CSSA 3-3-311 - NAAMAN, THE SYRIAN

Swahili

311.    NAAMAN, MSHAMI

"Hakuna Mungu duniani kote, ila Israeli"

"Kila andiko, limetolewa na uongozi wa Mungu na lina maana..." (2 Tim. 3:16). Hadithi ya uponyaji wa ukoma wa Naamani ni zaidi ya hadithi ya kuvutia. Inaashiria uhubiri wa injili kwa watu wa mataifa.Inaonyesha pia jinsi  ukosefu wa imani wa  Israeli (mfano wa Yehoramu na Gehazi) ilifungua mlango wa wokovu kwa mataifa mengine, kisha, umakini wetu unamwendea Naamani, tunaonyeshwa katika majibu ya Elisha ya awali, kuanguka, na hoja mbaya na kiburi ambacho mara nyingi kinasitisha nguvu za Neno Mungu kufanya kazi katika maisha ya binadamu.

Wakati hasira za Naamani zilipungua aliweza kwa hiari kukubali maagizo rahisi ya Mungu. Utii lazima utoke katika roho yenye unyenyekevu.

Lengo la somo hili ni kuonyesha kuwa kuna wokovu kwa Mungu wa Israeli pekee, na tunapaswa kutii kwa unyenyekevu kama tunahitaji mapenzi yake yatimizwe.

2 Wafalme 5

NAAMANI MWENYE UKOMA ANAENDA SAMARIA (2 Wafalme 5:1-5)

Hadithi ya Naamani mwenye ukoma ni moja ya kuvutia kwa wasomi wengi. Tukio hili hata hivyo, kama matukio mengine katika maandiko, ni kumbukumbu ili tupate kujifunza somo la kutusaidia katika ufahamu wetu wa Neno la Mungu na kusudi lake. Tumeona hapo awali jinsi injili ya nabii Elisha ilikuwa inafanana na ile ya Bwana Yesu Kristo, na hii ni tena inaonyeshwa katika hadithi ya uponyaji wa Naamani mwenye ukoma .

Ukoma katika Israeli ulikuwa ni ishara ya kifo na mtu yeyote wa Kiebrania ambaye aliambukizwa ugonjwa huu aliwekwa nje ya kambi na hivyo kuwekwa mbali na watu wake na ibada ya Mungu. kifo na hali ya mauti iliingia ulimwenguni kama mshahara wa dhambi (Mwa. 3: 17-19; 5:12 Rum; 6:23), Ili mtu azeeke na afe. Ili kuonyesha  WaIsraeli matokeo makubwa ya dhambi, Mungu alitoa umuhimu kwa kuleta ugonjwa sugu, wa ukoma. Ukoma ulikuwa kama kifo, hali ya kuoza inayo onekana wazi. Ilikuwa ni kifo kinachoishi. Mwili ulioharibika uliweza kuonekana juu ya mwathirika hata wakati bado yu hai. Miriamu alipigwa kwa sababu alitenda dhambi na Haruni akasema kumhusu, "Wacha asiwe kama liyekufa, ambaye nusu ya nyama ya mwili wake imeoza atokapo kwenye tumbo la mama yake" (Hes. 12:12). Kama vile ugonjwa ulikuwa na umuhimu wa kiroho, ndivyo ilivyokuwa tiba, kwani ilihusisha kumwaga damu (Law 14; Ebr. 9:22). Kwa watu wa mataifa mengine hata hivyo, haikuwa na maana yoyote ya kiroho. Ilikuwa ni kuepukwa kwa sababu ya madhara yake, lakini si jambo la aibu.

Naamani alikuwa nahodha wa jeshi la Shamu. Alikuwa  mtu mwenye kiburi, mwanajeshi shupavu na mwaminifu kwa Mfalme wake. Ilikuwa ni wazi kwamba  alikuwa ni mtu aliyeheshimiwa na mfalme na wote waliokutana naye. (neno "baba yangu" linatumiwa na watumishi wake, Mst.13).

Washami walijukana kwa ukaidi wao, hasa kwa maadui na mateka wao, hii ilikuwa wazi kutoka kwa kumbukumbu, mtu huyu alikuwa na hisia nzuri, kama ilivyoonyeshwa katika jibu kwa msichana wa kiebrania wakati alipendekeza Elisha kama angeweza kutibu ugonjwa wa bwana wake.

