CSSA 3-3-320 - DANIEL'S OUTLINE OF WORLD HISTORY

Swahili

320.    MPANGILIO WA DANIELI WA HISTORIA YA DUNIA

"Mungu atamjulisha Mfalme Nebukadzera yatakayo tokea katika siku za baadaye"

Ukweli kwamba Mungu huogoza hatima ya mataifa umeonyeshwa wazi katika ndoto ambayo Mungu alimpa Nebukadreza na tafsiri yake. Kama Nebukadreza aliwaza akiwa kitandani kuhusu hatma, alionyesha kwamba falme za duniani na nguvu zake zitahukumiwa na kunyenyekea chini ya Ufalme wa Mungu.

Utukufu wa binadamu ulionyeshwa kuwa wa muda mfupi. Hata kama Nebukadreza alifikiria mwenyewe kuwa mwamuzi wa hatma yake,  alifanywa kutambua kwamba  yeye alikuwa chombo katika mikono ya Bwana.

Lengo letu katika somo hili  ni kuona kwamba Mungu anajua kila kitu kuanzia mwanzo,na  ana mamlaka ya mambo ya hii dunia, anafanikisha malengo yake.

Daniel 2

 JARIBIO LA MFALME (Danieli 2:1-9)

Nebukadreza alikuwa na wasiwasi wa kile “kingekuja kutokea baadaye” (Mst.29), na Mungu kupitia ndoto alimwonyesha “ kile kitakachotokea siku za baadaye” (Mst.28) Ndoto ilimwacha mfalme akiwa kwa hali ya mshutuko, na kwa woga akawaita washauri wake. Alikuwa amepanga jinsi ya kutatua shida hii. Kuwa hakika kwamba ufumbuzi wake ulikuwa sahihi, alidai maelezo ya ndoto pamoja na maana yake.

Inayojulikana kama hekima ya Dunia ilitupwa kwa  hali ya kuchanganyikiwa na kuomba maelezo kuhusu ndoto. Lakini mfalme alikuwa na moyo mgumu- “najua kwa uhakika kwamba unajaribu kupata muda,kwa sababu unaona neno kutoka kwangu kuwa hakika” (Mst.8).

Kwa kutishiwa na kifo kwa kushindwa, washauri walikabiliwa na mgogoro halisi. Mflame alijua kama miungu ingeweza kuwapa nguvu za kutabiri siku za usoni basi wangeweza kukumbuka kwa urahisi yaliyopita, katika kesi hii ndoto ya Mflame. Walikasirika kwamba mfalme angeweza kufanya ombi kama lile, lakini hili lilidhibitisha uongo wao (Mst. 10, 11).

Mgogoro huu wa mambo ya Mungu ulidhibitisha kwamba “ Hekima ya hii dunia ni upuzi mbele za Mungu" (1 Kor. 3:19; 1:19-29; Isa. 29:14; 44:20, 25; Ayu. 4: 17- 21). Ujio wa baadaye wa Kristo na elimu ya Ukweli itafanya wengi kukubali kwamba “baba zao waliridhi uwongo na ubatili " (Yer.16:19; Zek. 10: 2).

 

KUANGAMIZWA KWA WATU WENYE HEKIMA KUNAAMRIWA (Danieli 2:10-16)

Majibu kwa ombi lake yalimkasirisha Nebukadreza na aliamuru utekelezaji wa haraka wa adhabu kwa watu wenye Hekima. Hii ilihusisha Danieli pia, hata ingawa yeye na marafiki zake watatu hawakuwa wamemaliza miaka yao mitatu ya mafunzo,walihesabiwa katika idadi hio(Taz. 1: 5 na 2: 1). Kutokuwepo wakati wa hukumu kutolewa, walishangazwa na  ziara ya Arioko, mkuu wa polisi. Dhibitisho la Danieli kwamba ange weza kutafsiri ile ndoto ulisababisha mfalme kuruhusu kuongezewa kwa muda, ingawa ombi la hapo awali la Wakaldayo, viongozi wa dini wa Babeli, lilikuwa limekataliwa.(Mst.8)

 

NGUVU ZA MAOMBI (Danieli 2:17-23)

Daniel na wenzake walifanya hitaji lao, shughuli ya maombi ya pamoja (Mst.17). kama Yawheh alivyokuwa amewabariki katika msimamo wao dhidi ya unajisi (1:8-17) kwa hivyo  waliamini kwamba atawaonyesha “ Siri zake kwa watumishi wake nabii” (Amo.3:7) Tunaweza kuwa na ujasiri kama huo katika ahadi ya Mungu kusikia maombi yetu (Mt.7:7) na kuwapa hekima (Zab. 25:14; Yak 1:.. 5). Waliomba kwamba “hawataangamia na watu wale wengine wenye hekima” (Mst 18).

