CSSA 3-3-306 - THE GLORY OF SOLOMONS REIGN

Swahili

306. UTUKUFU WA UTAWALA WA SULEMANI

"Tizama sikuelezwa yote: lakini hekima na ustawi umepita sifa nilizosikia”

Utawala wa Sulemani  ulianzusha kipindi cha utukufu katika historia ya Israeli ambao hungefikiwa na mwingine mpaka pale “mkuu kuliko Sulemani, Bwana Yesu Kristo, atakaa kwenye kiti cha enzi cha Mungu” Yerusalemu.

Sulemani alipokea ufalme uliotayarishwa kwa ajili yake. Alipewa hekima ya Mungu na akafanikiwa kama msomi mwenye hekima wa  nyakati hizo na  mataifa yote yakatuma mabalozi kutoa heshima zao kwa mfalme na pia kusikiza maneno yake ya Utajiri na heshima aliongea Yerusalem, hivyo akazidisha kivutio cha utawala wake. Miaka 40 ya utawala wa Sulemani unafananishwa na utawala wa milele wa Mungu utakao tawaliwa na Kristo katika ujio wake wa pili.

Lengo letu katika somo hili ni kuona ukuu wa utawala wa Sulemani, utawala unaofana  na ule wa Bwana Yesu Kristo.

1 Wafalme 10

URIDHI WA DAUDI

Kipindi hiki katika historia ya Israeli kiliwezekana kupitia kampeni za kijeshi zenye mafanikio ambazo Daudi alifanya dhidi ya adui zake. Kazi ya Sulemani hivyo ilikuwa kudumisha na kudhibiti sehemu kubwa iliyopewa na babake Daudi. Kama mwakilishi mwenye busara, Sulemani alikuwa latika nafasi ya kuvuna matunda ya ushindi wa Daudi.

Alitawala Israeli kwa kipindi cha miaka arobaini (2 Nya. 9:30), na ilikuwa ni katika kipindi hiki cha mafanikio ya Israeli ambapo Sulemani alibadilisha Israeli kutoka kwa hali ya awali ya Daudi  ya mataifa binafsi na kuifanya taifa lenye nguvu na utawala wa pamoja na shughuli nyingi zilizofanikisha utawala huu (1 Fal. 4: 20-21). Mipaka ya awali ya kikabila ilibadilishwa na wilaya za utawala. Katika kabila hizi kumi na mbili aliweka  afisa wa kuchukua kodi, ambaye kazi yake kuu ilikuwa kuhakikisha kwamba  wilaya imetoa mazao kwa ajili ya mahakama ya kifalme kila wilaya kwa mwezi mmoja. Hii ingekuwa mzigo, kwani tunaambiwa kwamba chakula kilicholiwa kwa siku moja kilikuwa magunia 240  ya unga, magunia 480 ya chakula, ng'ombe kumi waliononeshwa, ngombe ishirini wa kulishwa, kondoo mia moja na ndege na wanyama wengine wa aina mbalimbali (1 Fal. 4: 22-23).


SULEMANI — MJEZI (1 Fal. 7: 1-8, 9: 15-24)

Mbali na ujenzi wa Hekalu tukufu la Bwana katika Yerusalemu (kama ilivyoelezewa katika somo la 5) shughuli za Sulemani za ujenzi zinaonekana katika kuimarisha mji wa Yerusalemu, jengo la ikulu yake na makao ya utawala na pia majengo mengine ya “kuhifadhi” na miji ya magari ya farasi na waendeshaji wake”.

Kama vile hekalu lilikuwa Tukufu, majengo mengine yaliohusishwa na hekalu yalikuwa ya kupendeza pia. Jumba la Hukumu la Sulemani lilikuwa kubwa na lilijengwa na mwerezi na kuzungushwa na pembe zilizofunikwa na dhahabu na kusimamiwa na simba (Fal.10:18-20). Hapa Sulemani alitoa hukumu yake (1 Fal. 7.7) kuashiria utukufu na fahari ya Kristo, ambaye alisema kuwa yeye atakuwa na "kiti cheupe cha enzi" cha hukumu (Ufu. 20:11).

Karibu na Jumba la Hukumu na kushikana na “Nyumba kuu ya msitu wa Lebanoni” kulikuwa na Jumba la Nguzo, ambapo mahojiano ya biashara na sherehe za taifa yalifanyika.

