CSSA 3-3-304 - SOLOMON SUCCEEDS DAVID

Swahili

304.    SULEMANI ANAMRIDHI DAUDI

"Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Bwana kama Mfalme baada ya Daudi babake, naye akafanikiwa na Israeli yote ikamtii"

Wakati ulikaribia wa Daudi kufa. Mambo kadhaa muhimu ilibidi kutimizwa; Ufalme ulikuwa uwekwe kwa mikono ya Sulemani na mipango ya hekalu, ambayo ilikuwa imefunuliwa Daudi na Roho, lazima ingejulikana. Ilionekana kwamba fikra zake zilikuwa zimejaa na mipango ya Nyumba ya Bwana ambayo alikuwa amekatazwa kujenga. Ingawaje alikuwa amekusanya utajiri mkubwa ili kuhakikisha kwamba itakuwa “kubwa, ya kupendeza na yenye utukufu kote nchini" (1 Nya 22:. 5 ).

Lengo la somo hili ni kuona jinsi Sulemani alianzisha utawala wake akiwa na hali ya haki na huruma, kama vile Yesu kristo ataanzisha utawala wake.

1 Wafalme 1-3; 1 Mambo ya Nyakati 28 na 29

UASI WA ADONIJA (1 Wafalme 1: 1-31)

Ilikuwa ni wazi kwa wote kuwa maisha ya Daudi yalikuwa yanafikia mwisho. “Miaka yake ilikuwa imesonga sana na hakuweza kupata joto” Ilikuwa inajulikana kwamba Sulemani ndiye atachukua taji, lakini nafasi hii haikuwa imefanywa wazi kabisa. Daudi alikuwa amedhoofika kimwili, mwanawe Adonija aliyependa siasa alichukua nafsi hii kuanzisha uasi. Alitayarisha magari ya farasi wa waendeshaji wake na wanaume 50 kama walinzi wake wa kibinafsi. Alishauriana na watu mashuhuri katika ufalme wale ambao alihisi angeweza kuwaamini, watu kama Yoabu, jemadari wa jeshi na Abiathari, kuhani, na kuwaalika kwenye sherehe. Kulikuwa na watu maalum ambao hawakualikwa, miongoni mwao alikuwa, Nathani nabii, na Benaya, na mashujaa wake, Sulemani. Kondoo na ng'ombe walichinjwa na sherehe ya Adonija ikaendelea.

Lakini Nathani nabii alijua kuhusu mpango wa Adonija alitambua kwa haraka matokeo yake. Sio tu ahadi ya Mungu kwa Daudi ilikuwa inadhalilishwa, lakini wale ambao hawakualikwa wangehesabiwa kama waasi kama Adonija angekuwa mfalme.

Alimwambia Bethsheba, mamake Sulemani habari hio na akapendekeza mpango  wa kumhimiza mfalme aliyezeeka kumteua Sulemani kama mfalme hadharani. Alipendekeza kuwa Bathsheba aende kwa Mflame Daudi na kupokea uhakikisho kwamba mwanawe Sulemani ataahidiwa ufalme. Kisha akaambiwa alulize swali lingine, “kwanini Adonija anatawala?” wakati atakapokuwa akiongea Nathani atafika na kutilia mkazo maneno yake. Hivyo Bathsheba akafanya kama ilivyopangwa na kuelezea hofu yake na Sulemani baada ya kifo cha Daudi. Hapo ndipo Nathani aliingia. Akaelezea umuhimu wa hali ile na kudai kwamba kama Adonija alikuwa na ruhusa ya Daudi basi Sadoki na Benaya wakapokonywa heshima na nafasi zao za kijeshi (Mst.22-27). Daudi alitafakari maneno haya sana. Akamwita Bathsheba tena na akarejelea kiapo chake cha awali kuwa  Sulemani atatawala baada yake. Kisha akamwambia kuwa amtemteua kama mfalme wa Israeli siku hio.

SULEMANI ANATEULIWA KAMA MFLAME (1 Wafalme1:32-40).

