301. DAUDI ANAANZISHA UFALME WAKE
"Na Bwana akampa Daudi ushindi popote alipoenda"
Kitendo cha kwanza cha Daudi baada ya kuchukua Ufalme wa Israeli kilikuwa kurejesha Saduku la Agano katika mahali pake sahihi. Tofauti na Sauli, Daudi alijua kwamba mafanikio ya Ufalme yalitegemea taifa kumwona Mungu kama kitovu cha uwepo wao. Baada ya kutenda wajibu huu, Daudi aliendelea kupanua na kulinda mipaka yake. Hii ni kwa kutumia mfululizo wa kampeni saba alizotumia kushinda mataifa yaliyozunguka Israeli. Ingawa alipata ushindi huu kwa upinzani mkuu hakuwa na shaka kuhusu chanzo cha ushindi huo. Kufuatia ushindi wake dhidi ya magari ya farasi na muungano wa Shami aliandika âBaadhi wameweka Imani yao katika magari na wengine katika farasi, bali sisi tunalitaja jina la Bwana Mungu wetuâ (Zab. 20:. 7).
Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi Daudi alileta Israeli kwa nguvu na kushinda mataifa jirani.
2 Samweli 6; 8; 10; 12: 26-31
AGANO LINAFIKA SAYUNI. (2 Samweli 6)
Katika Agano ndipo palikuwa mahali pa Mungu pa kukutana na Israeli na hivyo ilikuwa ni ishara ya Uwepo na Utukufu wake (Kut. 25:22). Hivyo ilikuwa inafaa kwa Daudi sasa Yerusalemu ilikuwa chini ya mikono yake, kuanza mipango ya kuleta saduku la agano hadi Sayuni na kurudisha ibada ya Mungu.
Kwa miaka 20 iliyopita Saduku la Agano lilibaki katika nyumba ya Abinadabu katika Kiriath-yearimu. Ilikuwa imenyakuliwa na kurudishwa na Wafilisti baada ya kuchukuliwa na wafilisti katika vita vya siku ya Eli (linganisha Yos.18: 1; 4 ââ1 Sam. 3; 6: 1; 7: 1-2).
Daudi akatambulisha nia yake kwa watu na wakakusanyika kwa tukio hili kubwa. Agano lilipandishwa juu ya gari na kusukumwa na wana wawili wa Abinadabu, Uza na Ahio. Huu ulikuwa ni wakati wa furaha kuu. âDaudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanasherehekea mbele ya Mungu kwa nguvu zao zote, na nyimbo, vinubi, matairi na kayamba (2 Sam 6: 5).
Lakini ole wao, katika umati huu mkubwa janga likatokea. Uza akapigwa pigo na kufa wakati alinyoosha mkono wake kugusa Saduku la Agano lililotingishwa na ngombe. Daudi alishangaa na kushtuka. Kwa nini msiba kama huu utokee kwa nia yenye dhati kama hio.
Kuendelea na safari ya Agano hadi Sayuni hakukufaa kwa hivyo Saduku lilichukuliwa na kupelekwa hadi nyumba ya Obed-edomu. Daudi aliwaza kuhusu hukumu ya Mungu. Baadaye akatambua kwamba makosa yalikuwa yake; Neno la Mungu halikuwa limepewa heshima. Alisema â Hakuna anayepaswa kubeba saduku la Agano isipokuwa Walawi", na akasema kwa sababu ninyi (Walawi) hamkufanya hivyo kwanza, Bwana Mungu wetu ametukasirikia, ili tumtafute kwa utaratibu unaofaa. "(1 Nya. 15: 2, 13; Kum. 10: 8). Somo hili linatufunza umuhimu wa kutenda yale Mungu anahitaji. Haitoshi kuwa na moyo wa dhati katika nia zetu. Ni lazima pia tutafute ushauri kutoka kwa neno la Mungu ili kuona kama mipango yetu inalingana na mapenzi ya Mungu.Ni mapenzi ya Mungu kwamba binadamu wamwabudu kwa "roho na kweli" (Yos. 24:14;. Yn. 4:23).
Baada ya miezi mitatu habari zilimfikia Daudi kwamba nyumba ya Obed-edomu ilikuwa imebarikiwa. Hii ilikuwa ishara kwa Daudi kuendelea na mipango yake. Hivyo watu wote wa Isreali walikusanyika na Agano la Bwana likaletwa kwa shangwe na vigelegele hadi Sayuni. Tukio hili lilikuwa na umuhimu mkubwa. Daudi alivaa â"joho la kitani safi" (1 Nya. 15:27.); Alitoa sadaka; akabariki watu; na akatoa zawadi ya mkate, nyama na mvinyo kwa wote waliotajwa na kuhani. Hapa palikuwa na kuhani wa kabila la Yuda. Amevaa nguo za haki, ambaye alikuwa mflame wa Yerusalemu. Kwa kweli alionyesha jukumu la Mflame-kuhani, mfano wa Melkizedeki (linganisha. Ebr. 7). Maneno ya Zaburi 110, 132 na 68 na 1 Nya. 16: 8-36, ambayo yalitungwa wakati huu, yanaonyesha umuhimu wa tukio hili.
