CSSA 3-2-297 - DAVID IN EXILE

Swahili

297. DAUDI UHAMISHONI

"Nilikulilia ewe Bwana; akasema, wewe ndiwe kimbilio na chakula changu"

 

Wivu wa Sauli ungetoshelezwa na kifo cha Daudi. Kama mfalme alitumia raslimali zake zote kumuua Daudi ambaye alilazimika kutoroka akihofia maisha yake. Miaka iliyofuata haikuwa na uhakika lakini Imani ya Daudi iliendelea kuimarika na alijifunza kumtengemea Mungu pekee. (Zab. 142:4-5).

Upendo wa Mungu ulikuwa juu ya Daudi, kwa sababu ya wema wake. Ingawa alikuwa amechaguliwa kuwa Mfalme wa Israeli hakutarajia huruma ya Mungu lakini aliitafuta kupitia Maombi na alipojibu alitii (1 Sam. 23:02, 4, 10-12). Daudi aliyaheshimu maisha ya Saul kama aliyeteuliwa na Bwana. Hakukimbilia fursa ambayo ingempa zawadi ya Ufalme kwa haraka, lakini angekuwa amevunja amri inayosema “Kisasi ni changu; nitawalipizia asema Bwana” (Kum. 32:35;. Rum. 12:19).

Daudi alikubali kusubiri wakati na njia za Mungu. Haki ingeleta zawadi sahihi ya Mungu.

Lengo letu katika somo hili ni kuona vile Mungu navyowalinda wale wanaomtegemea na kumwamini.


1 Samweli 22, 23 , 24
 

DAUDI KATIKA PANGO LA ADULAMU (1 Sam. 22)

Bila kupoteza wakati Daudi alitorokea Nobu, Mji wa makuhani. Katika kukata tamma kwake alijifinya kuwa  alikuwa katika shughuli ya siri ya Saul kwa hivyo akapata chakula na upanga wa Goliathi. Kuwa wakati alifukuzwa hadi Akishi, kwa mfalme wa Gathi pale ambapo alijifinya kichaa kwa kuhofia maisha yake.

Aliondoka Gathi na kufika pango la Adulamu, pahali ambapa jeshi la wanaume mia nne lilikuwa limemgojea. Kwa sababu mbalimbali wanaume hawa hawakufuirahishwa na utawala wa Saul. “wote waliokuwa na dhiki, deni na wote ambao walikuwa na uchungu mioyoni walikusanyika na kutaka awe kiongozi wao.(V2)  Wengi wao hawakuwa wamekusanyika kwa ajili ya ushirika au huruma lakini chuki juu ya Sauli. (linganisha Zab. 57:4). Hata hivyo miongoni mwao palikuwa na kuhani Abiathari (1 Sam. 23:06), ambaye Daudi alikuwa amemuuliza kuhusu Mungu na pia nabii Gadi (Mst.5), ambaye angekuja kuwa mshirika wa karibu kwa miaka mingi (2 Sam. 24:11).

Wakati ule Sauli aliwaelezea Wabenyamini nia yake ovu kumhusu Daudi. Aliomba ushirika wao kwa misingi ya kuwa yeye alikuwa wa kabila lao wangepata upendeleo kuliko mfalme wa kabila la Yudah. Baada ya ombi hili, Doegi, Mwedomi, ambaye alishuhudia Ahimeleki akimpa Daudi mkate na Upanga alijitokeza na kumweleza Sauli jinsi kuhani alimsaidia Daudi na “Kumuulizia kwa Bwana” (Mst.6-10).

Chuki ya Sauli haikuwa na mipaka kwani hakuogopa Mungu wala binadamu. Ahimeleki na makuhani waliitwa mbele ya Sauli na Ahimeleki alipojaribu kutetea vitendo vyake, Saul katika kitendo cha ukatili ambacho hata watumishi wake walichukia aliangiza makuhani wa Mungu kuuwawa kwa upanga. Abiathari, mwana wa Ahimeleki ndiye pekee aliyetoroka na kwenda kwa Daudi. Habari za mauaji aliyoyafanya Sauli ilidhibitisha hofu kubwa ya  Daudi naye akamwambia Abiathari "Kaa nami, wala usiogope, kwa maana yule atafutaye maisha yangu anataka maisha yako pia  lakini ukiwa pamoja nami utapata ulinzi" (Mst.23). Sasa ilikuwa wazi kwamba yote haya yangeisha na Kifo cha Daudi.
 