 Daudi alitimiza neno lake haraka. Akamwita Sadoki, Nathani na Benaya pamoja na kuwaambia nini cha kufanya. "Twaeni watumishi wa Bwana wenu, na mfanye Sulemani kupanda punda wangu mwenyewe, na mumlete hadi Gihoni; na muwaruhusu Sadoki kuhani na Nathani nabii amteue kama mfalme wa Israeli; na mpulize tarumbeta, na  mseme, Mungu muokoe Mfalme Sulemani. Kisha nyinyi mtamfuata, naya atakuja na kukaa juu ya kiti changu; kwani yeye atakuwa mfalme baada yangu; nami nimemteua kuwa mtawala wa Israeli na Yuda” (Mst.33-35) Mapenzi ya Daudi yalitimizwa ipasavyo na kulikuwa na furaha  Yerusalemu. Ilikuwa ni wazi kwamba Sulemani alikuwa amekubaliwa na watu kwani walikuja wote na “kusherehekea kwa furaha, hadi dunia ikatikisa kwa sauti yao. (Mst.40)

SHEREHE YA ADONIJA INAKUWA HOFU (1 Wafalme 1:41-53).

Kilio cha furaha kilisikika hadi bonde la Kidroni na kusikika na wageni wa Adonija. Yoab alishtuliwa na  sauti ya tarumbeta na kuuliza kwanini kulikuwa na ghasia mjini. Wakati huo huo Jonathani mwana wa Abithari akaingia,na kuwaelezea. Adonija angefikiria kwamba mji umesikia kuhusu hatua zake na walikuwa wanamsherehekea yeye, kwani alimkaribisha Yonathani vizuri, “Karibu, wewe mtu mwema, unayeleta habari ya  mambo mazuri”. Lakini, ole wake, uchangamfu wake ukageuka kuwa hofu. Jonathani akatoa ripoti kamili, "Hakika bwana wetu, mfalme Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme..." (mst.43-48). Adonija, na wageni wake wakajawa na hofu. Kuwepo kwao pale kulionyesha uasi dhidi ya Daudi na Mungu. Kwa haraka walimtoroka Adonija na “ kila mtu akaenda njia yake” Adonija akatetemeka na akatambua kwamba maisha yake yalikuwa hatarini. Akaenda hadi kwa madhabahu na kushika pembe zake akitumainia kupata msamaha. Alitafuta kiapo kutoka kwa Sulemani kwamba hatauawa. Kwa hekima, Sulemani akampa afueni mradi tu  asipatwe na uovu wowote katika siku zijazo.

SULEMANI ANAFANYWA MFALME RASMI (1 Mambo ya Nyakati 28-29).

Upako wa kwanza wa Sulemani ulikuwa umefanywa kwa haraka kutimiza haja iliokuwa imetokea. Baadaye Israeli walikusanyika na Daudi akamteua Sulemani kama Mfalme na kumpa usukani. Maelezo ya mkutano huu yanapatikana katika 1 Nya. 28 na 29. Tunasoma kwamba "Daudi mfalme akasimama kwa miguu yake" kuhutubia watu wake.Alikuwa mzee na dhaifu and alikusanya nguvu zake zote. Kutoka kwa maneno yake ya imani na ujasiri aliyozungumza, tunaweza kuona kwamba alitamani kuacha taifa linalomwogopa Mungu. Alirejelea sauti ya  Mungu ya uteuzi wake kama mfalme kisha akakumbuka jinsi alivyomteua Sulemani kutoka kwa wanawe wote amridhi ufalme na “kukaa kwenye kiti cha ufalme wa Mungu wa Israeli”. Kuna uwezekano Adonija alikuwa katikati ya umati. Mapenzi ya Mungu na Daudi yalikuwa wazi. Alimhimiza Sulemani kumtumikia  Bwana na “Roho safi” na “akili sawa”, lakini alielezea wazi kwamba  laana itabadilisha baraka kama angemwacha Yahweh. Kwa kumbukumbu maneno haya yalikuwa ya mkasa na ya kinabii. Daudi alimpa Sulemani wajibu wa kujenga nyumba ya Mungu. Alimpa mipango ambayo Roho alikuwa amemjulisha. Alikuwa amepewa mipango hii moja kwa moja(28:12)

Mipango hii haikuwa imekuja kupitia Nathani wala Abithari. Kwa hili huruma ya Mungu inaonekana, kwani ingawa Daudi hakuruhusiwa kujenga ile nyumba kama alivyotamani, alipokea mipango. Daudi alielewa ukubwa wa kazi ya kujenga hekalu na akamuuliza mwanawe kufanya kazi hio vyema. Aliweka mfano wake mbele yao na akasema “nimetayarisha kwa nguvu zangu zote nyumba ya Mungu wangu”, Hakuwa ametumia vibara  utajiri wake na ushuru lakini alikuwa ametoa sadaka ya kibinafsi (29.3) Alikuwa ameionea furaha nyumba ile, je wakuu wagefanya hivyo?

