CSSA 3-2-295 - DAVID AND GOLIATH

Swahili

295. DAUDI NA GOLIATHI

"Yahweh anaokoa sio kwa upanga na mkuki"

 

Waisrael waliwekwa mikononi mwa wafilisti kwa sababu ya maovu yao (Amu. 13:01) ukandamizaji huu wa Wafilisti uliendelea wakati wa Sauli. Kwa haya historia ya Daudi inaonekana akiwa kijana mwaminifu.

Hadithi ya ushindi wa Daudi juu ya Goliathi ukaja kuwa hadithi itakayojulikana vyema kote duniani Wengi waliona ushindi wa Daudi kama bahati tu lakini Daudi alisema kwamba hii ilikuwa “ ndio dunia nzima ijue kwamba kuna Mungu katika Israeli” (1 Sam. 17:46)

Lengo letu katika kuchunguza ushindi wa Daudi ni kuona vile Imani inashinda vikwazo “ huu ni ushindi ambao unashinda hata imani yetu” (1 Yoh 5:04.)

 

1 Samweli 17

CHANGAMOTO YA WAFILISTI (1 Sam. 17:1-3)

Kuna kumbukumbu moja ya kuvutia zaidi katika uvamizi wa wafilisti  katika 1 Samweli 17. Hapa tunasoma kuhusu majeshi yaliyokusanyika kwa upande pande mbili za bonde la Elah.

Wafilisti walishambulia karibu na bonde na kunyakua kilomita kadhaa za ardhi. Sauli naye alijibu kwa kukusanya jeshi lake kwa upande mwingine wa bonde kuzuia adui kuingia zaidi. Pande zote mbili zilikuwa na nafasi nzuri iliyojificha kutokana na mashambulio lakini hawangeweza kusonga mbele. Kufanya hivi kungemaanisha kuacha ngome zao upande wa bonde na kuteremka chini ya bonde kisha kupanda upande wa pili hivyo kujiachilia wazi kwa ushambulizi wa silaha za maadui zao.

Taswira ya sehemu inayohusika inaweza kutusaidia kuelewa matukio haya, angalia Maktaba na utaona kwamba bonde la Elah lilisonga hadi nchi ya Yuda, kusini-magharibi mwa Yerusalemu, upande wa magharibi kupitia ardhi ya chini ya Ashdodi hadi ziwa la Mediterenea. Bonde hili lilitoa njia ya moja kwa moja kwa wafilisti kuingia hadi katikati kwa Israeli. Shochoh na Azeka zilikuwa milki za Yudah (mst. 1;. Yos. 15:35) lakini kwa wakati huu zilikuwa zimechukuliwa na Wafilisti (linganisha Josh 15:47.)

GOLIATHI, MTU WA MWILI (1 Sam. 17:4-11)

Kwa sababu majeshi walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, Goliathi aliyekuwa bingwa wa Wafilisti alijitokeza na kutoa changamoto kwa jeshi la Israeli kumpambana na yeye moja kwa moja. Alikuwa na umbo la kushangaza, urefu wa mita tatu na mwili wake ukifunikwa na ngao za aina tofauti, pia alikuwa na mkuki.

Mlio wake mkuu ulijaza woga kwa nyonyo za watu wa Jeshi la Sauli. Kesho yake alishuka bondeni huku akitoa changamoto yake kwa sauti kuu iliyosika kwenye bonde lote.

Angalia jinsi neno “Sita” na “Shaba” limetumika kumwelezea Goliathi. Zote zilikuwa alama zilizotumika kwa “mwili” na inonekana kwamba Mungu alikuwa anamtumia kuonyesha nguvu za watu wa mataifa.

Kimo cha Sauli kilipungua machoni pake. Kukakuwa na upweke wa katika maneno yalisemwa na Samweli mbele ya Sauli kabla ya kumchagua “ Hapana, lakini tutakuwa na Mfalme atakaye tutawala.....Mflame wetu atatuhukumu, na kutupigania vita vyetu” (1 Sam. 8:19-20) Alikuwa wapi mfalme aliyesimama wima juu ya watu wake (10:23)? Hata walio wakuu katika jeshi la Mungu, Abner na wenzake waliogopa kukubali changamoto hio.

