CSSA 3-3-315 - HEZEKIAH: THE CHALLENGE FROM ASSYRIA

Swahili

315.    HEZEKIA: CHANGAMOTO KUTOKA ASHURU

“Mungu ni kimbilio na nguvu, msaada wa karibu wakati wa Matatizo''

Wakati ufalme wa kaskazini ulifikia kikomo, ukweli ulikuwa unafufuliwa Yuda. Hezekia ambaye akikuja kwenye ufalme katika mwaka wa tatu wa Hoshea (2 Fal. 18: 1), ilikuwa imeanza mageuzi ya kiroho. Kumbukumbu inasema “Hezekia alifanya kile kilichokuwa sawa mbele ya macho ya Mungu, kulingana  kwa yale yote Daudi babake alifanya” (Mst.3) hivyo kimbilio likapatikana kwa Waisraeli wa kweli. Kama mataifa kumi ya Kaskazini, yalizama katika uasi, na kuenda utumwani, hapo kukaanza jaribio kubwa zaidi la mageuzi ya kiroho Yuda ambayo taifa lilikuwa limeona.

Lengo letu katika somo hili ni kuona wakati migogoro inatukumba  suluhu ni kumgeukia Mungu katika imani na Maombi.

2 Wafalme 18 & 19

MAREKEBISHO YA HEZEKIA

Hezekia alianza utawala wake akiwa na umri wa miaka ishirini na tano. Jina la mama yake lilikuwa Abiya ambayo inamaanisha “Baba yangu ni Yah” (2 Nya. 29: 1). Baba yake duniani ilikuwa dhaifu, mwovu Ahazi, lakini Hezekia hakufuata njia zake;  lakini alifuata kanuni za “Daudi baba yake” (Mst.2) katika mwezi wa kwanza wa mwaka alikuwa mfalme, Hezekia akaanzisha mageuzi yake. Alirekebisha na kusafisha hekalu, aliwatakasa makuhani na kuwaelekeza  jinsi ya kufufua hukumu ya sheria, akilezea kwamba wengi walikuwa wamechukuliwa mateka kwa sababu ya kutofuata sheria ya Mungu. Hata matoleo ya kila siku yalikuwa yamesahaulika kwa miaka kadhaa (2 Nya. 29:1-9; 2Fal. 18: 1-6.).

Hezekia pia alifufua sherehe ya Pasaka ambayo pia ilikuwa imesahaulika wakati wa utawala wa Ahaz. Alitakasa nchi dhidi ya sanamu, na akaanzisha ukuhani na Walawi katika zamu,  kama walivyokuwa chini ya Mfalme Daudi (2 Nya. 31: 1-4.). Alirejesha utoaji wa fungu la kumi kama ilivyokuwa katika sheria ya Musa na akateua wakuu wa kutekeleza na kusambaza fungu  la kumi. Bwana alifurahishwa na juhudi zake- “ akafanya yaliyo mema na haki na ya kweli mbele ya Bwana Mungu wake..... alifanya hivyo na moyo wake wote na akafanikiwa (2 Nya. 31: 20-21.).

Nguvu za Ashuru zilikuwa zinaongezeka kwa upande wa kaskazini na walivamia Israeli mara kwa mara. Hezekia hata hivyo, aliweka imani yake kwa Bwana na kurusha  nira ya Ushuru (2 Fal. 18: 7.).  kwa muda hakuna kitu kilicho tokea. Kisha katika mwaka wa sita wa Hezekia, mwaka wa tisa wa Hoshea, Mfalme wa Israeli, ufalme wa  kaskazini alichukuliwa mateka na mfalme wa Ashuru. Israeli walikuwa wametekwa nyara- Je ni Yuda ingefuatia? Je majibu ya watu wa Yuda yalikuwa ngani?

MAJIBU YA YUDA KWA TISHIO LA WASHURU (Isaiya. 22)

Nabii Isaya alikuwa tofauti na Hezekia na anatuambia jinsi  watu wa Yuda walikuwa wanafikiria wakati uliokaribia wakati wa kuvamia na Washuru.

Kuna waliotaka kutorokea Misri, lakini Isaiya alionya makosa ya hatua hio (Isa. 20: 3-6).Wengine  waliamini nguvu za kuwaokoa. Kwanini, kama wangeimarisha kuta za Yerusalemu, si wangeweza kuwahimili Washuru? Lakini walikuwa wamemsahau Bwana “Muumbaji, hakuna alikuwa na heshima kwake”  (Isa. 22: 8-11). Kundi lingine la watu lilichukua msimamo ulioshindwa tayari na kusema, “ wacha tule na tunywe, kwani kesho tutakufa” (Mst. 12-14). Kundi lingine, likiongoza na Shebna, walikuwa wanajiona wenye haki, wakifikiria kwamba sehemu ya mji iliosalia itakuchuliwa mateka, lakini wao walikuwa wenye haki zaidi na hili halingewatokea (Isa. 22: 15-19). Hatimaye, kulikuwa na wale walio muunga mkono Hezekia na uaminifu wake, kama Eliakimu, ambaye aliahidiwa na Bwana wokovu, sio tu kutoka kwa Washuru lakini nafasi ya kudumu miongoni mwa wana wa Nyumba ya Daudi (Isa. 22: 20-25). Hivyo tuna taswira ya majibu ya watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mgogoro huu.

