CSSA 3-3-314 - DECLINE AND CAPTIVITY OF THE TEN TRIBES

Swahili

314.    KUANGUKA NA UTUMWA WA MAKABILA KUMI

“Bwana alikuwa amekasirishwa na Israeli na akawaondoa machoni pake"

Katika somo letu la mwisho tuliangalia maisha ya Yona na ujumbe wake kwa Ninawi.Ilikuwa ni taifa hili la Washami ambalo liliteka Israeli nyara miaka 100 baada ya mahubiri ya Yona. Kando na ukamilifu wa Yehu katika kuharibu waabudu wa Baali, taifa liliendelea katika “dhambi ya Yeroboamu, ambaye alisababisha Israeli kutenda dhambi”, kama walivyofanya wafalme wa Israel waliomfuata, na taifa likaendelea kuanguka kiroho. Mwishowe katika utawala wa Hoshea, Israeli walishindwa na Washumi na kuchukuliwa mateka.

Lengo letu katika somo hili ni kufuatilia sababu ya kuanguka kwa Israeli na kuchunguza adhabu ambayo iliwakumba ili tuweze kuiepuka.


KUANGUKA KWA ISRAELI

Ibada potofu ilioanzishwa na Yeroboamu, chini ya uongozi wa makuhani “ ya watu wa chini, na ambao  hawakuwa wana wa Levi”, ulikuwa mwanzo wa kuanguka kwa Israeli. Wengi walitoroka kutoka ufalme wa kaskazini, wakitafuta dini ya baba zao Yuda na Yerusalemu. Miaka ishirini baada ya  mgawanyiko, Israeli walikuwa na jeshi la watu 800,000 (2 Nya. 13: 3), Lakini katika utawala wa Ahab nambari hii ilikuwa imepungua hadi 7,232 (1Fal. 20:15.). Yuda kwa upande mwingine walianza na jeshi la watu 180,000 (2 Nya. 11: 1.) na idadi hii ilizidi na kufikia watu 1,160,000 wakati wa Yosephati (2 Nya. 17:14-18).

Kulikuwa na ukosefu kamili wa utulivu katika ufalme wa kaskazini. Tofauti Yuda ambayo ilikuwa na msururu wa wafalme kutoka nyumba ya Daudi, Israeli ilikuwa na koo sita kutoka katika siku za Yeroboamu. Mji mkuu ulibadilika mara mbili, kutoka Shekemu hadi Tiza na baadaye kutoka Tiza  hadi ya Samaria. Kukosa utulivu ilikuwa ishara ya shida kuu- kuasi dhidi ya Mungu. Katika utawala wa Hoshea, mfalme wa Mwisho wa Israeli, imeandikwa kwamba  alitenda maovu mbele ya macho ya Mungu, lakini sio kama wafalme wa Israeli waliokuwa mbele yake” (2 Fal.17: 2). Hii ni kwa hakika sio tabia ya kutamaniwa, lakini ilikuwa nzuri kuliko wafalme wengine wa Israeli. Kila mfalme wa Israeli inasemekana alifuata dhambi ya Yeroboamu, kutenda dhambi dhidi ya Mungu na kufanya Israeli kutenda dhambi.  Sasa wacha tufuatilie mwisho wa ufalme wa Israeli mpaka pale walipotekwa nyara na Ashuru.

TISHIO KUBWA LA ASHURU (2 Wafalme 15:8-31)

Uovu wa Israeli umetiliwa mkazo katika utawala wa wafalme watano wa mwisho. Kila mmoja ( isipokuwa Manahemu) waliangushwa na vurugu na fitina. Zakaria mwana wa Yeroboamu II, wa ukoo wa Yehu, akachukua ufalme na kuendeleza ufisadi ulioanzishwa na Yeroboamu I. Alitawala kwa  miezi sita na aliuwawa na Shalumu (Mst.10)  Hili lilitimiza neno la Bwana katika 2 Wafalme 10:30 (linganisha. 15:12).  Lakini njama ya Shalum ilikuwa ya muda mfupi, kwani kwa muda wa mwezi moja, yeye pia aliuliwa na Menahemu (Mst.14).

Menahemu alitawala kwa muda wa miaka kumi. Miaka hio ilikuwa miaka ya vurugu katika israeli, kwa sababu ya hali ya kutotulia ya viongozi wake. Jicho la imani lingeweza kuona matatizo haya kama ishara ya kutofurahishwa kwa Mungu kutofurahishwa na watu wake, lakini waaminifu wa Israeli walikuwa wametorokea Yuda. Hata hivyo, kulikuwa na  tishio kubwa kwa Israeli kuliko mavutano ya kidani. Kuongezeka kwa nguvu ya Washuru ilikuwa mwanzo tu. Menahamu alilazimika kutoa heshima kwa Pul mfalme wa Washuru, ili kumsihi asishambulie Israeli (Mst.19-20.). Kwa kweli,Mambo ya Nyakati yanatuambia kwamba kuanzia wakati huu kuendelea, sehemu za makabila ya kaskazini yalianza kuchukuliwa mateka (1 Nya. 5:26). Badala ya kutafuta utajiri wa imani na uaminifu wa Bwana, Manehamu alitaka kuwahonga Washuru, lakini hakufanikiwa kwani hatima ya Israeli ilikuwa adhabu.

