CSSA 3-3-309 - ELIJAH WARNS THE HOUSE OF AHAB

Swahili

309.    ELIJAH AONYA NYUMBA YA AHAB

"Hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii lakini kulingana na neno langu"

Katika kipindi cha miaka iliofuatia ugawanyikaji wa ufalme., historia ya makabila kumi ya kaskazini ilikuwa ni ile ya kuharibika, umwagikaji wa damu na mateso. Falme zote zilizofuata zilizidi kila moja kwa ukaidi- kwanza  Yeroboamu (1 Fal. 14: 9), kisha Omri (1 Fal.16:25). Na hatimaye Ahabu (1 Fal. 16:30).

Hata hivyo licha ya uasi na kutotii kwao, Mungu alikuwa tayari kuwaonyesha huruma kwa wingi, kama wangemtafuta kwa Ukweli. Ilikuwa ni kazi ya Eliya, katikati ya pingamizi kutoka kwa Yezebeli, kurejesha ibada ya kweli na kuokoa Israeli.

Lengo kuu la somo hili ni kuonyesha kwamba Bwana pekee ndiye Mungu na maneno ya manabii wake ni yenye nguvu.

1 Wafalme 17; 18

TABIA YA AHAB NA YEZEBELI (1 Wafalme 16:30-33)

Mfalme aliyetawala katika kipindi kikubwa cha Huduma ya Eliya alikuwa Ahabu. Alikuwa ameoa Malkia wa Kifinisia, Yezebeli hivyo akawaingiza waisraeli katika ibada ya Baali, ushirikina wa dini wa aina ya kudhalilisha na kukasirisha. (1 Fal.16.31)

Yezebeli alikuwa mwanamke mwenye nia  na tabia kuliko Ahab, na alimchochea kufanya mambo ya kuchukiza (1 Fal.21: 25). Jina lake,kwa kejeli lilimaanisha “Safi” ingawa alikuwa tofauti, na alihusishwa na ibada ya Astarte, pamoja na ibada zake za kidini zilizohusisha mambo tofauti machafu.

KUTOKEA KWA GHAFLA KWA ELIYA (1Wafalme 17:1).

"Kwa ghafla ya umeme na ngurumo ya radi” (kama vile mwamdishi mmoja anasema), Eliya Mtishbi akatokea. Mtu aliyejaa nywele, na aliyevaa mshipi wa ngozi kwenye kiuno chake na joho likininginia mabegani mwake (linganisha 2 Fal. 1:8), mtu huyu shujaa alisimama mbele ya Ahab, na kwa jina la Bwana, akatabiri ukame juu ya Israeli. Ujumbe uliwasilishwa,Eliya akaondoka.

Ukame ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa sababu ya uasi (Kum. 11:16-17; 1 Fal. 8: 35-36), na katika mfano huu, ilikuwa ni kwa kuwa muda mrefu kwa miaka 3 (Lk 4:25; Yas. 5: 17).

Jina Eliya (“Mungu wangu ni Yah") ilikuwa tamko la kusudi kuonyesha nia yake kwamba Bwana, na sio Baali ndiye aliyekuwa Mungu wao (1 Fal.18:21).

ELIYA AKIWA KERUTHI (1 Wafalme 17:2-7)

Eliya alikuwa sasa hatarini kutoka kwa Yezebeli, na Mungu akamwelekeza kuvuka mto Yorodani na kujificha katika kijito cha Keruthi. Jinsi ukame ulivyozidi nchini, Ahab alimtafuta nabii ambaye neno lake lilikuwa limesabasha ukame huu. Wakati huo alitengemea maji kutoka kwa kijito, na mkate na nyama ilioletwa kila asubuhi na jioni na kunguru. Bwana alikuwa amesema “ nimeamuru kunguru wakulishe huko” (Mst.4). kati ya njia za maajabu ambazo Mungu alitoa chakula, ilikuwa ni kwa njia ya kufedhehesha kutegemea kunguru- ndege wachafu kwa Eliya! (Law. 11:15) Kana kwamba kudhihirisha nguvu za utawala za Mungu, ndege hawa wakati wa njaa wangekula chakula chote, lakini waligeuzwa  na kuwa watoaji wa chakula.

Lakini kulikuwa na somo lingine lililofundishwa.

Kama ndege wachafu, kunguru waliwakilisha watu wa mataifa, ambao hawajaoshwa na Neno la Mungu (Law 20:. 22-26). Lakini katika kesi hii “walio wachafu”  walikuwa “wameoshwa” na kutumika kumletea nabii chakula.Mnyama au ndege msafi angetumika, lakini haikuwa nia ya Mungu kufanya hivi. Eliya alikuwa anafunzwa kwamba wale ambao wanaonekana kama “wachafu” na Israeli wanaweza safishwa mioyo “kutakaswa na imani”. Eliya alikuwa karibu kuambiwa aende kwa mwanamke wa mataifa mwenye Imani, akiwa na ujumbe wa maisha. Mungu hana ubaguzi.