HOTUBA YA AMIRI YA KUKUFURU (2 Wafalme. 18:17-37)

Senakeribu akatuma  Tatani, Amiri kwenda Yerusalemu kwa jeshi la Washuri (Mst.17). Tizama mahali  walipofika- "mfereji wa birika la juu". Hapo palikuwa mahali ambapo Ahazi, babake hezekia, alikataa ishara ya Mungu, lakini hata hivyo alikuwa amepewa unabii wa ajabu wa (Isa. 7: 3-16.) Hili lilimpa moyo Hezekia kujua kwamba  katika sehemu hii Isaiya alikuwa  ametamka unabii usiobadilika kuhusu Immanuel, “Mungu Yu Pamoja nasi”. Hata hivyo maneno ya  Amiri ya kukufuru yalisikika, na kuleta woga katika nyoyo za watu wa Yerusalemu. Alisifu ushujaa wa Washuru juu ya mataifa Mengine. Je, Mungu wao alikuwa aneweza kuwaokoa? (Mst.19-21, 33-35). Alijaribu kudhoofisha ushirikiano wao na Hezekia kwa kusema kwamba alikuwa amechukua madhabahu ya Bwana na kuanzisha yake Yerusalemu (Mst. 22) Aliwakejeli kwa kusema kwamba jeshi dhaifu la Washuru lingeweza kuharibu jeshi ambalo Hezekia angeweze kukusanya juu ya farasi za Washuru. Alidai kwamba ushindi wake dhidi ya Yuda ulikuwa ni kwa amri ya Mungu (Mst.25) Pengine alikuwa ameelezwa kuhusu unabii wa Isaiya kuhusu kuvamiwa kwa Israeli na Yudah na Washuru (Isa.8 na 10). Lakini unabii huu pia ulitabiri kuangamizwa kwake katika kuta za Yerusalemu (Isa. 10: 24-34).

Hezekia kwa busara akaamuru watu wake kutotamka neno hata moja la kumjibu Amiri (Mst.36) hakukuwa na haja ya kujibu mjinga kwa upumbavu wake, na ingewakatisha watu tamaa zaidi. Jinsi gani Hezekia alikuwa na busara, hata katika wakati huu wa mgogoro.

NJIA YA HEZEKIA KWA YAHWEH (2 Wafalme 19:1-7)

Eliakimu, Shebna na Yoa walimleta Hezekia ripoti ya maneno ya Amiri. Hezekia akaenda kwa hekalu, akaweka jambo hili kwa mikono ya Bwana na akawatuma watumishi wake kwa Isaiya. (Mst.1-2) hezekia alitambua kwamba jambo hili lilikuwa zaidi ya uwezo wake. Aliwaagiza watumishi wake kumwambia Isaiya kuhusu ukufuru wa Amiri. Aliwaagiza Waisraeli kumsihi Mungu ajionyeshe, awakemee Washuru na kuwaokoa wale waliobaki, kwani “ hakuwa na nguvu za kufanya hivi”. Hezekia hakujaribu kutatua jambo hili mwenyewe. Ni mara ngapi tunajaribu kutafuta majibu ya matatizo ambayo  ni wajibu wa Mungu wetu wa Mbiguni? Je tunaweka matumaini yetu kwake ama kwa mkono wa mwili? Ombi la Hezekia halikuwa la bure, kwani Yahweh kupitia Isaiya, akawaambia watumishi wake kwamba  Washuri wote wataangamizwa na kwamba Amiri atakejeliwa katika nchi yake na kuangamia.

UJUMBE WA SENAKERIBU KWA HEZEKIA (2 Waflame 19:8-14)

Amiri alishindwa kuwatisha watu ama kuwavuta kutoka kwa Hezekia na ahadi ya imani na Ustawi (2 Fal. 18: 30-31). Kwa hivyo alitoka Yerusalemu. Lakini hakutosheka kuacha jambo hili. Barua kutoka kwa Sanakerubi ilitumwa kwa Hezekia ikirejelea maneno ya Rabashake ya kumtusi na kuasi dhidi ya Mungu wa Israeli. Tena madai ya kwamba miungu ya mataifa mengine hayawezi kuwaokoa yalitajwa, “Asikundangaye Mungu wako kwa kusema, Yerusalemu haitawekwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru” (Mst.10) Tena Hezekia akamgeukia Mungu kwa faraja na uongozi.

 

MAOMBI YA HEZEKIAH NA MAJIBU YAKE (2 Wafalme 19:15-37).