Menahemu alifuatwa na mwanawe Pekahia, ambaye alitawala kwa miaka miwili, akiendeleza ufisadi wa babake (Mst.23-24). Alingatuliwa, kwa vurugu na Peka aliyetawala kwa miaka ishirini (Mst.25-27). Peka alijaribu kuimarisha israeli. Lakini Juhudi zake zilikuwa kwa nguvu zake mwenyewe alipuzilia chanzo hasa cha nguvu. Alitafuta umuungano  wa Resini, mfalme wa Washami, na  alikutana na ndugu yake Yuda, na kuwashinda chini ya uogozi hafifu wa Ahazi.  Alilazimishwa na nabii Odedi  kurudisha mateka wake Yuda (2 Nya.28: 6-11). Hata hivyo, katika maneno ya Isaiaya “mkia wa....... " (Isa.7: 4.) ulizimwa kama vile. Katika utawala wa Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru aliendeleza maovu ya aliowafuata, akawateka Waisraeli mateka kule Ashuru (Mst.29) Israeli waliendeleza uovu. Peka iliangushwa katika njia ile aliotumiwa kuchukua ufalme-kwa njama na vurugu (Mst.30).

HOSHEA –MFLAME WA MWISHO WA ISRAELI (2 Wafalme 17:1-6)

Hoshea alichukua ufalme na kutawala kwa miaka tisa.Adhabu ya israeli ilikuwa imetiwa mhuri na Hoshea alifanya majaribio hafifu kuleta mabadiliko. Yeye hakuwa mwovu kama wafalme wengine mbele yake (Mst. 2), lakini kwa wakati huu Imani na uwezo angeweza kugeuza muundo wa kuanguka. Hoshea alitafuta muungano na So, Mfalme wa Misri, na akawacha kutuma kodi kwa mfalme wa Ashuru (Mst.4) Israeli ambao walikuwa wametoka Misri chini ya mkono wa Bwana, sasa walianguka na wakaungana na mwanzi huu uliovunjika. Kama "njiwa mpumbavu" walitaka muungano na nguvu za giza, kwani alisema Hoshea, “Israeli walikuwa wamesahau Muumba, na kujenga hekalu..... lakini nitatuma moto kwa miji na kuteketeza ikulu yake” (Hos.7:11;. 8:14). Moto ulikuwa Shalmanesa, mfalme wa Ashuru, ambaye alikuja Israeli na kuiharibu kabisa (Mst.5-6, 23). Utawala wa Israeli ukaisha kabisa.

SABABU YA KUANGUKA NA KUSHIKWA MATEKA (2 Wafalme 17:7-23)

Sababu ya Israeli kushikwa mateka imeelezwa wazi katika sehemu hii ya rekodi. Mungu ni mwingi wa huruma na fadhili, lakini hawezi waache wale waovu kukaa bila adhabu. Israeli walikuwa na nafasi nyingi za kutubu, lakini walifanya shingo zao kuwa ngumu dhidi ya manabii wake. Angalia orodha ya dhambi katika aya hizi:

• Walitembea katika amri ya miungu ya mataifa mengine na wala sio katika sheria ya Bwana (Mst.7-8).
•  Kwa siri, na uwazi, walifanya machukizo dhidi ya Mungu wao (Mst.9).
• Walianzisha mashamba na kujengwa sanamu za kuabudu wakiasa sheria ya Mungu (Mst.10-12).
• Waliwakataa manabii wa Mungu, wakafanya shingo zao kuwa ngumu na hakumwamini Bwana (13-14 Mst.) Mungu wao.
• Walifuata mambo bure, wakaabudu ndama wawili, walimtumikia Baal (Mst. 15-16).
• Waliwafanya wana wao wa kike na kiume kupita katika moto (Mst.17).

Bwana hakuwa tayari kuwavumilia tena. Walikuwa wameharibu nchi yake, wakakataa manabii wake na hivyo Yeye “aliondoa Israeli mbele ya macho yake,kama alivyokuwa amesema, manabii wote watumishi wake. Hivyo Israeli walichukuliwa kutoka nchini kwao hadi Ashuru mpaka leo hii” (Mst.23). Tena katika katika 2 Wafalme 18:12, Mungu anasisitiza sababu ya uhamisho wao: “kwa sababu hawakutii sauti ya Bwana Mungu wao na wakavunja agano lake, na yote yale Musa mtumishi wa Mungu alikuwa ameamuru, na hawakuyasikiza, wala kuyatii.”
 

