323. MALAKI
"Nani atakayestahimili siku ya kuja kwake?"
Kazi ya kujenga upya hekalu ilikuwa imepokea msukumo kutoka kwa manabii Hagai na Zekaria. Nehemia alikuwa amerudi na kuchukua kazi ya kujenga ukuta. Alibakia Yerusalemu kwa miaka kumi na miwili na kisha akarudi kwa Artashasta (Neh. 13: 6).
Wakati alikuwa mbali uozo wa kiroho ulirudi na kurudi kwake kulileta mwanzo wa mageuzi (Neh. 13.). Matatizo aliokumbana nayo ni yale yaliotajwa katika unabii wa Malaki na inaeleweka kuwa Malaki alitabiri kwa wakati huu.
Lengo letu katika somo hili ni kuona kwamba:
- Mungu anachukia ibada potovu.
- Ndoa nje Ukweli ni dhambi.
-
Hukumu juu ya waovu kwa mara nyingi huchelewa lakini kamwe haisahauliki
Malaki 3
NJIA ZA MALAKI ZA KUANDIKA.
Malaki ilikuwa mtu wa kuvutia na alikuwa na mtazamo tofauti kuhusu unabii alijitahidi kuwakumbusha watu wake majukumu yao. Nabii kwanza hufanya tamko: hili linakumbana na pingamizi kutoka kwa watu, kisha nabii anafumbua dhambi zao.
Kwa mfano, katika 1: 6-7:
- Tamko la nabii: Mwana humtii babake, na mtumishi humtii bwana wake: Basi kama mimi ni baba yenu wapi heshima yangu? Na kama mimi ni Bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi anawauliza ninyi, enyi makuhaniâ.
- Pingamizi la makuhani: âTumelidharau jina lako kwa jinsi gani?â
- Nabii anafumbua dhambi zao: âMnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhababhu yangu.â
Kuna maswali na majibu manane kama haya. Soma unabii huu na utambue maswali na majibu haya: hii itakisaidia kuelewa. Nabii alitumia njia ya mazungumzo kwa sababu ilionyesha wazi mapungufu ya Waisraeli. Hali ya ajabu ilitokea ambapo hawakutambua ukuu wa dhambi zao. Kama Laodikia, âhawakutambua kwambaâ walikuwa âwanyonge, wenye mashaka, maskini, kipofu, na uchi" (Ufu. 3:17) Sio tu kupotoka katika tabia na mazoea yake maouvu, lakini walijifanya kama watu wenye haki. Dhambi inadanganya, na ni tu kwa kijilinganisha sisi wenyewe na viwango vilivyowekwa katika Neno, tunaweza epuka kuanguka katika mtego huo.
WAJUMBE WATANO.
Maana ya jina Malaki ni "Mjumbe Wangu", Kama wengi wa manabii wengine, unabii wake unahusiana na maana ya jina lake.
Wajumbe watano wa Yahweh wamerejelewa katika unabii.
- Nabii mwenyewe (1: 1).
- Makuhani, ambao waliteuliwa kufundisha sheria ya Bwana (2: 7).
- Yohana Mbatizaji, ambaye alikuwa andae njia mbele ya Bwana Yesu Kristo katika ujio wake wa kwanza (3: 1).
- Bwana Yesu Kristo, "mjumbe wa agano" (3: 1).
- Eliya, ambaye atandaa mioyo ya Israeli katika ujio wake wa pili (4: 5-6).
UFISADI WA UKUHANI
Wakati Nehemia alirejea kutoka Babeli alikasirishwa kwa sababu Eliashibu kuhani mkuu alikuwa akishirikiana na Tobia, Mwamoni, na alikuw amempa chumba katika nyumba ya Mungu (2:10 Neh. 13:. 4, 7). Sio hilo tu, lakini mmoja wa wajuu wake alikuwa ameolewa kwa binti wa Sanbalati, Mhoroni. Wanaume hawa wawili walikuwa maadui wa Nehemia na Ukweli. Kwa upotofu wa kiasi hicho katika maeneo ya juu, utawala mzima wa Sheria ulikuwa umeanguka. Zaka hazikupewa Walawi (Neh. 13:10; Taz. Mai 3:.. 8), biashara ilikubaliwa katika siku ya Sabato (Neh. 13: 15-22), na ndoa geni zilikubaliwa (Neh. 13: 23-30, Mai. 2: 14-16).