Tena kwa njia ya ndoto (Mst.19), Mungu alimfunulia Danieli ndoto ya Mfalme na utafsiri wake. Punde tu Danieli alijibu kwa sifa, sio tu kwa sababu maisha yake hayakuwa hatarini tena, lakini kwa kuinua jina kuu la Bwana, hekima yake na nguvu katika kutawala ufalme wa binadamu. Hebu tuangalie kwa makini sala hii nzuri.

Mst. 20 “ Na lihimidiwe jina la Mungu”-Danieli alitambua tabia utukufu ya Bwana kama inavyoonyeshwa na Jina lake (Kut.34:. 6-7). "Hekima na uwezo ni wake" -Yahweh ana hekima kutengeneza kusudi Lake na nguvu za kufanikisha kusudi hio (Taz. Yer. 32:15).

Mst.21 “ Yeye hubadili majira na nyakati” – Linganisha “kwa imani tunatambua kwamba miaka imebadilishwa kwa  amri ya Mungu.....”  (Ebr. 11: 3).  Alibadilisha mwendo wa Historia kuingiana na lengo lake (Mdo. 17:26; Zab 75: 2). kuna “nyakati zilizowekwa” (Zab. 102: 13), na sio kwa bahati, lakini katika ratiba ya Mungu ya matukio ya ulimwengu.

“Anaondoa Wafalme na kuwateua wafalme”- Bwana anainua Mataifa na kuyanyenyekeza, akiongoza hatma yao kama Kiongozi mkuu, kwa mfano Nebukadreza "mtumishi wangu" (Yer. 27: 5-7), na Koreshi " Mchungaji wangu....watatenda yote kwa radhi yangu” (Isa. 44: 28-45: 1 tazama pia 1 Sam. 2: 7-8; Ayu. 12: 16-21; Zab. 75: 6-7; 113:. 7-8; Lk. 1: 51-52).. "Yeye huwapa  wenye hekima”- sio hekima ya ulimwengu kama ya Wakaldayo,  lakini wale wanaotafuta hekima ya Mungu kama Sulemani (1 Fal. 04:29; Mit. 2: 6-7; Kum.17: 18-21.).

“Maarifa kwa wale wanoelewa” – “kuelewa” ina wazo la “kutenganisha” au “Kutofautisha”. Hekima itapewa wale wanaoweza kutofautisha ukweli kutoka kwa uwongo (tazama Ebr. 5:14).

Mst.22 “Hufunua mambo ya fumbo na siri”- Haya hayajulikani kwa ulimwengu, lakini hufunuliwa kwa watu kama Yosefu (Mwa. 41:16, 25, 28, 39) na Manabii (Amo. 3: 7).

“Anajua yale yaliyo gizani, na mwanga hukaa kwake”- Yupo kila Mahali (Zab. 139: 11-12; Yer. 23:24..); mfumbuzi wa matendo ya siri (Eze. 8:12; Lk. 12: 2-3; Ebr. 4:13); na katika Mwanga wake ni Uzima (Zab 36: 9; 104:. 2; 1 Tim. 6:16; Yak. 1:17; 1 Yn. 1:5).

Daniel alihisi hisia kuu za shukrani wakati Mungu alimjibu. Alikuwa amejioyesha kama alivyofanya kwa mababu zake siku za awali. Danieli alimwita “Mungu wa Baba zangu” na alimshukuru. Hebu tuwe na shukrani ya maandiko na nguvu za maombi katika maisha yetu.
 

