CSSA 3-3-310 - ELIJAH AND ELISHA

Swahili

310.    ELIYA NA ELISHA

“Tazama wema na ukali wa Mungu"

Jukumu la Eliya ilikuwa ile ya kuhukumu na kulaani, unayodhihirisha ukali wa Bwana. Elisha alionyesha kipengele cha huruma kwa tabia ya Mungu (Rum. 11:22). Tabia ya Israeli ilihitaji hukumu ya Mungu na Eliya alikuwa chombo cha kuadhimisha hili kwa mfalme huyu mwovu na taifa hili potofu. Lakini ilibidi afunzwe kwamba ndani ya taifa kulikuwa na waliobaki walihitaji kuelimishwa na kutiwa nguvu. Ilikuwa ni suala la kuimarisha na kujenga msingi ambao ulileta jukumu la huruma la Elisha.

Mambo hayo mawili yalionyesha tabia ya usawa ya Bwana, ambayo ni kazi ya maisha yetu kuweka wazi.

Lengo la somo hili ni kuonyesha jinsi Mungu anavyorekebisha walio waovu kwa adhabu, lakini walio na haki wanajengwa na “sauti ndogo” ya maelezo ya Manabii wake.

1 Wafalme 19; 2 Wafalme 2
 

ELIYA NA YOHANA MBATIZAJI

Miaka mitatu na nusu ya ukame ilishindwa kumfanya Ahabu atubu, au kumgeuza mke wake Yezebeli mgeni kutoka ibada za sanamu, Eliya alimjia kwa mara ya pili kupendekeza mashindano ya Mlima Karmeli. Hii ilikamilika kwa mauaji ya manabii wa Baali. Baadaye nabii alikimbia na kufika kabla ya gari la Ahabu kilomita 25 katika bonde la Yezreeli mbele ya uso wa dhoruba kali. Kwa kufanya hivyo alifanya kazi ya mhubiri au mtangulizi wa Mfalme.

Kazi ya Yohana Mbatizaji alikuwa sawa na haya.  Alikuwa  "atengeneze njia" kabla kuja kwa mfalme, Bwana Yesu Kristo (Mai 3:1). Wakati wa kuzaliwa kwake ilibainika kuwa angeweza "kwenda mbele" ya Kristo "katika roho na nguvu ya Elia (Eliya), na kugeuza mioyo ya baba watoto na wakaidi kwa hekima ya haki" (Lk. 1:17). Hadi sasa kizazi cha Waisraeli waliokuwa hai wakati wa Kristo walifikiri kwamba, Yohana Mbatizaji ndiye "alikuwa" Eliya: "Kama mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya, atakekuja" (Mt. 11:14.). Katika ujio wa Kristo wa pili Eliya "atakuja kwanzaa" na kuandaa mioyo ya watu wake ili kumpokea Masihi (Mai 4:. 5-6; Mt. 17:11).

ELIYA AKIWA HOREBU — SAUTI NDOGO (1 Wafalme 19:1-18)

Madhara ya mageuzi ya Eliya katika Mlima Karmeli yalikuwa ya mda-mfupi. Wakati Yezebeli alisikia kuhusu matendo na hasa jinsi alivyowaangamiza manabii wa dini aliyoipenda, uabudu wa Baali, alimtuma mjume haraka kwa Eliya. Aliambiwa kwamba atauwawa vile alivyowaua manabii wa Baali na kama angeshindwa kufanya hivi basi aliomba kwamba miungu imfanyie vile angeshindwa kumfanyia Eliya. Ushujaa wa Eliya ukaisha baada la tishio hili na akatoroka akihofia maisha yake hadi Mlima Horeb (1 Fal. 19.: 1-3).

Alijificha katika pango ( linganisha, Kut.33:22) katika mlima na pale alipata changamoto na neno la Bwana “Unafanya nini hapa, Eliya?” katika kukata tamaa kwake “alifanya maombolezi dhidi ya Israeli”, akisema “Nimeona wivu sana kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi kwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, kutupa madhabahu na kuwaua manabii wako kwa upanga; na mimi niliyebaki pekee bado  wanataka kuchukua maisha yangu.”( Mst.10; Rum. 11:. 3). Aliamriwa kuondoka katika pango hilo na kusimama mbele ya Yahweh.  Pale alishuhudia matukio matatu makuu ya nguvu za Mungu, upepo mkali, tetemeko la ardhi na mwishowe moto (Mst. 11-12). Aliambiwa kwamba Bwana “Hakuwepo” katika matukio hayo. Kisha kulikuwa na tukio la nne la ufunuo wa tabia tofauti kabisa, “Sauti ndogo” (Roth, " sauti ndogo ya utulivu"). Ni wazi kwamba hii ilikuwa sauti ya Bwana (Mst. 12-13).
 