UKUHANI UNAKEMEWA (Malaki 2:1-9).
Katika Malaki 2 ukuhani unazungumziwa kwa njia ya moja kwa moja, âNa sasa, enyi makuhani, amri hii ni yenuâ (Mst.i) Hivyo, kwa mara ya mwisho kwa miaka 400, makuhani walionywa kuhusu majukumu na wajibu wao. Mungu aliwataka kuchukulia kwa makini maneno yake ya maonyo na hivyo akaendelea kutaja hukumu kama wasipofanya hivyo. Alitishia kugeuza baraka za ukuhani kuwa laana (Mst.2, Kut. 32:29; Kum. 33: 8-11). Hukumu yake ingeleta aibu juu yao- -"Uchafu WAO (sio wake) sikukuu ulienezwa juu ya sura zaoâ, na hatimaye âwangechukuliwa pamoja nayoâ. Hivyo uharibifu wa kutisha wa Yerusalemu uliotokea katika 70 K.K unatishiwa. (Mst.3) Lakini hili halikuwa lengo la kukemea la Bwana. Alitamani kwamba Agano lake lingeendelea kuwa na Walawi. (Mst.4) Mungu anawakumbusha Walawi hali ambayo ilisababisha kuchaguliwa kwao kwa heshima kubwa ya makuhani (Mst.5). Katika matukio mawili imani yao ilikuwa imezidi imani ya mataifa mengine na ari yao ilizawadiwa na ofisi ya juu:
- Wakiwa Sinai wakati wao "Wakiwa na hofu ya " Bwana na kukataa kuabudu ndama wa dhahabu (Kut. 32:. 26-29).
- Wakiwa Shitimu wakati Finehasi mwana wa Eleazeri, kuhani, ilijibu dhidi ya ukahaba wa Israeli katika Baal-Peori, hivyo akapokea ahadi ya amani na ukuhani wa milele (Hes. 25: 10-13).
Katika historia yao, kabila la Walawi walikuwa wameonyesha uaminifu na viogozi wa hapo awali kama (Samueli, Yeremia na Ezra) walikuwa wametoka katika kabila hili. Kama wasemaji wa Mungu walikuwa wameelekeza wengi âkwani maana kinywa cha kuhani kinahifadhi (" walinzi ") maarifa, na wanapaswa kutafuta sheria ya kinywa chakeâ (Mst.7). Lakini walikuwa na uwezo wa kuhimiza utendaji wema, au kufanya tofauti. Hii ilikuwa janga ya siku hio. âNyinyi mmeiacha njia yangu, ninyi mmesababisha wengi kuanguka kwa sheria (kwa maelekezo yako), mmeliharibu agano la Lawi" (Mst.8).
Kuna funzo kali katika hili. Wema ulikuwa umewashindia Walawi fursa kubwa. Upendeleo kwa upande mwingine ulileta hali ya wajibu kwa Mungu, lakini vizazi vilivyofuata vilishindwa kuishi kulingana na mfano wa bababu zao. Hii inatumika leo. Hakuna atakaye ingia katika Ufalme wa Mungu kwa sababu wazazi wao walikuwa Kristadelfiani. Jukumu kubwa liko juu ya watoto kijifunza Ukweli, kujitenga na âkulinda maarifaâ. Hukumu ya kutisha ilikuja juu ya Walawi kwa sababu hawakutii onyo, na wataanguka juu vichwa vya wale walioshindwa kutambua upendeleo wao.
NDOA NA WAGENI INAKATALIWA (Malaki 2:10-16)
Mungu, kwa hekima yake, alifanya sheria kwamba Waisraeli hawapaswi kuoa watu wa mataifa mengine âwatawageuza wana wenu wasinifuate mimi, ili watumikie miungu mingineâ, Alionya (Kum. 7:. 3-4). Katika siku za Malaki hata makuhani walikuwa wamevunja sheria hii na ndoa na mataifa mengine zilikidhiri. Watato waliozaliwa hawakuweza hata kuongea lugha ya Sheria na uasi ulikuwa dhahiri (Neh. 13:24). "Yuda mme unajisi utakatifu wa Bwana... na kuoa mabinti wa mungu mgeniâ (mst.11). Wale walioabudu sanamu walichukuliwa kama wana wa sanamu. Wale wote waliohusika âmabwana na Wasomiâ, wataondolewa licha ya sadaka ya dhabahu (Mst.12).
