CSSA 3-3-303 - MESSIAH IN DAVID'S PSALMS

Swahili

303.    MESSIA KATIKA ZABURI YA DAUDI

"Mambo yote yalioandika.... katika Zaburi kunihusu mimi ni lazima yatimia"

Kitabu cha Zaburi ndicho kitabu kikubwa zaidi katika Biblia na Daudi aliandika nyingi ya Zaburi katika kitabu. Akili ya Daudi ilikuwa pamoja na Mungu wa Israeli na kufuatia upako wake, “Roho wa Mungu ukawa juu yake (Sam.16:13 1). Katika njia hii fikra za Bwana ziliwasilishwa kwake, hivyo maneno alioandika yalikuwa ya Mungu.kama Daudi alivyoandika baadae "Roho wa Bwana unaongea nami na maneno yake yako kwa ulimi wangu” (2 Sam. 23:. 2). Daudi pia alikuwa anapenda Muziki. Hii ilidhihirishwa kwa kuwa alikuwa amechaguliwa kucheza kinanda mbele ya Sauli (1 Sam.16:. 16-23). Talanta hii ilitumika na maneno ya Roho yaligeuzwa na kuwa muziki unaojulikana kama “Zaburi”. Daudi ndiye aliwaongoza wana wa Asafu, Hemani na Yeduthuni, ili kutabiri wakitumia vinanda na vinubi”. Neno la Mungu liligeuzwa na kuwa wimbo na kwa njia hii watu walifunzwa njia zake (1 Nya. 25:. 1).

Lengo letu katika Somo hili ni kuona mifano ya jinsi Zaburi ya Daudi ilitabiri mambo kuhusu Kristo.

Zaburi 2; 16; 22; 69; 110


MUUNDO NA YALIOMO KATIKA ZABURI YA DAUDI.

Mengi katika Zaburi ya Daudi yaliandikwa katika hafla maalum na hii inadhihirishwa na chapa katika mwanzo wa kila Zaburi. Kwa mfano, Zaburi 63 ina chapa ya: “Zaburi ya Daudi, akiwa katika nyika ya Yuda”, na hii inahusiana na uzoefu wake kama ilivyoandikwa kwa kumbukumbu katika 1 Sam. 23, Maneno: “mwanamziki mashuhuri” yanatokea juu ya Zaburi 64, lakini yanapaswa kuwa katika sehemu ya chini ya Zaburi 63 ili kuunda chapa ya Zaburi hio. Hivyo kuna sehemu tatu za Zaburi; kuna chapa ya juu, Zaburi yenyewe na  chapa ya chini.  Mgawanyiko huu wa sehemu tatu unaonekana katika Zaburi iliandikwa katika kitabu cha Habakuki sura ya 3.

Kwa njia nyingi uzoefu wa Daudi ulifanana na ule wa mwana wake mkuu, Bwana wetu Yesu Kristo. Hisia alizokuwa nazo uhamishoni, wakati alikata tamaa ya maisha na akamkimbilia Mungu, zimefanywa kuwa msingi wa Zaburi ambazo zinagusia mateso ya Bwana. Katika Zaburi hii ya kinabii “Roho wa Kristo...ulitoa ushahidi wa mateso ya Kristo na utukufu utakaofuata” (1 Pet. 1:11).  Maisha na kazi ya Kristo yanawekwa wazi kabisa; hivyo kwamba itawezekana kugusia matukio makuu katika somo hili kama ilivyo rekodiwa katika sehemu za Zaburi ya Daudi; yaani (Zab.2, 16, 22, 69 na 110).

Umuhimu wa Zaburi hizi haiwezi sisitizwa zaidi. Zimenukuliwa katika Agano jipya ambapo kuna nukuu nyingi zilizotumika katika mahubiri ya kitume. Bwana Yesu aliwaomba na kuwashawishi wanafunzi wake waliochanganyikiwa kwamba kuteseka kwake na kifo chake kulikuwa uhakikisho wala sio kuondolewa kwa Umesiya wake. “ na yeye akawaambia....vitu vyote lazima vitimizwe, vile vyote vilivyoandikwa kunihusu katika Sheria ya Musa, Nabii, na katika Zaburi...hivyo ilikuwa inapaswa Kristo kuteseka na kufufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu”(Lk. 24:. 44-46).


KUTESEKA NA KIFO (Zaburi 22 na 69)
Zaburi hizi mbili hasa zinaonyesha mateso hadi kifo cha Masiya, hata kama ilikuwa imeandikwa na Daudi. Maneno ya Zaburi 61:9 “ wivu wa nyumba yako umenila” ilikuwa wito kwa wafuasi  katika siku za kwanza za huduma ya Bwana, wakati alikasirishwa na wafanyi biashara katika hekalu ya Bwana (Yn. 2:17). Kuzidishwa kwa adui zake, kwa sababu kwa uaminifu alifanya mapenzi ya Baba yake, na chuki yao kuelekea kwake imeonyeshwa kwa  maneno, "Wale wanao nichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu" (Mst.4; Yn.15:25), na "Kashfa (matusi) wanazo kutolea wewe zimenipata mimi" (Mst.9; Rum.15:. 3). Katika uzoefu wa Daudi unapatikana kwa Messia katika ombi lake la ukombozi (mst. 13-18) Hata kutoa siki kwa Bwana aliyesulubiwa ilitabiriwa (Mst.21;. Mt. 27:48).


