CSSA 3-2-299 - FROM THE SHEEPCOTE TO THE THRONE

Swahili

299. KUTOKA KATIKA NGOZI YA KONDOO HADI KITI CHA UFALAME

"Kisha mataifa yote ya Israeli wakaja kwa Daudi pale Hebroni"

Miaka mingi ilikuwa imepita tangu Daudi apakwe mafuta na Samweli kama mfalme wa nyumba ya Israeli. Tunaweza fikiria kwamba upako huu ulimaanisha Daudi angewekwa kwa kiti cha ufalme mara moja, lakini badala ya hivyo Daudi mchungaji kwanza akawa mkuu wa jeshi maarufu sana, kisha mpwa wa  mfalme, kisha akaenda uhamishoni, akawa mkuu wa jeshi lake kule milimani, akaungana na wafilisti. Hatimaye akakubaliwa kama mfalme wa sehemu ndogo wa sehemu ndogo ya ufalme wa Israeli kabla ya kuendelea na kutimiza kusudi la Mungu.

Tunajifunza kwamba Mungu hakuwa na haraka na mda uko chini ya mamlaka yake. Uvumilivu wa Daudi ulijaribiwa na Imani yake ikazawadiwa. “Daudi akaendelea kuwa na nguvu, na nyumba ya Sauli ikazidi kuwa dhaifu zaidi” (2 Sam. 3:01), mpaka mwisho Ufalme wa Sauli ukasabaratika na utawala wa Daudi ukaanzishwa kote katika nchi. Kanuni haikuwa imebadilika kwa kupita kwa wakati. “majaribio huleta subira; na subira huleta uzoefu; na uzoefu huleta matumaini" (Rum. 5:3, 4). “Nyinyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini yule atakayevumilia ataokolewa mwishowe” (Mat. 10:22). Nafasi kama ile Daudi alichukua ya enzi inatolewa kwa walio waaminifu, na mfalme atakaye tawala milele “ Yule atakaye shinda atapata nafasi ya kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi” (Ufu. 3:21; Lk. 1 :32-33).

Lengo letu katika somo hili  ni kuona jinsi Mungu anavyo wazawadi wale wanavumulia hadi mwisho.

2 Samweli 2 to 5

 

DAUDI, MFLAME WA YUDA, HEBRONI (2 Sam. 2:1-7)

Daudi alichukua kifo cha Sauli kama ishara kwamba wakati umefika wa kuchukua kiti cha enzi (linganisha 1 Sam. 26:10). Hata hivyo hakuchukua mambo mikononi mwake mwenyewe lakini alimuuliza Mungu “Je, niende kwa miji yoyote ya Yuda ?" Baada ya kupokea jibu kutoka kwa Mungu, yeye na watu wake wakaenda hadi miji ya Hebroni, ambapo walifanya makazi. Israeli wakawa hawana Mflame na wakawa wamechanganyikiwa. Baada ya kusikia kwamba Daudi alikuwa amerudi kutoka uhamishoni na wakikumbuka ahadi ya Mungu kwake, watu wa Yuda wakamteua aliyepakwa  mafuta kama shujaa na Mfalme wao. (kifungu cha 4).

Swali lililomsumbua Daudi akilini ni jinsi gani mataifa yote ya Israeli yangekusanyika kwake? Alipotambua kwamba  watu wa Yabesh-Gileadi walihusika katika kumpa Sauli mazishi ya heshima, aliwashukuru kwa jina la Mungu. Pia aliwakumbusha kuwa Sauli alikuwa amekufa na sasa yeye ndiye Mflame wa Yuda. Ni wazi kwamba alikuwa anamaanisha kwamba wanastahili kuongoza na waje wajiunge naye. Lakini hili halikutokea wakati ule.

KUGAWANYIKA KWA ISRAELI (2 Sam. 2:8-32)

Abner alitabiri matumaini ya kuunganisha Israeli kwa kumweka Ishboshethi, mwana wa Sauli, kwenye kiti cha enzi. Abner alikuwa mkuu wa Jeshi la Sauli na ndiye alikuwa nguzo ya ufalme huu dhaifu. Ilionekana kama alijua kwamba Daudi atakuja kuridhi nyumba ya Sauli, lakini aliweka ufalme kando, labda kuhifadhi nafasi yake (3:9-10, 17-18).

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka kati ya nyumba mbili za Israeli. Yoabu, mwana wa Seruya, akawaongoza watumishi wa Daudi na Abneri akiongoza watumishi wa Ishboshethi. Pande zote mbili  zikakabiliana kwa pande tofauti za kidibwi cha  Gibeoni na kikosi cha watu 12 kutoka kila upande kikaangamia katika mapambano haya.  Kama kawaida hili hutokea wakati ndugu wanapigana, kunakuw na waathiriwa wa pande zote mbili.