Benhadi alichukua pendekezo hili kwa haraka na kutayarisha zawadi ya dhamani ya kumtumia Mfalme wa Israeli kama tu kiongozi wa jeshi lake. Akiwa na barua ya utambulisho na rufaa kutoka kwa Mflame wa Washami, Naamani alijitokeza kwa Yehoramu.

AIBU YA YEHORAMU (2 Wafalme 5:6-7)

Wakati Mfalme wa Israeli alisoma barua kutoka kwa Benhadi, Mfalme wa Washami, alikuwa karibu na yeye. Akirarua nguo zake alisema “je mimi ni Mungu, niue ama nipatiane uhai, eti mtu huyu anitumia mtu mwenye ukoma nimponye, nakusihi, na utizame kwamba anataka kugombana nami” (2 Fal. 5: 7). Kwake barua ilimaanisha tangazo la vita! Jambo alilokuwa akiagizwa lilikuwa haliwezekani.

Yehoramu hakuwa na imani ilioonyeshwa na mjakazi mdogo wa kiisraeli ambaye alikuwa amependekeza safari ya Naamani. Katika hili alikuwa mkuu kuliko Mfalme wake. Alikuwa amesahau nguvu za Mungu  zilizojionyesha kupitia mkono wa Elisha, hapo awali katika utawala wake, alikuwa ameenda dhidi ya Mfalme wa Moabu ( 2 Fal.3: 13-18). Pia angesahau funzo la tukio hili wakati Benhadi alishambulia Israeli baadaye kidogo.

Nguvu za Mungu hazikuingia katika akili Yerohamu. Alikubali pale ilionyeshwa wazi mbele  yake,  kwa sababu ilimfaa wakati ule. Hakutambua kwamba ni Bwana alikuwa anaonyesha Nguvu zake ili apate sifa. Yerohamu  alikuwa na fikra za kibinadamu na hakuweza kutambua mambo ya kiroho. Hakuwa amejifunza chochote kutokana shughuli za Mungu na akawa wa kwanza katika familia ya Ahab kuangamizwa na mkono wa Yehu.

NAAMANI ANATUMWA KWA ELISHA (2 Wafalme 5:8-9)

Wakati huo huo Elisha alisikia kuhus safari ys Mshami na akatuma ujumbe kwa Yerohamu: “Wacha aje sasa kwangu, na  atajua kwamba kuna nabii katika Israeli” (2Fal.5: 8). Na hivyo Naamani akaelekezwa katika nyumba ya nabii.

Mpaka hapo mambo yalikuwa yameenda kulingana na mpango wa Naamani. Bila shaka akilini mwake alikuwa ameona jinsi nabii angemwamkua, amponye ugonjwa wake na kisha kuzawadiwa na mkuu wa jeshi la Washami.

Lakini Mungu hakuwa na haja ya kupata neema kutoka kwa Naamani. Ukosefu wa utambuzi wa  Mungu wa Israeli, na Washami ulikuwa sawa na tabia za watu wengi ambao wanaonyesha tamaa ya kielimu kwa neno la Mungu. Jambo la kuvutia ni kwamba  Naamani hakutia shaka kwamba angepokea uponyaji Israeli,  lakini alikuwa na mtazamo wake binafsi jinsi hili lingetekelezwa. Naamani alijifunza kwamba Bwana pekee ndiye wa kupewa sifa- Binadamu hata kama ana cheo gani lazima ashushwe.

KIBURI CHA NAAMANI NA UNYENYEKEVU (2 Wafalme 5:10-19)

Mtizamo wake wa jinsi uponyaji ungetekelezwa ulikatizwa kwa ghafla wakati Elisha alituma mtumishi wake kupeleka ujumbe: “Nenda, uoge katika mto Yorodani mara saba”. Katika kiburi na hasira Naamani akarudi. Katika fikra zake alidhibitisha hili kwa kutoa sababu, akilinganisha mito mizuri ya Shami  na mto Yorodani uliojaa matope. Na akarudi Damascus akiwa amejaa na hasira, ukoma wake ukabaki naye.