Watu walifurahishwa na roho wa Daudi na wakaitikia wito wake.  Jambo hili linataka tafakari yetu: “watu walifurahi, kwa hivyo walitolea, kwani kwa roho  safi walikubali kujitolea kwa Bwana. Mfalme Daudi alifurahi furaha kubwa zaidi.” (Mst.9) Hili likasababisha ombi la kutoa shukrani ambalo lilifanywa na Daudi na ambalo sehemu yake ni msingi wa Sala ya Bwana (Taz. mst.10, 11). Moyo wake ulijaa shukrani kwa Bwana na akatambua kwamba Alikuwa chanzo cha utajiri wake na kwamba binadamu alikuwa mgeni tu huku duniani. Daudi kisha akafanya ibada kwa Bwana. Watu wakambariki, kwa kutoa sadaka na kufurahia wakati Sulemani aliteuliwa kwa “mara ya pili” kama mflame “kwenye kiti cha enzi cha Bwana baada ya Daudi babake” (Mst.20-23)

USHAURI WA MWISHO KWA SULEMANI (1 Wafalme 2: 1-9)

Wakati Daudi alitambua kwamba kifo chake kilikuwa karibu alimpa Sulemani ushauri wa mwisho. Alimshauri kuweka amri za Mungu. Kwa kufanya hivyo angefaulu katika njia zake na maneno ya ahadi, kuhakikisha kwamba kutakuwa na msururu wa wafalme wa laini ya Daudi mpaka ujio wa Messia, utakuwa umetimizwa (Mst.1-4)

Daudi alimshauri Sulemani jinsi ya kukabiliana na watu fulani katika ufalme wake ambao walikuwa  waasi na hatari. Kwa sababu ya dhambi, miaka yake na mazingira, Daudi hakuweza kuwaadhibu watu hawa waovu. Alimwelekeza Sulemani kumwondoa Yoabu kwani alikuwa amevunja  amri ya mfalme, wakati aliwauwa “wakuu wawili wa jeshi” Abneri na Amasa (Mst.5-6; 2 sam. 2: 27-39; 20:10). Shimei pia alipata adhabu hio hio kwani alikuwa amemlaani Daudi wakati aliondoka Absalomu (Mst.8-9; 2 Sam. 16:. 6-14). Kwa upande mwingine wana Barzilai walikuwa waonyeshwa wema, kwani walikuwa wamemsaidia Daudi wakati wa mahitaji. (Mst.7)

 HUKUMU YA SULEMANI DHIDI YA WATENDA DHAMBI (1 Wafalme 2: 10-46)

Daudi alifariki baada ya miaka 40 kama mfalme aliyeishi maisha yenye furaha, huzuni na shughuli nyingi. Sulemani alianza shughuli ya  kuimarisha ufalme wake. “Sulemani akakaa juu ya kiti cha enzi cha Daudi babake; na ufalme wake ukawa umeanzishwa rasmi. (Mst.12) watenda dhambi waliondolewa kwenye uogozi  ama kuuawa.