Ezra hapo awali alihamiza watu kubadilika na kuweka kando wake wao wa kigeni (Ezra 10: 10-13). Sasa tatizo lile lile likatokea âtenaâ katika wakati wa Nehemia (mst. 13). Machozi ya wake maskini ilijaa katika madhabahu ya Bwana, hivyo kwamba hakuweza kukubali sadaka za waume zao. Jambo hili liliwakasirisha waume na wakaleta pingamizi, âkwa nini?â (Mst.14) walikuwa wamepotoka na hawakuona makosa katika matendo yao. Bwana alikuwa ameshuhudia nadhiri za ndoa zao na ibada iliokubalika haingewezekana kwani nadhiri hizi hazikutiliwa maanani. Hakuna umuhimu mdogo unaweza wekwa katika chaguo la mchumba na heshima ya ndoa leo. Ndoa inapaswa kuwa "katika Bwana tu" (1 Kor. 7:39). Kuchagua vinginevyo ni "kunajisi utakatifu wa Bwana." Madhumuni ya ndoa katika Kristo ni "mbegu ya kimungu" inapaswa kulinda (Mst.15)Ndoa za mchanganyiko huzaa matunda ya uasi. âMsifungwe nira pamoja na wasioamini... kwani pana urafiki gani kati ya haki na uasi?â (2 Kor. 6:14). Kidokezo ni âHakunaâ. Zaidi ya hayo, Malaki anaoyesha wazi msimamo wa Mungu kuhusu talaka; âkwani Bwana, Mungu wa Israeli, anasema kwamba anachukua utenganoâ (mst.16)
HUKUMU INAYOKUJA (Malaki 2:17-3:6; 3:14-4:3)
Kwa sababu hukumu ya Mungu haikuwa imekuja kwa wale waliotenda maovu, watu wa siku za Malaki walidhania kwamba juhudi zao za haki hazikuwa na maana. Kwa kweli hawakujishughulisha na Mungu wala njia zake za Haki na hazikuwafunga. Walifanikiwa kwani walikuwa na muda wa kujishughulisha na mambo yao. Hivyo wakasema âKila mtu atendaye maovu ni mzuri mbele ya Bwana, naye hufurahishwa nao" (2:17). Ukosefu kabisa wa hukumu ya haraka na kuzuiwa kwa watenda dhambi uliwafanya kuuliza maswali kama kulikuwa na Mungu mwenye haki- âHukumu ya Mungu iko wapi?â Walikuwa wamekataa kuwepo kwa Mungu na wakasema kama alikuwepo basi maadili yake yalikuwa yameanguka. Haya yalikuwa madai makali sana na Mungu aliwapa jibu la haraka (3: 1-6)
Hata ingawa Mungu hakujitokeza wazi katika hukumu juu ya watenda maovu katika siku za nabii, hii haikumaanisha kwamba alikuwa ameiweka kando. Lengo lake lingejionyesha siku ile walio na haki na wale waovu watapata malipo kwa njia zao. Uovu haungeonekana kama wenye faida (3:14) "Mjumbe wa agano", ambaye walikiri kutafuta, kwa âGhaflaâ angekuja katika hekalu lake, njia yake ikiwa imetayarishwa na mjumbe mwingine, Yohana mbatizaji (3:. 1; Mk. 1: 2-4). Kuja kwake hakukuwa na shaka, kwani kunatajwa mara mbili. Swali muhimu ni, watakuwa tayari?- âlakini nani atasimama siku ya kuja kwake?â Atasafisha kama mtu asafishaye na sabuni dobi, na wote mpaka Walawi, watajaribiwa siku hio, ndani Yake (Yesu), Bwana âatakuwa karibu na hukumuâ na kuwa âshahidi mwepesi" dhidi ya wale wanaotenda maovu (3:5). Kwa kweli walikumbushwa kwamba ni kwa sababu tu ya Agano lake walikuwa wanahifadhiwa (Eze.3: 6; 36: 20-24.).
