CSSA 3-3-312 - JUDGMENT ON THE HOUSE OF AHAB

Swahili

312.   HUKUMU YA NYUMBA YA AHAB

“Watenda dhambi wote wataondolewa, lakini wale, wanaomsubiria Mungu wataridhi ardhi"

Ahabu alikuwa mtu aliyekosa nguvu na uamuzi. Alijua kilicho sawa katika macho ya Mungu lakini alishindwa kutekeleza. Sababu kuu ya hili ilikuwa Mkewe Yezebeli. Alikuwa binti ya Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, na mcha Baali. Hakuwa na heshima kwa Mungu wa Israeli na kwa sababu alikuwa na tabia imara aliweza kumgeuza  na kumfanya atende mambo yaliyokuwa kinyume and  nafsi yake.

Katika Somo hili tunaangalia nyuma katika siku za Eliya na kuona umbali ambao Yezebali na Ahab walikuwa tayari kwenda ili wawaangamize watumisho wa Mungu. Kisha tutaangalia baadae wakati hukumu ya kutisha kwamba vitendo kama hivyo vilitendwa na mkono wa Yehu.

Lengo la somo hili  ni kuonyesha jinsi mafanikio ya wenye dhambi ni ya muda mdogo, kwani hatimaye watamezwa na ardhi.

1 Wafalme 21; na 2 Wafalme. 9
 

NABOTHI AUAWA NA YEZEBELI (1 Wafalme 21:1-14)

Mfalme Ahabu alipenda anasa na raha na  alitamani kutengeneza shamba la mizabibu. Kufanikisha hili alihitaji  ardhi zaidi and  ardhi iliofaa ilikuwa kipande cha shamba la mizabibu  kando na ikulu katika mlima wa Yezreeli. Hivyo akaenda kwa mmiliko, Nabothi, kwa kile kilionekana kama ombi la dhati; “Nipe ardhi yako....nami nitakupa kipande kingine cha shamba la mizabibu nzuri kuliko hiki; ama ukiona inafaa, nitakupa  fedha kwa dhamani yake” (Mst. 2)lakini Nabothi alikataa kwa sababu za kidini; “ Bwana amanikataza, mimi kukupa uridhi wa baba yangu”. Sheria pia inakaza kupeana au kuuza uridhi wa mtu ila tu kwa sababu zinazomfanya kufanya hivyo. (Hes.36: 7-9). Hata hivyo ardhi ilibidi kurudishwa kwa mmiliki wake wa awali katika mwaka wa yubile (Law.25: 13-16).

Majibu ya Ahabu kwa ombi hili inaonyesha tabia  yake. Alijua kwamba sheria ilikuwa na matakwa hayo na hakujaribu kupinga maneno ya Nabothi, ila alinuna na kukasirika. “akajilaza kitandani, na kugeuza uso wake na hakula chakula” (Mst.4) haupita muda mrefu kabla mkewe Yezebeli alitambua kuwa alikuwa na huzuni. Alipomuuliza, alimwambia kile kilichotendeka lakini hakumwambia mkewe sababu ambazo Nabothi alikuwa ametoa za kukataa kumpa shamba lake. Kuvunja sheria ya Mungu hakukumjalisha Yezebeli. Akijua hili, Ahab hakujishughulisha kumwelezea sababu za Nabothi. Yezebeli alimkemea Ahab kwa udhaifu wake, “ Hujui ni wewe mmiliki wa ufalme wa Israeli?” na kumwambia atupilie mbali matatizo yake na kufurahia kwani atahakikisha kwamba mapenzi yake yametimizwa. (Mst.7)

Yezebeli alipanga njama ambapo mashahidi wa uwongo walikuwa wadai kwamba  Nabothi alikuwa amemtukana Mungu na mfalme mbele ya watu. Wakuu wa Israeli waliotishiwa walikuwa watekeleze mpango huu. Nabothi alituhumiwa na kutolewa nje ya mji na kupigwa mawe pamoja na wanawe(Mst.13, 2 ​​Fal. 09:26.). Basi  Nabothi akauawa kwa sababu ya imani yake na bila shaka  alikuwa  mmoja na waaumini ambao wanaelezewa katika Ebr. 11:37, ambao “walipigwa mawe” kwa imani.