MBELE YA MFALME MKUU (Danieli 2:24-30)

Danieli alipelekwa hadi mbele ya Uwepo wa mfalme,  lakini kabla ya kumwelezea ndoto na utafsiri wake alikuwa makini kuhusisha hekima yake  kwa Mungu wa Mbiguni (Mst.28). Maarifa haya  yalikuwa tofauti na ya washauri wa Mfalme (Mst.27, Taz. Isa. 41: 21-24). Danieli kwa ujasiri alielezea ndoto ile ikizingatia matukio ya  “baadaye”. Kwa kweli kiwango cha upungufu cha utawala wa Babeli ulikuwa umetabiriwa (Isa. 13:19; Yer. 51:37, 43, 58),  na kipengele muhimu zaidi kilibainisha kuanguka kwa Sanamu “katika siku zijazo” (Mst.28).

NDOTO (Danieli 2:31-35)

Danieli alielezea chombo katika ndoto kama sanamu kubwa ya binadamu wa kutisha, sanamu ilikuwa ya vyuma vya dhamani kuanzia kichwa hadi miguu. Jiwe likachongwa hata bila ya kazi ya mikono, likapiga miguu ya ike sanamu na kuifanya kuanguka. Vyuma vilivunjika na kugeuzwa kuwa vumbi, lakini jiwe likakuwa mlima mkubwa ulijaa duniani.

 

UTAFSIRI (Danieli 2:36-45)

1.   UTAWALA WA BABELI.

Ingawa Nebukadreza alikuwa amefikiria kwamba yeye binafsi alikuwa na uongozi wa nguvu zake, Danieli alimfunulia kwamba “Mungu wa mbiguni ndiye alikuwa amempa ufalme, nguvu, na utukufu” (Mst.37) Mungu alikuwa amemfanya mtawala wa mataifa yote (Mst.38, Yer. 27: 4-5.), na kama mfano wa mji wa dhahabu (Isa.13:19; 14: 4.), alielezewa vizuri kama “Kichwa cha dhahabu”. Baadaye alielezewa kama Simba. (7:4)  

2.   UTAWALA YA KIAJEMI

Babeli ilichukuliwa na Darius, Mmedi kwa kushirikiana na Koreshi mjemi katika mwaka 539 Kabla Kristo. Mto Frati uligeuzwa na majeshi ya Darius yakaingia mjini kupitia mkondo wake na Babeli ikaanguka(Dan 5; 45 Isa: 1-3). Hivyo Ufalme wa Babeli uliridhiwa na kifua na mikono ya shaba, ufalme duni wa Wamedi na Waajemi, ulifananishwa na dubu (7:5) na kondoo (8:3). Utukufu wake ulikuwa duni ukilinganishwa na wa Babeli, uliodumu kwa miaka 200

  1. UTAWALA WA KIGIRIKI

Utawala huu wa Medo-Kiajemi uliridhiwa na “ufalme mwingine wa shaba, ambao ulichukua utawala wa dunia yote” (Mst.39) “tumbo na mapaja ya shaba" ni sawa na "chui" wa 7:6 na “beberu” wa 8:5, na jibu kwa himaya ya Kiyunani. Katika vita  viwili vya kupambanua, vya Granicus na Issus katika mwaka wa 334 na 333KK, Aleksanda Mkuu wa Ugiriki aliupindua utawala wa Uajemi na kwa haraka akapanua utawala wake. Maelezo yaliongezewa kuhusu ufalme huu “kutawala ulimwengu mzima” ni kielelezo cha Aleksanda na “Wagiriki wake walifunikwa kwa shaba”, kuushinda upinzani wote, kama hadithi zinavyoelezea, “Alilia kwa sababu hakukua na nchi wa nyingine zaidi ya kunyakua”. Baada ya kifo cha ghafla cha Aleksanda, majenerali wanne wa jeshi lake waligawanya utawala wake Seleukia (shamu), Ptolemy (Misri), Lysimachus (Pergamo) na Kasanda (Makedonia na Ugiriki).

