317. YOSIA ANASIMAMA KWA UKWELI
" hapakuwa na mfalme mwingine kama yeye mbele yake"
Kifo cha Hezekia kulimfanya mwanawe Manase kuwa ufalme. Utawala wake wa miaka 55 ulikuwa mrefu zaidi wa wafalme wote wa Yuda, lakini ulikuwa na sifa mbaya kwa uovu wake (2 Fal.21:1). Alichukua kiti cha ufalme akiwa na umri wa miaka 12 na aliendeleza ibada ya sanamu,akageuza yale yote mazuri baba yake alikuwa amefanya (2 Fal. 21: 3.). Manase kwa maksudi alitaka kufanya mambo ya kumkasirisha Mungu. Aliweka sanamu kote Yuda na kuongoza watu kutenda maovu kuliko wakanaani halisi. Hata aliweka sanamu ndani ya Hekalu, ambalo Mungu alikuwa amesema, âkatika nyumba hii, nitaweka jina langu mileleâ. Manabii walitangaza hukumu ya Mungu inayokuja dhidi ya Mfalme na watu wake. âchuki ya Mungu ilionekana kwa mauaji ya maelfu ya watu wasio na hatia: âalijaza Yerusalemu na damu yao.â Inapaswa kukumbukwa uovu wa utawala Manase ulibandikwa katika Yuda, kwani baada ya miaka hamsini Wababeli walipingana na Yerusalemu, ilikuwa ni utawala wa Manase ambao ulipata lawama kubwa (2 Fal. 24. 3-4).
Katika miaka ya baadaye Manase alitubu na kujaribu kutengeneza mabaya aliyokuwa ametenda (2 Nya. 33:. 11-17). Lakini haikusaidia chochote. Kwani wakati mwanawe Amon, alifuata njia ovu za babake za hapo awali baada ya miaka miwili Amoni aliuliwa kwa njama. Watu wa nchi waliwauwa waliopanga njama na kumteua Yosia, mwana wa Amon, kama mfalme.
Lengo letu katika somo hili kuhusu Yosia ni kuona haja ya kutekeleaza mageuzi katika maisha yetu wakati neno la Mungu linapoonyesha mapungufu yetu.
2 Wafalme 22 na 23
MZIZI KUTOKA KWA NCHI KAVU
Akiwa na historia kama ile, hadithi ya muhstasari wa maisha ya Yosia ni ya kuvutia: âalifanya yale yaliyo mema machoni pa Bwana, akatembea kwa njia za Daudi babake, asiaguke kwa kuume wala kushoto (2 Nya. 34: 2.).
Ni jambo la kuvutia kuona kutajwa kwa kifungu, âDaudi baba yakeâ kwani ilikuwa kweli alikuwa kwa laini ya Daudi lakini kulikuwa na lengo kubwa zaidi ya hili. Alikuwa âMwana wa Daudiâ kwa sababu alifikiri na kutenda kama Daudi, kinyume na Amon baba yake hasa. Yosia = Yah anasaidiaâ, au âYah huponyaâ, Jina la mama lilikuwa Yedida, maana yake "mpendwa wa Yah", na alitoka Bozkathi, maana âpenye maweâ. Tangu Yosia alikuwa mtu muhimu katika mpango wa Mungu tunaweza kuona katika maelezo haya kivuli cha Mwana mkuu. Maria alikuwa mpendwa wa Bwana na akajifungua mmoja aliyekua kama mzizi kutoka nchi kavu (Lk. 1:30, 32, 38; Isa. 53: 2.).
MWANZO WA HAPO AWALI.
Alikuwa mtoto wa miaka minane tu alipoanza kutawala. Ushawishi wake katika siku hizo za awali haungekuwa na maana yeyeto, lakini akiwa na miaka 16 âalianza kumtafuta Mungu wa Daudiâ na imani yake ikampa motisha wa kutekeleza kazi kubwa za mageuzi. Kile kilichomfanya Yosia kumtafuta Mungu wa baba yake Daudi, wakati taifa lote liliasi? Walikuwa katika wakati ule wakuu kadhaa waaminifu, kama vile Hilkia kuhani mkuu (2 Fal. 22: 8.), Shafani mwandishi (baba wa watoto watatu waaminifu, Yer. 26:24; 29:. 3; 36:10)., Akbori (baba Elnathani jasiri, Yer. 36:12 25), Asaya, mtumishi wa mfalme (2 Fal. 22:12), Maaseya mkuu wa Yerusalemu, na wengine (2 Nya. 34: 8) kulikuwa pia na sauti nabii Yeremia (Yer. 1:2) na Sefania (1: 1), na Hulda nabii (2 Nya. 34:22). Kutoka kwa watu hawa mfalme alipokea ushauri wa njia za Mungu. Akiwa katika miaka yake ya ujana alipata jibu ya swali alilomuuliza Daudi: âkwa njia gani kijana atasafisha njia zake? Kwa kutii na kulifuata neno lako?" (Zab.119: 9).