Zaburi 22 inatuchukua hadi kwenye msalaba. Utabiri huu ulikuwa sahihi hadi pale Bwana aliye sulubiwa alisema, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha" (Mst.1;. Mt 27:46). Maneno ambayo yalitoka kwa vinywa vya wauaji wake bila kujua yalijulikana na Roho: “Alimwamini Mungu kwamba atamwokoa, Mwache amwokoe kwani alifurahishwa sana naye.” (Mst.8; Mt. 27: 43). Kugawanywa kwa mavazi yake na kupigiwa kura  pamoja na unabii mwingine mdogo pia kulitabiriwa na kutimizwa(Mst.18; Mt 27:35.). Utabiri wa usahihi wa kifo chake, kudungwa mikono na miguu bila kuvunjika kwa mifupa, kulileta kushikana kwa ajabu kwa matukio haya (Mst.16; Zab. 34:20; Yn. 19:31-37).

Hivyo Zaburi inaonyesha mateso na kifo cha Mesiya, pia inatufunz kuhusu kufufuka kwake, kwani inahitimisha kwa hali ya furaha. Kilio chake hakikuwa cha bure. Baba yake alisikia kilio chake na “ kumwinua” (Zab. 22:24;. 69:29). Zaburi 22 inamalizia na taswira ya ushindi wa Bwana katikati ya Eklesia na mazungumzo ya mwisho ya “mwisho wa kila ncha ya dunia” (Mst. 25-31; linganisha 69: 35-36).

UFUFUO (Zaburi 16).

Ahadi zilizofanywa kwa Daudi zilihitaji mwanawe kuwa mtu aliyefufuliwa. Daudi aliambiwa kwa uhakika kwamba “tunda la mwili wako” Mungu atamwinua ili akalie kiti cha enzi na kwamba ufalme wake “utakuwa wa MILELE” (2 Sam. 7:16). Swali linaloibuka katika akili ya Daudi-kwa njia gani mzaliwa wa binadamu anaweza kusihi milele? Daudi alipata jibu la swali hili kwa kutambua kwamba uzao wake lazima uwe umefufuliwa kutoka kwa wafu. Mtume Paulo anatuambia mambo haya katika Matendo ya Mitume 2:25-31. Baada ya kunukuu Zaburi 16, ambayo iliandikwa na Daudi, anaendelea na kuelezea maana yake. Maneno muhimu yanayopatikana katika Zaburi hii hayawezi kutumika kwa kila binadamu aliyeishi kitambo. “hutaiacha roho yangu kuzimu, wala kumruhusu mtakatifu wako apotelee kwa ufisadi" ingawa iliandikwa na Daudi, maneno haya hayangetumika kwake kwani “aliona ufisadi” (Mst. 29)

Petro anasema kwamba Daudi alikuwa anatabiri wakati alikuwa anaandika Zaburi 16, kwani alielewa matakwa ya ahadi- kwamba mwanawe wa mwili ataishi milele (Mst.30). Baada ya kuona kwamba kaburi la Kristo lilikuwa tupu na kwamba  walikuwa wamemwona na kumsikia Bwana, katika matukio ya karibuni na unabiii ulikuwa kulingana na mkataba.(Mst.32) Mungu alikuwa amemfufua mwanawe kutoka kwa wafu kulingana na Maandiko.

Hakuna shaka kwamba Zaburi hii ilikuwa uthibitisho ulioongoza mafunzo ya mitume, kwamba Messia lazima angekuwa mtu aliyefufuliwa. Mungu “alifunua kuelewa kwao”. Baadaye mtume Paulo anatumia Zaburi hii kwa njia sawa(Mdo 13: 34-37).

KUPAA NA KUJA KWA MARA YA PILI (Zaburi 110)

Kama Mungu alifufuka, je yuko wapi? Hili swali lililowakumba mitume katika kuhubiri kwao. Hili limeelezewa kwa nukuu katika Zaburi 110;1, “Mungu akamwambia  Bwana wangu, kaa kwa mkono wangu wa kiume mpaka pale nitawaweka adui zako chini ya miguu yako”. Kupaa kwa Mungu kulikuwa kumetabiriwa (Linganisha Matendo 2: 33-35).

Zaburi pia inatabiri kuhusu tukio la muhimu la kupaa, katika kutokuwepo kwake Bwana Yesu atakuwa kuhani wa mfano wa Melkizedeki (Mst.4) kwa sababu alifufuka kutoka kwa wafu, lazima angekuwa buila dhambi-"Mfalme wa Uadilifu" ("Melkizedeki") – na sasa akiwa na  uzima wa milele angeweza kuwakilisha akiwa  kwa mkono wa Mungu wa kulia, mahali palipo katazwa binadamu aliye na mwili wa kufa. Zaburi 110 haikatazi hili. Kikomo cha mda kimewekwa katika kukaa kwake mbiguni.  Atakuwepo “HADI adui zake watakapowekwa  kama kibao chini ya miguu yake”. Hivyo Zaburi inazungumzia kuingilia kati kwake katika vita vya Armageddon na ushindi wake (Mst.2, 5-7).