 

DAUDI ANAKUBALI CHANGAMOTO (1 Sam. 17:12-37)

Wakati huo Daudi alikuwa akichunga mifugo ya babake karibu na kambi ya Israeli iliyokuwa kilomita 23 (Mst.15) Alipofika na chakula cha ndugu zake kama alivyoagizwa na baba yake (Mst.17-18) alimsikia Goliathi akijigamba na kutoa changamoto (Mst.23-25)

Daudi alishtuka na kufadhaika kuona kwamba jina la Yahweh,  Mungu aliye hai likidhalilishwa kwa njia kwani baada ya siku arobaini hakuna mtu kutoka jeshi la Israeli aliyejitolea kwenda kupigana na Goliath. (mst.26)

Moyo wake ulisisimka. Bila kujijali alitamani kufanya  kitendo kwa ajili ya Mungu. Asili ya maneno yake na imani yake ndio ilimfanya kujulikana na mfalme. Wakati ule ndugu zake walihisi kwamba maneno ya Daudi yalikuwa yanawakemea wao wenyewe walimshtumu kwamba  anaacha kazi  yake ya uchungaji ili apate sifa za kivita. (Mst.28) lakini Sauli aliposikia maneno ya Daudi alitumana aitwe (mst.31) Daudi alijitolea kupigana na bigwa wa Wafilisiti.

Sauli aliangalia kwa kile wengi wangeita ujana hafifu, lakini huu haukuwa wakati wa maringo ya bure. Hata hivyo Sauli alifikiria kwamba Daudi alikuwa amechukulia hali ile kwa wepesi. Alianza kufikiria kijana kama yule angeweza aje kupigana na shujaa wa aina ile? Alikuwa na uzoefu gani? Lakini ilikuwa ni Sauli ambaye alikuwa amemchukua Mungu wa Daudi kwa wepesi. Hakuna kisichowezekana kwake. Mara mbili hapo awali kwa nguvu za Yahweh, Daudi alikuwa ameokoa mifugo wake kutoka kwa wanyama wakali kama simba na dubu- na huyu Mfilisti hakuwa tofauti na wanyama hao, (Mst.32-37) Tatizo kuu la Daudi na huyu mfilisti ni kwamba alikuwa amejitokeza na kupigana na Mungu wa Israeli na kosa hili lazima lingefutiliwa mbali.

IMANI INASHINDA MWILI (1 Sam. 17:38-53)

Sauli aliweka ngao yake kwa Daudi, hili lilikuwa onyesho la dharau kwani hakutenda hili kwa imani kwani ngao ile ingesaidia nini? Sauli hakuwa tayari kuvaa ile ngao na kwenda kupigana na jitu lile. Daudi aliikataa ngao ile na kubaki na nguo zake za uchungaji alipoenda kumtafuta Goliathi. Aliteremka bonde kwa haraka, akachagua mawe matano laini kutoka kwa mkondo wa mto na kuwakaribia wafilisti.  Bigwa yule hakuamini macho yake akamrushia maneno ya dharau kijana yule akisema kwamba atamfanya mlo wa wanyama wa mwituni.

Katika hali ya kimwili nafasi za ushindi za Daudi zilikuwa ndogo sana, lakini silaha zake za kivita hasikuwa za kimwili. Imani yake haikuwa kwa teo aliyobeba wala shauku ya jicho lake- ingawa hivi vingetumika katika huduma ya Mungu wa majeshi ya binguni. Alikuja kwa jina la Mungu aishiye. Lengo lake lilikuwa “wote walioko duniani wajue kwamba kuna Mungu Israeli” (mst.46)

Wakati Goliath wa Gath alimlaani Daudi na miungu yake alikuwa ameshachagua kuangamia kwake. Yahweh bila shaka atateta heshima yake na Daudi alijua kwamba yeye ni chombo cha kufanya kazi hii. Kwa kujiamini alimwambia Mfilisti yule “umekuja kwangu kwa upanga na mkuki pamoja na ngao; lakini mimi naja kwako kwa jina la Yahweh, Mungu wa majeshi ya Israeli ambaye umemkaidi (mst.45)

