amri ilikuwa rahisi, lakini alikuwa ameivunja kwa hivyo ilibidi aondolewe (Mst.17-19) Samweli alimkumbusha kwamba wakati alikuwa mdogo mbele ya  macho yake, Mungu alimfanya kuwa Mfalme. Hivyo alipaswa kutii amri za Mungu. Sauli alijaribu kwa mara nyingine kuhalalisha vitendo vyake. Alidai kwamba alikuwa ametii sauti ya Yahweh” lakini watu na wanyama alionusuru walikuwa wawe sadaka kwa Mungu”  kujitetea huku kungekubalika mbele ya macho ya mwanadamu wa kawaida lakini sio kwa mwakilishi mteuliwa wa Mungu Samweli.

Maneno ya Samweli ya kukemea yalifuata, thamani ya sadaka na utii inaonekana wazi kwa mara ya kwanza.  Kiini halisi cha sadaka na  ni utii. Samweli alisema “  Yahweh anafurahia sadaka za kuteketeza ama kutii sauti yake? Hivyo basi kutii ni bora kuliko sadaka, na kusikiliza kuliko mafuta ya kondoo”

Wengi wanatoa sadaka lakini ni wachache wanao sikiza Neno na kutii- ambayo ni muhimu kuliko nia yoyote nzuri.  Dunia ya kidini katika jitihada za kuwafurahisha watu imetupilia mbali Neno la Mungu kama Sauli. Katika madhebehu mengi imani ya injili na ubatizo hufuzwa kuwa muhimu kwa wokovu. Badala yake wanaamini kwamba kazi nzuri italeta wokovu na kutafuta kukubalika mbele ya macho ya Mungu.

Msingi wa dhambi ya Sauli ulikuwa kukosa imani- alikuwa awajali watu kuliko Mungu na kutenda kulingana na mapenzi ya binadamu.(linganisha 1 Nya. 10:13-14.) Tazama jinsi vifungu vifuatavyo vimeandikwa katika wakati ujao, vinaonyesha utii kuwa muhimu kuliko sadaka. (Zab. 40:6-8; 50:8-9; 51:15-17;. Mit 15:08; 5:01 Ekk. na Yer. 7:22-23) ili kusisitiza ukubwa wa dhambi ya Sauli kabla kuangalia mtizamo wake wa kiroho uliokuwa hafifu, Samweli alilinganisha uasi na uchawi pamoja na ukaidi na uovu. Hii ina ukweli kama inavyoonekana katika matendo ya mwisho ya maisha ya Sauli wakati ukosefu wake wa Imani ulimpelekea kwa uchawi (1 Sam. 28) Mbeleni ni uzao wake uliokuwa umekataliwa kuridhi ufalme na sasa ni yeye “aliyekataliwa kuwa mfalme”

MAFUNZO KWETU:

  • Sauli hakufikiria kwamba  dhambi yake ilikuwa kubwa. Ni bora kwetu kufikiria kwa makini matendo yetu mbele ya macho ya yule anayeona yote.
  • Hakuna anayeweza jifikiria ana hatia kwa kuabudu miungu ama uchawi, lakini katika maisha yetu ya kila siku fikra na matendo yetu yamezungukwa na haya.
  • Sauli alikuwa muasi kwani hakufuata maagizo ya Neno la Mungu ila alifuata hisia na ushauri wake mwenyewe.
  • Leo tunaishi katika jamii ambapo utii na heshima ya walio mamlakani inadharauliwa na wengi na kuna hatari kwamba tunaweza ambukizwa tabia hii.
  • Baba yetu wa Mbiguni amejaa na huruma na msamaha lakini “hatawaondolea hatia wenye hatia” kama vile Sauli alivyotambua kwa msiba wake.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Man David" (H. Tennant)—kurasa 15-18

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—sura 23

MASWALI YA AYA:

  • Jinsi gani Sauli alijaribiwa kule Gilgal na alishindwa kwa njia gani ?
  • Kwa nini Mungu aliwachagua Wamaleki kwa uharibifu kamili?
  • Toa muhstasari wa mazungumzo ya Samweli na Sauli aliporudi baada ya kuwaangamiza Waamaleki.

MASWALI YA AYA

  1. “Utii ni bora zaidi kuliko dhabihu” Elezea sentensi hii na utoe mifano kutoka kwa maisha ya Saul.
  2. Kwanini Sauli alikaliwa kama mfalme?
  3. Ni mafunzo gani tunayojifunza kutoka kwa kuanguka katika maisha ya Sauli?

 

 

Swahili Title
293. KUANGUKA KWA SAULI
English files
Sub type
Sub sub type