Vita viliendelea na watu wa Abneri wakatawanyika. Asaheli, nduguye mdogo Yoabu, alimfuata kwa kazi Abneri aliyekuwa mzoefu wa vita, huku akupiizilia onyo la kutofanya hivyo. Asaheli akauwawa kwa mkuki wa Abneri. Kifo cha Asaheli kiliwasha moyo wa kisasi kwa ndugu zake, Yoabu na Abishai, hivyo wakamkimbiza Abneri  na jeshi lake katika nyika ya Gibeoni.

Hapa Abneri alipata msaada kutoka kwa Wabenyamini. Vita vikasitishwa kwani Abneri aliwakumbusha kuwa wote walikuwa ndugu na upanga ungeleta machungu mwishowe, hivyo vita vikamalizwa. Wakati hesabu ilifanyika ilipatikana watu kumi na tisa pekee waliokufa kutoka jeshi la Daudi lakini watu 360 wa Abneri walikufa. Ni wazi kwamba Mungu alikuwa na Daudi (3:01); Ujinga wa Abneri, ni kumkataza Daudi ufalme ulijitokeza. Mwishowe hili lingemgharimu maisha yake. Kukataa kumtii Mungu husananisha kifo (Prov. 8:34-36).

DAUDI AKAZIDI KUWA NA NGUVU NA ISHBOSHETHI AKAZIDI KUWA DHAIFU (2 Sam. 3)

Nguvu ya nafasi ya Daudi imesisitizwa kwa taarifa ya moja kwa moja katika kitabu (v 1), na pia vijana sita walizaliwa naye kule Hebroni. (Mst.2-5). Lakini katika nyumba ya Sauli kulikuwa na mgawanyiko. Abneri alikuwa amemchukua Rispa, suria wa Sauli, kama mke, pengine kuonyesha kwamba  yeye ndiye alikuwa nguvu ya nyumba ya Sauli (linganisha 16:22). Wakati Ishboshethi, alimhukumu kwa kosa hili la yule mwanamke, alikasirika sana na kuapa kumpa Daudi ufalme wa kaskazini. Alitangaza kwamba angekuwa anafanya mapenzi ya Mungu kwani Alikuwa ameapa kumpa Daudi Ufalme juu ya Israeli kuanzia Dani hadi Beersheba (Mst.6-11).

Alituma wajumbe Kwa Daudi kumwelezea nia yake, lakini Daudi alikataa kuungana naye hadi pale mke wake Mikali atarudishwa kwake (mst.12-16) Kidiplomasia Abner waliongea na wakuu wa Israeli na baadaye Wabenyamini. Walifurahishwa na kauli yake ya kupatiana ufalme wa kaskazini kwa mikono ya Daudi. Abneri sasa angeweza kuongea na Daudi akiamini kwamba matendo yake yamekubalika na WaIsraeli. Daudi aliwapokea Abneri na watu wake kwa shangwe kubwa na walirudi kwa amani kama nia ya kuunganisha Israeli chini ya Daudi. (Mst.18-21). Lakini,  Yoabu hakushiriki mkataba huo. Alikuwa mbali akipigana vita bya mfalme. Aliposikia kilichotendeka alimkemea Daudi kwa kushirikiana na adui zake. Bila Daudi kujua, Yoabu alimwita Abneri ambaye hakujua nia ovu ya Yoabu, hivyo akauliwa na upanga mkali wa Yoabu (Mst.22-27). Alikuwa amelipiza kisasi kwa kifo cha ndugu yake Asaheli. Lakini Mungu anasema, "Kisasi ni changu mimi nitawalipizia kisasi," (Rum 12:19). Baada ya muda, katika hekima ya Mungu, yeye pia akawa mwadhiriwa wa upanda kwa usaliti wake. (1 Fal. 2:28-34).

Matendo ya Yoabu yalikuwa  ya kipumbavu. Israeli ilikuwa inalekea kuungana chini ya Daudi. Mambo yalikuwa yakiendelea sawa. Sasa mzungumzaji mkuu wa Israeli akauliwa Yuda. Daudi akatangaza laana kali katika nyumba ya Yoabu na akaweka wazi kwamba hakufurahishwa na matendo ya Yoabu. Aliwafanya watu kurarua nguo zao ili kutengeneza jeneza. Alifanya maombolezi ya hadhara juu ya Abneri na kusifu fadhila zake, akakataa kukula mpaka jua lizame. Daudi alikuwa mfalme akiwa na moyo wa hekima na kuelewa. Watu wake walifurahishwa na haya, isistoshe ilikuwa dhahiri kwamba Israeli yote ilipingana na vitendo vya Yoabu vya kikatili. (Mst.28-39).