Tofauti na Ahabu, Yezebeli hakuwa na  aibu kwa kile alichokitenda na hakusita kutenda. Alikuwa amepanga kifo cha mtu mwaminifu katika Israeli kwa njia ambayo ilomwondolea shaka mbele ya macho ya watu. Alipokea habari ile kwa furaha kwani mipango yake ilikuwa imefanikiwa.

 

MAPAMBANO NA ELIYA: NYUMBA YA AHABU INAADHIBIWA (1 Wafalme 21;15-24)

Yezebali alitosheka kusikia kwamba njama yake ilikuwa imefanikiwa, akamwambia Ahab “inuka,  nenda ukachue shamba la mizabibu la Nabothi...... ambalo alikuwa amekataa kukupa kwa fedha” (Mst.15) kwa furaha Ahab aliinuka ili akachukue umiliki (Mst.16) lakini Ahab aliweka jambo moja mbali na fikra zake-Bwana alikuwa ameona uovu uliokuwa umetendeka. Kwa sababu ya hili alikuwa ameamua kuharibu kabisa nyumba ya Ahabu. Hapa kuna somo kuu kwetu sote. HatuwezI kuficha kitendo ama fikra zote  kutoka kwa Mungu (3:12 1 Pet; Zab. 66: 7; Yer. 17:10). Utambuzi huu unapaswa kuwa nasi kila wakati kwani utatusaidia kuweka mbAli fikra ovu na pia kutenda dhambi.

Bwana alimwelezea Eliya yale yaliyotokea na kuweka kinywani mwake maneno ya kumhukumu Ahab; “asema Bwana, Je umeua na kumiliki?.....katika mahali ambapo mbwa walilamba damu ya Nabothi, watailamba damu yako pia” (Mst.19)

Furaha ya Ahabu iligeuka na kuwa hofu. Wakati alimwona Eliya akija kukutana naye dhamiri yake ikaanza kumsuta na akasena, "Je! Umenipata, ewe adui yangu?" (Mst.20). Eliya akaendelea kutamka hukumu ya kutisha zaidi kwa Ahab na nyumba yake. Sababu ya kwanza- alikuwa amejiuza katika kazi ya uovu katika macho ya Mungu- alijua kilichokuwa haki,  lakini kwa makusudi alikuwa amekuwa chombo  cha uovu. Katika mwanga  wa maneno hayo tunapaswa kujiuliza swali, je ni kwa nani tumejiuza, kwa Mungu ama kwa dhambi. Tunaweza tumikia Bwana mmoja. Kama hatumtumukii  Mungu katika kweli, basi tutakuwa kuwa tunatumikia dhambi (Rum. 6: 16-17; Mt. 6:24).  Ahab aliambiwa  kwamba uzao wake utaangamizwa kabisa na hakuna mtu hata mmoja atabaki: ili kusisitiza hili aliambiwa kwamba nyumba yake itafanya kama ile ya Yeroboamu na Baasha, ambazo zote ziliangamizwa kwa kifo cha haraka(1 Fal.16: 3, 11). Kulingana na Yezebeli, mwisho wa uasi  ulikuwa umetangazwa. Kwa sababu alikuwa amemchochea mumewe kutenda dhambi mbele ya macho ya Mungu, “mbwa wangetafuna Yezebeli katika ukuta wa Yezreeli".

AHABU ANATUBU (1 Wafalme 21:25-29)

Kwa sababu Yezebeli alikuwa na tabia dhabiti kuliko Ahab, alimtawala an kumfanya tutenda dhambi. Aliharibu dhamiri yake wakati alitaka kumuua Eliya (19: 1-2), na pia katika kesi ya Nabothi. Kupitia ushawishi wake ibada ya Baali ilianzishwa Israeli na maadili potovu ya watu wa Wamori yalirudishwa. Maovu haya  yalikuwa sababu ya Mungu kuwafukuza watu wa Mataifa mbele ya wana wa Israeli katika siku za Yoshua (Mst.25-26; Mwa.15:16; Law. 20: 23-24). Ahabu, hata hivyo hofu ya Bwana na hii ilikuwa wazi kutokana na majibu yake ya adhabu hii ya kutisha iliyowekwa juu yake; "akararua nguo zake, na kuvaa magunia juu ya mwili wake, akafunga na kulala kwa magunia, akaenda kwa upole (Mst. 27) Neema ya ajabu na huruma ya Mungu inaonekana katika majibu yake kwa toba Ahabu – kungekuwa na huruma katika huruma; “ Sitaleta mabaya katika siku zako; lakini kwa siku za mwanoa, nitaleta uovu juu ya nyumba yake” neema hii ya ajabu kwa kweli kwamba Mungu “Hafurahiswi na kifo” cha walio na dhambi, lakini atawapa wanadamu nafsi  ya kutubu na kuokolewa (Eze.18:23, 32; 1 Tim. 2: 4; 2 pet.3:. 9; Kut. 34: 6, 7).