KUKOSA KWA SHUKRANI KWA WATU WA KEILA (1 Sam. 23:1-12)

Habari zilimfikia Daudi kwamba Wafilisti, adui wa asili wa WaIsraeli walikuwa walikuwa wanawapigana watu wa keila na kuiba unga wao. Uovu ulimkasirisha Daudi, na akasahau shida zake na akiwa na uhakika wa msaada wa Mungu alimuuliza Mungu “ Niende niwapige Wafilisti hawa”? Nguvu za Mungu hufanywa kuwa kuu wakati wa unyonge hivyo akaambiwa aende. Lakini kuna wale katika kundi la Daudi kwani hawa kumtumainia Mungu. Kwani walikuwa wanamwogopa Sauli, walijiuliza kwanini waongeze maadui kwa kupigana na Wafilisti. Walimuuliza Bwana tena na jibu likawa la uhakika “nitawatia Wafilisti kwenye mikono yenu” hivyo Daudi na watu wake wakaelekea keila na kwa ujasiri wakawapiga wafilisti na kuchukua ngombe wao. Hivyo wakazi wa Keila wakaokolewa (Mst.1-6).

Ripoti ilimfikia Sauli kwamba Daudi alikuwa Keila, mji wenye kuta na milango. Sauli akachukulia hili kama nafasi maalum aliyopewa na Mungu kuondoa tishio la Daudi. Matumaini ya Sauli yalikuwa bure kama hoja zake. Kwani haikuwa wazi kwamba Mungu alikuwa paoja na Daudi? Si ni Mungu aliyewatia Wafilisti mikononi mwake? Sauli aliwakusanya watu wake wote na kuelekea Keila.

Lakini matayarisho makubwa  kiasi hiki hayangefanyika bila Daudi kujua. Hivyo kwa mara nyingine Daudi alimuuliza Mungu “ ewe Bwana Mungu wa Israeli,mtumishi wangu amesikia kwa uhakika kwamba Sauli anataka kuja huku Keila, kuharibu mji kwa ajili yangu. Je waru wa Keila watapatiana mikononi mwake? Je sauli atakuja kama vile mtumishi amesikia? Ewe Bwana Mungu wa Israeli, nakuomba niambie mimi mtumishi wako "(Mst.9-11).

Ombi hili la imani lilipokea majibu ya ghafla “Macho ya Bwana yako juu ya  wenye haki, masikio yake husikia vilio vyao " (Zab. 34:15). Daudi aliambiwa kwamba Sauli angekuja na kwamba watu wa Keila wangempatiana mikononi mwake. Labda watu wa Keila walikumba kile kilichowatokea makuhani wa Nobi, kushirikiana na Daudi kungewangarimu maisha yao. Imani yao ilikuwa kwa binadamu na wala sio Mungu kwani wangemsaliti yule aliyekuwa amewaokoa. Kuna kukosa kwa shukrani katika nyoyo za binadamu, hivyo Daudi aliokolewa na Mungu.

Maneno ya shukrani na sifa yalioandikwa katika Zaburi 31 pengine yaliandikwa wakati huu “oh jinsi gani wema wako ulivyo mkuu, amboyo umeweka kwa wale wanaokuogopa na ambao umeweleta kwa uaminifu mbele ya watu wote" (Mst.19).

 

SAULI ANATAFUTA NYIKA YA SIFU (1 Sam. 23:13-18)

Daudi na watu wake waliokuwa wamefikia mia sita, walitoroka na kujificha nyikani katika milima ya Judea. Wakati huu wote Sauli na watu wake walimtafuta, ingawa aliweza kumtoroka Sauli, alipatana na rafiki yake wa dhati Jonathani ambaye alipata na kumwongeza “nguvu za mkono wake kwa Mungu” kuna upweke katika nyika na marafiki hawa wawili walikutanisha nyoyo zao na matumaini yao katika kumwogopa Yahweh "Usiogope kwa maana mkono wa Sauli, baba yangu, hautakupata; na utakuwa mfalme wa Israeli, na mimi nitakuwa wa pili kwako, na hilo babagu Sauli, analijua "(Mst.17).

Lakini matumaini haya hayakutimia, haya yalikuwa mazungumzo ya mwisho pamoja. Kifo kiliingilia kati na Jonathani hakumuona Daudi akiwa mfalme. Lakini kwa huruma na ukweli wa Mungu ambaye wote wawili walimtumaini wote wawili watafufuka na kuungana tena katika sifa na utumishi wa Mfalme mkubwa zaidi hata kuliko Daudi. (Zab. 110:1).

