CSSA 3-3-316 - THE CALL AND MISSION OF JEREMIAH

Swahili

316.    WITO NA KAZI YA YEREMIA

"Neno lako kwangu lilikuwa furaha na shangwe kwa moyo wangu"

Maisha ya nabii Yeremia yanaonyesha mfano wa ajabu wa subura katika kutenda mema. Alikuwa na majukumu makuu na alipitia upizani mkubwa kama kijana mdogo. Hivyo ana zawadi nzuri inayomgonjea katika ufalme. Kwa njia nyingi wizara yake inatabiria uzoefu wa Bwana Yesu Kristo. Majaribio yake yote yakiwa nyuma yake, na matumaini ya ufalme yakiwa mbele yake, sasa mwishowe angeweza kutangaza;

“Ni vyema kwamba binadamu anapaswa kutumaini na kusubiri wokovu wa Bwana.

“Ni vyema kwamba binadamu abebe Nira katika ujana wake (Maombolezo ya Yeremia 3: 26-27).

Lengo letu katika somo hili ni kujifunza kuwa imara wakati tunakumbana na mateso na upinzani kwa kile Mungu amebaini.

HALI YA UFALME WA YUDA

Unabii wa kitumishi wa Yeremia ulianza katika mwaka wa Kumi na Tatu wa Mfalme Yosia na uliendelea kwa miaka arobaini kupitia utawala wa  Yehoahazi, Yehoyakimu, Yekonia na Sedekia (Yer. 1: 1-3.). Ingawa ufalme wa Yuda ulikuwa umefikia kikomo katika mwaka wa 11 wa ufalme wa Sedekia, kazi ya Yeremia iliendelea kati ya  waliobaki katika nchi hata wakati wa kuondoka Misri  (Yer. 40: 2, 4, 6; 43: 7. , 8).

Maisha yake kwa hivyo yalikuwa yamewekwa katika majanga ya siku hizo na si jambo la kushangaza kwamba alijulikana kama nabii wa adhabu. Manabii walitumwa kwenda  kuonya dhidi ya vita, uovu na tauni (28:7-9), kwani Yuda ilikuwa taifa la kiroho na uozo wa madili. Watu wote kuanzia walio juu hadi walio chini na kuweka mioyo.

"Nimeona kwa makuhani wa Yerusalemu jambo  mbaya; walitenda usherati, na walitembea kwa uwongo na  wakaimarika katika  mkono wa watenda dhambi, kwamba  hakuna hata mmoja aliyerudi kutoka kwa uovu wake; wote wamekuwa kama Sodomu kwangu, na wenyeji wa Gomora"(Yer. 23:14).

Haikuwa kwa hiari kwamba Yeremia aliwashtumu watu wa rika yake. Alikuwa anaongozwa na upendo na uaminifu wa Mungu wa Israeli. Haikuwa rajua iliyokuwa tabia ya  mtu huyu, lakini ilikuwa imani ya ajabu na uso wa ujasiri wakati wa upinzani na mateso. Hii inaonekana kama anavyotoa ushahidi kwa Mungu kwa majanga yatakayokuja.

VIJANA WAWILI NA WASHIRIKA WAAMINIFU

Yeremia anatambulika kama “Mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi katika nchi ya Benyamini" (1: 1). Anathothi kilikuwa kijiji kidogo mita tano kaskazini mwa Yerusalemu, iliopewa na Walawi na kabila la Benyamini (Yos. 21:18).  Inaonekana kwamba laini muhimu ya makuhani iliishi katika mji huu, kwani ilikuwa karibu na Yerusalemu na hekalu ambapo walihudumu. Katika 2 Fal. 22: 8 tunajifunza kwamba Hilkia alikuwa kuhani mkuu katika utawala wa Yosia. Yeye anaweza kuwa baba wa Yeremia. Katika maisha ya Yeremia ilibidi kutokea mbele ya Wafalme na wakuu na kazi hii ingekuwa rahisi kama familia yake ingekuwa mashuhuri.