  1. Adonija (Mst. 13-25). Alikuwa amepata msamaha baada ya jaribio lake la kuchukua ufalme bila idhini kwa sharti “angekuwa mtu mwema”. Lakini kupita Bathsheba, mamake Sulemani, aliagiza  Abishagi awe mkewe. Adonija alifanya ombi hili kwa msingi wa majonzi. Alimwambia Bethsheba “Wewe unajua kwamba ufalme ulikuwa wangu... Lakini ufalme umegeuka na kuwa wa ndugu yangu”. Abishagi alikuwa mwanamke aliyekuwa amepewa Daudi, Mflame wakati wa uzee wake. Ombi hili la majonzi lilikuwa la dhulma na uasi. Sulemani akaona  jambo hili na kutoa hukumu ya haraka.
  2. Abiathari (Mst.26-27). Aliondolewa kwa ofisi yake kama kuhani na kufukuzwa hadi Anathothi kwa sababu alikuwa amemuunga mkono Adonija, na  kusaliti Neno la Bwana ambalo lilikuwa limeonyesha pendezo la Mungu la Sulemani. Hivyo hukumu ikatekelezwa, nje ya nyumba ya Eli (Mst.27; 1 2 Sam: 31-35.). Sadoki, kuhani mwaminifu, aliteuliwa badala yake kutembea na wateuliwe wa Bwana (Mst.35).
  3. Yoabu (Mst.28-34) Aliposikia hasira za Sulemani alijua atafuata hatima ya Adonija. Kama Adonija hapo awali, alikimbilia madhabahuni na kushika pembe zake kwa matumaini ya  kupata msamaha. Aliuwawa na upanga wa  Benaya, mwana wa Yehoyada. Benaya aliteuliwa mkuu wa jeshi badala Yoabu.
  4. Shimei (Mst.36-46). Aliruhusiwa kuishi bila kuingilia masharti ya kuishi Yerusalemu au kuvuka kijito cha Kidroni. Kwa miaka mitatu mkataba huu ulizingatiwa, lakini watumishi wake wawili walitorokea Gathi na Shimei akatoka kwenda kuwarudisha.

Neno likamfikia Sulemani kwamba mkataba ambao ulikuwa umewekwa kupitia kiapo mbele ya Mungu umevunjwa. Hivyo Shimei akauwawa. Katika nyakati hizi haki na hali ya kuwa imara kwa Sulemani ilionekana. Waasi hawakuwa na nafasi katika ufalme na pia ufalme wake haungesumbuliwa (mst.46) Tunaweza jifunza mafunzo hay mawili wakati huu;

  1. Kucheleweshwa kwa adhabu katika dunia ya leo ni motisha kwa watenda dhambi kuzidisha uovu wao. Sulemani alitambua hili na baadaye akasema “kwa sababu hukumu dhidi ya tendo ovu haitimizwi kwa haraka, hivyo mioyo ya wanadamu imedhibitisha ndani yake kutenda maovu"(Mhu 8:11).
  2. Wakati Bwana atakuja, kama Sulemani,  atawangoa wafanyikazi waovu, kwa haraka na hukumu yake itakuwa ya haki na italeta amani duniani (Mai. 4: 1-3; Isa.11: 4-5; 32: 1-6).

YAHWEH ANAMTOKEA SULEMANI KULE GIBEONI (1 Wafalme 3: 2-15).

Sulemani alikuwa na mwanzo mwema. “alimpenda Mungu na alitembea katika nyayo za babake Daudi” (Mst.3) Akiwa Gibeoni akitoa sadaka Bwana akamjia na kumuuliza “unataka nikupe nini” Solomoni alitafakari jinsi familia yake ilikuwa imeunganishwa na mipango ya Mungu; Bwana alikuwa ametimiza Neno lake kwa Daudi na kumweka mwanawe katika kiti cha enzi; alikuwa bado kijana na alikosa uzoefu; watu wake walikuwa watu wa Mungu na walikuwa wengi sana. Kwa mtizamo huu alijibu kwa unyenyekevu:

“Nipe mimi mtumishi wako moyo wenye maadili ya kuwahukumu watu wako, ili niweze kutambua mema na mambaya: kwani nani anayeweza kuwahukumu watu hawa wako wakuu” (Mst.9)

Ombi hili ni mfano wa kuigwa kwa toleo kama hilo. Vijana wote ambao wana matumaini ya kuwa wafalme na makuhani katika siku zijazo wanapaswa kuomba ombi kama hili.  Hekima kama hii inapatikana kwa urahisi kutoka kwa Biblia na hasa katika ufunuo kamili wa Baba wakati alizungumza na Mwanawe na mitume watakatifu.