YEHU ANAHARIBU NYUMBA YA AHAB (2 Wafalme 9, 10)

Hukumu ya nyumba ya Ahabu iliahirishwa mpaka baada ya kifo chake. Ahab  aliuwa vitani na Washami huko Ramoth-Gileadi. Gari lake la farasi lililojaa damu yake lililetwa na kuoshewa katika Bwawa Samaria pamoja na ngao yake. Kulikuwa na ukweli katika maneno ya Bwana yakatimia- “mbwa waliramba damu yake” (1 Fal. 22:38; 21:19.).

Kulikuwa ushairi wa haki kwa kila njia; kuona Ahab alikuwa amewaua Nabothi na wanawe,  hivyo yeye na wanawe wataangamizwa. Mtu ambaye Mungu alimchagua kutimiza hili alikuwa Yehu, mwana wa Nimshi. Alikuwa amechaguliwa mfalme na moja wa  wana wa manabii na kupewa jukumu ya kuteleza hukumu ya Bwana katika nyumba yote ya Ahab. Kwa ustadi mkubwa na hila yenye ukatili aliangamiza kila mtu kwa familia ya Ahab.

Orodha ifuatayo inaonyesha jinsi Yehu alitekeleza shughuli hii

 

  1. 2 Wafalme 09:26. Aliwaua Yoramu mwana wa Ahabu na kumtupa katika uwanja Nabothi, hivyo kutimiza unabii wa Eliya (1 Fal. 21:29).
  2. 2 Wafalme 09:27. Aliamrisha mauaji ya Ahazia, mfalme wa Yuda, mwana wa Athalia ambaye alikuwa binti ya Ahabu na Yezebeli.
  3. 2 Wafalme 9: 30-37. Alimua Yezebeli katika Yezreeli na kumkandamiza chini ya mguu wake.
  4. 2 Wafalme 10: 1-10. Aliwatia hofu watu wa Samaria, kwa kuwaua  wana 70 wa Ahabu.
  5. 2 Wafalme 10: 12-14. Aliwaua wakuu 42 wa mahakama ya Ahazia, mfalme wa Yuda, jamaa wote wa Ahabu kupitia Athalia ambaye alikuwa ameolewa na Mfalme wa Yuda.
  6. 2 Wafalme 10:17. Aliwaua wale wote waliokuwa Samaria wenye uhusiano na Ahabu.
  7. 2 Wafalme 10: 18-28. Alifutilia kabisa uabudu wa Baali katika Israeli.

 

ROHO YA YEZEBELI KATIKA IKLEZIA (Ufunuo 2:20-23)

 Tukiwa na historia ya wakati huu akilini, Ufunuo. 2:20-23 inataja Yezebeli. Aliendeleza uabudu wa uwongo katika Israeli na kuwaangamiza manabii ya Bwana, lakini mwishowe yeye na wanawe waliharibiwa kabisa. Katika siku za mwisho walimu waongo walikuwa wanajipenyeza katika njia za kiroho za Israeli na kuharibu ibada ya kweli;  “ Zinazowashawishi watumishi wangu kuzini, na kula vitu vilivyotolewa kama sadaka kwa sanamu”. Kwa pamoja waasi hawa waliitwa “Huyo mwanamke Yezebeli”. Hatma ya Yezebeli na wanawe  ni sawa na ya waasi;  “nitawatupa  kwenye kitanda na wale wazinio pamoja naye wapate dhiki kubwa....na nitawaua watoto kwa mauti ... "(Ufu. 2: 22-23). Hivyo tunajifunza somo ni kushikamana na Neno la Mungu wetu, na sio kupotishwa na mafunzo na philosophia za uwongo ambazo chanzo chake in akili dhaifu ya binadamu (1The. 5:21; Mdo. 17:11).