Safu za nguzo kubwa za miraba ya mwerezi ilishikilia paa la "Nyumba ya Msitu wa Lebanoni" (1 Fal.7: 1-5). Katika ukuta kulikuwa kumewekwa ngao 500 za dhahabu (1 Fal.10:16, 17), zilizotumika katika sherehe za Mfalme, onyesho ambalo lilimfurahisha Malkia Sheba aliyekuwa amekuja kutembea.. hata vyombo vya kunywea na sahani zilizokuwa kwenye nyumba hii kuu zilikuwa za “dhahabu”. Shaba “ haikuwa kitu cha kuhesabiwa katika siku za Sulemani” (Mst.21) utukufu zaidi ungeonekana latika majumba matukufu ya Siku zijazo (Tazama Isa. 60:11, 13, 17).

Kama vile majengo ya serikali, Sulemani alikuwa na makazi yake ya faragha pamoja na ikulu iliojengwa kwa ajili ya mmoja wa wake zake, binti ya Farao (1 Fal. 3: 1, 7: 8). Pia alianzisha shamba la kifalme na mbuga yenye maziwa bandia, shamba ya maua na matunda (Mhu. 2. 4-6).

Wanaakiolojia  wamepata ushahidi dhabiti wa majengo ya Sulemani kote nchini hasa Hazori, Megido na Gezeri, mabaki ambayo yanatoa ushahidi wa ukweli wa 1 Wafalme 9:15. Megido ni muhimu kwa vibanda vyake vya magari ya farasi 450. Jeshi kubwa la Sulemani lilihitaji jengo lenye vibanda 4,000  vya farasi na vilijengwa karibu na mipaka ya Israeli na kulindwa na waendeshaji magari ya farasi(1 Fal. 9:. 15-19; 10:26; 2 Nya. 09:25 ).

Sulemani  pia aliendeleza viwanda vya kusafisha chuma, pamoja na kuchimba madini katika Araba, kusini mwa Bahari ya Chumvi, na kiwanda kikubwa cha kuyeyusha vyuma cha Esion-geberi, mahali ambapo palikuwa bandari karibu na Bahari ya Shamu. Katika kuelezea sehemu hii, mabaki yameandikwa “ Biashara nzuri lazima  iwepo ili kurekebisha mtiririko wa faida kutoka kwa malighafi na bidhaa zilizokamilika na zile hazijakamilika. Hapo tunajua kwamba  ni mtu mmoja aliyekuwa na nguvu, uwezo, utajiri na hekima ya kuanzisha na kuendeleza shughuli hii ngumu. Alikuwa Mfalme Sulemani. Yeye pekee katika nyakati hio alikuwa na uwezo, maono na nguvu ya kuanzisha kiwanda muhimu na bandari kwa umbali na mji mkuu Yerusalemu. Esion-geberi anawakilisha moja ya mafanikio yake makubwa tunayojua  sasa hivi”- Nelson Glueck, "The Other Side of the Jordan". (Upande wa pili wa Yorodani)

SULEMANI — MFANYI BIASHARA (1 Wafalme 10: 21-29)

Sulemani alipata faida kwani Israeli ilikuwa sehemu nzuri katikati mwa bara la Asia na Afrika.  Alitawala  njia za kaskazini na kusini na kwa usaidizi wa Wafoeniki, alijenga meli  nyingi  pale  Esion-geberi ili zitumike kubeba shaba iliosafishwa na bidhaa zingine. Meli hizi zilifanya  safari ya  kusini hadi Ethiopia, Yemen na India Arabian mara moja kila miaka mitatu, na kuleta dhahabu, fedha, na pembe, nyani na tausi (1 Fal. 9:26; 10:22).

Biashara yake iliyofaulu iliweza kuonekana pale alipokuwa wakala maalum ambaye kupitia kwake Wahiti, na Waarmenia ilibidi kujadiliana ili wanunue farasi kutoka Kue (Kilikia) au magari kutoka Misri (1 Fal. 10:28, 29 ). Makampuni haya na biashara zingine zilifanya fedha kuonekana kama chuma cha kawaida na mierezi kama mkuyu katika Yerusalemu. Katika mwaka mmoja talana 666 za dhahabu ziliingia katika hazina ya Sulemani (1 Fal.10:14).

 

MALKIA WA SHEBA (1 Fal. 10.: 1-10).