Goliath wa Gath alilazimika kukutana na mpizani wake. Daudi alisonga kama umeme. Alichagua jiwe kutoka kwa mfuko wake, akilenga shabaha, aligonga jitu lile kwa kichwa mahali hafifu. Alianguka chini kama kigogo. Daudi aliendelea kukimbia na kuchukua upanga wa lile jitu na kulikata kichwa. Mlio uliotoka kwenye kambi ya waIsraeli ulikuwa ule wa furaha na mshangao. Wafilisti walitoroka kwa mshtuko, wakati ule Daudi alichukua ngao ya Goliathi na kuileta kwenye hema yake, kichwa kile kikubwa mwishowe kilizikwa karibu na Yerusalem (mahali ambapo dhambi yenyewe ingekuja kuharibiwa)

Kwa njia hii Mungu alimfanya Daudi kuwa mashuhuri mbele ya watu na Sauli (vv 55-58) Alikuwa ameanza maisha yake ya umma na karibuni angesimama katika mahakama ya Sauli.

AKILI YA DAUDI

Ufahamu wa akili ya Daudi  wakati huu inatusaidia katika kupata ufahamu wa mtu wa imani, sehemu mbili zifuatazo zina baadhi ya maelezo kutoka kitabu cha Zaburi 8 na 144.  Ya kwanza ni zaburi ya ukumbusho wa ushindi mkuu and ya pili ni ombi la ukombozi wakati alipokuwa anaenda kukutana na Goliathi.

Zaburi inatusaidia kuelewa akili ya Daudi wakati alipokuwa anajitayarisha kukutana na mtu wa kimwili. Hakuna shaka kwamba uamuzi wa Yahweh ulikuwa sawa wakati alipomchagua Daudi kama mrithi wa Sauli katika kiti cha ufalme.

 

(a)  Ombi la Daudi la Ukombozi — Zab. 144

Katika toleo la “Septuagint” zaburi hii inapewa kichwa “ Zaburi ya Daudi kuhusu Goliathi” inaonyesha msimamo wa Daudi kwa tukio lile na pale alipoandika maneno haya katika zaburi.

Mistari. 1-4:       Daudi anamtumainia Bwana, kwani  licha ya unyonge wa binadamu Atamkomboa.
Mistari. 5-8:       Daudi anaomba msaada kwa Mungu kwa mtazamo wa kashfa  ya asiyetahiriwa.
Mistari. 9-11:     Daudi anaahidi kumpa Bwana sifa na utukufu kufuatia ukombozi.
Mistari. 12-15:   Baraka itakayopatikana Israeli itakuwa ni matokea ya ukombozi kutoka kwa Mungu.

 

(b)  Wimbo wa Daudi wa Ushindi—Zab. 8

Maneno yaliyoandikwa katika Biblia zetu kama kichwa cha Zaburi 9 yanaunda  sehemu ya mwisho ya Zaburi 8. Inasoma “ kwa mkuu wa muziki juu ya Muthlabben", na neno "Muthlabben" maana yake "kifo cha bingwa". Hivyo zaburi 8 inasherehekea kifo cha Goliathi and kumpa sifa mshindi wa kweli.

MST.1: Apewe sifa Mungu Muumbaji, Bwana wa mbigu na nchi

MST.2: Inaelezea jinsi Yahweh anapata ushindi dhidi ya  maadui zake kupitia mtu mnyonge (1 Sam 17:42, 56.).

Mistari. 3-4:   Inatukuza Mungu mkuu na jinsi anavyo  wajali watu wake.

Mistari. 5-8: kukumbuka kusudi la Mungu katika uumbaji wa binadamu, kumpa mamlaka juu ya vitu vyote licha ya udogo wake (Mwa. 1:26).

MST.9: Inarejelea mstari wa kwanza na kutangaza umoja na mamlaka ya jina la Mungu. Hiii ndio ilikuwa kusudi la Daudi alipomwangamiza Goliathi (1 Sam. 17:45-47).