Jinsi muda ulivyopita waalimu wa uongo walipata umarufu katikati ya eklezia; na Ukweli ukapotoshwa na kupotea, isipokuwa kwa wachache waliobaki na kuteswa. Darasa la Yezebeli likaendelea na kukomaa kwa kuibuka kwa kanisa la Kirumi kama kichwa cha makanisa yote na mhukumu wa mashahidi wa kweli. Katika saa yake ya hukumu yeye (kama Yezebeli, linganisha. 2 Fal. 9:30) anafananishwa na mwanamke aliyevaa nguo ya zambarau na nyekundu na yeye inaitwa "mama wa wazinzi". Kama katika kesi ya Yezebeli, siku za mwisho Yehu, Bwana Yesu Kristo, kwa haraka ataharibu mfumo huu wa dhambi (Ufu. 18: 21-24).

 

TATHIMINI YA YEHU — KUSHINDWA (2 Wafalme 10:19-36).

Ingawa Yehu alitumika kuharibu nyumba yote ya Ahab, yeye mwenyewe hakuwa mtu mwenye tabia nzuri. Alikuwa mtu mbaya, mwenye kuwahukumu wengine kwa haraka, ilhali yeye mwenyewe alitembea katika “dhambi ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alifanya Israeli kutenda dhambi (Mst. 29) Sisi pia tunahitajika kuchukua hatua dhidi ya maovu, ni muhimu kujisafisha kutoka kwa njia za kimwili maishani mwetu. Hivyo basi tunaweza pata usawa wa “Wema na ukali” kuonekana ndani yetu. Yehu aliweza kuona makosa ya wengine lakini alishindwa kutekeleza Ukweli katika maisha yake.

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Ni lazima tuwe imara na thabiti tukitembea kuelekea kwenye Ufalme. Ahabu alipotoshwa kwa urahisi na mkewe mwovu na abudiae sanamu na hivyo uharibifu ukaletwa juu yake, nyumba yake na Israeli.
  • Ndoa na mwenye akili mmoja inazuia uovu huu (Mit.19:14; Efe. 5: 25-33). Ni inazalisha utulivu na maelewano.
  • Bwana anawaangalia wale ambao wanateseka kwa ajili ya uadilifu na ataleta adhabu juu ya wale ambao wanawatesa. Mafanikio ya waovu ni ya muda (Zab. 37: 1, 2; 73: 3-19).
  • Bwana ni mwenye haki na huruma. Huruma yake ya ajabu na inaonekana wakati aliahirisha hukumu juu ya nyumba ya Ahabu kwa sababu alijinyenyekeza
    mwenyewe. Lakini ingawa yeye ni uvumilivu, wale wanaokataa huruma yake wataharibiwa kwa haraka.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 5, Nam. 2, 6-7

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 20

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)— Sura 27

"Elijah the Tishbite" (J. Martin)— Sura 9

MASWALI YA AYA:

  1. Elezea tukio kuhusu Nabothi Myezreeli, kuonyesha kwa ufupi jinsi tabia yake ilitofautiana na tabia ya Ahabu na Yezebeli.
  2. Wakati gani Eliya alitangaza adhabu ya Mungu juu ya Ahabu na nini ilikuwa adhabu hii?
  3. Yehu alitekeleza hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu, lakini Mungu hakupendezwa naye. Kwa nini na ni somo gani tunalojifunza kutoka hili?

MASWALI YA INSHA:

  1. Andika kuhusu tabia utafiti juu ya Ahabu.
  2. Yezebeli ni jina linolopew katika kitabu cha Ufunuo kwa walimu wa uongo ambao walienea ndani ya eklezia katika karne ya kwanza. Onyesha jinsi hii ni sahihi kwa kupitia maisha yake kama yalivyowekwa wazi katika kitabu cha wafalme.
  3. Toa Muhtasari wa masomo makuu tunayojifunza kutoka maisha ya Ahabu na Yezebeli na uharibifu wa nyumba yao na Yehu.

 

 

Swahili Title
312. HUKUMU YA NYUMBA YA AHAB
Sub type
Sub sub type