Ilikuwa katika mwaka wa 13 wa utawala wa Yosia na neno la Bwana lilikuwa la kwanza kwa Yeremia. Kutoka 2 Nya. 34: 1-3 tunaweza ngamua kwamba Yosia alikuwa na miaka 21 na hiyo ilikuwa mwaka wake wa kwanza wa mabadiliko.Yeremia alikuwa pia kijana mdogo, kwani katika Yer. 1:6 anaitwa mtoto ( Ebr "nar" = kijana, mtumishi, kijana, kwa mfano Zab. 119: 9). Hivyo katika ufalme wa Yuda kwa wakati huo kulikuwa na vijana wawili walio na roho ya bidii, walioshi kilomita tano kutoka kwa mwengine, na kuna uwezakano kwamba walijuana kwa sababu ya historia za kifamilia. Mungu alikuwa anawapa Yuda nafasi ya mwisho ya kutubu; Nabii na Mflame waliungana katika kujitolea kubadilisha taifa. Katika siku za awali za ufalme wa Samweli nabii-kuhani walishirikiana na mfalme Daudi (1 Nya. 9:22). Sasa mwisho wa Yuda ulipokaribia, ushirikiano sawia wa viongozi waaminifu ulichibuka.

Baadaye hakuna aliyeomboleza kifo cha ghafla cha Yosia kuliko Yeremia (2Nya. 35:25). Alikuwa amepoteza mshiriki mwenye nguvu na mwaminifu ambaye angetarajia msaada wake; hivyo shutma zake ziliweka maisha yake hatarini.

KUJULIKANA NA MUNGU KABLA YA KUZALIWA (Yeremia 1:4-10).

Yeremiah, kama Yosia, ilikuwa "anajulikana" na Mungu kabla ya kuzaliwa (Yer. 1:5, 1 Fal. 13: 2.). Alikuwa chombo kilichotayarishwa na Bwana: “kabla nikuumbe katika tumbo, nilikujua; na kabla uzaliwe nilikutasa na nikakuchagua (Ebr." Nathani "=" alitoa "Isa 9. : 6) wewe nabii wa mataifa”. Yeremia alikuwa kijana mdogo, majukumu na ugumu wa  wito wake ulimfanya kupinga upungufu wake, “Eee, Bwana Mungu! Tizama, siwezi kunena: kwani mimi ni mtoto” (Mst.6) Lakini Mungu hakukubali pingamizi yake: “usiseme wewe bado kijana kwani utakwenda kote nitakako kutuma, na utanena chochote nitakachokuamuru. Lakini usiogope....... kwani niko na wewe na nitakuokoa, akasema Bwana”. (Mst.7-8)  alikuwa kama Musa, ambaye alikuwa mpole na aliyekataa wito na majukumu ambayo Mungu alikuwa amemuita kutekeleza (Kut. 4:10;. 3:12). Bwana alinyoosha mkono wake na kugusa mdomo wa Yeremia na kusema “Tazama nimetia maneno yangu katika kinywa chako." Kama Isaya mbele yake na "nabii kama Musa" watakaokuja baada yake, Yeremia kwa hivyo alitayarishwa kwa kazi yake (Isa 6: 5-7; Kum. 18:.. 15-18).

ISHARA MBILI ZA KUTIA MOYO (Yeremia 1:11-16)

Kama Mungu alimtia moyo Musa kwa kutumia miijiza miwili, sasa alimtia nguvu Yeremia kwa  kutumia maono mawili ya kuvutia. Ya kwanza ilikuwa ile ya fimbo ya mlozi ilifuatiwa na tamko la ajabu, “Nitaharakisha neno langu kufanya hivyo”, Ujumbe wa Mungu unafanywa kuwa wazi wakati tunatambua kwamba neno "mlozi" ni sawa na neno “harakisha” au “tazama”. Mti wa Mlonzi ulikuwa wa kwanza kuchanua wakati miti mingine ilibaki kimya. Wakati wa hukumu ya Yahwe kwa mataifa ulikuwa unakaribia; alikuwa “anawaangalia” au “kuharakisha”  kutimizwa kwa neno lake. Hivyo mti wa mlonzi uliwakilisha kujitolea kwa Bwana katika kutimiza Neno lake, ambalo Yeremia angetamka.