Kuna hali ya kinabii katika Zaburi hii ambayo inasisitiza mtizamo wetu wa tukio hili kama mfano wa mapambano wakati Yesu ataharibu nguvu za mwili katika maandalizi  ya kuanzishwa kwa Ufalme. Katika Ebr. 2:6-8 Paulo ananukuu Zab. 8:4-6 na kutumia maneno ya Daudi katika  mamalaka ya ulimwengu mzima ambayo Yesu kristo atasisitiza wakati Atakaporudi na kutimiza kusudi la Mungu la kumpa binadamu mamlaka juu ya ardhi. (Mwa. 1:26).

 

DAUDI—MFANO WA KRISTO

Maneno haya yanatuonyesha uzoefu wa Daudi na ni mfano wa mwana Mkuu wa Mungu. Mapambano yake na Goliathi ni sawa na mapambano ya Kristo na nguvu za mwili mfano katika Nebukadneza mfano wa binadamu (Dan. 2:31-33). Kama Goliath mfano huu uliangushwa na jiwe ndogo-Mwana wa Mungu.  Wakati hili litatokea katika kurudi kwa Yesu kristo, matokeo yatakuwa kuharibiwa kwa nguvu za binadamu (Mst.35, 44). Mungu pekee ndiye atakayetukuzwa siku hio (Eze. 39:17-22; 1 Sam 17:45-47.).

Kama sisi ni wenye busara tutajitahidi kuwa na nafasi na Yesu siku hio (Zab. 149:6-9). Imani ya Daudi inapaswa kufuatwa nasi leo. Hakuna vita vilivyo vigumu kwa Mungu. Imani yetu inastahili kuwa kwa kapteni wa Wokovu wetu (Ebr. 2:10), ambaye tunaweza kuwa na uhakika wa mafanikio. Kristo ndiye Mchungaji Mkuu, (1 Pet 5:04;. Yohana 10:11), anaweza kutulinda and kutukomboa kutoka kea kila adui.

MAFUNZO KWETU:

  1. Mashindano kati ya Daudi na Goliathi hayakuwa tu vita kati ya wanaume wawili au majeshi, lakini mapambano kati Mungu aishiye wa Israeli na sanamu za Wafilisti.
  2. Kushindwa kwa Sauli kupambana na Goliathi kulikuwa kushindwa kwa imani na jukumu lake la kuwaongoza watu wake.
  3. Uwazi wa imani alionyesha Daudi ni msukumo kwa wanafunzi wote-“ kama Mungu yuko nasi nani atakayekuwa dhidi yetu” (Rom. 8:31)
  4. Goliathi anaoyesha dunia na tamaa, uasi na ukufuru wake. Tunaangalia wakati utawala wa binadamu utaangushwa na Mwana wa Mungu na kutupiliwa mbali.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 15

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Kurasa 417-420

"Letter to the Hebrews" (J. Carter)—Kurasa 26-28

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Toleo. 3, Nam. 8, 9

"Nelsons Bible Atlas"—Ramani 13, 15

"Oxford Bible Atlas"—Kurasa 60-63

"The Historical Geography of the Holy Land" (George Adam Smith)—1966 Ed., Kurasa 160-162

"The Man David" (H. Tennant)—Kurasa 24-32

MASWALI YA AYA:

• Jinsi gani imani ya Daudi ilionyeshwa katika ushindi wake wa Goliathi

• Ni jinsi gani vita na ushindi wa Daudi juu ya Goliathi unaashiria matukio ya baadaye?
• Vita kati ya Daudi na Goliathi ilikuwa ni zaidi ya mapambano dhidi ya watu wawili. Ni masuala gani yaliyohusika.
• Ushindi wa Daudi juu ya Goliathi unaweza kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku.  Kwa Jinsi gani?

 

MASWALI YA INSHA:

• Eleza jinsi Daudi alimwamini Mungu wakati alipoenda kukutana na Goliathi.
• Ni jinsi gani Zaburi 8 na 144 zinavyotafakari juu ya Ushindi wa Daudi dhidi ya Goliathi?
• Andika insha juu ya Ushindi wa Daudi juu ya Goliathi. Je, unafikiri ni masomo gani muhimu zaidi?
• Linganisha nia Daudi na nia ya Sauli wakati walikabiliwa na Goliathi.

 

Swahili Title
295. DAUDI NA GOLIATHI
English files
Sub type
Sub sub type