Maombi ya Hezekia katika mistari 15-19 hutoa mfano mzuri, sio kama mfumo wa maombi ya Mungu. Yeye kwanza anatangaza utukufu na nguvu ya Mungu wake juu ya mataifa na falme zote, kwani wote wamekuja kutoka kwake. Kisha anamsihi Bwana kusikia maneno ya Senakerubi na kuweka Imani yake kwa Mungu na kukataa kwa madai ya Sennakerubi- hakukuwa na Miungu, lakini kazi ya mikono ya binadamu”. Alihitimisha kwa kumsihi Mungu kuhifadhi Israeli- ili “falme zote za dunia zipate kujua kwamba wewe ndiye Bwana Mungu.

Isaiya Nabii kisha akaja  kwa Hezekia akiwa na jibu la kutuliza kutoka kwa Mungu. Hakuwa amesahau maneno ya Senakerubi, na katika mistari wa 20-34 tuna jibu la kina la maombi ya Hezekia. Katika maneno ya kupendeza,yaliyo mwambia Hezekia kwamba Bwana atawaokoa watu wake, kwamba Sennakerubi hatachukua mji na hata pata fursa ya “kurusha mshale kule, ama kufika huko akiwa na ngao, wala kurusha  mshale.......(mst.32) Katika sura ya mwisho, tunaona unabii huu ukitimizwa, kwani malaika ya Bwana  aliwapiga Washuri na ikifikia usiku Senakerubi mwenyewe aliuawa na wanawe katika nchi yake wakati akiabudu katika hekalu la Nisroki, mungu wake. (Mst.35- 37).

Zaburi 46-48 pengine iliandikwa wakati huu. Walielezea shukrani na nafuu kwa kuokolewa na Bwana, na  kutafakari matukio ya tishio la  Mwashuri, Kashfa ya  Amiri na  kuokolewa na  Yerusalemu na Yuda- “ Tumetafakari kuhusu mapenzi yako, ewe Mungu, katikati ya Hekalu lako...” (Zab. 48;9)  kuna marejeleo mengi ya matukio haya katika Zaburi.

Wakati mgogoro kama ule Hezekia alipitia unatufika, tunajibu kama vile Hezekia alijibu? Wakati mgogoro unaisha, tunaonyesha shukrani zetu kwa Bwana, kama alivyofanya kwenye Zaburi hizi? Tunaweza jifunza mengi kutoka kwa maisha ya mfalme huyu mwaminifu.

Hata kama sio sehemu ya somo hili, tunataja kwamba Hezekia alikuwa  mgonjwa hata kufa wakati wa matukio ya 2 Wafalme 19 (matukio mawili yanahusiana na 2 Fal. 20:5-6). Kwa mara nyingine Mungu alimwomkoa na kuumpa miaka mingine kumi na mitano. Imependekezwa kwamba Nyimbo za Zaburi 120-134, zilitungwa kama ukumbusho wa wema wa Mungu. Mada hii ingefanya  utafiti wenye faida kwa kushirikiana na somo hili.


MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Hezekia alichukua jukumu la kuleta mageuzi kwa watu na kuwahamasisha katika njia za Mungu. Tunahitaji kuwa na bidii daima kuhusu mambo ya Baba wetu wa Mbinguni, kwa kushikilia kanuni za kweli, kama Hezekia (1 Tim. 4: 12-16; Tit. 2:. 6-8; 3: 8-9).
  •  Imani yetu lazima iendane na vitendo. Hezekia aliweka imani yake katika Bwana, akaenda kuuimarisha mji. Imani yetu.Hatupaswi kuwa watazamaji tu, lakini "hodari, kupitia Mungu, kwa kuangusha ngome" (2 Kor. 10: 4-5.).
  • Katika wakati wowote wa mgogoro na kesi, tunapaswa, kama Hezekia, kumgeukia Mungu kwanza. Nguvu zake na hekima yake itatuongoza na kutuokoa. (Zab. 127: 1; 1 Kor. 10: 12-13; Rum. 8: 31-39).
  • Dharau ya mjinga kama Amiri ni bora kujibu kwa kuwa kimya. Wenye mzaha hubomoa na kuharibu. Wanataka kudhoofisha imani yetu. Wakati tunapaswa kutoa ushahidi ukweli, lakini hatufai "kumjibu mpumbavu kulingana na upumbavu wake" (Mit. 26: 4; 1 Pet. 2. 21-23).
  • Wakati tunapata ukombozi wa Mungu na uongozi tunapaswa kukumbuka hili katika shukrani, kama vile Hezekia alimsifu Bwana kwa fadhili zake (1 The. 5:18;. Kol. 3:15; Flp. 4:11.).

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 5, Nam.  12, Kur. 188-194; Tol. 6, Nam. 1, Kur. 3-36

"The Ministry of the Prophets" (R. Roberts and C.C. Walker) — Kur. 517-524.

"The Ways of Providence" (R. Roberts) — Kur. 179-181.88

MASWALI YA AYA:

  1. Ni mageuzi gani Hezekia alianzisha Yuda and Yerusalemu?
  2. Kwa jinsi gani Imani ya Hezekia inaonekana katika vitendo wakati wa uvamizi wa Ashuru?

 

Swahili Title
315. HEZEKIA: CHANGAMOTO KUTOKA ASHURU
Sub type
Sub sub type