MWANZO WA WASAMARIA (2 Wafalme 17:24-41).

Waashuri walikuwa mazoae ya kuweka mateka wao katika nchi zingine. Lengo lao lilikuwa kuondoa roho ya  utaifa kukua katika nchi walizotawala na hivyo kuzuia uasi. Sehemu iliobaki ya sura ya 17 ni hadithi ya tabia katika miji ya Samaria; watu wengi walihamishwa hadi Israeli, na wakaishi kule pamoja na miungu yao. Mungu alisababisha simba kuja kwa wakazi hawa kutoka mataifa mengine (Mst. 25-26) Waashuri kisha wakamrudisha mmoja wa makuhani wa Israeli ili awaelekeze wageni katika njia “za Mungu wa nchi”. Matokeo yake yalikuwa yakuchanganyisha na ya ufisadi na yakawa mfumo wa ibada uliojulikana kama dini ya Wasamaria. Tizama mstari 32-33 “walimwogopa Mungu wakawafanya walioko chini kati yao kuwa makuhani wa mahali pa juu, ambao walitoa sadaka kwa ajili yao katika nyumba za mahali pa juu. Waliomwogopa Mungu na wakatumikia miungu yao,  kwa njia ya mataifa ambayo walikuwa wamechukuliwa kutoka kwao” kama Yesu alivyosema kwa mwanamke Msamaria katika Yn. 4;22 “Nyinyi mnaabudu msichokijua”.

 

ISRAELI BADO HAWAJAKUSANYWA TENA.

Ufalme wa kaskazini ulitawanyika kwa mataifa yote ya  dunia, na tofauti na ufalme wa kusini Yuda, ambao ulibaki vivyo hivyo hadi kizazi cha sasa. Wakati unakaribia wakati ufalme wa Kaskazini wa Efraimu atakuwa mshale na Yuda upinde wa Bwana (Zek. 9: 13-14). Israeli na Yuda bado hawajaungana pamoja chini ya mfalme wao wa Haki, Bwana Yesu Kristo (Eze. 37:16-28). Hata Hosea, ambaye aliandika mengi kuhusu uovu na uasi wa Israeli, ametabiri kuhusu wakati huu (angalia 1: 10-11; 3: 4-5; 6: 1-3). Tunaona sehemu za utabiri huu na Isreali katika nchi, lakini watapata utimizo kamili wakati Yesu Kristo, kupitia Eliya, atawarudisha “kama katika siku za awali” (Mik.7: 14-15; Eze. 20 : 33-44).

 

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Israeli walishindwa hapo awali kwa kuharibu ibada ambayo Mungu alikuwa ameanzisha kupitia Musa. Ni lazima tuwe makini ili kudumisha usafi wa mafundisho na ibada mbele za Mungu (Gal.1: 6-9; 2 Tim. 3: 14-17.; 2 Pet. 3: 15-18).
  • Israeli walianzisha tabia zenye madhara, katika umma na kwa siri, kuwatoa sadaka watoto wao kupitia kwa moto; na kugeuza ibada ya Mungu wa kweli na sanamu za mataifa. Ni lazima tujiweka kando na sanamu, yaani kitu chochote kinachoweza kugeuza mioyo yetu kutoka kumtumikia Mungu (1 Yn. 2: 15-17; 5:21).
  • Israeli walikuwa na shingo ngumu, walikataa kusikiliza sauti ya manabii wa Bwana, na mioyo yao ikawa migumu dhidi ya amri zake. Ni lazima tuwe tayari kupokea Neno la Mungu na sio kuasi dhidi ya maagizo yake (Isa. 57: 15-17; 66: 1-2.).
  • Kama Wasamaria tumetoka katika mchanganyiko na mfumo wa rushwa ya kidini na maneno ya Yesu ni muhimu hasa - "Waabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli" (Yn. 4:23).

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts) — Sura. 19, 20

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield) — Tol. 5, Nam. 11 na 12, Kur. 175-186.

"The Minstry of the Prophets" (R. Roberts and C.C. Walker) — Kur. 95-98.

 

MASWALI YA AYA:

  1.  Dini ya Msamaria ilianza vipi?
  2. Tofautisha kwa ujumla wafalme wa Israeli na wale wa Yuda.
  3. Ni hatma gani iliwapata wafalme wa Israeli? Toa maelezo mafupi.
     

MASWALI YA INSHA:

  1. Eleza sehemu ambayo wafalme wa Israeli walichangia katika kuanguka kwa ufalme wa Israeli.
  2. Nini ilikuwa sababu ya msingi kwa ajili ya kuanguka na kutekwa nyara kwa ufalme wa kaskazini mwa Israeli?
  3. Ni masomo gani tunajifunza kutoka kuanguka kwa makabila 10 ya Israeli na kuondolewa kwake katika mateka?

 

Swahili Title
314. KUANGUKA NA UTUMWA WA MAKABILA KUMI
Sub type
Sub sub type