CSSA 3-3-307 - THE WARNING OF SOLOMON'S OLD AGE

Swahili

307.    ONYO LA UMRI MZEE WA SULEMANI.

"Wakati Sulemani alipokuwa mzee ...  moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama Ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake"

Kuwasili  kwa  Malkia wa Sheba kuangalia ustawi wa ufalme wa Sulemani  na kusikiza hekima yake ilikuwa pengine kipengele cha juu zaidi cha ufalme wa Sulemani. Alikuwa tayari amehakikisha uwepo wa Imani kwa kila upande, amejenga  hekalu ya  kubwa na kurudisha  Agano katika Mahali Patakatifu Zaidi, sasa Malkia wa watu wa mataifa alikuwa amekuja kuona yote aliyofanya. Lakini inasikitisha kwamba Sulemani baadaye hakukumbuka maoni ya Malkia  "Heri iwe kwa Bwana Mungu wako, ambaye amefurahishwa nawe na kukuweka katika kiti cha enzi cha Israeli;  kwa sababu Mungu ameipenda Israeli milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme kwa ufanye hukumu na haki "(1 Fal.10: 9).

Malkia wa Sheba alitambua kwamba kila kitu Sulemani alikwa nacho likuwa ni kwa ajili ya Mungu. Kwa huruma yake kuu alimuinua Sulemani na ufalme wake juu ya mataifa mengine yaliyomzunguka. Kama tu Sulemani angeweka haya akilini, rekodi ya kusikitisha haingepatikana katika maandiko.
 

Lengo letu katika somo ni kuona mambo ambayo yalisababisha Sulemani  kupotaka ili tuweze kuyaepuka katika maisha yetu.

1 Wafalme 10:24-11:25

IMANI YA SULEMANI INAANZA KUYUMBAYUMBA (1 Wafalme 10:24-29)

Upungufu wa Sulemani kutoka mtu wa Imani ulikuwa wa polepole wala sio wa ghafla. Wakuu wa mataifa mengine kando na Malkia wa Sheba, pia walikuja kusikia hekima ya Sulemani  na bila shaka kujionea utukufu wa Ufalme wake. Kila mgeni alileta zawadi ya kifahari za vyuma, viungo, ngao na wanyama, ambazo Sulemani  aliongezea kwa mali aliyokuwa nayo tayari.

Hali ya  kujigamba ilianza kuingia maisha mwake. Hali ya unyenyekeve aliyo-oyesha kule Gibeoni wakati Mungu alinena naye akiwa mdogo ilianza kupungua. Maono yake  yakaanza  kuharibika na hakumtumikia Mungu tena kwa moyo wake wote. Tamaa ya mambo mengine ilianza kuchukua muda wake.

Alipata tamaa ya utukufu wa kimwili  na akaanza kuangalia  mambo mengine na  kutimiza tamaa hizi. Maadishi yanatuleza kwamba Sulemani alikusanya magari ya farasi na farasi kutoka Misri. Alikuwa ameanza kuwa kama wafalme wa mataifa  mengine, kuamini nguvu za mwili. Wakati Sulemani alitazama haya, alikuwa ameanza  kumgeukia Mungu,nguvu ya kweli ya Israeli. Miaka mingi baadaye Isaiya alitoa onyo dhidi ya kuweka imani kwa farasi: “Ole wao ambao wanaoenda Misri kuomba msaada: na kupanda kwa farasi na kuweka imani yao kwa magari ya farasi  kwa sababu ni wengi, na wenye nguvu: lakini hawamwangalii aliye Mtakatifu katika Israeli, wala kumtafuta Bwana "(Isa. 31: 1 - tazama pia Zab.147: 10-11; 33: 16-19). Mungu alikuwa ametoa ushauri maalum kwa wafalme wa Israeli.

Kupitia Musa  aliamuru kuwa mfalme wa  dunia wa Israeli hakupaswa kujiinua kupitia farasi, wala utajiri, au mabibi. Kila moja  kati ya haya  yangesababisha mfalme kutoka katika imani ya Mungu na kuamini katika hali ya mwili. Tizama kwa makini (Kum. 17: 16-17) Sulemani alishindwa katika kila moja ya mambo hayo.

Hakukuwa na shaka kwamba Sulemani alitambua amri za Mungu kwa mambo haya,  kwani kila mfalme aliamriwa binafsi  kuandika nakala ya sheria wakati alipochukua  ufalme(linganisha.Kum. 17:18). Pamoja na onyo hili Sulemani alishindwa. Kama kuna wakati tunapata picha kamili ya undanganyifu wa dhambi, na jinsi mtu anavyoweza kujiondoa polepole kutoka kwa njia ya  Ukweli, basi tuna mfano kamili katika Sulemani. Alikuwa mtu mwenye hekima, na pengine alifikiri kwamba alikuwa na hekima na nguvu za kitabia angeweza kushinda majaribio yote ambayo yangetokea na utajiri wake wengine wangeshindwa lakini yeye angeweza kustahimili.