4.    UTAWALA WA ROMA

Pergamo alipewa Roma katika mwaka wa 133 k.k na Filomita. Roma ilichukua fursa hii na kuja Pergamo. Hivyo wakaelekea mashariki, katika  mwaka wa 65 k.k Pompey alielekea kusini na kuteka Uajemeni kwa niaba ya Roma. Hatua kwa hatua Roma iliinuka, na kuwa na “Nguvu kama chuma; maadamu kama chuma inavunjika vipande na kufunika mambo yote; na kama vile chuma inayovunjika itavunja haya yote vipande vipande na kuziharibu" (Mst.40). Makundi ya Warumi yalileta nchi za Uropa, Uigereza na Mesopotamia chini ya miguu yao.  Wayahudi pia walikuwa chini ya utawala wa  Roma  katika wakati wa Kristo (Kum. 28:. 48-57). Lakini moja ya matokeo yenye manufaa ya utawala wa kibeberu wa Roma ilikuwa ujenzi wa barabara katika bara Asia na Ulaya, kuwezesha upanuzi wa injili kwa jina la Kristo aliyefufuka. Dunia iliyojulikana iligeuzwa “kichwa chini” na uwezo wa ujumbe huu (Mdo. 17: 6), na kuacha alama kubwa juu ya watu  kuliko nguvu ya Roma.

Hadi 324 B.K utawala ulikuwa na makao makuu katika Roma, lakini katikati ya wakati huo na 476 B.K (wakati utawala wa magharibi ulianguka), Utawala uligawanyika mara mbili; Roma na Constantinople. Wakristo  walirejelea uasi na kuingiliana katika mfumo huu wa utawala, na kutengeneza  utawala Mtakatifu wa Kirumi, wakati makanisa halisi yaliendelea katika Mashariki au utawala wa Byzantine ulikuwa katikati mwa Constantinople.

Mgawanyiko huu wa kisiasa na baadaye wa kidini unajibu miguu miwili ya picha.

Ni jambo la kuvutia kuona kwamba hakuna utawala wa dunia ambao uliteka Roma. Utawala ulitawanyika: ukagawanyika kwa makundi ya kikabila, mpaka mataifa kumi madongo yakawa msingi wa jumuiya ya mataifa ya Ulaya ya leo.

Falme 10 zinajibu vidole kumi vya picha. Baadhi ya mataifa haya ni dhaifu, mengine yana nguvu, na hii inaonyeshwa na muundo wa miguu na vidole, chuma na udongo (Mst.42). Ukweli ni kwamba chuma na udongo haziwezi kuchanganyika, katika Unabii, kuonyesha ukweli kwamba ingawa mataifa haya yatavutana, hakutakuwa na ushirika wa kweli katikati yao. (Mst.43) Hii inaonekana leo kwamba mataifa yaliyogawanyika ya Ulaya na  utaifa uliopo licha ya jitihada za kuungana.


UFALME WA MUNGU

Mbali na muhtasari wa historia ya dunia,  tunaonyeshwa picha imesimama kwa  miguu yake, ivunjwe vipande vipande na jiwe.  Bado kuna  siku ijayo ya ushirika wa mataifa chini ya mamlaka ya nguvu ya mtu mmoja wa kibeberu, atakayepata ukuu juu ya maeneo yaliyojulikana kama tawala za Babeli, Uajemeni, Ugiriki na Kirumi. Unabii kama vile (Eze. 38; Dan. 11; Yoe. 3; Zek. 14, nk, )pamoja na Dan. 2, zote zinaonyesha nia ya Bwana ya kujisafisha mbele ya macho ya mataifa yote katika kupinduliwa kwa falme za binadamu na hasa, kuharibiwa kwa jumuiya ya Urusi (Eze. 38: 2-7).

Jitu hili linaloogozwa na urusi litaonekana kama  lisilogusika. lakini nguvu zake kama simba, ukali wake kama dubu na mbio zake kama chui, na  tamaa yake ya kutawala dunia  nzima, itagongwa na kuanguka kwa  mkono wa nguvu za jiwe. Atafikia mwisho wake. Atavunjwa “ sio kwa mkono wa binadamu” (Dan. 8:25).