Sawa na wale wanaosikia Neno la Mungu na kukataa kunyenyekea na  utii wa  amri zake hawataoshwa dhambi zao. Naamani alikuwa tayari dhabihu ya mambo fulani, lakini je alikuwa tayari kutii? "Utii ni bora kuliko dhabihu", kwani sadaka ya wenye dhambi ni chukizo kwa Bwana  (1Sam: 15;22, Zab. 15: 8).

Kwa bahati nzuri, kesi ya Naamani ilifanikiwa kwa neema ya watumishi wake. Pendekezo la kufikiria upya maneno ya Elisha yangemkasirisha zaidi. Lakini alibadilisha msimamo wake na kukubali ushauri wa watumishi wake. Sasa alitambua ujinga wake mbele ya watumishi wake na aka-nyenyekea mbele ya Mungu. Hili lilikuwa jambo la kufedhehesha kwa Naamani, lakini lilifaa ili apate moyo wa kunyenyekea unao mpendeza Mungu. Ilibidi atambue kwamba maji machafu ya mto Yorodani yalikuwa mazuri kuliko yale ya Abana na Farpari.

Alipotoka mtoni kwa mara ya saba shughuli ilikuwa imekamilika. Mwili wake ulikuwa umeoshwa ugonjwa na akili yake kusafishwa kutokana na kiburi kilicho kuwa kati yake na na uponyaji. Kurudi kwake katika nyumba ya Elisha kulionyesha kubadilika kwa moyo wake: “Sasa nimetambua kwamba hakuna Mungu mahali pengine duniani ila Israeli”, Mtu wa mataifa alikuwa amekuja kwa Mungu wa Israeli (linganisha Lk. 4: 25-27).

Nabii alifurahi kumpokea wakati huu, vivyo hivyo, Bwana Yesu Kristo atafurahi kupokea wote watakaokuja kwake kupitia njia ya ubatizo “wenye roho ya kutubu na ya kunyenyekea” (Isa. 57:15; 66.: 2).
SAMBAMBA NA UBATIZO

Usawa kati ya kuoshwa kwa Naamani Mshami na ubatizo wa wale wanaomfuata Yesu Kristo ni dhahiri kabisa. Kuamini na ubatizo ni muhimu katika wokovu. Bwana Yesu alisema, " kama Mtu hajabatizwa na maji na roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu”, “Endeni ulimweguni wote mkahubiri Injili kwa kila kiumbe. Yule atakaye amini na kubatizwa ataokolewa; lakini yule hataamini atahukumiwa” (Yohana 3: 5; Mk. 16: 15-16). Katika kila kesi ambapo kuna kumbukumbu ya kugeuka inapatikana katika kitabu cha Matendo Ya Mitume, Imani inafuatia ubatizo (linganisha Mdo. 2:38, 41, 44, 8:12-16, 10: 45-47, 18: 8; 19: 2, 4, 5, 22: 16-19). Kuna wale wanachukulia ubatizo kama jambo la hiari. Roho hii ya kiburi inafanana ile ya Naamani kabla ya kujinyenyekeza. Amri ni maalum kwamba wale wote watakataa kutii “Watahukumiwa” isitoshe neno “tumbikiza” katika Septugia ni "baptiso" (2 Fal. 5:14). Kutokana na neno la kiingereza “Ubatizo” linatolewa hapo na linapoandikwa katika agano jipya linatafsiriwa kama “kubatiza”

Vijana wanapokaribia hatua hii lazima wafikirie kwa makini somo la Naamani na kutafuta nyoyo zao ili kuhakikisha nia ya matendo yao.

UCHOYO WA GEHAZI NA HUKUMU(2 Wafalme 5: 20-27).
Gehazi alikasirishwa na hatua ya Elisha kukataa zawadi yoyote kutoka kwa Naaman. Alionyesha kukosa mtizamo wa kiroho wa matukio yaliotokea mbele yake. Alikuwa ameona kiburi cha Naamani na udhalilishaji. Alikuwa pia ameona jibu la Elisha kwa wakuu wa Washami waliporudi kutoka Yorodani wakitambua na kumtukuza Mungu wa Israeli.