Katika maono ya pili, sufuria iliyotokota ilionekana kwa upande wake ukielekea upande wa kaskazini. Mateso ya kutisha yalikuwa yanatokota kwa Yerusalemu na Yuda. Katika joto la ghadhabu yake, Bwana alikuwa ameunganisha mataifa yote ya kaskazini chini ya bendera ya Wakaldayo na anaenda kumwaga chuki yake juu ya watu wa Yuda. (Mst. 13-16)

Kwa njia hii ya wazi, Yeremia alifurahishwa na nguvu na uharaka wa Neno ambalo Mungu angenena kupitia kwake. Hakukuwa na muda wa kusubiri au kusita. “Kwa hiyo jifunge kiuno na uamke ukanene yote nitakayo kuamuru” (mst.17, Eze. 3: 8-9).

KUWEKWA JUU YA MATAIFA (Yeremiah 1:17-19)

Ujumbe hasa wa Yeremia ulikuwa kuhubiri ujumbe wa hukumu inayokuja juu ya Yuda. Onyo la hukumu inayokuja ilikuwa kazi kuu ya kuhani. Kama Yeremia alivyoelezea, “makuhani waliokuwa mbele yangu na mbele yako walitabiri kuhusu nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, juu ya vita, uovu na tauni (28:7-9. ) Hata hivyo kuna mengi katika sura za Yeremia 52 kuhusu imani na utukufu wa  Yerusalemu katika siku za usoni; lakini haya yangetoa baada ya hukumu. “Tizama”, alisema Mungu, ("nimekuweka juu ya mataifa na juu ya falme, kuongoa, kubomoa, kuharibu na kuangamiza ili kujenga na kupanda (1:10) Hivyo wakati alipokuwa alitangaza kwamba nchi itakuwa na ukiwa, miji ya taka, Yerusalemu bila wakazi (mfano 4: 7; 25: 34-38; 26: 9; 4: 23-31), pia alitabiri  siku ambayo Yerusalemu itachukuliwa na wana wa Daudi wenye haki (23: 5-8; 33: 15-16);  Wakati mataifa yote yatakusanyika (3:17); wakati falme mbili za Israeli zitaungana (3;18;31:1); wakati nchi itarejeshwa na miji kujengwa tena wakati wa shukrani na furaha (30: 11-22; 31: 2-29; 50: 4-5, 19-20, 33-34). Ujumbe wake hivyo ulikuwa na upande mzuri na mbaya.
Kazi yake haikuwa ya Yuda peke yake. “kwa mataifa na falme” Mungu alimchagua, na hivyo tunapata uongozo wa maneno yake “ falme zote za dunia, ambazo zilikuwa kwa uso wa dunia” zimeonyeshwa kwa uovu wao na kuonywa dhidi ya hukumu itakayokuja (1:10; 25: 26-31; Sura. 44-49) katika moja ya tukio Yeremia alituma pingu la kuni kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro kuashiria utumwa wao unaokaribia kwa mfalme wa Babeli (27: 1-8; 28: 12-14). Hata hivyo sura ya 50 na 51 inaelezea kuharibiwa kwa ufalme mkuu wa Babeli.

Kabla  ya siku hizo kuwasili Yeremia alikuwa amewashauri wakaazi wa Yerusalemu kujisalimisha kwa Wakaldayo; hivyo wangesalimisha maisha yao. Kupinga, kwa upande mwingine, hii ingeleta kifo (21: 8-9; 27: 1-8). Tena, aliwatuma wale waliokuwa washachukuliwa mateka, akisema "Ombeni kwa ajili ya amani ya Babeli" (29: 1-7). Bila swali maneno ya Yeremia yalifikia masikio ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Wakati hatimaye Babeli ilichukua Yerusalemu,  wakuu wa Babeli, kwa maagizo ya Nebukadreza walimtafuta  Yeremia. Walimwachilia kutoka gerezani  na vifungo, wakampa kila kitu na hata zawadi (39: 11-14; 40: 1-6). Mfalme wa Yuda alikuwa amemtupa jela na watu walimkataa lakini mfalme mkuu Nebukadreza alitoa amri, "Mchukueni, mtuzeni, na msimdhuru; lakini mtendeeni chochote atakacho waambieni (39:12). Kwa njia za ajabu nabii alijifunza maana ya jina lake “Bwana Huinua”.