Kiwango cha dhambi zao kinaweza pimwa na maneno yao katika 3:14-15. Maneno haya ya uasi kwa mara nyingine yalijibiwa na Mungu kwa maneno yaliyobaki. Mabaki ya waaminifu â ambao waliongea na kila mmojaâ kuhusu Ukweli ungechukuliwa na Bwana kama âhazina maalum" (chapa 3:17 ; linganisha 1 Pet.2: 9) na âalimfadhili kama mtu aliyemfadhili mwana wakeâ. Lakini kiburi (4: 1; Taz. 3:15) na wale ambao hufanya maovu âwatakuwa makapi" na "siku ile inayokuja atawachoma..... na haitawacha mzizi wala tawi hata mojaâ.
Leo tunaweza fanya tathmini isiyo sahihi kama vile watu wa siku za Malaki walifanya. Tunaweza fikiria kwamba Mungu ameiwacha ardhi na hajali kama tunafanya mazuri ama maovu. Tunaweza fikiria hivi kwa sababu wale waovu wanaonekana kufaulu na hakumu ya haraka kutoka kwa Mungu. Lakini wakati Bwana Yesu alikuja, hawakuwa wamemtarajia na katika mwaka wa 70 B.K makuhani na mataifa yalihukumiwa. Ishara za nyakati zinatuonyesha â Siku ya Bwana iko karibuâ na ametuonya kwamba â kama mtego itakuja kwa wale wote wanaoishi katika sura ya duniaâ. Tunaweza tu kuwa na uwezo wa âkusimama mbele ya Mwana wa Mtuâ kama â tutakesha na kuomba siku zoteâ (Lk. 21:36).
HAKUNA MAONO YALIYO WAZI.
Baada ya kifo cha Malaki sauti ya manabii ikawa kimya kwa miaka 400. Mika alikuwa ametishia kwamba uovu ulivyoendelea ungeleta âgizaâ juu yao, na âhawatakuwa na maonoâ (Mik. 3: 6; Taz. Amo. 8:11.). katika kipindi hiki, nchi ilikuwa chini wa utawala wa kidunia. Waajemi walishindwa na Wagiriki, ambao waliongozwa na Alexanda Mkuu. Wagiriki walihimiza dini, tabia na lugha yao juu ya ulimwegu walioteka. Hii inaelezea sababu iliofanya lugha ya kigiriki kuzungumzwa sana katika kipindi cha Agano Jipya. Mbeleni wakati wa Agano la kale maandiko yalitafsiriwa katika lugha ya kigiriki na toleo hili hujulikana kama Septuagint. Pamoja na lugha ya kigiriki iliozungumzwa kote, tafsiri hii ilikuwa ya kuendeleza na kuenezwa kwa injili dunia.
Ukandamizaji wa ibada ya Bwana na Wagiriki, hasa Antioko Epifania, ulifuatia uasi wa moja kwa moja ukiongozwa na Wamakabayo. Katika 165 K.K Yuda Makabayo alinyakua Yerusalemu, akasafisha hekalu na kuitakasa tena. (Sikukuu katika Yohana 10:22. Alikumbuka tukio hili.) Uhuru ulifurahikiwa kwa miaka 100 kama watu wa familia ya Wamakabayo ilivyotawala. Warumi kisha wakaenda Palestina katika K.K 66 wakiongozwa na generali mzuri Pompei. Yulio Kaisari, generali wa Kirumi na mpinzani wake, alipata ushindi dhidi ya Pompei na alisaidiwa na Antipateri, Muidume. Kwa msaada wake Antipateri alizawadiwa kwa kupewa uongozi wa Yudea. Kufuatia Waparthi wakachukua Yerusalemu na kumweka Antigonus, Mmakabayo, juu ya kiti cha enzi. Baadaye Herode mkuu, kwa msaada wa Warumi, alichukua Yerusalemu na alifanywa âMfalme wa Wayahudiâ. Alimuua Antigonia na akaoa wake kumi akiwemo mariamne, Mkabayo. Alikuwa na tuhuma na uchungu na akamuua Mariamne na wana wake. Alianza kujenga hekalu na pia Kaisarea, kwa heshima ya Kaisari Augusto (Lk. 2: 1). Wakati wa kuzaliwa kwa Kristo ilikuwa ni yeye aliyewaangamiza watoto wa Kibethlehemu. Baadaye ufalme wake uligawanyika kati ya wana wake watatu, Arkelio alipokea uongozi wa sehemu ya nnne ya Yudea. Ilikuwa ni baada ya kifo chake ambapo Kristo na Wazazi wake walirudi kutoka Misri (2 Mat: 1, 16, 22.).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Malaki aliwakemea makuhani kwa ajili ya ukosefu wao wa ujuzi na kushindwa kufundisha na kutekeleza Ukweli. Kutofautiana na kutojali kwa upande wa vijana, wa Kristadelfiani kutaleta hukumu hiyo.