Katika matukio haya ya ajabu kulikuwa na ujumbe kwa nabii ambao haku-uelewa kwa haraka. Jukumu lake lilikuwa ni lile la ukali na hukumu ambayo alikuwa ameleta ukame kwa Israeli na kuitisha moto na kifo-alikuwa kama upepo, tetemeko la ardhi na moto. Hakutambua kwamba kulikuwa na wale waliokuwa bado waaminifu kwa Israeli na wale ambao hawakuwahi piga goti mbele ya Baali (Mst.18) Wakati aliona kwamba yeye “pekee” ndiye aliyebaki, hii haikuwa sahihi kwani kulikuwa na waaminifu zaidi ya 7,000.

Alikumbushwa hili na kuambiwa kwamba alipaswa kuwa Israeli pamoja na Waumini: “unafanya nini hapa Eliya?” (Mst.13). Walihitaji kusikia sauti ndogo ya huruma na maagizo ili imani yao iweze kujengeka tena. Dhihirisho la nguvu linaweza kuharibu, lakini huruma na maagizo yanajenga na kuinua imani. Hakuna mahali pa hukumu kwa Mungu na Bwana “kilio, na kishindo” wakati  atakuja kwa mara ya pili; lakini mara ya kwanza sauti yake “haikuwa imeinuliwa” kwa kuhukumu lakini aliongea maneno ya maagizo na kutuliza ambayo yalijenga imani na ujasiri wa watu. (linganisha Isa. 42:13-14 na Mst.1 na 2).

Elijah iliamriwa kurudi na alipewa majukumu matatu:
1. Amwagilie mafuta ya upako Hazaeli awe mfalme juu ya Shamu.
2. Amwagilie mafuta ya upako Yehu mwana wa Nimshi, mfalme juu ya Israeli.
3. Amwagilie mafuta ya upako Elisha mwana wa Shafati, awe mrithi wake mwenyewe (Mst. 15-18.)


ELISHA ANAMRIDHI ELIYA (1 Wafalme 19:19-21)

Kati ya amri hizi tatu, mbili za kwanza zilikuwa zifanywe na Elisha, na moja ya mwisho ilifanywa na Eliya mwenyewe wakati alimkuta Elisha akilima. Kwa kutupa vazi lake juu yake, Eliya alionyesha kuwa alitamani Elisha awe mrithi wake. Hivyo, Elisha aliacha njia yake za maisha ya zamani na kumfuata Eliya (Mst.20-21), na kukanza ushirikiano ambao uliendelea kwa miaka kadhaa mpaka Eliya alipochukuliwa na kimbunga hadi mbinguni.

Katika miaka ya mwisho ya huduma yake, na kwa msaada wa Elisha, Eliya aliweza kurejesha shule ya manabii ambayo mauaji Yezebeli alikuwa amejaribu kuharibu (linganisha 1 Fal. 18: 3-4, 13.). Kwa hiyo, kulikuwa na uhakika kwamba kutakuwa na mahali pa heshima kwa Neno la Mungu katika Israeli. Kabla ya Elisha kuchukuliwa katika upepo wa kisulisuli, alikuwa ameanzisha shule imara kule Betheli (2 Fal. 2: 3), Yeriko (Mst.5), na Gilgali (4:38). "Sauti ndogo" ya Neno la Mungu ilikuwa inaujenga mwili wa binadamu na kuwa kama chanzo cha nguvu ndani ya taifa, na ilikuwa kazi hii ambayo Elisha aliendeleza.

KRISTO MKUU KULIKO ELISHA (1 Wafalme 19:19-21; Luka 9)

Jibu la Elisha la kuitikia wito wa Eliya ni la kuvutia. "Naye akawaacha ng'ombe wake, akamfuata Eliya mbio, akasema, nakuomba, niruhusu nikawabusu baba na mama yangu na kisha mimi nitakufuata". Eliya hakukataa ombi hili, na kwa kweli, bali aliliunga mkono, "Nenda basi: Kwa nini nimekufanyia nini mimi" Hivyo basi akaenda nyumbani na kumuua ng'ombe na kuchemsha nyama zake,kisha  akawapa watu. Alikuwa ameyaacha mambo ya dunia hii: wito wa Eliya kwake ulikuwa wito kutoka kwa Mungu. Kisha akaondoka, akaenda kwa nabii Eliya na kumhudumia.