USALITI WA WAZIFITI (1 Sam. 23:19-28)

Ilikuwa ni jambo moja kumwogopa Sauli na kutaka kumpa Daudi, lakini vibaya zaidi kumpa Sauli habari za aliko Daudi, kama vile Wazafiti walifanya. Sauli aliwaambia Wazafiti kuhakikisha habari yao kwani alikuwa amepata ugumu wa kumpata Daudi na alikuwa amekuja kumtafuta kila kona ya Yudah (W. 22-23). Wazafiti walirudi, lakini kwa wakati huu Daudi alikuwa katika nyika ya Maoni. Saul na watu wake walishuka nyikani waliposikia kwamba yupo katika nyika ya Moani. Kukawa na vurugu na Daudi akawa hatarini - "Sauli akaenda upande mmoja wa mlima na Daudi na watu wake wakaenda kwa upande wa pili wa mlima. Daudi akaharakisha kuondoka akimwogopa Sauli, kwani Sauli na watu wake walikuwa wamemzunguka Daudi na watu wake tayari kumchukua"(Mst.26). Yote yalionekana kufikia mwisho kwani Daudi angetekwa nyara. Lakini Daudi alikuwa na nguvu moja aliyoificha ambayo hata adui zake hawakujua. Alikuwa amejitoa kumwani Yahweh “Niokoe, ewe Mungu kwa jina lako na unihukumu kwa nguvu zako. Sikia maombi yangu, ewe Mungu, sikia maneno ya kinywa changu. Kwani maadui wameungana kwa ajili yangu na wanyayasaji wanatafuta nafsi yangu, hawajaweka Mungu mbele yao. Tazama Mungu ndiye msaidizi wangu. Bwana yu pamoja na wale wanailinda nafsi yangu "(Zab. 54:1-4 - iliyoandikwa kwa wakati huu, kwa mujibu wa maandishi).

Tukio lisilotarajiwa lilitokea. Mjumbe aliwasili katika kambi ya Sauli akiwa na habari ya dharura. Wafilisti walikuwa wamevamia nchi yake. Sauli alilazimika kurudi hata kama hakutaka “ Upendo wa Bwana, enyi watakatifu; kwani Bwana Humlinda aliye mwaminifu, na anamzawadi vilivyo mtendaji mwenye kiburi" (Zab. 31:23).

DAUDI ANAMNUSURU ALIYETEULIWA NA MUNGU (1 Sam. 24)

Punde tu Sauli alimaliza vita na wafilisti alirudi kuendelea kumkimbiza adui yake. Wakati huu Daudi alikuwa katika jangwa la Engedi ambapo kulikuwa na mapango makubwa yaliyotoa ulinzi. Ikatokea kwamba Daudi akatafuta mapumziko katika moja ya mapango amabyo Daudi na watu wake walikuwa wamejificha. Mbele ya macho yao kwenye kiza, Sauli alifunga macho na akalala. Hii ilitoa fursa ambapo ukuu wa Daudi ungeonekana. Watu wa Daudi  hawakuongozwa na  mitizamo wala nia ya Mungu. Kwao tukio hili lilitoa fursa ya kumwangamiza adui waliyemchukia. Kwa kweli hii ilikuwa nia ya Mungu. lakini Daudi aliheshimu mafuta ya upako ya Bwana. Aliwakataza watu wake kumuua na kwa siri alitambaa na kukata kipande cha vazi la Sauli. Hata nafsi yake ilipigana naye kwa kufikiria kutenda hili,  wakati ule akiwa zuia watu wake kwa maneno “Bwana amenikataza nisifanye kitendo hiki kwa bwana wangu, mwenye upako wa Bwana, kuinua mkono wangu dhidi yake, na nduye aliyeteuliwa na Bwana. (mst.6)

Kulipokucha Sauli aliamka na kwenda zake, lakini alisitishwa na mlio wa Daudi “Mungu wangu Mfalme” Sauli alitizama nyuma na kuona kuona umbo la Daudi sura yake ikiwa imetizamia chini. Hapa nguve za haki zilionekana. Akiwa ameshika kipade cha vazi la Sauli alimwonyesha kwamba maisha yake yalikuwa mikononi mwake siku ile na ni kwa kupenda kwake alikuwa hai (Mst.9-10). Kwa uhakika hii ilikuwa ushahidi wa kutosha wa haki yake. Alimkemea Sauli kwa kujihusisha na mtu mmoja asiyekuwa wa maana(Mst.14) alimkumbusha kwamba Mungu ndiye atatoa hukumu kati yao.