Hizi ni fikra za kibinadamu. Wakati hatua inachukuliwa katika mwelekeo usio sahihi basi, hatua zingine zaidi zinaweza kuchukuliwa kujaribu kuhalalisha zile zisizo za haki. Hivyo tunaweza danganywa na hoja zetu ambazo zinaweza kuwa na  matokeo mabaya. Eva alitambua katika shamba la Edeni kwamba hoja za kimwili zilisababisha adhabu ya kifo. Sulemani vivyo hivyo alitambua kwamba wakati mtu anaongozwa na mambo ya kidunia basi matokeo yanakuwa hatari. Majaribio yanaweza kushindwa “anasema Bwana”, lakini mkishindwa basi kuna matokeo mabaya ambayo yameandikwa katika maandiko kama mafunzo kwetu sisi sote.

KUANGUKA KWA SULEMANI (1 Wafalme 11:1-8)

Hamu ya Sulemani ya utajiri na farasi ilidhoofisha imani yake. Lakini alimtambua Bwana kama Mungu mmoja na wa kweli. Lakini alikuwa amepanda mbegu ya kimwili na katika hekima yake ya ajabu haikutosha kumzuia kuanguka katika kosa kubwa.  Tunasoma kwamba “Mfalme Sulemani alipenda wanawake wengi tofauti, hii ikiwa ni pamoja na binti ya Farao, wanawake wa Wamoabi, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti" (Mst.1).

Hali ya kuwa na mke zaidi ya mmoja ilikuwa imekubalika katika wakati wa Sulemani, na aliona kuwa na wake wengi na masuria kama hali ya kuweka heshima yake.  Uchaguzi wake wa mabibi, ulikuwa mbaya. Kila mke alitoka katika mataifa ya nje ya Israeli. “ kuhusu mataifa ambayo Bwana alikuwa amewaonya  wana wa Israeli, “Msiende kwao, wala msikubali waje kwenu: kwani bila shaka watageuza nyoyo zenu na kuzielekeza kwa miungu yao’” (Mst.2). Lakini rekodi inaonyesha wazi kwamba, "Sulemani aliambatana nao kwa upendo". Kando na haya  wake hawa walioorodheshwa katika mstari wa kwanza, Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300. Katika uamuzi wake alikuwa amefanya makosa na kupuuza onyo lililoko katika maandishi.

Jambo lililotarajiwa likatokea,  kwani tunasoma kwamba “ Wake zake wakageuza moyo wake, kwani  wakati ulifika wakati Sulemani alizeeka na wake zake wakageuza moyo wake kwa miungu mingine; na moyo wake ukawa hauko sawa na Bwana Mungu wake, kama ilivyokuwa moyo wa babake Daudi” (Mst. 3, 4). Kile kilichokuwa cha kutisha ni kuwa Mfalme mpendwa na mwenye hekima wa Israeli alikuwa ameanguka. Upendo wa mambo ya dunia na raha zake zilikuwa zimeharibu roho yake na kufumba macho yake. Neema ya Bwana ikamwondokea. Mwana wa Daudi mwaminifu, badala ya kuonyesha  hekima, utulivu na uongozi, akawa  Mfalme mzee na mjinga. Sulemani anaonekana kukuri haya  “Heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo. (Mhu. 4.13)

Kupitia ushawishi wa wake zake wapagani, Sulemani akawa mwabudu wa miungu na akaabudu sanamu za  miti na mawe mbele ya hekalu alilomjengea Mungu wa kweli. Alimwendea Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni. Mfano wa ibada yao ulihusisha vitendo vilivyo kuwa kinyume na maadili na vipotofu. Jambo hili lilikuwa na madhara ya kudhalilisha kwa  taifa, mbali na mfalme mwenyewe Milcom, au Moleki, chukizo la Waamoni, ni mungu mwingine Sulemani alimgeukia. Kwa hili wana wa Mungu walitolewa kama sadaka na ngoma zilipigwa ili kuficha vilio vyao wakiteketezwa. Ibada hii ya kuchukiza ikawa hali ya maisha ya waIsraeli na ilifanyika katika bonde la Hinomu. Haikuwa mpaka utawala wa mfalme mwenye haki Yoshua miaka mingi baadaye dini hizi za kuchukiza ziliondolewa. (2Fal. 23.10)

 

MUNGU ANAMHUKUMU SULEMANI KWA MAKOSA YAKE (1 Wafalme 11:9-25)