ISRAELI INAANGUKA BAADA YA KIFO CHA ABNERI (2 Sam. 4)

Baada ya kusikia habari za kifo cha Abneri, “ujasiri wa  Ishboshethi ukaisha” (Mst.1, RSV). WaIsraeli wakachanganyikiwa. Wakatambua hili na kuona haja ya kuungana kwa haraka na Daudi, Ndugu wawili Rekabu na Baana, wakapanga kuleta  umoja kwa njia ambayo ingewapatia heshima. Wakamuua Ishboshethi akiwa kitandani mwake na kumtumia Daudi Kichwa chake kama ushahidi wa kwamba siku ya kisasi cha Bwana katika nyumba ya Sauli ulikuwa umefika. Lakini Daudi hakufurahishwa na hili. Alikuwa mtu aliyeamini sheria “ Usiue” Rekabu na Baana walikuwa wamemuua mtu mwenye haki akiwa kitandani (Mst.11). (Ishboshethi alikuwa katika mstari wa kwanza kumrudisha Mikali kwa Daudi (3:15), na alikuwa, bila shaka, alitumainia kwamba ufalme ungehamishwa mikononi mwa Daudi kwa imani)

Daudi alikuwa na wasiwasi. Ndugu hawa wawili wangelipwa na aibu wala si heshima. Waliuliwa mara moja na kutundikwa katika kidibwi cha Hebroni kama ushahidi kwa umati kwamba mflame Daudi hataruhusu uovu (Mst.9-12).

Mikono na miguu yao ilikatwa kwani “Mikono humwaga damu ya wasio na hatia.... na miguu inawapeleka kutenda uovu” ni "chukizo" Bwana (Mit. 6:16-18).

Jinsi gani hukumu ya Mungu itakuwa kwa ulimwengu kwa vurugu na maovu? Wafuasi wa kweli wa Bwana hawastahili kuhusika katika fujo na kisasi kutimiza malengo yao. Bwana wao amewaamuru kuwakata mikono na miguu yao kama viungo hivi vitakuwa vikwazo. (Mk. 9:42-45).

ISRAEL NA YUDAH YAUNGANA CHINI YA ALIYETEULIWA (2 Sam. 5:1-10)

Uongozi wa Daudi uliojaa na huruma uliwavutia mataifa ya ya kusini yaliyokuwa yametengana. Bila kulazimishwa mataifa yote yaliungana chini ya Daudi kule Hebroni na kwa hiari wakaamua kutii. Waliapa mambo matatu:

  1. “Sisi ni mifupa ya mifupa yako”
  2. “Pia katika wakati uliopita, wakati Sauli alikwa mfalme wetu wewe ndiwe ulikuwa kiongozi uliyeletwa Israeli” na
  3. Bwana akasema “wewe utawalisha watu wangu wa Israeli, na utakuwa kiongozi wao” (Mst.1-2).

Akiwa amepata heshima ya wote, agano lilifanywa Hebroni na Daudi akateuliwa kuwa mfalme wa Isreali. Daudi alikuwa na miaka 30 wakati alipoteuliwa kuwa Mflame wa Yuda na ilikuwa mika saba na nusu baadae wakati alipoteuliwa kuwa Mflame wa Israeli yote (Mst.4-5). Hivyo neno la Mungu la ahadi likatimia kwa njia ya ajabu- bila ya Daudi kuchukua uongozi kwa nguvu. Kweli Mungu angesema baadae kwamba "Mimi nikakupa nyumba ya Israeli na ya Yuda" (2 Sam. 12:08).

Kisha Daudi akachukua mji wa Yerusalem kutoka mikono ya watu wa mataifa.Yerusalem (au Yebusi) ilikuwa Benjamini katika mpaka wa Yuda na hivyo plaikuwa pahali mwafaka kwake kutawala makabila yote. Taifa la Israeli sasa lilikuwa tayari kuendelea katika kipindi cha cha utukufu katika historia.
 

DAUDI MFANO WA KRISTO

Kwa njia nyingi kutawazwa kwa Daudi katika kiti cha enzi ilikuwa mfano na Bwana Yesu Kristo- Yule ambaye atachukua kiti cha enzi cha Daudi (Lk. 1:32-33). Jedwali katika ukurasa huu inaonyesha jinsi Daudi anavyolinganishwa na Yesu Kristo.

 

DAUDI — MFANO WA KRISTO

 

DAUDI

KRISTO

1.  Wote walikuwa wachungaji wa watu wao.

Zab. 78:70-72

Mat.. 26:31.

