CSSA 3-3-321 - RESTORATION UNDER CYRUS

Swahili

321.   MAREJESHO CHINI YA KORESHI

"Fahari ya mwisho ya nyumba hii itakuwa kuu kuliko ya kwanza"

Yuda alikuwa imepelekwa uhamishoni Babeli kwa sababu walikuwa wamemwacha Bwana. Uvamizi wa kwanza wa Nebukadreza ulifanyika katika mwaka  wa 606 K.K , katika kipindi cha miaka 3 na 4 cha utawala wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda (2 Fal. 24: 1; Yer. 25: 1). Danieli na wengine wengi walichukuliwa utumwani wakati huu (Dan. 1.1) katika kipindi cha miaka mingi ya utumwa mateka waaminifu walihimizwa na unabii wa Ezekieli na Yeremia ambaye aliwahakikishia kurejea. Yeremia alikuwa amekiri kwa ushujaa kuhusu kuanguka kwa Babeli na pia ukombozi wa Israeli uliofuata (Yer. 50:. 17-20). Alikuwa ametangaza kwamba  uhamisho utachukua miaka 70 pekee (606-536 K.K). Danieli aliishi katika kipindi hiki na alishuhudia kuanguka kwa Babeli na Darius Mmede (Dan 5:. 30-31). Danieli aligundua kwamba  Neno la Mungu lilitaka kukamilishwa kwa utumwa na uharibifu wa Yuda. Alimsihi Mungu ipasavyo kufanya uso wake kung’aa juu ya mahali pake patakatifu ambapo palikuwa na ukiwa (Dan 9: 2, 17).

Lengo letu katika somo hili ni kuona kwamba Mungu huwabariki wale ambao huamka na kufanya kazi katika huduma yake na wale ambao hawakatishwi tamaa na upinzani.

Ezra 1-6; Hagai

AMRI YA KORESHI (Ezra 1)

 Koreshi alitawala pamoja na mjomba wake Dario, Mmedi, kwa miaka miwili. Wakati Dario alikufa, Koreshi Muajemi alitawala juu ya Babeli peke yake na  ilikuwa katika mwaka wa kwanza wa utawala wake pekee ambapo alifanya maamuzi ya muhimu juu ya uhamisho wa Wayahudi kurudi na kujenga hekalu. Historia imerekodi kwamba sera ya Koreshi ilikuwa kuendeleza utaifa kati ya nchi  za utawala wake, na hivyo kuweka amani.  Alidai kuwa ameamriwa na Mungu wa mbiguni kumjengea nyumba katika Yerusalemu. Kwa hiyo aliwaita mateka wayahudi na kuwasihi kurudi. Alirejesha samani ambazo  Nebukadreza alikuwa amechukua, na  akaamuru zirejeshwe katika Hekalu Yerusalemu (Ezr. 1). Karibu watu 50,000 walihusishwa katika urejeshi wa kwanza (2:64-65). Zerubabeli aliteuliwa gavana na Yoshua, kuhani mkuu (3: 2). Maelezo ya ujenzi mpya wa Hekalu, yatapatikana katika sehemu iliobaki ya mafunzo haya, na yatapatikana katika Ezr. 3-6. Baadaye kulikuwa na marejesho ya pili chini ya Ezra, kuhani, katika mwaka wa saba wa Artashasta (Ezra 7-10) na miaka kumi na mitatu baadaye Nehemia alirudi (Neh 1: 1.).
 

MADHABU YANATENGENEZWA NA MISINGI KUWEKWA (Ezra 3)

Ilikuwa ni katika mwezi muhimu wa saba, wakati siku ya Siku ya Upatanisho (siku 10) na Sikukuu ya Vibanda (siku 15-22) ilifanyika (Law. 23:. 27-43), kwamba watu walikusanyika Yerusalemu.Hakuna muda uliopotezwa kuanzisha sheria za sadaka za sheria za Musa. Madhabahu ya Mungu wa Israeli” yalijengwa na sadaka ya kufaa ilifanywa (W. 3-5).  Sikukuu ya Vibanda ingechukua umuhimu mpya. Katika nafasi ya kwanza ni sherehe ya ukombozi wa Bwana kwa Israeli kutoka utumwani Misri. Lakini sasa ukombozi kutoka Babeli ungeongeza maana yake. Katika siku za usoni  sherehe hii ingesherehekewa kwa furaha  kutoka mwaka hadi mwaka ili kuadhimisha ukombozi wa mataifa yote kutoka utawala wa watu (Zek. 14:16).

Katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili wa kazi ya msingi ulianza. Wakati misingi iliwekwa, makuhani wakiwa na tarumbeta na wana wa Asafu, wenye matoazi walimsifu Bwana  kwa huruma yake. Lakini watu hawakuwa na nia moja. Wakati vijana walipiga kelele kwa furaha, wazee walilinganisha misingi na ile ya hekalu la Sulemani na kulia. Haikuwa wazi siku hiyo kama kulikuwa na huzuni au furaha na nabii Zekaria baadaye akawakemea wale ambao walilinganisha kwa maneno,  “ ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo” (Zek. 4:10; Hag. 2: 3).  Hii pia inaweza kuonekana katika kazi ya Mungu katika  dunia ya leo. Wakati moyo unajitolea na una ari ya kazi ya kristo, baraka za baba zitafurika na hata kama waaminifu ni wachache humu duniani. Nani anayedharau siku ya mambo madogo?

UPINZANI — KAZI INASIMAMA (Ezra 4)

Habari za undelezi wa ujenzi ulifikia watu wa sehemu jirani. Walikuwa wana wa mataifa mbalimbali ambao walikuwa wameletwa pale na wafalme wa Ashuru (Mst.2, 2 Fal. 17: 24-41). Ibada yao ilikuwa mchanganyiko wa Ukweli kidogo na  makosa mengi. Walikuja kwa wajenzi na kutoa msaada wao, wakiomba “Tunamtafuta Mungu Wenu”! lakini Yoshua na Zerubabeli walijua kwamba Muungano huu wa pamoja utasababisha kuharibiwa kwa Ukweli, na hivyo walikatazwa kuchanganyikanaa na washirikina. Hivyo walikataa: “Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba: lakini sisi wenyewe tutamjengea BWANA Mungu wa Israeli, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi alivyotuamuru" (Mst.3).

Jibu hili lilileta upinzani ambao hatimaye ulifanya kazi kusimamishwa. Maadui wa Yuda waliwavunja moyo na kuwakwaza watu. Hata pia waliwajiri washauri kuwagawanyisha na kuvunja nia yao. Waliandika barua zilizojaa shutma kwa Ahasuero (Cambyses, mwana wa Koreshi), lakini walishindwa kupata amri ya kifalme kusimamisha kazi. Baadaye, barua nyingine alitumwa kwa Artaxerxes, kuhani wa mataifa ambaye alikuwa amepora kiti cha enzi na alikuwa anachukia Wayahudi. Alikubali matakwa yao na akatoa wito wa kuagiza kusimamishwa kwa ujenzi (Mst. 17-22).  Punde maadui wa Yuda walipopokea jibu, waliharakisha hadi eneo la jengo na kuwalazimisha Wayahudi kusimamisha kazi ya ujenzi.

MANABII WANAWAOKOA (Ezra 5).

Watu walikata tamaa na wakakosa ari ya kazi ile na kurudia kazi zao binafsi. Baraka ya Mugu iliondolewa na  kukawa na mateso. Huu ndio mwanzo  wa unabii wa Hagai. Ilikuwa ni hali hii ambayo manabii Hagai na Zekaria walizungumzia katika maneno yao. Inaonekana kwamba watu walijiondoa katika wajibu wa kazi, kwa sababu wakati haukua umefika wakati  nyumba ya Bwana ingejengwa! Kando na kutabiri miaka sabini ya utumwa  (606-536 KK), Yeremia alikuwa ametangaza kwamba kutakuwa na miaka ya ukiwa, itakayoanza na kuharibiwa kwa Yerusalemu katika mwaka wa 586K.K (2 Fal. 25;. Yer. 25:11.). Hagai aliongea na watu katika mwaka wa pili wa Darius (K.K 520), wakati kulibaki miaka minne zaidi kabla ya ile sabini ya ukiwa kuisha (Ezr 4:24). Hivyo waliomba radhi, lakini mtazamo wao ulikuwa na makosa. Walijishughulisha na mambo yao wenyewe. Kwa hiyo, pia, tunaweza kuanguka kama tutajiingiza katika mambo ya kidunia na kusema ndani ya nyoyo zetu, "Bwana wetu anakawia kuja." (Mt. 24:48).