Viungo kutoka Sheba viliuzwa kupitia “Njia ya Uvumba”  iliogawanyikia  Esion-geberi kwa upande wa kaskazini mwa Yerusalemu, Shamu au kusini kwa Misri. Ujenzi wa viwanda vya Sulemani katika kituo hiki Malkia wa Sheba alitambua utufuku wa wa Ufalme. Zaidi ya hayo, 1 Fal, inaonyesha kwamba  Malkia wa Sheba alisikia “kutajwa kwa jina Yahweh” jina hili likihusishwa na ufalme wa Sulemani. Alichukua gamia wengi wakiwa wamebeba viuongo, dhahabu na mawe ya dhamani yaliyofaa utawala muhimu kiasi hiki, Malkia wa Sheba alikuja Yerusalemu na ghafla akaanza kumuuliza Sulemani maswali huku akichunguza ibada katika Hekalu na ushahidi wa taifa hili lililofanikiwa na lenye furaha. Alishangazwa na utukufu wa utawala wa Sulemani, maneno yake yanaonyesha  kuelewa na kukubali utawala wa Bwana, Ufalme wa Mungu wa awali (Mst. 6-9).

Ziara ya Malkia wa Sheba na zawadi zake na kisha kumsifu mflame wa Yerusalemu ni mfano wa viongozi wa mataifa, hasa Uingereza, kukubali aliye mkuu kuliko Sulemani, Bwana Yesu Kristo. Wakati viongozi hawa wa “kisasa” wanaona  utukufu wa ufalme wa Kristo, ukubwa wa mahakama yake pamoja na watumishi wake wa milele, uzuri na usafi wa ibada na israeli iliookolewa na yenye imani, pia wao watatangaza kwamba “hawakulezwa  yote”. Kwa kufurahishwa na nguvu hizi watarudi nyumbani kwa watu wao wakiwa wamejaa na sifa kwa Mfalme wa Sayuni (Zab;72:10 Isa. 60: 3-11; Zek. 14:16.).

HEKIMA YA SULEMANI (1 Fal. 4:29-32)

Uchaguzi wa Busara wa Sulemani kwa kumwomba Bwana “Moyo adili wa kuwahukumu watu wako” (1 Fal. 3:. 5-9), ulisababisha idhini ya Bwana na utoaji wa "moyo wa hekima na ufahamu" na kuongezewa "utajiri na heshima "(1 Fal. 3:13; 4:29).

Hekima yake alitambulika na wote wa rika lake katika Misri, Arabia, Kanaani na Edomu (Mst. 30-31), kusababisha mataifa yaliyozunguka Yerusalemu pamoja na wafalme wao kufika Yerusalemu ili kupokea  hekima hii. Kwa njia sawa mataifa ya siku zijazo yatatamani kuelimishwa katika nyumba ya Mungu wa Yakobo (Isa. 2: 2-4), na kutambua kuwa hekima ya dunia katika nyakati hizi za watu wa mataifa zilikuwa “uwongo, ubatili na mambo yasiyo na faida"(Yer. 16:19).

Mchanganyiko wa makubaliano ya kimataifa, utajiri na kutokuwa na vita kulisababisha kuweko kwa wakati maalum wa maendeleo ya uandishi. Sulemani alikusanya  na kutunga maelfu ya methali na nyimbo (Mst. 32). Pia alijifunza mambo ya mimea na wanyama (Mst.33).  Akizitumia katika  uchunguzi wake wa asili katika methali zake (kwa mfano Mithali 30: 24-31). Makusanyiko mkubwa wa vitabu katika  Kitabu cha Mithali ni sifa kwake (10: 1 hadi 29:27) na mkusanyiko huu wote una jina lake kama mchangiaji mkuu (1: 1). Wimbo wa Sulemani na Mhubiri pia zina ushuhuda wa kutosha wa hekima yake.


SULEMANI ANALINGANISHWA NA KRISTO.

Kuna mambo mengi ya kulinganisha kati ya Sulemani, mfalme mwisho kutawala Israeli ilioungana, na Kristo, Mfalme wa pili kutawala Israeli yote (Eze. 37: 20-24).