Miaka mingi baadaye mwanaume mmoja alikuja kwa Mwana wa Mungu, na kumtambua kama Bwana, na kusema, "mimi nitakufuata; lakini niruhusu kwanza nikawaage wale, ambao wako nyumbani kwangu." Ombi hili lilifanana na lile Elisha alifanya. Hakika lilikuwa ombi la busara kwamba lazima angetoa taarifa kwa jamaa wake wa karibu kuhusu wito wake mpya! Lakini  kwa hali tofauti kabisa na Eliya Bwana Yesu Kristo alikataa ruhusa; " mtu, aliyeweka mkono wake kulima na kuangalia  nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu" (Lk. 9: 61-62). Kwa nini Bwana alikataa kile Eliya alikuwa ameruhusa? Jibu liko katika ukweli kwamba aliye mkuu kuliko Eliya alikuweko. Somo hili limesisitwa,lakini bado haijaeleweka kwa kiukamilfu, katika matukio yaliyotangulia. Walishindwa kutambua jinsi alivyo mkuu. Je sisi? Tushawahi toa majibu sawa?

Wakati wa kubadilika Petro alimfananisha Mungu na Musa na Eliya, wakati alipendekeza watengeneza vibanda kwa kila mmoja wao. Kisha sauti kutoka mbinguni ikamwelezea ubora wa Kristo, "HUYU NI MWANANGU MPENDWA, MSIKILIZENI" (Lk. 9:. 33-35).

Baadaye wakati Bwana alikuwa anafunga safari yake kwenda Yerusalemu, alikatazwa njia na Wasamaria (Lk 9:. 51-53). Mahali hapa palikuwa karibu na sehemu moja ambayo Eliya alikuwa amefanya miujiza. Katika matukio mawili Eliya alikuwa ameitisha moto kutoka mbinguni kuwaangamiza watu hamsini, na wakuu yao, waliokuwa wametumwa kutoka kwa mfalme mwovu Ahazia kumtia nguvuni (2 Fal. 1). Aliwambia wakuu wale, "Kama mimi ni mtu wa Mungu, na moto ushuke kutoka mbinguni uwateketeze nyinyi na watu wenu hamsini". Mkuu wa tatu aliepuka tu wakati alimsihi nabii kwa ombi, "O mtu wa Mungu, nakusihi, basi maisha yangu, na maisha ya watumishi wako hawa hamsini ziwe na thamani machoni wako ..." Hivyo maisha ya nahodha na watu wake hamsini wakaepuka kifo kutoka kwa malaika.


Wakati Wasamaria walimkataza Bwana Yesu Kristo njia kwenda Samaria, Yakobo na Yohana ("wana wa ngurumo") waliomba ruhusa kuita moto kuonyesha ushahidi wa ujumbe wake Mungu, " kama Elia alivyofanya." Hapa walishindwa kutambua ukuu wa Bwana wao na asili ya kazi yake. Hawakujua kusudi la Mungu la kumtuma Mwana wake mpendwa katika ulimwengu (Yn. 3:16). Aliwageukia na kuwakemea, akisema, "Hamjui ni roho ya aina gani mlio nayo, kwa Maana Mwana wa Mtu hakuja kuyaangamiza maisha ya watu, bali kuyaokoa. (Lk. 9: 54-56) " Sauti ndogo" inaleta uongozi kwa toba na maisha, wakati moto na tetemeko la ardhi zilikuwa vyombo vya kisasi na mauti (linganisha Isa. 42: 1-3.).

MTU ELISHA (2 Wafalme 2)

Kabla ya Eliya kuchukuliwa, Elisha alitaka "fungu mara mbili" ya roho yake. " fungu mara mbili " ilikuwa ni haki ya mzaliwa wa kwanza (Kum. 21:17), Hivyo Elisha alikuwa akitafuta haki ya kumridhi Eliya. Hii alipata kutokana na uamuzi wake wa kubaki na Eliya mpaka mwisho. Hadithi katika 2. Wafalme 2: 1-15 imeandikwa katika kumbukumbu ili tuweze kuchukua mfano wa ahadi ya Elisha usio na mwisho kwa bwana wake katika maisha yetu wenyewe.