Aidha, saduku, utukufu wa Bwana, ambao ulikuwa umeondoka kwa muda mrefu ulikuwa unarudi kwa nguvu na utukufu na mflame mwenye nguvu alikuwa aeneze utukufu wa Ufalme wa Mungu kwa njia kubwa zaidi. Bwana Yesu alikuwa kama Saduku la Agano kwani alionyesha utukufu wa Baba yake kati ya wanadamu(Yn.1:14 Diaglott). Baada ya muda mrefu ya kutokuwepo, atarudi kwa nguvu na utukufu mkuu na âkujenga hekalu la Daudiâ na kuunganisha mataifa yote katika Ufalme wake (Mdo 1:11; Zek. 14:. 4; Eze.. 43: 2. ; Mdo.15: 16-17).
DAUDI ANAPANUA MIPAKA YAKE. (2 Samweli 5:17-25).
Wakati Wafilisti wa kusini-Magharibi walisikia kwamba Daudi alikuwa amechaguliwa kama mflame wa Israeli, walimpa changamoto. Walienea katika nyika yenye rotuba ya Warefai iliyo kusini-Magharibi mwa Yerusalemu kuelekea Bethlehemu. Daudi alidumisha ngome yake ya Sayuni. Alimuuliza Bwana anafaa kuwashambulia, na kama watawekwa juu ya mikono yake. Jibu kutoka kwa Mungu lilikuwa la mara moja na mfalme mwenye ujasiri wa Israeli alihakikishiwa ushindi. Hivyo Daudi aliwaangamiza wote na kuhusisha ushindi wake kwa Bwana. â Bwana amevunja adui zangu mbele ya macho yangu, kama mafuriko ya majiâ Miili ya Wafilisti iliyotapakaa ilikusanywa na kuteketezwa. Lakini ushindi huu haukuwa kamili na kwa mara nyingine Wafilisti walijitokeza Refaimu. Kwa mara nyingine Daudi alitafuta ushauri wa Mungu na wakati huu aliamriwa kutumia njia tofauti. Hakuwa ashambulie kama alivyokuwa amefanya hapo awali, kwani hili lilikuwa jambo ambalo Wafilisti walikuwa wanatarajia, lakini aliambiwa â achore dira nyuma yaoâ karibu na miti ya miforsadi, na kusubiri ishara ya Mungu kabla ya kushambulia. âMtakapo sikia Sauti ya upepo ikipitia juu ya miti ya miforsadi " Daudi alifuata mpango huu wa Mungu kwa makini na akaangamiza maadui wake kuanzia Geba hadi Gazeri. Umaarufu wa Daudi ukazidi na âBwana akaleta hofu kwa mataifa yote " (1 Nya. 14:17). Kuna somo hapa. Je, sisi tunafuata mwendo wa Neno la Mungu wakati matatizo yanatukumba, ama tunafanya yale yaliyo haki mbele ya macho yetu.
KAMPENI SABA ZA DAUDI (2 Samweli 8:1-14; 11:1; 12:26-31).
Kufuatia utoaji wa ahadi kubwa kwa Daudi na nyumba yake (2 Sam. 7. Rejea Hatua ya 2, somo la 25) tunajifunza kwamba alipanua mipaka yake kufikia kipimo alichoahidiwa Abrahamu. âKuanzia mto wa Misri hadi mto mkuu wa Frati. "(Mwa 15:18; 1 Nya. 18: 3, 1 Fal. 04:21.). Haya ndio mafanikio katika kampeni saba: -
- Dhidi ya Wafilisti (2 Sam. 8.1). Unafiki wa Wafilisti haukuwa umemalizwa kabisa kwani waliungana tena na kumpinga Daudi kwa mara nyingine. Wakati huu waliangamizwa kabisa ikiwa ni pamoja na Gath na miji yake na hivyo hawakuwa tishio kwa ufalme wa Daudi(1 Nyakati 18: 1.).