Kwa sala na kutafakari juu ya Neno alikuja kuona uzuri wa njia za Mungu. Kisha Yosia akatambua kiasi ambacho uovu ulikiwa unatekelezwa katika utawala wake. Hili lilikuwa na adhari kubwa kwa akili ya mfalme yule mchanga. Moyo wake ukawaka moto wa haja ya mageuzi, na akiwa na umri wa miaka 20 alianza kuondoa uasi na kufanya mageuzi (2 Nya. 34: 3).
MAGEUZI YA YOSIA (2 Fal. 23:5-20).
Alianza kwa kuwaondoa makuhani walioabudu sanamu katika Yerusalemu yote na miji ya Yuda. Kisha mfalme akaondoa sanamu katika nyumba ya Bwana and kuzichoma katika katika bonde la Kidroni. Akaiponda hadi kuwa mavumbi, ambayo alitupa kwa makaburi ya wana wa watu (Mst.6). kwa kufanya hivyo alionyesha kwamba ubatili na kifo ndio ungekuwa hatima ya wale wanaoabudu sanamu. Alibomoa nyumba ya Wasodomu (tazama Kum. 23:17).Kisha Mfalme akawapeleka wabomoaji wake katika vijiji vya Yuda. Katika kila mji waliharibu maeneo yote ya juu ya sanamu (Mst.8). Akageuka kwa bonde la Hinomu mahali ambapo watoto walikuwa wametolewa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Moleki na kuharibu madhabahu yake (yaliyoitwa Tofethi) (Mst.10, 2 Fal. 21. 6). Alifanywa hivyo kwa makini, na hakuondoa tu machukizo yaliyokuwa yamewekwa na Amoni na Manase, bali hata yale yalikuwa yamebaki ya utawala wa Mflame Ahazi na Sulemani.
Tamaa ya Yosia ya kumwabudu Mungu kwa kweli ilimpeleka hadi miji ya kaskazini mwa Israeli. Mapenzi yake kwa Bwana na watu wake yalimfanya kufuata malengo yake mbali kwa upande wa kaskazini hadi Naftali. Hakukuwahi kuwa na jaribio la dhati la kuondoa uovu wa sanamu na ushirikina. Yosia mwenyewe alisimamia ile kazi na alirudi Yerusalemu pale tu ilipokamilika (2 Nya. 34:. 3-7). âMTOTO ATAZALIWA- KWA JINA, YOSIAâ. Ya kutilia mkazo ni matendo ya Mflame wakati alienda kwa madhabahu ya Betheli, kilomita 16 kaskazini mwa Yerusalemu. Madhabahu haya yalikuwa na historia ya muhimu. Wakati ufalme uligawanyishwa, Yeroboamu aliweka sanamu, ndama kule Betheli, na hii ikawa chanzo cha uasi katika historia ya makabila kumi(1 Fal. 12: 27-33; Amo. 3:14; 4; 4; kuona. somo la 8) Muda mfupi baadaye, Mungu alituma nabii asiye na jina kutoka Yuda kukemea madhabahu haya na kutangaza maneno haya â Tazama mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, Ataitwa Yosia, na juu yenu atawatoa makuhani wa mahli pa juu na kuchoma ubani juu yenu,na mifupa ya binadamu itachomwa juu yenuâ. Maelezo ya matukio haya yalitolewa katika 1 Fal.13: 1-10. Hii inaonyesha umuhimu wa Yosia katika kusudi la Mungu. Miaka mia tatu na sitini na mfalme mchanga akaharibu madhabu kule Betheli na kuchukua kutoka karibu na makaburi mifupa ya makuhani ambao walikuwa wametolewa hapo awali na kuichoma katika madhabahu (2 Fal. 23. 15-23). Jukumu la Yosia katika kusudi la Mungu lilikuwa kuondoa ibada ya sanamu katika Israeli. Alifanya hivi kwa urefu na upana wa nchi, na hivyo sanamu zilizokuwa zimewekwa katika siku za Sulemani na Yerobaoamu hadi Manase na Amoni zikaharibiwa.
KUREKEBISHA NYUMBA NA KUPATA KITABU CHA SHERIA (2 Nyakati 34:8-33)
Katika mwaka 18 wa utawala wake, wakati mfalme alikuwa na umri wa miaka 26, alianza kurejesha ibada ya kweli. Kundi la watu wanne waaminifu walitumwa kusimamia ukarabati wa nyumba ya Mungu, iligharimiwa na kiasi kikubwa cha fedha ambacho kilikuwa kimetolewa na Israeli na Yuda wakati walipotembelea Hekalu katika miaka ya matengenezo (Mst.8 -9). Mafundi wenye ujuzi waliitikia wito wa mfalme na hesabu ya pesa haikuwekwa kwani waliaminika (2 Fal. 22: 7). Katikati ya matukio haya katika kitabu cha Sheria ya Musa kiligunduliwa (Mst.14 - kiasi). Shafani, mwandishi mwenye busara na mwaminifu, alipeleka hati hizi za dhamani kwa mfalme. Wakati maneno yake ya kutishia hukumu (mfano Law. 26; Kumb 28) yalisomwa mbele ya mfalme, alirarua nguo zake na kulia kwa uchungu. Alitambua jinsi watu walikuwa wamepotoka na akatambua kwamba hukumu ya Mungu inakuja (Mst.9) Punde tu alituma ujumbe kwa Hulda yule nabii. Akabaini kwamba laana iliokuwa imeandikwa kwa kitabu ingekuja kwa taifa, lakini mfalme ataokolewa kwa sababu ya unyenyekevu wake mbele za Mungu (Mst.23-28).