• Hekalu la Sulemani lilikusudiwa kuwa nyumba ya sala kwa mataifa yote: Kristo atajenga Hekalu la Siku za Usoni kwa lengo lilo hilo (Zek. 6:12, 13; Isa. 56: 7).
• Katika ujenzi wa hekalu la Sulemani, watu wa Tiro walihusika pamoja na watu wa Israeli: katika Kristo, watu wa mataifa mengine na Wayahudi walitengeneza hekalu la Mungu la kiroho (linganisha Waefeso 2:19-22 na 1 Pet. 2: 4- 5); na katika ufalme ujao, watu wa jamii zote watamwabudu katika Nyumba ya Maombi (Isa 56:. 7).
• Chini ya Sulemani, Israeli ilikuwa yenye mafanikio na yenye furaha, na hivyo ndivyo taifa litakanyo kuwa chini ya  Kristo (Zek. 8:13.).
• Sulemani aliungana na wanabiashara wenye nguvu wa Tiro ili kuanzisha ufalme wake; Kristo atafanya  vivyo hivyo na watu wanao-ongea lugha ya Kiingereza, Tiro ya siku za usoni (linganisha 1Fal. 10: 22-23; 2Nya. 9:. 10-22 na Isa. 23: 17-18).
• Sulemani aligawanya taifa katika wilaya kumi na mbili, na kuziweka chini ya wakuu kumi na wawili (1 Fal 4:. 7): Kristo atafanya vivyo hivyo (Eze. 48.) Na wakuu (Mt. 19:28.).
• Chini ya Sulemani, utajiri wa dunia uliingia Israeli, na hii itakuja kutokea tena chini ya Kristo (linganisha 2 Nya 9: 13-14 na Hag. 2: 8-9 na Isa 60:11).
• Watu kutoka sehemu zote za dunia walikusanyika ili kusikiliza hekima ya Sulemani (1 Fal. 04:34, 10.: 23-25), na wakati Kristo atatawala Yerusalemu kila mtu ataenda kusikiliza maneno yake ya hekima (Zek. 14: 16; Isa 2: 2-4; Yer. 16:19)..
• Sulemani alikuwa mtu wa amani - Kristo ni Mfalme wa amani (Isa 9: 6; linganisha 72 Zab: 7).
• Dunia ilifurahishwa na utukufu wa Sulemani, na wakati Kristo Mfalme  atatawala "dunia yote itajaa utukufu wake" (Zab.72:19).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA

Kipindi maalum cha ufanisi katika historia ya Israeli kilitokana na maandalizi ya Daudi na hasa kwa baraka za Bwana katika kukabiliana na ombi la Sulemani apewe hekima na ufahamu.

• Wakati wa utawala wa Sulemani kulikuwa na amani Israeli na nje ya Israeli, watu walikuwa na furaha na usalama na watu wa mataifa mengine walivutwa na ibada ya Bwana; mambo haya yote yataonekana kwa ukamilifu katika Ufalme utakao anzishwa na Mwana wa Mungu.
• Sisi pia tunaahidiwa baraka za Baba kama kwanza tutatafuta Ufalme wa Mungu na haki yake (Mt.6: 24-34).
• Kama tutaepuka kujihusisha na mambo ya  dunia na tujitoe kwa unyenyekevu kwa Mungu katika kila nyanja ya maisha yetu ya kila siku, tunaweza kuangalia mbele na matarajio ya furaha ushiriki katika Ufalme mtukufu wa yule aliye mkuu zaidi kuliko Sulemani.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 4, Nam. 7-9

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—Sura 24

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 18

"Biblical Archaeology" (G. Ernest Wright)—Sura 8

"The Companion Bible" — Kiambatisho. 68.

 

MASWALI YA AYA:

  1. Maoni ya Malkia wa Sheba yalikuwa yapi wakati alimtembelea Mfalme Sulemani? Jinsi gani ziara hii itarudiliwa katika siku za usoni?
  2. Utawala wa Suleimani ulikuwa mfano wa Ufalme Ujao. Kwa kifupi elezea na uonyesha taarifa hii.

MASWALI YA INSHA:

  1. Eleza jinsi Sulemani alipanua kazi ya awali ya Daudi katika kuanzisha Ufalme.
  2. Eleza mafanikio ya Ufalme wa Sulemani.
  3. Linganisha utukufu wa utawala wa Sulemani na ile ya utawala wa baadaye wa Kristo.

MFANO WA UTAWALA WA SULEMANI

Chati ifuatayo inaorodhesha njia ambazo utawala wa Sulemani ni mfano wa ule wa Bwana Yesu Kristo. Kama zoezi weka alama katika Biblia yako.

 

 

Swahili Title
306. UTUKUFU WA UTAWALA WA SULEMANI
Sub type
Sub sub type