-
Dhidi ya WaMoabi (2 Sam 8:. 2). Kupitia bibi mkuu wa Daudi aitwaye Ruthi aliyekuwa Mmoabi na ingawa alikuwa ametafuta hifadhi huko kwa wazazi wake akitorokea kisasi cha Sauli, waMoabi walikuwa wamempa Daudi sababu ya kuwashambulia (Rut. 4:. 21-22; 1 Sam. 22: 3-4) walishambuliwa na theluthi mbili yao wakauawa na waliobaki wakasamehewa 2 Sam 8:. 2 RSV). Hivyo vitisho kutoka kusini-mashariki vikawa vimeondolewa.
- Dhidi ya Zoba (2 Sam. 8:. 3-8). Zoba ilikuwa kaskazini mwa Damasko katika sehemu ya Labanoni. Daudi alivyoelekea kaskazini kurudisha nguvu katika mto Frati (2 Sam. 8:. 3) alipata upinzani kutoka kwa Hadadezi mflame wa Zoba aliyekuwa na jeshi kubwa la magari ya farasi. Mungu alijibu maombi ya Daudi na wote wakaangamizwa, magari ya farasi 1,000, waendeshaji 700 and majeshi 2000 walitekwa. Kama ishara ya dharau Daudi kwa utumizi wa magari ya farasi , Daudi akawavunja mishipa farasi na kubakisha wachache wangetoshea magari 100 pekee. Zaburi 20 inaonekana kutafakari tukio hili â, "Sasa najua ya kuwa Bwana anaokoa mteuliwa wake; atamsikiliza akiwa mbiguni na kumpa nguvu za mkono wake wa kulia. Baadhi wanaamini magari ya farasi; lakini sisi tunakumbuka jina la Bwana Mungu wetu(Mst.6-7) Roho hii ilikuwa ni ushauri wa Mungu kwa wafalme wa Israeli, lakini ole wao kwa kizazi kimoja hamu ya usalama ukasababisha tamaa ya kutaka kuongezwa kwa farasi bila kutilia maanani imani ya Bwana (Kum. 17:16; 1 Fal. 10..: 26). Kuna onyo gani katika mfano huu.
Ushindi wa Daudi ulikuwa na matokeo mawili, kwanza Washami wa Damascus walijitokeza kumsaidia Hadadezeri, - lakini 22,000 wakapigwa na Damascus ikatekwa; âBwana alimhifadhi Daudi popote alipoendaâ (Mst. 6) Pili, Toi, Mfalme wa Hamathi, kaskazini mwa Soba, alitumana na kumpongeza Daudi. Daudi aliletewa dhahabu, fedha na shaba lakini Daudi alizitoa kwa Bwana, kama chanzo cha ushindi wake (W. 9-12) hivyo mpaka wa kaskazini ukahifadhiwa.
- Dhidi ya Edomu (2 Sam. 08:13, 14;. Katika mstari wa 13 "Washami" wanapaswa kuwa âWaedomuâ Sifa ya Daudi ilizidi kuenea mbali. Abishai na Yoab walipewa jukumu la kungia katika mji wenye nguvu wa Edomu na wakaangusha adui huyu wa jadi wa Isreali (1 Nya. 18:12; 1 Fal. 11: 15-16). Yoabu alikaa huko miezi sita zaidi na akawaua watu 12,000, ikiwa ni pamoja na "kila mwanaume katika Edomu". Hivyo Daudi akawa salama kutoka kwa maadui hawa kutoka upande wa kusini.Zaburi 60 imeandikwa kuhusu ushindi huu. Mtazamo wa Daudi ni muhimu kufuata: "Moabu ni chombo changu cha kuoga; na nitarusha kiatu changu Edomu......Nani atanipeleka katika mji huu wenye nguvu? Nani ataniongoza hadi Edomu? Kama sio wewe Mungu ambaye hujatutupa... tupe msaada kutoka kwa matatizo; kwani msaada wa binadamu ni bure. (Mst. 8-11).
Wakati binadamu anapotukuzwa mara nyingi anamsahau Mungu. Daudi alikuwa tofauti kwani kwa ukuu wake alitambua ushindi wake kwa msaada wa Mungu.
