298. KUSHINDWA GILBOA
"Vita vikawa vikali upande wa Sauli"
Katika somo hili tunafuata Sauli ili tuone jinsi alivyojishusha hadhi na kutafuta msaada wa mchawi wa Endori. Hatimaye anapata malipo ya uovu wake- kifo kupitia mikono ya Wafilisti aliowachukia. Sauli alipaswa kutambua kwamba wivu wake juu ya Daudi ilikuwa dalili ya kiburi kilichoumizwa. Badala yake alikataa kukubali nia ya Mungu ya kumwinua Daudi na akawa mbaya zaidi, na kuliletea jina la Mungu wa Israeli na lake mwenyewe aibu. Kwa hivyo somo hili linatuonya kwamba fikra za kidunia lazima ziondolewe. Fikra za chafu zinazokua kwa miaka, zinaweza kutuongoza na inaweza kuwa vigumu kwetu sisi kuziacha (linganisha 2 Kor 10:4-5;.. Phil 04:08;. Isa 55:7; Met. 23:07).
Kwa upande mwingine, Daudi aliendelea kuvumilia majaribio and magumu ya uhamishoni âalikuwa amefukuzwa mbali na uridhi wa bwanaâ hata hivyo hakuwa amewacha kanuni za maisha ya haki na alimdhamiri Mungu. Ilikuwa ni katika kipindi hiki aliandika mambo mengi katika Zaburi ambayo ni kama kioo kwa fikra za ndani za Yesu kristo. Mateso na majaribio yana mahali maalum katika nia ya Mungu Wale watakaoitwawatavumulia kwa ajili ya haki na kuhakikishia nyoyo zao kuwa ni wana wa Mungu(linganisha Mat. 5:10-12;. Mat. 5:41; 1 Pet 3:14;. 4:12-14 ).
Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi kuasi neno la Mungu kunaleta maafa mwishowe.
1 Samweli 26-31; 2 Samweli 1
DAUDI ANAJIFICHA SIKLAGI (1 Sam. 26 and 27)
Wazafiti kwa mara nyingine wanatafuta njia ya kumsaliti Daudi katika mikono ya Sauli lakini Sauli mara kwa mara nyingine anawekwa kwa huruma ya Daudi. Daudi na na binamu yake Abishai walivamia mipaka ya Sauli usiku, lakini kwa mara nyingine Daudi alikataa kumgusa aliye na upako wa Bwana. Sauli alipoamka aliona mkuki wake na chupa ya maji ikiwa mikononi mwa Daudi, na akakiri kwamba Daudi alikuwa mwenye haki kumliko hivyo akarudi nyumbani (1 Sam. 26). Daudi akawa amekata tamaa kwani hakujua vitendo vya baadaye vya Sauli, akaona atakuwa salama zaidi katika nchi ya Wafilisti na yeye na watu wake wakaondoka kwa Akishi katika Gathi. Baada ya hapo Sauli hakumtafuta Daudi tena (27:1-4).
Labda kwa sababu za faragha, Daudi akamuuliza akishi kama wangemchagulia mahali mjini aweze kuishi. Akishi wakampa Siklagi alipokaa kwa miezi 16. Sasa Daudi alikuwa huru kujifurahisha. Akiwa mahali hapa yeye na watu wake walivamia mataifa kusini mwa Yuda kwa umbali ulio karibia Misri na hakuna laiyeachwa hai kuelezea yaliyotendeka. Akishi alitaka kujua ni wapi Daudi alifanya ufamizi wake. Daudi alimjibu âkusini mwa Yuda...â hivyo Akishi akadhania kwamba Daudi alikuwa amewasahau kabisa watu wake hivyo angeweka imani kamili kwa Daudi.
Mwanzoni alikuwa akimshuku Daudi kwamba siku moja atakuwa Adui yake. Bila shaka alikuwa amesikia fununu za Daudi kuwa Mfalme wa Israeli
DAUDI ANAANDAMANA NA WAFILISTI (1 Sam. 29)
Ikawa kwamba Wafilisti walikuwa wamekusanya majeshi yao dhidi ya WaIsraeli. Daudi alikuwa na nafasi ya upendo katika moyo wa Akishi hivyo alialikwa kushiriki. Daudi aliungana na kuondoka na jeshi la Wafilisti hadi nyika ya Israeli yenye maji ya Shunemu, naye Sauli akakusanya WaIsraeli pamoja katika Mlima wa Gilboa. (28:1-4; 29:1-2).