Bwana alifurahishwa na jibu la Sulemani na hakumpa tu hekima kubwa zaidi kuliko mtu yeyote bali alimwongezea vitu vingine ambavyo angeomba kama, utajiri na heshima na maisha marefu kama angefuata amri za Mungu.


HEKIMA YA SULEMANI: MAKAHABA WAWILI (1 Wafalme 3: 16-28).

Hekima kuu ya Sulemani ilionekana wakati alipitisha hukumu dhidi ya makahaba wawili waliofika kwake. Waliishi peke yao ndani ya nyumba moja na kila mmoja alikuwa amejifungua mtoto siku tatu tofauti. Usiku mtoto mmoja aliifariki baada ya kulaliwa na mamake. Baada ya kugundua kilichotokea akawabadilisha wale watoto. Siku iliofuata mwanamke yule mwingine akangudua kwamba mtoto aliyekufa hakuwa wake. Kesi hii ikaletwa mbele ya Sulemani. Ilikuwa ni ngumu kutoa hukumu kwani hakukuwa na shahidi; pia hili lilikuwa jambo lenye hisia nyingi, kila kahaba alidai mtoto aliye hai ni wake. Nini kilikuwa kifanyike?

Sulemani aliitisha upanga na akapendekeza kwamba mtoto aliye hai agawanyishwe vipande viwili na kila mmoja aende na kipande kimoja. Pendekezo hili lilileta majibu ya haraka. Mzazi wa kweli alimtamani mwanawe na alikuwa tayari kumsalimisha mtoto yule ili apate kuishi. Yule mwingine alikubali kwa haraka pendekezo la kumkata yule mtoto kwa vipande viwili.

Hukumu ikawa wazi na mzazi wa kweli akaonekana wazi. Mfalme Sulemani akatawala kwa haki na hukumu. Sifa zake zikaenea mbali. “Israeli ikasikia kuhusu hukumu ambayo mflame alikuwa ametoa: wakamwogopa; kwani waliona kwamba hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, akitoa hukumu hii. (mst.28)

 

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Unafiki na tamaa ya uongozi inayohushisha kuvunja sheria haina manufaa. Hofu, aibu na kifo kilimfuata Adonija.
  • Upendo wa Daudi kwa Bwana na Nyumba yake ulitawala fikra zake za mwisho. Ukarimu wake aliwaongoza wenzake. Vyote tulivyo navyo ni mali ya Bwana na vinapaswa kutumiwa katika huduma yake. Yeye anapenda mtu anayetoa kwa moyo mkunjufu. Tunawekeza kwa busara  wakati tunatumia muda na fedha katika ukweli.
  •  Hukumu imara ilileta heshima. Ufalme utahakikisha wafanyikazi wote waovu wameharibiwa. Lazima tusimame imara na tuondoe uovu, kiburi na usherati sasa kama tunataka kutawala baadaye (2 Kor. 10: 4-5).
  • Sulemani alikuwa na hekima kuu na nguvu za kutambua. Kristo ana zaidi ya hizi na tunapaswa kukumbuka hili kila wakati.
  • Ombi la Sulemani la kupewa “Moyo wa kuelewa” ni mwongozo wa kila kijana mkristo katika maombi yake.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 4, Nam. 7

"The Man David" (H. Tennant)—kur. 207-215

MASWALI YA AYA:

  1. Jinsi gani Adonija alitaka kumridho babake Daudi kama Mfalme?
  2. Nini Sulemani alimfanyia Yoabu na ni kwanini?
  3. Sulemani aliomba nini wakati Mungu alimwambia “niambie nikupatie nini"?
  4. Je ni nini Sulemani angeomba lakini hakuomba?
  5. Kwa kifupi elezea matukio mawili ambayo yalionyesha kuwa Sulemani alitawala kwa uadilifu na haki.

 

MASWALI YA INSHA:

  1. Simulia kile Daudi alichofanya kumweka Sulemani katika kiti chake cha enzi.
  2. Fanya utafiti na uandike kuhusu tabia ya Adonija.
  3. Jinsi gani Sulemani alianzisha ufalme wake kwa njia imara baada ya kumridhi babake?
  4. Andika insha juu ya hekima ya Sulemani.


 

Swahili Title
304. SULEMANI ANAMRIDHI DAUDI
Sub type
Sub sub type