ELIYA SAREPTA (1 Wafalme 17:8-24)

"Ondoka,uelekee Sarepta, ambayo iilikuwa Sidoni, na ukae huko: kwani nimemuamuru mwanamke mjane akulishe”. (Mst.9) Tizama jinsi  mjane yule anafananishwa na kunguru (Mst.4)

Amri hii ya Mungu ya kwenda hadi kwa mjane wa watu wa mataifa kutoka sehemu moja na  Yezebeli bila shaka ilikuwa ya kushangaza kwa Eliya. (16:31 linganisha na 17.: 9). Mjane huyo alikuwa katika kundi la watu wa chini, maskini na waliofinyiliwa, ambao Mungu aliona sawa kuwapa sheria maalum ya ulinzi kuhakikisha wanaishi pamoja na watu wake. Mwanamke huyu alionyesha imani ya ajabu kwa Mungu wa Israeli. Alikuwa tayari kujinyima yeye mwenyewe na mwanawe chakula chao cha mwisho, kwa sababu Nabii wa Mungu wa Israeli aliahidi uwepo wa mafuta yasiyoisha. Kama Ibrahimu, baba yake wa kiroho, aliamini na kutenda (Mst.11-15)

Yeye alikuwa mwanamke wa Watu wa mataifa, aliyenusurika ukame ilhali waisreli wengi waliangamia. Alikuwa na imani iliokosekana Israeli, bila imani haiwezekani kumfurahisha Mungu (linganisha Ebra.11: 6, 35 na 1  17:23.).

 

SEHEMU MBILI ZA MAREJELEO KATIKA AGANO JIPYA.

1. Luka 4: 22-32. Wakati Bwana alikuja nyumbani kwake katika mji wa Nazarethi watu hawakuamini na walimpa changamoto arudie miujiza mbele ya macho yao. Kwao alikuwa “Mwana wa Yosefu” na sio Mwana wa Mungu. Ukosefu wao wa imani kuliweka kiwago kwa yale aliyofanya. Hata kama walikuwa wa uzao wa Abrahamu walikosa imani. Kuonyesha kwamba Mungu anawapokea wale wanaoamini, bila kujali kabila, alitumia mfano kwa Eliya: “ Amini, yale ninayokwambia, Hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake. Lakini mimi nakwambia ukweli, wajane wengi walikuwa Israeli, katika siku za Eliya wakati mbigu zilifunga kwa miaka mitatu na miezi sita, wakati ukame ulivamia nchi; lakini Eliya hakutumwa kwa hata mmoja wao, alitumwa Sarepte, mji wa SIDONI, kwa MWANAMKE, MJANE.

2. Matendo 10. Katika sura hii, mtu wa kwanza wa Mataifa anabadilishwa na kushika Injili ya kristo na mtume Paulo. Mtume Paulo alikuwa ametayarishwa kwa kazi hii kwa njia sawa na Eliya. Wote hawa walikuwa Waisraeli na walikuwa na ubaguzi dhidi ya watu wa mataifa; lakini kama Eliya, Petro alifunzwa  kwamba wanyama wachafu wanaweza kutakaswa na Mungu na katika ndoto yake aliamriwa “kuamka na kuua na kula”. Baada ya tukio hili alitumwa hadi kwa ofisa wa Kirumi Korneliasi, pale petro alijifunza funzo kwamba “Mungu hana ubaguzi: katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki anakubalika kwake" (Mdo.10: 34-35).

 

MKUTANO NA OBADIA (1 Wafalme 18:1-20)

 Wakati ulikaribia na Mungu alitaka kumaliza Ukame na akamwambia Eliya kujitokeza kwa Ahab. Ukame huu ulikuwa mkali hadi ikafikia mahali Ahab na Wakili wake mkuu waliongoza shughuli ya kutafuta chakula wao wenyewe wakitumia farasi na punda waliosalia. Ni huyu Obadia ambaye “Alimwogopa Mungu” na aliwatunza kwa siri mamia ya manabii wake wakati walikuwa wanauawa na upanga wa Yezebeli. Eliya alikutana naye njiani na akamtambua mara moja. “ Je wewe ndiye bwana wangu Eliya?” akauliza (Mst. 7) Eliya akajibu kwa haraka, “ ni mimi: nenda umwambie bwana wako kwamba Eliya ako hapa.”

Wakati Ahab alimwona Eliya, alimlaumu kwa “Kusumbua taifa la Israeli” lakini nabii huyu shujaa alipinga madai haya na kumlaumu Ahab. Chanzo cha matatizo ya Israeli yalikuwa yametokana na kumkataa Bwana na kumwabudu Baali. Eliya alichukua fursa hii na kumwambia Ahab kuwakusanya Waisraeli pamoja na manabii mia nne na hamsini wa Baali kule Mlima karmeli.