Hagai aliwahimiza watu kufikiria kuhusu njia zao na akatangaza kwamba majanga yao ya kilimo yalikuwa matokeo ya ulegevu wa kiroho. Lakini kama  wangebadili njia zao, aliwahakikishia kwamba, baraka zingechukua nafasi ya laana (Hag. 1: 7-11; 2: 15-19). Walihimizwa kuchukua hatua. Licha ya uhasama kwa upande wa Tatenai na Shethar-Bozenai, kazi iliendelea: “Jicho la Mungu lilikuwa juu ya viongozi Wayahudi,  kwamba hawakuweza kusababisha wao kusita” (5:5)

Maono ya Zek. 3 ni msingi wa tukio hili. Yoshua, kama kuhani mkuu, anawakilisha taifa la Israeli: “Shetani” ndiye mpinzani; na “Malaika wa Bwana” ndiye “Jicho la Mungu”. Malaika anahalalisha Yoshua lakini analaani wapinzani kwa maneno kwa haya “Mungu anawalaani ninyi”. Katika Yuda 9 tukio hili linarejelewa tena “Mwili wa Musa” ni mabaki yaliyorudi Yuda, “ubatizo katika Musa” (1Kor. 10: 2.).  "Shetani" anawakilisha wapinzani, na “Mikaeli”, Malaika mkuu anatambulika kama malaika wa Bwana, aliyekuweko katika tukio hilo.

Wapinzani waliuliza swali, “Nani amewamuru ninyi kujenga nyumba hii?” Wayahudi walijibu walifanya hivyo kwa amri ya Koreshi na wakapuuza amri ya Artashasta aliyewakataza kujenga. Tatenai, Shethar-Bozenai na wenzake walichukua jambo hili na kumwandikia Darius.  Alidai kwamba  Wayahudi walikuwa wanataka kuasi  kwani waliharakisha ujenzi na hawakutaka kutangaza majina  ya wakuu waliokuwa wakiongoza ujenzi. Wakitilia shaka kwamba Koreshi alikuwa ametoa amri, walipendekeza kwa Daria kuchunguza jambo hili (5: 6-17).

HEKALU INAKAMILIKA (Ezra 6).

Dario alipokea barua na kuidhinisha uchunguzi kudhibitisha kwamba Koreshi alikuwa ametoa amri ya kujenga Hekalu katika Yerusalemu. Kwa neema ya Mungu kumbukumbu sahihi ilipatikana ambapo Koreshi alikuwa ametoa amri na baraka zake (Mst.1-6). Dario alionekana kujawa na ari kama ile ya Koreshi. Aliandika barua ya ajabu kwa “Shetani” wa Yuda akiwa laani. Bwana mwenyewe alikuwa anawa bariki mabaki wake waliokuwa  wanajenga nyumba yake kwa bidii. Kwa njia hii maneno ya Zek. 3: 2, "Bwana anawakaripia ewe, O Shetani", yalitimia.

Dario alimwambia Tatenai na wenzake kusita kupinga ujenzi na kuanza kusaidia! Aliwaambia kwamba gharama ya ujenzi  wa hekalu ingetolewa kutoka kwa kodi za Wasamaria! Isitoshe walikuwa watoe sadaka zote zilizohitajika na Walawi-siku baada ya siku! Alitishia kifo kwa yeyote atakaye taka kupinga amri hio  na kuomba kisasi cha Mungu wa Yerusalemu kwa  yeyote atakaye haribu hekalu! (Mst.6-12).

Wakati barua hii ilipokelewa, wasamaria waoga walijawa na hofu na kuharakisha kukubaliana na amri ya mfalme. Ujenzi, gharama na masharti zilianza kuwasili na kazi  iliendelea hakdi kukamilika katika mwaka wa sita wa Dario (W. 13-15). Ujenzi ulichukua miaka minne (Linganisha 4:24).

Kuna somo katika jambo hili. Wakati Wahayudi walimsahau nyumba ya Mungu waliteseka, lakini walipoirudilia kazi na kushinda pingamizi walibarikiwa zaidi ya matarajio yao. Hivyo pia ni kweli leo, kwani Bwana hajabadilika. Kama sisi “tutasogea karibu naye, atatusongelea pia” Yeye ana “uwezo wa kutenda mambo makuu kuliko yale tuombayo au tuwazayo” (Yak. 4: 8., Efe 3:20.).


 HEKALU KUU IJAYO.