Nani nguvu-za jiwe? Sio mwengine ila Bwana Yesu Kristo. Angalia kwa makini Danieli 2:44 pale ambapo tafsiri imetolewa. Linganisha unabii wa  “Jiwe” ufuatao uliotimizwa na Yesu Kristo:

  • Mchungaji, JIWE la Israeli limefanywa kuwa na nguvu kwa mkono wa Mungu (Mwa. 49:24).
  • JIWE la thamani na msingi la Sayuni (Isa. 28:16.).
  • JIWE la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba zote mbili za Israeli (Isa. 8:14).
  •  JIWE lililokataliwa na binadamu, lakini likachaguliwa na Mungu (Zab. 118:.. 22; 21:42 Mt., Mar. 12:. 10-11; Mdo 4: 11-12).
  • JIWE kuu la Pembeni la Iklezia (1 Pet. 2: 4-8; Efe. 2:.. 20-22).
  • JIWE la kupiga la Ufalme wa Mungu (Mt. 21:. 43-44; taz. Dan. 2:34.).

Jiwe lililochongwa  kutoka kwa mwamba  kwa nguvu za Mungu kubainisha mwangamizi wa sanamu  na mwana wa Mungu ambaye alikuwa "wa pekee wa Baba" (Yn. 1:14;. Lk. 01:35;. Taz. Kut. 20.; 25; Kum. 27: 5., Ebr. 13:10). Ingawa kwa kipengee cha unyenyekevu (Taz. Isa. 53: 2.) Jiwe lingepata ushindi juu ya  aina ya Nguvu kutoka kwa Sanamu. Nguvu za jiwe  zinawakilisha Kristo na watakatifu kama kiini cha ufalme wa Mungu ambaye mataifa yatatawaliwa (2The. 1: 8., Mdo 17:31; Ufu. 11:15). Kiini cha ndoto (Mst.35) kinaelezea vita vya mwisho pale ambapo mataifa yatakuwa kama vile jina linaonyesha “makundi ya maganda katika bonde kwa ajili ya hukumu” (angalia Mic. 4:. 11-13; Yoe. 3: 9- 14; Ufu.. 16:16;. Isa 41:16). Hukumu hii itaendelezwa kote ulimwenguni  kwa sheria ya haki zitokazo Sayuni (Isa. 2:. 2-4).

 

 MAMBO YUNAYOJIFUNZA:

  • Kama Daniel alivyohitimisha, "ndoto ni hakika, na tafsiri yake pia ni thabiti" (Mst.45). Hebu tukiri na Nebukadreza kwamba Mungu wetu ni Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri (Mst.47).
  • Daniel 2 inatupa kipengele muhimu cha kuelewa unabii. Sisi tunaishi katika siku za mwisho za watu wa Mataifa, wakati matukio ya sasa  yanaonyesha usahihi wa neno la unabii.
  • Mungu hivi karibuni atamaliza nyakati za watu wa Mataifa pamoja na ujio mkubwa wa Mwana wake. Ushiriki wetu unahitajika.
  • Tunapaswa tujiandae sasa kwa wakati "ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, utapewa watu watakatifu wa Aliye juu" (Dan. 7:27).

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 6, Nam. 10, Kur. 148-154

"Exposition of Daniel" (J. Thomas)—Sehemu 1-2

"Elpis Israel" (J. Thomas)—Sehemu ya tatu, Sura. 1

"Daniel" (M. Stewart)

MASWALI YA AYA:

  1. Ni mambo gani  tunayojifunza kutokana na mfano wa Danieli wakati maisha ya watu wenye hekima yalitishiwa na Nebukadreza?
  2. Orodhesha umuhimu wa kihistoria wa miguu na vidole vilivyotengenezwa kwa udongo na chuma kwa mfano wa Nebukadneza katika Daniel 2.
  3.  Kwa njia gani Daniel 2 inaonyesha kwamba Mungu anamiliki ufalme wa wanadamu?
  4. Tambua nguvu za jiwe katika Daniel 2 na ueleze lengo lake.
                 

MASWALI YA INSHA:

  1.  Onyesha kutoka kwa hadithi katika Daniel 2 jinsi "Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi" (Yak. 5:16).
  2.  Chora picha ya mfano wa Daniel 2, pamoja na maelezo mafupi kuelezea tafsiri ya maeneo ya picha.
  3. Onyesha jinsi mfano wa Daniel 2 ni muhtasari wa historia ya dunia.

 

 

Swahili Title
320. MPANGILIO WA DANIELI WA HISTORIA YA DUNIA
Sub type
Sub sub type