2. Wote walienda uhamishoni na kukataliwa na watu wao.

1 Sam. 26:19

Yoh. 11:53-54;
Isa. 53:3
 

3. Wote waliheshimiwa na kupendwa kwa uadilifu na haki na walifuatwa na watu.

1 Sam. 18:16,30

Ma. 3:7-9

4. Wote waliahidiwa kiti cha enzi cha Israeli.

1 Sam. 16:1, 13

Lu. 1:30-33

5. Bwana wetu Yesu kristo, kama Daudi ataokoa Yuda kwanza.

2 Sam. 2:1-4

Zech. 12:7

6. Bwana wetu Yesu kristo, kama Daudi ataunganisha nyumba zote za Israeli.

2 Sam. 5:3

Eze.. 37:22

7. Kama Daudi, Kristo atawakomboa waresalemu kutoka kwa uovu wa watu wa mataifa na kutawala kutoka hapo.

2 Sam. 5:7

Lk. 21:24;

Yer. 3:17;

Yoe. 3:16

 

MAFUNZO KWETU:

• Nia ya Daudi ilikuwa mbaya zaidi aliporudi Siklagi na kupata imeteketezwa kwa moto na jamaa zake waote hawako. Hata hivyo alikuwa amekaribia siku ya utukufu wake.
• Kama Daudi sisi  tunajaribiwa katika tanuru ya mateso, lakini wakati ukifika tutapata mavuno kama tu hatutakata tamaa.
• Huu sio wakati wa kujisifu na kujitukuza. Ni lazima tunyenyekee kwa nira ya Kristo na kuweka kando mambo ya dunia, tunapaswa kutoa sadaka na  kujinyima kwa ajili ya Kristo ili tupate njia ya utukufu, heshima na maisha ya milele katika Ufalme unaokuja hivi karibuni.
• Mwisho unaostahili hauhalalishwi na njia zisizokuwa za uaminifu. Ingawa Abner na Ishboshethi ilibidi waondolewa ili kutengeneza njia kwa Daudi, alilaumu vurugu iliotumika katika matukio hayo.
• Haki ikawa msingi wa utawala wa Daudi (linganisha Zab. 72:2).

MKATABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—sura 17

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 3, Nam. 12

"The Man David" (H. Tennant)—Kurasa 88-105

MASWALI YA AYA:
1. Kwa nini Daudi alimwadhibu Rekabu na Baana kwa kumuua Ishboshethi?
2. Kwa nini Daudi alijitenga kutoka kwa Yoabu, wakati alimua Abneri?
3. Katika matukio gani Daudi aliteuliwa kama mfalme wa Hebroni?

MASWALI YA INSHA:

 

1. Eleza jinsi Mungu alileta Yuda na Israeli chini ya uongozi wa Daudi.
2. Ni kwa njia gani Daudi mfano wa Kristo?
3. Daudi alibidi kusubiri kwa miaka mingapi kabla awe mfalme juu ya Israeli. Jinsi gani tabia yake ilikuzwa katika miaka hio? Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutokana na hili?

 

 

 

1. Baada ya kutoroka kutoka Gathi, Daudi anafika pango la Adulamu ambapo watu 400 walikusanya karibu naye. Kwa ushauri wa Gadi, anaondoka na kwenda msitu wa Harith (1 Sam. 22:1-5).
2. Wakati akiwa mafichoni katika msitu wa Harith, Daudi anasikia Wafilisti wako vitani dhidi ya Keila na anachukua hatua ya kupigana nao na kuikomboa Keila, kisha anaifanya makao yake mapya (23:1-6).
3. Sauli anashambulia Keila na jeshi lake, lakini Daudi na watu wake wanatorokea nyika ya Zifu, wakijua kwamba Watu wa Keila wangewatia  mikononi mwa Sauli (23:7-14).
4. WaZiphites wamwambia Sauli pale Daudi alipojificha. Watu wa Sauli wanamzunguka  Daudi, lakini ghafla Sauli anaitwa kwenda kupambana na Wafilisti na Daudi anatorokea Engedi (23:19-29).
5. Sauli, baada ya kurudi kutoka vitani na Wafilisti anazidi kumwinda Daudi tena. Anaingia pango ambapo Daudi na watu wake walikuwa wamejificha na Daudi anakata sehemu ya vazi lake lakini hamdhuru Sauli. Mfalme anaguswa na huruma ya Daudi na anarudi Gibea (24:1-22).
6. Waziphites kwa mara nyingine wanamjulisha Sauli aliko Daudi. Daudi na Abishai wanavuka mipaka ya Sauli wakati wa usiku, na kuchukua mkuki wake na chupa ya maji. Tena Sauli kuguswa na huruma Daudi na anarudi nyumbani (26:1-25).
7. Daudi anajificha kwa Akishi, mfalme wa Gathi, na anakaa na watu wake katika Siklagi (27:1-7).

 

 

Swahili Title
299. KUTOKA KATIKA NGOZI YA KONDOO HADI KITI CHA UFALAME
English files
Sub type
Sub sub type