Ujenzi wa hekalu hii katika Yerusalemu ukawa msingi wa unabii uliofika mbali. Yoshua, kwa sababu alikuwa  kuhani mkuu, na Zerubabeli, kwa sababu alikuwa Gavana, ni aina ya Bwana Yesu Kristo (dhibitisha. Zek. 3 na 4). "Atajenga hekalu ya Bwana” na “awe kuhani katika kiti cha enzi”. Ndani yake ofisi za kifalme na kikuhani zitaunganishwa na kutakuwa na umoja kati yake kwa mara ya kwanza katika historia. Zekaria na Hagai, manabii wawili waliongozwa na Roho wa Mungu kuandika mambo ambayo yanaweza kutumika kimamilifu katika siku za Bwana. Kwa kweli Wayahudi walitiwa moyo kufanya kazi kwa sababu walikuwa wanafanya aina ya kazi  ya Messia-hata kama kwa kiwango kidogo. Mungu akawaambia kupitia nabii kwamba nyumba waliomjengea itaharibiwa (Taz. Hag 2:. 6-7; Ebr. 12: 26-27.), lakini akawahakikishia, licha ya hayo, “Atajaza  nyumba HII na utukufu wake” Hekalu la Messia ingekuwa nyumba hio, nyumba yake, hata kama itakuwa nyumba tofauti. “Shaba na dhahabu ni zangu, anasema Mungu wa Majeshi. Utukufu ujao wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko wa kwanza” (Hag. 2:. 8-9). Ukuu wa hekalu la Messia unahusishwa katika  Ezekieli 40-48. Kuna marejeleo mengi kuhusu hekalu kuu ambayo itakuwa “ Nyumba ya sala kwa mataifa yote” (kwa mfano Zek. 14:16; Mk. 11:17; Isa. 56: 7; 2: 1-5; Zab. 122).

Lakini Mungu hana haja na nyumba ya mawe na matofali. Nia yake kamili ni katika moyo wa binadamu. Ni pale tu ambapo Neno lake litachukua mizizi na kuheshimiwa kwa imani na utii wa upendo (Isa. 57:15; 66:.. 1-2; 2 Kor. 6:16; Efe. 3:17.). Tunaweza kuwa hekalu ya Mungu kama tutakubali Ukweli kututakasa na kuelekeza fikra zetu, maneno na matendo yetu. Tunaweza fanya kazi kubwa zaidi kuliko ujenzi hekalu la Zerubabeli.
 

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Mungu anadhibiti madhumuni ya wafalme na hivyo unabii wa miaka sabini ulitimizwa.
  • Mungu atatulaani sisi kama  "tutadharu" kazi ya Ukweli kwa sababu ni ndogo leo - lakini atubariki kama sisi tutainuka na kufanya kazi katika huduma yake.
  •  Wapinzani hawakuweza kusimamisha kazi ya ujenzi na Mungu aliwafanya kulipa kwa ajili ya kazi!
  • Ni Lazima tutakase mioyo yetu kwa kuondoa takataka za tamaa za kishetani na kujenga katika maisha yetu sifa ambazo zinaonyesha kuwa Mungu anakaa ndani yetu. "Hamjui ya kuwa ninyi ni hekalu la Mungu?"

MAKTABA YA KUREJELEA:

"Prophets after the Exile" (J. Carter)

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 7, Nam. 1, 2

"Consider Your Ways" (H.P. Mansfield)

MASWALI YA AYA:

  1.  Elezea jinsi unabii wa Yeremia wa miaka sabini la ukiwa ulitimizwa.
  2. Zekaria alisema, "Ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo?" Alisema hivi wakati gani?Jinsi gani maneno yake yanaweza kutumika leo?
  3. Tunawezaje kujenga "hekalu la Mungu" leo?
     

MASWALI YA AYA:

  1.  Ni mafunzo gani  yanaweza kuchukuliwa kutoka kwa mtazamo wa Wayahudi wakati wa ujenzi wa Hekalu?
  2.  Ni sehemu gani ambayo Zekaria na Hagai walitimiza katika ujenzi wa Hekalu? Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutokana na kazi zao?
  3. Ni matangazo gani matatu makuu yaliontangazwa na mfalme wa Kiajemi ambayo yaliathiri ujenzi wa Hekalu?
  4. Kwa kifupi simulia kazi ya ujenzi wa hekalu chini ya Yoshua na Zerubabeli, Jinsi gani walishinda matatizo yaliyowakumba?

 

Swahili Title
321. MAREJESHO CHINI YA KORESHI
Sub type
Sub sub type