 MTUMISHI ALIYETESEKA NA MWENYE HURUMA

Baada ya kifo cha Yosia, maisha yake yalitakana na watu wa mji wake wa Anathothi (11:19); njama ilipangwa dhidi yake (18: 18-23); alidhalilishwa (20:10); kutukanwa na kukejeliwa  siku mzima (20: 7); alitukanwa na  watu kama vile walitukana wale walio kula riba (15:10) akatuhumiwa uwongo (37: 13-15); kuwekwa katika hifadhi (20: 2, 3); kupelekwa mahakamani kwa Ukweli (26: 10-24); kutupwa jela (32: 1-2); na kutolewa akauawe (37:15; 38: 4-5). Katika njia zote hizi alionyesha mfano wa mtumishi wa Bwana anayeteseka atakaye kuja (Yer. 15:15; Isa.52: 13-15).

Hata hivyo Yeremia hakujitukuza juu ya ndugu zake. Licha ya  uchungu wa upinzani aliwaombea mara nyingi (mfano 10: 23-25; 11: 5; 14: 7-9); aliongozwa na huruma kwa sababu ya hatma yao (4:19); na alitamani macho yako kuwa kisima ili aweze kulia kwa sababu ya maafa yanayokuja (9: 1-2; 13:17).  Kwa uzuri  alitabiri roho wa Mungu “ ambaye, wakati alipochukiwa, hakumchukia; wakati aliteseka hakutishia”, na  aliwaongoza wanafunzi wake, “wabariki wale wanao kulaani, watendee mema wale wanaowachukia, waombee wale wanaowatumi na kuwatesa” "(1 Pet. 2:23;. Mat.05:44.).

UJUMBE USIO NA SULUHU

Hata hivyo mtu huyu wa ajabu, ambaye macho yake  yalilia watu wake, hakuwa na suluhu katika ujumbe aliohubiri. Hakukosa kuwaambia  matokeo ya kutisha ya njia zao za uovu. Mafunzo kwetu ni kwamba mapenzi sio kuvumilia tu. Mapenzi ni uvumilivu, “ yanateseka kwa muda mrefu na ni karimu”, lakini wakati  ubaya unaendelea na  maadili kuzorota, basi upendo unatutaka tuchukue msimamo wa Yeremia. Tunapaswa kujishughulisha na mambo ya milele na hatupaswi kukaaa kimya wakati  mambo ya milele ya wale tunaowapenda yanahatarishwa. Inaweza kuleta kashfa kama ile nabii mwaminifu aliyopitia. Hata hivyo,  Mungu  hamtupi mtu milele, maana ajapomhuzunisha atamrehemu kwa kadri ya wingi wa huruma zake. (Omb. 3: 31-32).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Vijana wawe na busara na kuwasikiliza kwa makini wazee waaminifu wanaofundisha Neno la Mungu.
  • Uasi na kutojali katika maisha ya Ekklesia si ya kukabiliwa kwa mshangao.
  • Tunapaswa kushukuru sana kwa wenzatu katika Ukweli.
  • Kujitosheleza kwetu ni kwa ajili ya Mungu ambaye tunaweza kufanya mambo yote (Flp. 4:13.).
  • Wote wanaoishi maisha ya kiMungu katika Kristo Yesu watateseka kwa udhalimu.
  • Upendo wa kweli kwa wafuasi wetu ni mnyenyekevu na mstahimilivu.
  • Kuvumilia maovu siyo upendo.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Prophecy of Jeremiah" (C.C. Walker)

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 6, Nam. 6, 9

MASWALI YA AYA:

  1. Ni ishara gani mbili Yeremia alipewa kuimarisha kazi yake kubwa?
  2.  Kwa njia gani Yeremia alikuwa aina ya Kristo?
  3. Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka katika maisha ya Yeremia?

MASWALI YA INSHA:

  1. Toa Muhtasari wa wito na ujumbe wa Yeremia.
  2. Mateso gani Yeremiah alivumilia? Ni kwa njia gani yeye ni mfano kwetu?
  3. Ujumbe wa Yeremia ulikuwa chanya na hasi. Onyesha kwa kurejea unabii wake.
  4. "Roho wa Kristo alikuwa na manabii" (1 Pet.1:11). Andika insha kuonyesha jinsi hii ilikuwa kweli kwa nabii Yeremia.
  5. Andika kuhusu utafiti wa tabia ya Yeremia.

 

 

Swahili Title
316. WITO NA KAZI YA YEREMIA
Sub type
Sub sub type