Somo lilikuwa limepotea kwa Gehazi. "Tazama Bwana wangu amemwachilia Naamani Mshami, kwa kukataa kupokea mikononi mwake vile vitu alivyovileta". Alishangaa sana kuona kwamba mtu wa mataifa, mwanajeshi mwenye cheo cha juu angewachiliwa kwa urahisi hivyo baada ya Bwana wake kumponya. Hakumpa Mungu sifa kwa muujiza wa uponyaji. Yote yaliyokuwa yametokea kwake ilikuwa ni kama jambo la kawaida. Hivyo akawafuata na kwa kutumia uwongo akapata  magunia mawili ya shaba na jozi mbili za mavazi. Kwa kufanya hivi alidhalilisha utukufu wa Mungu kwa kuchukua aina ya zawadi kwa muujiza ambao Mungu alikuwa ametenda (Mst.16).

Gehazi alikuwa ameshuhudia nguvu za Mungu mara nyingi katika huduma yake kwa Elisha. Hakukosa imani au utambuzi wa Mungu wa Israeli, lakini alikosa kutambua kanuni moja ambayo Mungu alitaka kuonyesha katika tukio hili- Neema ya Mungu haiwezi nunuliwa na pesa za binadamu (Isa. 55: 1-3; Mt 10: 8;. linganisha Mdo 8:20). Umuhimu wa uponyaji wa Naamani haukumaanisha chochote kwake. Alifananishwa na Israeli ambao Nguvu za Mungu zilikuwa zimeonyeshwa kwao, na hawakutambua kanuni za msingi zilizo katika sheria, ambayo ingewaongoza kwa wokovu (Gal. 3: 23-25).

Elisha aliweka wazi udanganyifu wa Gehazi na mtumishi aliyetoka usoni mwake akiwa na ukoma, ugonjwa wa Naamani umemkwamilia. Alitafuta zawadi na akapata utajiri kutoka kwa mtizamo wa kidunia. Hata hivyo, utajiri wake haukumletea furaha ya kudumu na ilimbidi kuishi maisha yake yaliyosalia na adhabu na aibu ya ukoma.

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • "Wokovu ni kwa Wayahudi". Nahodha wa jeshi la Washami mwenye kiburi hakuweza kukabiliana na ugonjwa wa kimwili wa ukoma. Ilibidi atafute nabii wa Mungu wa Israeli ili aponywe.
  • Yehoramu alikuwa mfalme aliyekosa imani, na hata kama miujiza ya Elisha ilikuwa imefanyika katika nchi yake, alitememeka na kuogopa wakati alisikia kwamba Naamani alikuwa anakuja kuponywa ukoma. Tusitende kama kwamba hakuna Mungu. Kuna miujiza katika mbingu na maajabu katika viumbe ambayo inaweka wazi kwamba Mungu yupo.
  • Naamani alijinyenyekeza dhidi ya mielekeo yake ya asili na kwa sababu ya utii wake akaponywa. Sisi sote ni binaadamu na, kama mtu mwenye ukoma, "mgonjwa" na anayekufa. Dhambi inasimama kati yetu na Mungu lakini Yeye Ametoa ukombozi kwa njia ya imani na ubatizo. Tukitii kwa unyenyekevu sisi pia tutaokolewa.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 5, Nam. 5

MASWALI YA AYA:

  1. Somo gani  tunajifunza kutokana na ugonjwa wa Naaman kuhusu Israeli?
  2. Nini ilikuwa ubaya wa tabia ya  Naamani wakati alipofika kwa Elisha kuponywa? Je, alitarajia nini kitendeke?
  3. Jinsi gani Naamani alifundishwa somo kwamba utii ni bora kuliko dhabihu?

MASWALI YA INSHA:

  1. Elezea jinsi tabia ya Naamani iliathiri nafasi yake ya kuponywa ukoma.
  2. Elezea jinsi tiba ya Naamani ni mfano wa utii unaohitajika kwa yoyote ambaye anataka kubatizwa katika Kristo.
  3. Elezea umuhimu wa ukoma.
  4. Kwa kifupi elezea umuhimu wa mitazamo ya Yehoramu na Gehazi kwa Naaman.

 

 

 

 

Swahili Title
311. NAAMAN, MSHAMI
Sub type
Sub sub type