Amri ilikuwa wazi na hakukuwa na sababu yoyote ya kuondoka kwa Sulemani. Kando na maagizo yaliyo wazi kutoka Sheria za Musa, Mungu alikuwa amemtokea Sulemani mara mbili:-

  1. Gibeoni, ambapo aliahidiwa baraka kama angetii amri za Mungu (3:13-14)
  2. Yerusalemu, wakati Hekalu lilitakaswa, alionywa kuhusu hukumu kama yeye pamoja na taifa wangefuate miungu mingine(9:6-8)

Ni kanuni ya maandishi kwamba yule anabarikwa na mengi, vivyo hivyo mengi yanahitajika kutoka kwake.Hivyo Ilikuwa yule aliyependelewa sana apate hukumu kali: “Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, mengi yamefanywa kwako na wewe hujatii agano na sheria nilizo amuru mimi, hivyo nitakuchukua ufalme kutoka kwako na kuupa mtumishi wangu” (11:11).

Hii ilikuwa kweli adhabu kali na Sulemani bila shaka alikumbuka adhabu sawia iliadhibiwa Sauli kwa upumbavu wake (1 Sam. 13:13-14). Hata hivyo, kwa sababu ya maisha ya haki ya Daudi, Mungu aliamua kwamba hukumu hii haitatendeka katika wakati wa Sulemani, lakini katika siku za mwanawe Rehoboamu. Aidha sio ufalme wote ungekuwa chini ya Rehoboam, lakini ni makabila mawili tu ambayo yangebaki kuendeleza familia ya kifalme na Yerusalemu ikiwa mji mkuu. Huruma ya Mungu haingeondoka katika uzao wa Daudi kama ilivyochukuliwa kutoka kwa Sauli (2 Sam. 7:15). Kulikuwa na wafalme wazuri katika uzao wa Daudi (kwa mfano Yehoshafati, Hezekia, Yosia), na walisaidia katika kuhifadhi Ukweli, uasi ndio ilikuwa sifa ya wafalme wa makabila kumi ya kusini.

Ingawa hukumu kubwa iliahirishwa, Mungu alileta adui wa mfalme, kwa jina Hadadi, Mwedomi. Hadadi alikuwa ametoroka kutoka kwa shambulizi lililofanywa kwa Wadomi na Yoabu  na kuelekea hadi Misri ambako alikaa wakati Daudi alikuwa Mfalme, hata hivyo aliposikia kuwa Daudi na Yoabu wamefariki, alirudi katika nchi yake akiwa na nia ya kuwaunganisha Wedomu waasi dhidi ya Sulemani.

Yosephusi anarekodi kwamba Hadadi alishindwa kushawishi taifa kuasi, na hivyo akaenda Shamu kule akaungana na Rezoni katika kuvamia Israeli na kusababisha kero kubwa.  Rezoni anatajwa katika mstari.23-25 kama adui mwingine aliyeletwa na Mungu kumsumbua Sulemani. Rezoni alitawala Shamu kutoka Damasko na kutoka pale alivamia israeli, kwani aliichukia.

Hukumu kubwa ilikuwa bado inasubiri katika siku za usoni. Yeroboamu, mmoja wa Watumwa wa Sulemani alichochea makabila kumi kuasi. Siku za mafanikio, umoja, amani na ustawi ulikuwa umefikia mwisho na haugepatikana tena hadi kristo arudi, na kisha Mungu atampa kiti cha enzi (Eze. 21:27; 37: 22-25).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA

• Hakuna jambo lenye huzuni tunaweza kufikiri kuliko uasi wa Sulemani. Uasi ulianza kwa kile kilichoonekana kama kisicho na madhara - ukusanyaji wa polepole wa utajiri. Katika hili kuna onyo kwetu sisi ambao tunaishi katika nyakati za utajiri mkubwa. Vijana wa sasa wana mali na fedha nyingi kuliko walizokuwa nazo wazazi wao. Vijana tahadharini! Kama Sulemani, mfalme mwenye hekima kubwa, hakuweza kuhimili majaribu na raha ya umri wake, je sisi tunaweza kuyahimili? "Yule anayedhani amesima atahadhari asije akaanguka" (1Kor. 10:12).
• Kama vile Mungu alimuonya Sulemani, vivyo  hivyo Yesu Kristo alituachia onyo wazi juu ya hatari katika nyakati zetu. Siku zetu zinafanana na siku za Nuhu wakati watu walimkemea Nuhu na Mungu na walikuwa wamejitosa katika anasa za dunia (Mt. 24:. 36-41). Bwana akasema kuwa siku ya kurudi itatokea katika ulimwengu usio-jitayarisha; "Tahadharini, msije mkaacha mioyo yenu kudanganywa na anasa, ulevi na shughuli za maisha kwani siku hio itawajieni ghafla" (Lk. 21:. 34-36). "Anasa" ni neno la zamani kumaanisha uasherati na karamu za kidunia ilhali neno "ulevi" halikuhitaji maelezo yoyote. Dunia ya leo imejaa tabia hizi, na ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya vijana wamejiingiza katika shughuli  hizi katika tamaa yao ya  kuonja ladha ya mambo dunia.
• Kando na ushawishi wa tabia mbaya ya dunia, tunaweza pia adhirika na shughuli za maisha haya. Heshima kwa Mungu na Neno lake ni mambo yaliopitwa na wakati katika dunia ya leo ambapo watu wanadhani kuwa wanaweza kujitegemea. Hawatambui haja ya  Muumba wao. Tunaweza ambukizwa tabia hii urahisi kama hatutambui majukumu yetu katika maisha. Utajiri unaweza kutufunga macho kwa utegemezi wetu wa kiroho wa Mungu. Wakati  na nguvu zetu pia zinaweza tumika kwa urahisi tukitafuta utajiri wa humu duniani, kuabudu vile tulivyo navyo na kushikwa na wasiwasi kwa vile tumekosa, au ama vile tunataka kupata ama vile tunavyoweza kupoteza. Katika fikra hizi za kuelewa marupurupu yetu kama vijana wa Kristadelfiani wanaweza kupotea.
• Jambo la kutisha zaidi ni kijana ambaye anatafuta nje ya Ukweli mshirika wa maisha. Ibrahimu alikuwa na uhakika sana kwamba Isaka hapaswi kuchukua mwanamke wa Kikanaani awe mke wake, wala kurudi Ukaldayo kutafuta mke huko (Mwa. 24: 3-6). Isaka na Rebeka walihuzunishwa na chaguo la Esau la wanawake Wahiti na kumwelekeza Yakobo kutafuata mke kati ya jamaa zake (Mwa.26: 34-35; 27:46, 28: 1-2). Vigezo sawa vinatumika leo, na kama Sulemani alivyotambua kwamba, huzuni hatimaye huja kwa njia ya wale ambao wanakiuka amri hii ya Mungu (Kum. 7: 3-4; 2 kor. 6: 4; 7 Zab: 24-27).

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" Tol. 4, Nam. - 10 (H.P. Mansfield)

MASWALI YA AYA:

  1. Kitu gani sheria ya Musa ilisema nini kuhusu farasi, utajiri na wanawake kuhusiana na wafalme? Jinsi gani mambo haya yalisababisha kushindwa kwa Sulemani?
  2. Jinsi gani mabibi wa Sulemani walimfanya kupotoka na kutoka kwa Mungu? Ni masomo gani tunayojifunza kutokana na hili?
  3. Ni adhabu gani Mungu alimwadhibu Sulemani kwa kuondoka kwa njia ya kweli?
  4. Ni nini kilichomfanya Sulemani aondoke kwa njia za Mungu?
     

MASWALI YA INSHA:

  1. Elezea mazingira ambayo yalisababisha kuondoka kwa Sulemani kutoka njia za Mungu.
  2. Mambo gani tunayoweza kujifunza kutokana na ujinga wa Sulemani?
  3. Ni kwa njia gani majaribu tunayokumbana nayo katika siku zetu ni kama yale ambayo Sulemani alishindwa? Tupaswa kufanya nini kushinda majaribu haya?

 

 

SEHEMU YA PILI

UFLAME UNAANGUKA
 

Baada ya ufalme wa Sulemani, Israeli ilianguka kwa hali mbaya zaidi, mbegu ambayo ilikuwa imepandwa na Sulemani mwenyewe. Kwanza taifa liligawanywa na fitna za kiraia na mipaka ikapanuliwa naye Yeroboamu akatengeneza dini yake  kwa upande wa kaskazini  ili kuweka watu wake mbali na Yerusalemu kwa upande wa kusini. Uasi ukaanza kwa upande wa Kaskazini na Kusini na ibada ya Yahweh ikasahaulika. Hata hivyo kwa upande wa Kusini kulikuwa na Wafalme wa mara kwa mara ambao walianzisha mageuzi makuu, lakini pande zote mbili zilikuwa na zimechukua mkondo ambao ungeishia na adhabu ya uhamisho.

Hata hivyo kati ya yote haya, shahidi mwaminifu alihifadhiwa na sauti ya manabii zilikashifu dhambi iliokidhiri na katika kutaja lengo kuu la Bwana. Kuna wale waliosikia ujumbe huu, licha ya uovu wa nyakati hizi, walibaki imara katika imani yao. Walitoa mfano mzuri kwa ajili yetu katika siku hizi ovu za mwisho za watu wa mataifa.

 

 

Swahili Title
307. ONYO LA UMRI MZEE WA SULEMANI.
Sub type
Sub sub type