Elisha ilikuwa tofauti na Eliya, makazi yake yalikuwa nyikani, na alichukia maisha ya ustaarabu ya jamii. Alitoka jamii ya wakulima kwani (familia yake walikuwa na jozi  12 za ng'ombe katika Abel-Mehola ) na, ingawa alikuwa kijana mdogo, alipata upara (2 Fal. 2:23) tofauti kabisa na Eliya (1: 8).

Kuna tofauti kati ya miujiza yao (rejelea jedwali katika mwisho wa somo).

Miujiza ya Eliya ilikuwa ya hukumu - ukame na moto kutoka mbinguni - yote katika  "upepo, tetemeko la ardhi na moto", alama ya uamuzi wa Mungu kung'oa wasio haki na kutimiza Neno lake. Mtu lazima ajitenge, Na atumie nguvu za "sauti ndogo". Eliya aliambiwa kwamba arudi Israeli, akawatafute wale waaminifu waliobaki, na kuwajenga na Neno la Mungu.

Muijiza ya Elisha ilikuwa ya huruma-uponyaji, uwepo wa Mungu, kutiwa moyo katika maisha ya amani, onyo dhidi ya dhambi, uhakika wa hukumu na juu ya yote nia ya Mungu ya kuwaokoa wale wanamwamini- yote katika kudumisha “Sauti ile dogo”.

Upanuzi wa huruma hii ulitegemea kuelewa kwa haki ya Mungu na hukumu, kama ilivyoonekana katika muujiza wa kwanza aliofanya. Haikuwa kupiga maji kwa vazi la Eliya ambalo liligawanyisha maji, lakini kutambua wito wake na nguvu za Mungu (2 Fal. 2:14).

Matukio mawili katika huduma ya Elisha yanaonyesha usawa kwamba Neno linahitaji wale ambao watamtafuta Mungu.

1. Watu wa Yeriko walitoa wito kwa nabii, kuhusu kijito chenye maji machungu nje ya mji (2 Fal. 2: 19-22). Maji yakaponywa. sio chumvi ilifanya muujiza, ila ni nguvu za Mungu zilifanya kazi kupitia Elisha. Israel walijtambua umuhimu wa chumvi (Hes. 18:19.) - Ni kihifadhi na hivyo ni ishara ya msingi wa kudumu wa agano la Bwana na Israeli. Hivyo sadaka ilitakiwa kutengenezwa na chumvi (Law. 2:13).

2. Baadaye, wakati nabii alikaribia mji wa Betheli, alidhihakiwa na baadhi ya vijana wa mji (katika 2 Wafalme 02:23 anasema wao walikuwa "watoto wadogo" lakini kulinganisha matumizi ya neno la Kiebrania 'Naar' katika Mwa. 21:12; 22: 5; 41:12, na kwa ajili ya askari wa Ahabu katika 1 Fal. 20:14).. Elisha aliwalaani na vijana arobaini na miwili waliangamizwa na  dubu wawili wenye hasira. Neno la Mungu si la kudhihakiwa. wakati Yeye ataonyesha huruma yake kwa wale wote ambao watageuza nyoyo zao kwake, Mungu pia ataleta hukumu kwa wale ambao huasi na kutofuata maagizo yake.

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Mungu alimtumia Eliya kuleta hukumu juu ya Ahabu na Israeli kwa sababu ya uovu wao. Hukumu iliharibu waovu, na kuonya wenye haki. " Sauti ndogo" ya kufunza Neno la Mungu, hata hivyo, hujenga binadamu ili waweze kushindana na uovu na kutembea kwa uaminifu mbele ya Mungu.
  • Ujumbe wa mafundisho na wokovu ni mkuu kuliko ule wa uharibifu, na hata kama Kristo alikuwa mkuu kuliko Eliya. Ni lazima tufundishe Neno kwa marafiki zetu ili wapate kuokolewa. Wema wa Mungu huongoza watu katika wokovu (Rum. 2: 4).
  • Vijana ambao hudhihaki manabii wa Mungu wataangamizwa, ingawa manabii hao hutangaza huruma ya Mungu. Huruma ya Mungu si tofauti na utakatifu wake.

     

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—Sura. 27-30

"Elijah the Tishbite" (J. Martin)—Sura. 7-8, 10

 

MASWALI YA AYA:

  1. Jinsi gani kazi ya Elia ilikuwa sawa na ile ya Yohana Mbatizaji?
  2. Nini Eliya alipaswa kuelewa na "sauti ndogo"?
  3. Kwa njia gani miujiza ya Eliya ilitofautiana na ile za Elisha?
  4. Orodhesha tofauti kati ya kazi ya Eliya na kazi ya Elisha?