Hakukuwa na shaka kwamba Daudi angekuwa mshiriki wa kuogopwa kama angekubaliwa kukaaa nao. Hisia zake kwa neno la Mungu na kuchukizwa kwake kes wale wasio tahiriwa, maneno aliyotamka alipomwangamiza Goliathi hayakuwa yamebadilika (linganisha 17:26, 45-47). Isitoshe, alihisi uchungu zaidi aliposikia jinsi waIsraeli walivyishindwa, hii inaonyesha wazi msimamo wake. (2 Sam. 1:19-21). Wakati wakuu wa Kifilisti walipotambua kwamba Daudi alikuwa miongoni mwao, wakamwita Akishi na kumwambia amfukuze Daudi. Wakati Akishi alipotetea uaminifu wa Daudi, hawakuridhika âMfanye mtu huyu arudi, ili achukua nafasi yake ambao amechaguliwa, hivyo asiende nasi vitani, kwani atakuwa kama adui kwetu. (Heb - Shetani) si anaweza patana na bwana wake? (Mst.4-5)Licha ya kuogopa ujasiri wake, hawakuweza kumwamini. Hofu yao ilikuwa na msingi. Akishi alimjumlisha Daudi uamuzi huu na hivyo Wafilisti wakaelekea Yezreeli kukabiliana na Sauli naye Daudi Siklagi (Mst.6-11).
SAULI NA MCHAWI (1 Sam. 28)
Mfalme wa Israeli alipona ukubwa wa jeshi la Wafilisti aliingiwa na woga. Kwa jinsi gani Saul alikuwa tofauti na Daudi. Kwa haraka alitafuta msaada na nguvu kutoka kwa Mungu lakini Yahweh âhakumjibu, sio kwa ndoto wala kwa Urimu, na sio kupitia makuhaniâ (Mst.4-6). Alikuwa amekata tamaa, ni nani angemgeukia? Samweli alikuwa maekufa na alikuwa manabii wote ambao wangemsaidia. (mst.3;. Law 19:31;. Kum. 18:9-14).
Katika mwisho wa kukata tamaa Sauli alimtafuta mwanamke mwenye roho, karibu na Endori na kwa unafiki wa kutisha Mflame wa Israeli alijibadilisha umbo na kupitia katikati ya Wafilisti usiku akienda kwa nyumba yake akiwa na watumishi wawili. Mwanamke yule alianza kwa kusita kutimiza matakwa ya Sauli kwani alifikiria kwamba amekuja kumkamata. Kuna utata mwingi kwa wale wanao acha njia za Bwana, Sauli akamhakikishia kwa kiapo alichoapa kwa jina la Mungu, mwanamkw yule akakubali ombi lake na papo hapo kwenye giza umbo la mtu likatokea akiwa amevaa jozi. Sauli alifikiria ni Samweli (Mst.13-14 linganisha 15:27.)
Sauli akafanya ombi kwa Samweli akiuliza nini anapaswa kufanya, baada ya kuona kwamba Mungu alikuwa amemwondokea na alikuwa naogopa jeshi la Wafilisti. Hofu kubwa ya Sauli ikadhibitishwa kwa jibu sahihi na dhabiti alilopokea, Sauli aliambiwa kwa sababu ya uasi wake Mungu alikuwa amemwacha yeye na ufalme ungepewa jirani yake Daudi. Pia aliambiwa kwamba jeshi la Israeli litashindwa siku itakayofuata na yeye na wanawe wangeangamia. Aliposikia hayo sauli alianguka chini (Mst.15-20).
Sauli alikuwa ametoka kwa njia za Mungu na sasa alikuwa amewachwa peke yake. Hii ni picha ya kutisha mfalme wa Israeli alioyesha wakati alijaribu kutafuta njia ya kujikomboa. Lakini alikuwa amechelewa kwani wakati wa hukumu ulikuwa umefika. Ni busara kumtafuta Mungu pahali alipo na hakuna wakati mzuri kuliko sasa.Hatuwezi kuweka mbali mambo ya Mungu ama kuahisha mpaka kesho kwani hatujui kama hio siku itafika.