Bwana Yesu aliweka swali mbele ya Wafarisayo kwa kutumia msingi wa Zaburi 110:1.  Akawauliza  Mesiya atakuwa mwana wa nani. Wakajibu bila kusita "Mwana wa Daudi". Lakini katika Zaburi 110: 1 Daudi anamuita mwanawe kama “Bwana” wake. Bwana Yesu aliuliza kwa nini David alifanya hivyo, kwani kwa  mila za Kiyahudi mzazi wa kiume alikuwa na heshima kuliko mwanawe – kwa hakika hii ingetumika kwa mfalme mwenye sifa kama Daudi. Hii haikuwa  katika hali ya Messia. –Kwanini? Wafarisee walishindwa kujibu na hawakujaribu kumuuliza maswali mengine (Mt. 22: 41-46).

Lakini kwa nini mwana wa Daudi alikuwa pia "Bwana" wake? Jibu linapatikana kwa ukweli kwamba  alikuwa pia Mwana wa Mungu. Ilikuwa ni hili ambalo Wayahudi walikataa kukiri na kukubali, na kwa ajili hii walimwita kafiri (Yn.5:18; Mt.26: 63-65).

 NGUVU NA UFALME WAKE (Zaburi 2).

Zaburi hii inaweza kuwa imeandikwa na Daudi kufuatia ushindi wake juu ya muungano ulikuja dhidi yake wakati alipowashambulia Waamoni (2 Sam. 10: 6-19). Ndani ya haya kunaonekana mgogoro ambao atakumbana nao Yesu wakati atakaporudi kuanzisha utawala wake Sayuni. Mataifa yatajaa hasira na kukusanyika pamoja dhidi ya mteuliwa wa Mungu (Mst 1-3) lakini hasira ya binadamu ni kitu kidogo katika hukumu ya Mungu na atacheka na kuwakejelii (mst.4-5) kwa sababu yeye ni Mwana wa Mungu na  ana “Jina tukufu” na ataridhi” kila sehemu ya dunia” kuwa Mwana wa Mungu kulimpa haki ya uridhi and atatumia nguvu za Mungu kuangamiza mataifa. (mst 8, 9). Mstari wa 9 katika Ufu. 2.27 Mungu anaahidi nguvu sawia kwa watakatifu. “ Yule ashindaye na kuzingatia kazi yangu hadi mwisho, nitampa nguvu juu ya mataifa; na atayatawala na fimbo ya chuma. Sisi pia tunaweza kuwa wana wa Mungu kwa njia ya ubatizo hadi kwa jina Mwana na kama “Wana” basi tutakuwa waridhi wa Mungu pia (Rom. 8:17.).

Zaburi inamalizia kwa kutoa ushauri kwa viongozi wakati Kristo anarudi. Wanaitwa kunyenyekea kwake ama watangamia (Mst. 10-12). Nukuu zifuatazo zinatuonyesha kwamba kuna wale watanyenyekea na kuna wale watakataa. (Mik 4:. 2-3; Zab. 72: 9-11.).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Zaburi inatuonyesha hisia  za ndani za Daudi na taabu zake. Hisia na kutaabika huku kunachukuliwa na Roho Mtakatifu ili kuweze kutabiri vilivyo uzoefu wa Messia.
  • Kutafakari juu ya unabii  uliofanyika miaka 1,000 kabla kuja kwa Yesu Kristo, na jinsi ulivyotimizwa inapaswa kuimarisha kuelewa kwetu na mamlaka ya Neno.
  • Baadhi ya Zaburi zinalelezea kuhusu matukio yote mawili ya ujio. Ukweli kwamba unabii wa ujio wa kwanza umetimizwa, unapaswa kutuhakikishia kutimizwa kwa matukio mengine katika siku zijazo.

 

MASWALI YA AYA:

  1. Jinsi gani tunajua kwamba Zaburi ya Daudi ilikuwa imeteuliwa?
  2. Kwa nini Petro alinukuu Zaburi 16 katika hotuba yake iliyorekodiwa katika matendo2?
  3. Kwa nini Daudi alimwita mwanawe Bwana wangu? Jibu lako lizingatie Zab. 110: 1  na utaje kwanini Yesu aliwauliza Wafarisee swali lile.

 

MASWALI YA INSHA:

  1. Jinsi gani Zaburi ya Daudi ilifunua kuhusu maisha na kazi ya Bwana Yesu Kristo? Toa mifano kutoka Zaburi 2.
  2. Onyesha jinsi Zaburi 22 na 69 zinaonyesha mateso na utukufu wa Kristo.
  3. Zaburi 2 na 110 inasema nini kuhusu ujio wa pili wa Kristo?

 

Swahili Title
303. MESSIA KATIKA ZABURI YA DAUDI
Sub type
Sub sub type