- Ndoa nje ya Kristo ni uvunjaji wa amri na unasitisha kusudi la Mungu la kuhifadhi "mbegu takatifu".
- Viapo vya ndoa vinapaswa kudumishwa wakati bora au mbaya. Mungu "anachukia" talaka.
- Mpenzi wetu wa ndoa hivyo lazima achaguliwe kwa uangalifu na kwa kipindi cha muda.
-
Ingawa waovu wanaweza kufanikiwa, ni kwa muda tu. Mungu hajapuuzilia hukumu lakini ameihirisha tu. Mjumbe wa agano atakuja kwa ghafla na sisi tunapaswa kukesha na kuomba daima ili tupate kuwa wastahilivu na tuweze kutoroka hukumu juu ya waovu (Zab. 37:1-3; Zab. 73; Lk. 21:36.).
MAKTABA YA KUREJELEA:
"Prophets After the Exile" (J. Carter)
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol.7, Nam. 9, 10
"Malachi" (J. Ullman)âC.S.S.S. Notes
MASWALI YA AYA:
- Ndoa za mchanganyiko zilikuwa nyingi katika siku za Nehemia. Kwa nini ni muhimu sisi kuchagua mchumba kwa Haki?
- Kwa nini Walawi walichaguliwa kuwa Makuhani? Je, ni majukumu gani walikuwa nayo?
- Orodhesha mfululizo wa utawala ambao ulitawala Palestina kutoka siku za Nehemia hadi kuzaliwa kwa Kristo.
-
Katika nyakati za Malaki watu alisema, "Mungu wa hukumu yuko wapi?" Je, nini maana yake? Jibu la Malaki lilikuwa lipi?
MASWALI YA INSHA:
- Ni wajumbe gani watano wanaotajwa katika unabii wa Malaki? Orodhesha majukumu yao.
- Ni dhambi gani za watu ambazo Malaki alikaripia? Ni mambo gani tunaweza kujifunza kutoka kukaripia kwake?
- Kwa jinsi gani hali ya kutojali iliwekwa wazi wakati Nehemia alirudi Yerusalemu? Alifanya nini kubadilisha hali hii?
- Malaki alisema nini kuhusu ndoa za Wayahudi wa siku zake?
- Ni mambo gani sisi tunajifunza kutoka kwa Malaki ambayo ni kweli kuhusu ndoa za leo?
SEHEMU YA 4: MESSIAH ANAWASILI
Baada ya kufariki kwa Malaki, jua lilikuwa limezama kwa manabii. Miaka mia nne ya giza ilitanda juu ya ulimwengu, lakini Mungu hakuwa amelala. Mungu Alikuwaanatayarisha ulimwengu kwa ajili ya tukio kubwa katika historia yake.
Roma ilikuwa imenyakuwa kwa upana na umbali. Sheria ya Warumi ilihakikisha imani na barabara nzuri za kusafiria. Utamaduni na lugha ya Kigiriki zilikuwa zimetumika katika tafsiri ya Maandiko ya Kiebrania katika Kigiriki na kuupa upana neno la Mungu. Kwa wote ila wanafunzi wachache wa Neno la Mungu, dunia bila kujua walisubiri kwa ajili ya kuja kwa mwanga wa kweli ambayo kazi ingewatuma wafuasi wake mpaka pembe zenye giza za dunia kutangaza mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu.
Kisha malaika Gabrieli akatokea- kwanza kwa Zekaria katika hekalu, kisha kwa Maria katika mji wa Galilee ulioitwa Nazarethi. Malaika akawafunilia baadhi ya wachungaji wa Bethlehemu: âkwenyu nyinyi leo amezaliwa katika mji wa Daudi, Mwokozi, ambaye ni Kristo Bwanaâ. Umri mpya ulikuwa umeanza. Matumaini ya manabii yalikuwa yamewasili, Mesia alikuwa amefika.