MASWALI YA INSHA:

  1. Elezea kile kilichotokea kwa Eliya wakati alikimbilia Horebu? Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutokana na tukio hili?
  2. Nini ilikuwa kazi kuu ya Eliya baada ya kuungana na Elisha?
  3. Jinsi gani Eliya alimwita Elisha? Na majibu ya Elisha yalikuwa yapi?

 

MIUJIZA MINANE YA ELIYA

Nam.

Muujiza

Rejeleo

Umuhimu wa kiroho

1.

Kufungwa kwa mbigu

1 Wafalme 17:1

Ukame wa kiroho (Amo. 8:11).

2.

Kuzidishwa kwa mafuta

1 Wafalme 17:14

Chakula kwa wacha mungu wakati wa ukame.

3.

Mwana wa mjane anafufuliwa

1 Wafalme 17:22,23

Ufufuo.

4.

Moto kutoka mbiguni

1 Wafalme 18:38

Ushahidi wakati wa hukumu.

5.

Mvua

1 Wafalme 18:45

Kujaa kwa roho (Yoe. 2:23).

6.

Kuangamizwa kwa hamsini

2 Wafalme 1:10

Kukataliwa wakati wa hukumu.

7.

Kuangamizwa kwa hamsini

2 Wafalme 1:12

Kukataliwa wakati wa hukumu.

8.

Kugawanyika kwa maji

2 Wafalme 2:8

Ishara ya utawala juu ya maji (linganisha Ufu. 17:15).

 

 

 

 

 

MIUJIZA KUMI NA SITA YA ELISHA

Nam.

Muujiza

Rejeleo

Maana ya koroho

1.

Kugawanyika kwa maji

2 Wafalme 2:14

Vazi la Eliya linawekwa juu ya Elisha.

2.

Maji yanaponywa

2 Wafalme 2:21

Kuponywa kupitia "chumvi ya agano" (Law. 2:13; Nah. 18:19).

3.

Dubu wanawaangamiza wadhihaki

2 Wafalme 2:24

Adhabu kwa wadhihaki wote na wanao-asi neno la Mungu.

4.

Maji katika nchi kavu

2 Wafalme 3:20

Utunzaji wa Mungu katika nchi kavu.

5.

Mafuta kwa mjane

2 Wafalme 4:1

Neno la Mungu la daima kuwaendeleza wale wanao-mwamini.

6.

Zawadi ya mwana wa kiume

2 Wafalme 4:16

Huduma ya upendo inaleta mbegu ya Kimungu

7.

Kufufua kijana aliyekufa

2 Wafalme 4:35

Kufufuka kwa Mbegu iliotolewa na Mungu.

8.

Kuponya kwa chakula

2 Wafalme  4:41

Kuongeza matokea katika chakula cha Mungu katika "kifo katika chungu", lakini kutosheka na "mkate wetu wa kila siku" unatupa afya.

9.

Mkate unazidishwa

2 Wafalme 4:43

Hata katika ukame, Mungu atahifadhi "mkate wa uzima" kwa wale wote wanakuja kwake.

10.

Naamani anaponywa

2 Wafalme  5:10

Kuamini na mazishi katika maji yanaosha dhambi na kuosha dhambi na kuleta upya wa maisha.

11.

Gehazi anaangamizwa

2 Wafalme 5:27

Tamaa ya utajiri wa dunia ni kuitisha hukumu ya Mungu.

12.

Chuma inafanywa kuelea

2 Wafalme 6:6

Wale waliopotea (chuma) wanaweza kupatikana katika kitendo cha msalaba (chuma kikakatwa na kutupwa kwenye maji).

13.

Kuona kwa vipofu

2 Wafalme 6:17

Imani inawezesha watu wa Mungu kuona ulinzi na uongozi wake.

14.

Washami wanapigwa kwa upofu

2 Wafalme 6:18

Ulinzi unaolinda watu wa Mungu kutoka kwa wale wanaotaka kuwaangamiza.

15.

Kuponywa upofu

2 Wafalme 6:20

Ni pale tu tunaongozwa na Mungu vita vitaisha natutapata Amani ya kweli.

16.

Maisha kupitia kifo

2 Wafalme 13:21

Yesu Kristo "kupitia kifo, aliharibu kile kilichokuwa na nguvu ya kifo" (Ebr. 2:14) na akaungana na hali ya ufufuko.

 

 

Swahili Title
310. ELIYA NA ELISHA
Sub type
Sub sub type