 

MASHINDANO KATIKA MLIMA KARMELI: HAKUNA MAONI MAWILI TENA(1 Wafalme 18:21-40).

Israeli yote na manabii wa uwongo wakafika mbele yake, na  nabii yule jasiri akatoa changamoto, “mpaka lini mtatatizika dhidi ya maoni mawili? Kama Yahweh ni Mungu, mumfuate: lakini kama ni Baali basi mumfuate” watu walikuwa kimya. Eliya akaseme yeye ndiye mwakilishi wa pekee wa Mungu: na alikuwa amekasirishwa na manabii 450 wa Baali. Aliweka jaribio rahisi ambapo suala hili lingetatuliwa. Watu wakakubali.

Manabii wa Baali wakamwita mungu wao kuja na kuteketeza ndume aliyekuwa juu ya madhabahu waliokuwa wametengeneza. Na ingawa walimwita kuanza asubuhi hadi mchana, hawakupata jibu (Zab. 115:. 3-9). Jambo hili lilikuwa la kuaibisha hadi Eliya akaanza kuwakejeli. Pengine Baali alikuwa anafanya mambo yake ya kibinafsi kama kuongea,kutafuta ama hata kulala- mambo yasiyo ya kimungu kabisa. Maombi yao ya bure “O Baali utusikie", yaliendelea mpaka wakati wa sadaka ya jioni, lakini bado hakuna kitu kilichotokea. Basi zamu ya Eliya ikafika. Akawaita watu wote karibu kisha akafanya mambo ya muhimu: -

 

1.  Alirekebisha madhabahu ya Bwana  yaliyokuwa yamezeeka na kuvunjika, kitendo hiki ni mfano wa jambo  alilokuwa akijaribu kufanya katika Israeli, yaani, kurejesha hofu ya Bwana (Mst. 30, 37, Linganisha. 19:10).
2.  Mawe kumi na mawili yalichukuliwa kwa ajili ya madhabahu kuwakilisha  makabila kumi na mawili ambao yangekuwa roho moja na kweli wakati Masihi atarudi kuwatawala (Mst.31, Linganisha. Eze.. 37:22).
3.  Aliashiria asili ya taifa na mabadiliko ya jina la Yakobo kuwa "Israeli" ambayo ni kusudi la Mungu la kukumbukwa.
Israel ina maana "mkuu aliye na Mungu". Israeil ingeshamiri kwa msaada wa Mungu, lakini bila msaada huu haya hayatatokea (Mst 31, 21; Mwa. 32:. 28-31; Mik. 4:. 7).
4.  Alihitaji matakwa magumu kufanywa. Mtaro mkubwa  kuchimbwa kuzunguka madhabahu na maji kumwagwa juu ya sadaka na
kuni mpaka mtaro ukajaa (Mst.33-35).
5. Wakati wa sadaka ya jioni, wakati wa ibada, Alimwita Mungu wa Israeli kwa jina lake agano (Mst.36 linganisha Ezr.9:. 4-5).
 

Eliya aliomba kwa dhati kwamba Bwana atajidhibitishe mwenyewe, na Eliya kama nabii wake “Nisikize, ewe Bwana, ili watu hawa wajue kwamba wewe ndiye Bwana Mungu, ili wageuze mioyo yao kwako tena”.

Ghafla, moto kutoka mbinguni ukashuka kwenye sadaka, ukigeuza hali ya asili kwani uliteketeza ukielekea chini na kuteketeza sadaka, kuni, mawe, vumbi na maji yaliokuwa kwenye mtaro. Kwa woga na mshangao watu walianguka kwa nyuso zao kwa kuona udhihirisho wa Nguvu za Mungu.

“Bwana, yeye ndiye Mungu! Yahwe, Yeye ni Mungu”, wakapiga kelele. Hivyo wakatambua maana ya jina la nabii, “Mungu wangu ni Yah”. Hivyo hawakutatizika na maoni mawili kwani suala hili lilikuwa limetatuliwa.Eliya hakupoteza mda na katika wakati ule manabii wale wa uwongo waliangamizwa katika kijito cha kishoni.

Kuna Mungu Mmoja na Imani Moja. Hatuwezi kutumikia mabwana wawili (Mt. 6:24.). Kama tutamtumikia Mungu, basi lazima tufanye hivyo na moyo wetu wote, si kujaribu kuingiza maoni ya dunia.