Hivyo uaminifu wa mfalme ukahifadhi kizazi cha Yuda. Hata hivyo kwa yote haya, hawakujibu ndani ya mioyo yao, kwa Yeremia, akitabiri kila mara kuhusu mageuzi ya Yosia, akiwaonyesha kwa nguvu ya njia njia zao ovu (Yer.2:20;. 6:13, 19).
Licha ya hukumu isiyobadilika ambayo ilikuwa imepitishwa kwa taifa kupita Hulda yule nabii, Yosia hakutosheka kukaa tu, baada ya kupata ukombozi wake mwenyewe, na kusubiri kilicho lazima. Kama laana haingezuilika kwa taifa, basi pengine baadhi ya watu wangeokolewa. Aliwakusanya wazee pamoja na kufanya agano jipya na Bwana (2 Nya. 34:. 29-33). Licha ya mfano kitoka kwa mfalme wao, watu hawakuadhiriwa na kile kilichofanyika. Mageuzi yalikuwa ya mda; na sio ya roho: âna pamoja na haya yote dada yake, Yuda mwenye hila hajanirudia kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki anasema Bwanaâ (Yer. 3:10).
PASAKA KUU (2 Nyakati 35:1-19)
Kilele cha kazi ya Yosia ya marekebisho ilikuwa kutayarisha sherehe kuu ya pasaka, sherehe ambayo ilikuwa imesahaulika baada ya miaka ya uasi. Kila kitu kilitayarishwa kwa njia iliofaa- sadaka kulingana na Sheria ya Musa; makuhani, na walawi. Huduma ya Hekalu ilikuwa kulingana na maandishi ya Daudi na Sulemani (Mst. 2-6, 15). Ukubwa wa roho wa mflame uliwaleta wengi kutoka makabila ya kaskazini kwenye sherehe (Mst. 17-18). Kwa amri yake binafsi kila kipengele kilinakiliwa (Mst. 6, 10). Hakukuwahi kuwa na sherehe kubwa zaidi ya Pasaka kama iliokuwa katika mwaka wa 18 wa mfalme Yosia.
MPENDWA WA YUDA (2 Nyakati 35:20-27)
Farao-Neko, mfalme wa Misri, alipitia Israeli akiwa kwa safari yake ya kufanya vita katika Karkemishi karibu na Mto Frati (2 Fal. 23:29). Yosia akaenda Megido kuwapiga Wamisri,lakini alijeruhiwa vibaya na mishale na akarudishwa Yerusalemu. Kule alizikwa katika mazishi yenye huzuni na ya kukumbukwa. Wakati taifa lilikuwa linafikiria kuhusu imani yake kubwa walipatwa na huzuni na majuto. Miaka mingi baadaye nabii Zekaria alitumia tukio hili kuelezea kina cha maombolezo ambacho kitawafika Wayahudi wakati watatambua kwamba walimdunga mwana wa Mungu (Zek.12. 9-14).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Licha ya nyakati ngumu, ni lazima tufanye kazi kwa bidii sawa na Yosia, kuimarisha Ukweli katika siku za mwisho.
- Ni muhimu kuomba na kujifunza Neno la Mungu kama tunataka kuwa vyombo muhimu katika Iklezia.
- Uvumilivu na kujinyima ni muhimu katika maisha ya viongozi wa watu wa Mungu.
- Hatuwezi kumpenda Mungu bila kupenda watu wa Mungu. Moyo wa Yosia ulifikia Israeli yote na alitaka kuleta mageuzi kwa taifa zima.
- Ingawa uaminifu haukubaliwi daima na binaadamu wenzetu, tutalipwa na Kristo katika siku ya ufufuo.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol. 6, Nam. 4
MASWALI YA AYA:
- Je Yosia alifanya nini wakati Kitabu cha Sheria kilipatikana?
- Ni unabii gani ulitimizwa wakati wa mageuzi ya Yosia?
- Kwa nini mabadiliko ya Yosia yalishindwa hatimaye?
- Tunawezaje kuwa kama Yosia leo?
MASWALI YA INSHA:
- Andika akaunti ya mabadiliko ya Yosia.
- Nini lilikuwa kusudi la Mungu katika kumwinua Yosia?
- Toa Muhtasari wa matukio muhimu katika maisha ya Mfalme Yosia.
- Andika kuhusu utafiti wa tabia ya Mfalme Yosia. Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa maisha yake?