-
Dhidi ya Amoni (2 Sam. 10:. 1-14). Daudi aliendelea kuandaa utawala wake, kutekeleza mamlaka kwa âhukumu na Hakiâ (2 Sam. 8: 15-18.). Huruma haikusahaulika katika utekelezaji wa mamlaka, kama inavyoonekana katika kuonyesha huruma kwa Mefiboshethi, mwana kilema wa Yonathani (2 Sam. 9). Kisha Nahashi, mfalme wa Amoni, akafa na mwanawe, Harun, akamiliki baada yake. Daudi alituma risala za rambirambi kwake, lakini wakuu wa Amoni wakatilia shaka nia yake. Walishuku kwamba wajumbe wa Daudi walikuwa wamekuja kupeleleza mji hivyo walitiwa aibu. Hii haikuwa njia sahihi ya kumchukua mtu aliye waonyesha huruma, hasa ikiwa ni jirani mwenye nguvu. Waamoni walipata habari ya hasira za Daudi na kwa woga wa kisasi wakaomba msaada kwa Washami wa Rehobu, na Soba, kutoka kwa mflame wa Mika na pia kwa jeshi la Tob. Hivyo jeshi la watu 33,000 likaja kuwasaidia. Yoab aliwagawanya wenyeji wake na kwa kuchagua jeshi lake aliwashambulia mamluki waliokuwa nyuma ya Israeli. Walitoroka na hili liliwatia Waamoni woga na wakatoroka mbele ya Abishai mpaka Raba mji wake mkuu. Huu ulikuwa mpango mzuri wa Kijeshi ambao Yoabu alikuwa ametekeleza.
- Dhidi ya Washami (2 Sam. 10:15-19). Washami walijiunga pamoja na wengine katika kingo za mto Frati na kutoa changamoto kwa Israeli. Habari hii ilipomfikia Daudi, alivuka Yorodani, na kuelekea kaskazini na kuupiga ushirika wa Helamu. Mkuu wao akaangamia na wafalme wote wakaomba amani na kutumukia Israeli.
-
Dhidi ya Waamoni (2 Sam.11: 1; 12: 26-31). Ingawa Daudi alikuwa tayari amewapiga Waamoni, fikra zake zilielekezwa kaskazini kwa changamoto ya Washami. Baada ya kuwashinda, alimtuma Yoabu na jeshi Mashariki na kuharibu Waamoni na kuwacha mji mkuu, Raba. Mji huu mwishowe ulichukuliwa na Daudi.
USHINDI WA DAUDI MFANO WA KAZI YA BWANA
Kama Daudi alivyowashinda adui zake kupitia msururu wa kampeni saba, hivyo ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo atakavyofanya. Malaika wa Upinde katika ufunuo 10 unawakilisha Kristo na watakatifu na upinde unaonekana ukiwa chini ya bahari na ardhi kuonyesha utawala kamili(Ufu.10: 1-7). Uso wake ni kama jua na miguu yake ni kama nguzo za moto, kuonyesha kwamba nia yake ni moja ya kuhukumu kwa moto (linganisha Mal. 4:1-2; Mik. 4:13; 2 The.1: 8). Sauti yake ni kama ngurumo ya simba na inatoa âNgurumo Sabaâ inayo ongea kuhusu siku ya Bwana ya ghadhabu. Yohana alikatazwa kutoa maelezo zaidi kuhusu ngurumo saba lakini kutoka katika sehemu zingine za neno ni wazi kufuatia kuingilia kati kwa Israeli, hukumu ya Mungu itafuata kanisa la katoliki Ulaya hadi mwisho wa Ufalme wa Kristo na kufikia sehemu zote za dunia (Zek. 14: 9; Zab. 2: 8; 72: 8).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA
- Daudi alimweka Mungu kwanza na akataka kuleta Saduku la Agano Sayuni baada ya kuteuliwa.
- Alitafuta ushauri kutoka kwa Mungu kabla ya kuanza Kampeni na kwa hivyo alipokea baraka ya Mungu katika kampeni zake.
- Alimsifu Mungu, akawa tofauti na wanaume wengine ambao walitegemea mafanikio yao na kumsahau Mungu.
- Kuna masomo muhimu katika kurudishwa kwa Saduku na ushindi wa Daudi ambayo zinaimarisha imani yetu kwa mambo yatakayokuja humu nchini.
MAKTABA YA KUREJELEA
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol.4, Nam. 1, 2, 3
"The Man David" (H. Tennant)âSura 6
MASWALI YA AYA:
1. Ni mafunzo gani tunaweza kujifunza kutokana na kifo cha Uzza?
2. Kwa nini Daudi alifanikiwa katika kampeni zake za kijeshi?
3. Kwanini Daudi hakuwaokoa farasi wote wa mfalme wa Zaba kwa matumizi yake?
MASWALI YA INSHA:
- Kwanini Daudi alileta Saduki la Agano Sayuni? Ni kwa jinsi gani matendo yake katika tukio hili yaliashiria ukuhani wa Kristo?
- Eleza ushindi wa Daudi na kuonyesha jinsi ulivyoashiria ushindi wa Yesu atakaporudi.
- Bwana akampa Daudi ushindi kila mahali alikokwenda". Toa mifano katika nukuu hii kuanzia wakati Daudi alishinda mataifa jirani.