Dhambi ya Sauli ilifikia kikomo wakati alitafuta ushauri kutoka kwa mchawi. Wakati watu wanaondoka katika njia za Mungu, Mungu anawachagua mambo yatakayokuwa vikwazo mbele yao ili waangukeâ kwani wamepokea upendo wa ukweli ili wapate kuokolewa. Na kwa sababu hii Mungu atawafanya kuchanganyikiwa, ili waamini uongo "(2 The. 2:10-12;.. Isa. 66:3-4; Yoh. 12:39-40). Hivyo wakati Sauli alimtafuta Samweli, maono ya Samweli yalitumwa kwake pamoja na utabiri uliotia muhuri adhabu yake.
Wakati mchawi alipomwona Sauli akisujudi akiwa chini akili yake ikiwa na matatizo inaonekana kwamba alifikiria kua lawama ingewekwa kwake. Akamwambia kwamba alikuwa nafuata maagizo yake. Pengine alifikiria kwamba angeadhibiwa kwa kutoa habari zile mbaya. Alipendekeza Sauli apewe kipande cha mkate ili apate nguvu, kwanza Sauli alikataa. Baada ya mda alikubali na wakala. Kisha Sauli na watumishi wake wakaondoka usiku wakifuata njia yao mioyo yao ikiwa na hofu kubwa ya siku inayofuatia. (Mst.21-25).
KIFO CHA SAULI (1 Sam. 31)
Siku ya pili vita vikaanza na WaIsraeli wakatoroka Wafilisti. Wafilisti walikuwa na nia ya kuchukua ushindi kwa kuwaua watu wote wa familia ya kifalme ya Israeli; âwakawafuata mbio Sauli na wanawe " (Mst.1-2). Baada ya mda wanawe watatu walianguka na wakapigwa mishale na kujeruhiwa sana. Kifo kilimkondolea Sauli macho. Badala ya kuwapa wale wasiotahiriwa fursa ya kumuua na kumdihaki, alimwamuru mtumishi wake aliyembebea sihala âkundunga na upangaâ Alipokataa Sauli alichukua upanga wake na kujiua. Baada ya kuona Bwana wake amejiua katika uwanja wa vita mtumishi wake aliyembebea silaha pia yeue akajiua vivyo hivyo. (Mst.3-6).
Habari za tukio hili la simanzi zilienea kwa haraka na kuleta hali ya hofu na kukata tamaa kwa Israeli, lakini furaha kwa Wafilisti. Wafilisti walikata kichwa cha Sauli na kikizungusha kwa umati wa Wafilisti. Ushindi hii ulihusishwa na ibada yao ya sanamu. Silaha zake ziliwekwa kwa maonyesho katika nyumba ya Maashtorethi, wakati mwili wake uliokuwa bila kichwa ulitundikwa katika ukuta wa Bethshan. Utukufu wa Israeli ukawa umeondoka. Uasi wa Sauli kwa Mungu ulikuwa umeleta aibu kwa taifa nzima na kwa jina la Mungu. Kuna tofauti gani katika siku hii na ile siku Daudi aliyekuwa mwaminifu alimuua Goliathi.
Lakini roho yote haikuwa imepotea. Mashujaa wa Yabesh-Gileadi; ambao walikuwa wameokolewa na Daudi kutoka kwa Waamoni (1 Sam. 11), wakaondoka na kwenye kuchukua miiili ya Sauli na wanawe kutoka kwa ukuta wa Bethshan na kuwapa mazishi ya heshima katika Yabeshi.
HABARI YA KIFO CHA SAULI INAMFIKIA DAUDI (2 Sam. 1)
Wakati huo huo Daudi na watu wake walikuwa wamerudi kutoka kwa Wafilisti na kukuta Siklagi imeteketezwa kabisa na wakazi wote kuchukuliwa. Hali ya kukata tamaa iliwashika watu wa Daudi lakini yeye alijipa nguvu ndani ya Mungu na vyote vikapatikana. (1 Sam. 30).