Sauli alishangazwa na uadilifu wa Daudi na akashikwa na kipindi cha kichaa. Alitambua kwamba Daudi alikuwa mtu mwenye haki hata kumliko kwani ali zawadi uove wake kwa wema na kuyanusuru maisha yake (linganisha Mat.. 7:12).  Hata alimwomba Mungu kumbariki Daudi, na kuendelea kukiri kwamba Daudi atamridhi kwa kiti cha enzi cha Israeli, na akamuuliza Daudi onyeshe neema nyumba yake (Mst.16-21).

Tunaweza uliza swali, kama huo ndio ulikuwa mtizamo wake kwanini Sauli hakumwinamia? Kiburi na nguvu, hukumu na mizani. Kuna hekima kwa walio maskini. Ingawa alikuwa mdogo mbele ya macho yake, Sauli alikuwa ameshikilia ufalme sana na hangeuwacha. Hata hivyo kwa kulipa uovu kwa wema, Daudi alikuwa amemshangaza Sauli. Jambo ambalo Sauli angefanya ni kwenda nyumbani, wakati Daudi alibaki kwa umbali penye usalama.

MAFUNZO KWETU:

• Katika magumu ya uhamisho wake Daudi alimtengemea Mungu, kwani msaada wa binadamu ulikuwa bure. "Mtu huyu maskini alilia, na Bwana alimsikia, na kumwokoa kutoka kwa matatizo yote" (Zab. 34:6).
• Imani ya Daudi alifanya aweze kuepuka  njia zote mbaya, hata kama njia hizi zilikuwa zimejaa ahadi ya  kufikia lengoaliloahidiwa na Mungu kwa haraka.
• Watakatifu lazima wakizuie na kusubiri kwa uaminifu kwa siku ya kurudi kwa Yesu Kristo na kutimizwa kwa matumauini yao. Kisasi ni cha Mungu.

 

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—sura 16

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)— Toleo. 3, Nam. 10

"The Man David" (H. Tennant)—kurasa 46-66

MASWALI YA AYA:

1. Ni mafunzo gani ambayo Daudi alijifunza akiwa uhamishoni?
2. Orodhesha yaliyompata Daudi akiwa Keila.
3. Kwa nini DaUDI alimnusuru Sauli katika pango la Engedi?
4. Elezea kwa muhtasari mazungumzo kati ya Daudi na Sauli baada ya Daudi kuyanusuru maisha yake katika pango la Engedi.

 

MASWALI YA INSHA:

1. Jinsi gani Daudi alihifadhiwa akiwa uhamishoni? rejelea matukio katika Keila, nyika ya Zifu, na mapango ya Engedi.
2. Eleza tukio wakati Daudi aliyanusuru maish ya Sauli katika pango Engedi? Ni masomo gani tunajifunza kutokana na hili?
3. Udhaifu wa msingi wa Sauli ulikuwa upi? Jinsi gani hili lilionyesha matendo yake kwa Daudi? Toa mifano.

 

1. Wafilisti walijiandaa kwa ajili ya vita dhidi ya Israel katika Yezreeli. Daudi alikutana nao, lakini aliambiwa kurudi Siklagi (29:1-11).
2. Sauli anakusanya jeshi lake Gilboa. Anatafuta ushauri kutoka kwa mchawi wa Endori lakini anaambiwa kuhusu kushindwa kwake na kifo chake (28:4-20).
3. Wakati huo huo Daudi na watu wake, wakirudi kutoka Siklagi, wanaipata  imeteketezwa na Wamaleki, kini vyote vilivyochomwa vinapatikana tena (30:1-20).
4. Sauli anashindwa katika Mlima. Gilboa. Miili yake na ya wanawe inatundikwa juu ya kuta za Bethshan, lakini watu wa Yabesh-Gileadi wanawachukua na kuwapa mazishi yanayostahili (31:1-13).
5. Daudi analetwa Hebroni na kuteuliwa kama mfalme wa Yuda (2 Sam. 2:1-4).
6. Abneri, jemadari wa jeshi la Sauli, anamtambulisha Ishboshethi mwana wa Sauli kama mfalme wa Israeli katika Mahanaimu (2:8-11).
7. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinazuka  Gibeoni kati ya nyumba mbili za Israeli, wakati Abner anamuua Asaheli, ndugu wa Yoabu (2:12-32).
8. Kufuatia mauaji ya Abner na Ishboshethi, njia inkuwa wazi na Daudi anateuliwa mfalme wa Israeli huko Hebroni (5:03).
9. Daudi inaichukua Yebusi (Yerusalemu) na kuifanya mji mkuu (5:6-9).

 

 

Swahili Title
297. DAUDI UHAMISHONI
English files
Sub type
Sub sub type