UKAME UNAISHA (1 Wafalme 18:41-46)

 Baada watu kutambua kwamba Mungu pekee ndiye alikuwa Mungu wa kweli, Eliya alitangaza mwisho wa ukame. Akamwambia amke ale and anywe “kwani kuna sauti ya wingi wa mvua”. Eliya mwenyewe alienda katika kilele cha mlima Karmeli na kuomba kwa dhati (Yak. 5:18). Mtumishi wake aliambiwa aangalie baharini kwa dalili yoyote ya mvua. Mara sita Eliya aliomba na mara sita mtumishi hakuwa na cha kuripoti. Lakini mara ya saba mtumishi alikuwa na jambo la kuripoti kwani alikuwa ameona wingu dogo, ambalo lilizidi kuongezeka mpaka “mbigu yote ikajaa mawingu meusi na upepo, na kukakuwa na mvua kubwa”.

Ahabu akaendesha magari ya farasi akielekea Yezreeli, akijua kwamba kama hangefika kabla mvua ifike basi angezama katika bonde la Esdraloni. Wakati huo huo, mkono wa Bwana ulikuwa juu ya  Eliya na aliweza  kupita gari la  farasi. Eliya akafika mbele ya mflame wa Israeli Yezreeli akiwa kama mtangulizi, kitendo lilichoonyesha kazi yake ya usoni katika “siku za Yezreeli" (Hos.1:. 10-11; 2: 21-22).

Kazi zake haikuwa imekamilika na mageuzi yake yalikuwa ya muda mfupi. Atachukua kazi yake tena baada ya ufufuo na atatayarisha nyoyo za waisraeli kwa mfalme wao, Bwana Yesu Kristo (Mal. 4:. 5-6). Basi siku ya Yezreeli itakuwa kubwa kweli, kwa wana wa Yuda na Israeli “watakusanyika, na watajichagulia kichwa kimoja” (Hos. 1:11).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA

  • Hebu tukumbuke jinsi neno la Bwana lina nguvu vinywani vya manabii – kufunga ama kufungua mbingu; kuleta mvua au moto. 
  • Watu wa mataifa mengine na sio Waisraeli wa ukoo wa Ibrahimu, sisi, kama mwanamke wa Sarepta, tunaokolewa kwa imani na utii.
  • Hatupaswi  "kusita" katika kuchagua kati ya hoja hizi mbili. Kwani hatuwezi kutumikia mabwana wawili, kumpenda Mungu na dunia. Mungu anatuhitaji kumtumikia kwa roho, akili na fikra zetu zote. Na hii ndio amri kuu.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 5, Nam. 1

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—Sura: 25-27

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura: 19

"Elijah the Tishbite" (J. Martin)—Sura: 1-6


MASWALI YA AYA:

  1. Ndege mchafu, kunguru, alimlisha Eliya katika kijito cha Keruthi. Somo gani Eliya anajifunza kutokana na hili?
  2. Ni kwa misingi gani mwanamke wa Sarepta aliokolewa?
  3. Jina la Eliya maana yake ni "Mungu wangu ni Yah". Ni kwa njia gani hii inaonyesha madhumuni ya utume wake?
  4. Ni masomo gani tunayojifunza kutoka mashindano ya kati ya Eliya na manabii wa Baali juu ya Mlima Karmeli?

MASWALI YA INSHA:

  1. Elezea ziara ya Elia hadi kerurithi na Sarepta. Ni masomo gani tunayojifunza kutokana na matukio hayo?
  2. Elezea mashindano kati ya Eliya na manabii wa Baali juu ya mlima wa Karmeli.
  3. Andika kuhusu tabia za Ahabu na Yezebeli.
  4. Ni kwa njia gani ni matukio mawili yanafanana?
    (a) Ziara Elia Keruthi na Sarepta.
    (b) Maono ya Petro kuhusu wanyama wachafu kubadilika kwa Cornelius.

 

  1.  Eliya anakuja kutoka Gileadi na kurabiri mbele ya Ahabu kwamba hakutakuwa na mvua (1 Wafalme 17: 1).
  2. Anatorokea kijito cha Keruthi ambapo analishwa na kunguru (17: 5-6).
  3. Wakati kijito kinakauka, Elia anatumwa kwa mjane wa Sarepta (17: 9-10).
  4. Eliya anashindana na manabii 450 wa Baali kwenye Mlima Karmeli. Manabii wa Baali wanauliwa katika mto wa Kishoni (18:19, 38-40).
  5. Elijah anafika mbele ya gari la farasi la Ahabu kutoka karmeli hadi kwa Yezreeli (18: 45-46).
  6. Kwa tishio la kisasi cha Yezebeli, Eliya anakimbilia Horebu (19: 1-3, 8).
  7. Anamwita Elisha mwana wa Abel-Mehola kuchukua jukumu lake (19:16, 19).
  8. Anakabiliana na Ahabu katika shamba la Nabothi, ambaye anapigwa mawe kwa uamuzi wa Yezebeli (21: 17-19).

 

 

Swahili Title
309. ELIJAH AONYA NYUMBA YA AHAB
Sub type
Sub sub type