Siku mbili baadaye mtu akaingia katika Kambi ya Daudi akiwa na nguo zilizochakaa na kuchafuka. Baada ya kutambua kwamba ametoka katika kambi ya Israeli, Daudi alimuuliza matokeo ya vita. Kijana yule Mwamaleki, taifa ambalo Sauli alikuwa ameamriwa kulimaliza(1 Sam. 15:03) alielezea kisa cha kifo cha Sauli, alikiri kwamba yeye ndiye aliyehusika katika mauaji ya Sauli. Akampatia Daudi Taji na bangili za Sauli kama ushahidi, akidhani kwamba angepata neema kutoka kwa Daudi. Lakini Daudi alijawa na majonzi, na wala sio furaha. Yeye na watu wake âWalilia na kuomboleza na wakafunga kula na kunywa kwa ajili ya Sauli, Jonathani, wanawe wengine, nyumba ya Yahweh na nyumba ya Israeli kwa ujumla" (Mst.12). Kijana huyu aliuliwa kwa âkunyanyua mkono wake na kumuua aliyeteuliwa na Munguâ
Maombolezo ya Daudi kwa Sauli na Jonathani yanaonyesha ukuu na neema ya tabia yake. Akahisi aibu juu ya Israeli binafsi. Ukweli ulikuwa umeangamizwa mbele ya adui. Kuna somo hapa. Tunapaswa kuepuka kuleta aibu katika Jina kuu tunalobeba. Watu wa nje hawapaswi kuwa katika nafasi ambayo wanajigamba kuhusu makosa ya wale wanaobeba jina la Kristo (linganisha 1 Kor. 6:1-8) Zaidi ya hayo, Daudi alikumbuka Fadhila za Sauli na ushujaa wake vitani âSauli na Jonathani walikuwa wapendwa wakiwa hai na hata walipokufa hawakutenganishwa; walikuwa wepesi kuliko tai walikuwa na nguvu kuliko simba" (Mst.23). Hata mabinti wa Israeli, amboa hapo awali walikuwa wamechochea wivu wa Sauli kwa Daudi (1 Sam. 18:6-7), waliamriwa kukumbuka baraka za Sauli (Mst.24).
Maneno ya mwisho katika maombolezo yalihusiana na rafiki yake mpendwa Jonathani na yalijaa na uchungu na huruma. Aliongea ni kama kwamba Jonathani alikuwa bado hai "Nimesikitika kwa ajili yako, ndugu yangu Jonathan: kwani umekuwa mwema kwangu; upendo wako kwangu ni wa ajabu, kushinda wa upendo wa mwanamkeâ na mwishowe akakubali ukweli huu â"Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita kuharibiwa" (Mst.26-27).
MAFUNZO KWETU:
⢠Kukataa kutii Neno la Mungu kulisababisha Sauli kuachwa katika wakati wake wa haja kubwa zaidi.
⢠Wakati watu wanaondoka katika njia za Mungu, Mungu anawaachilia wajichanganye wao wenyewe, "ili waamini uongo" (2Thess. 2:10-12).
⢠Sisi, kama Daudi, tukimsogelea Mungu, naye atatukaribia (Yak. 4:08). Hakuna muda bora wa kujifunza kumwamini na kumtii Mungu kama wakati wa ujana wakati akili zetu hazijaingia mawazo mabaya na kukubali kwa urahisi Neno.
⢠Daudi alikuwa neema sana kuelekea hata mtu ambaye alimwonea wivu.
⢠Ni jambo zuri kuendeleza urafiki katika Ukweli ambayo utabaki imara na utakuwa msukumo wa imani yetu katika nyakati za shida. Huu ndio uliokuwa uhusiano wa Daudi mwaminifu Jonathan.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Visible Hand of God" (R. Roberts)â Sura 23
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)âTol. 3, Nam. 11
"The Man David" (H. Tennant)âkurasa 67-87
MASWALI YA AYA:
1. Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa kushindwa kwa Sauli juu ya mlima Gilboa?
2. Kwa nini ziara ya Sauli kwa mchawi wa Endori ilikuwa ya kinafiki? Hili linatufunza nini kuhusu wale wanadharau neno la Mungu kimakusudi?
. Kwa kifupi elezea kile kilichotokea baada ya Sauli kushindwa juu ya mlima Gilboa. Nini ilikuwa sababu ya msingi ya kushindwa kwa WaIsraeli?
4. Je, watu wa Yabesh-Gileadi walifanya nini kufuatia kifo cha Sauli? Kwa nini walifanya hivyo?
MASWALI YA INSHA:
1. Elezea kuhusu ziara Sauli kwa mchawi wa Endor na matukio matukio yaliyofuata kesho yake.
2. Kwa nini Mungu alimuondokea Sauli? Je, hili linatufundisha nini?
3. Ni masomo gani tunajifunza kutokana na maisha na tabia ya Sauli? Kwa nini Mungu alikataa kujibu maombi yake kabla ya vita vyake vya mwisho na Wafilisti?
4. Eleze kwa kina fikra za Daudi aliposikia kuwa Sauli na Israel ilikuwa imeshindwa na Wafilisti.