325. KUZALIWA KWA YESU
"Kiumbe mtakatifu atakayezaliwa na wewe ataitwa Mwana wa Mungu"
Somo hili limeandikwa kuhusu tukio kuu zaidi katika historia kufikia wakati huo. Kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu kulifikisha kikomo ahadi ya kwamba mwokozi angekuja. Huyu ndiye angeleta baraka za Mungu kwa mataifa yote. Dunia iliyolaaniwa kama adhabu ya dhambi hatimaye itatukuzwa na binadamu kurejeshwa kwa neema ya Mungu.
Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi unabii ulivyotimizwa katika kuzaliwa kwa Yesu, na kutafakari hali ya unyenyekevu iliozunguka kuzaliwa kwake.
Mathayo 1, Luka 1: 26-38; 2: 1-10
NENO LIKAWA MWILI.
Mpango wa Mungu tangu mwanzo ulikuwa kujaza ulimwengu na heshima na utukufu wake. Hii ilikuwa imetajwa kuanzia mwanzo wakati alimwahidi binadamu utawala juu ya mambo yote. Dhambi iliharibu nia hii ya hapo awali na kuleta kifo duniani (Rom. 5:12). Lakini Mungu alikusudia kuharibu dhambi na kumpa binadamu aliyeanguka mkombozi. Hili liliwekwa wazi katika kulaaniwa kwa nyoka - mbegu ya mwanamke âatakuponda kichwa chakoâ (Mwa. 3:15). Pia , utoaji wa "mavazi ya ngozi" kama kufuniko cha dhambi ilikuwa utabiri wa Yesu-â Mwana-kondoo aliyechinjwa tangu mwanzo wa ulimwengu" (Mwa 3:21; Ufu. 13: 8).
Agano la Kale limejaa ujumbe wa Messia na Agano Jipya linadhibitisha agano hili hivyo maandiko yote yanaungana ndani yake.
Tangu mwanzo tunaona kwamba maisha hasa ya watu yamechukuliwa na Mungu mpaka yenyewe ni mifano ya Messia(Mf.Yosefu) Musa akawapa Sheria, ambayo katika maelezo na ibada zake ilitangaza kwamba mwokozi alikuwa anakuja. Na hivyo mengi katika maisha yake yalikuwa kama Yesuâ, kwamba Mungu alitangaza kwamba atamwinua nabii kama Musa (Kum. 18:18; Mdo. 3:23).
Kabla ya sheria, kuja kwa yesu kulikuweko katika ahadi zilizofanywa kwa baba Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Waliambiwa kwamba katika uzao wao mataifa yote yatabarikiwa na uzao wao utaridhi nchi milele (Mwa. 13: 15-16). Baadaye Daudi aliahidiwa mwana, ambaye pia yeye angekuwa Mwana wa Mungu. Sio tu angekuwa Mwokozi bali Mfalme, atakaye tawala akiwa juu ya kiti cha Daudi katika Yerusalemu milele (2 Sam 7:. 12-16). Zaburi na Manabii walifafanua ahadi na kutoa maelezo zaidi ya maisha na huduma ya Massia (Angalia somo la 3) Injili imeandika habari au injili ya Mflame-mwokozi, lakini ili kumtambua wakati wa kuzaliwa kwake, marejeleo yanatajwa ya ukoo wake kutoka kwa Ibrahimu na Daudi (Mt.1: 1; Lk. 1: 32-33, 54-55, 69-73).
GABRIELI ANAMTEMBELEA MARIAMU (Luka 1:26-38)
Miezi sita baada ya Gabrieli kumtokea Zekaria, alitumwa na Mungu kwenda Nazarethi kwa Mariamu. Nazarethi ilikuwa katika Galilee iliodharauliwa karibu na ukingo wenye mwinuko juu ya tambarare la Esdraeloni. Mariamu alikuwa Bikra aliyeposwa na Yusufu, wa kabila ya Yuda. Maandiko yanaelezea wazi kwamba Massia angekuwa Mwana wa Mungu na mwana wa Daudi (2 Sam 7: 12-16). Aidha, mtoto atazaliwa na mimba ya Mungu, kwani Isaiya alikuwa ametabiri kwamba bikra atapata mimba na kujifungua kijana, ambaye jina lake ataitwa "Immanuel", au "Mungu pamoja nasi" (Isa. 7:14). Baadaye katika Utabiri wa Immanuel ( Isa 7-12) maneno muhimu ya ahadi yanapatikana âKwetu sisi mtoto amezaliwa, kwetu sisi mtoto ametolewaâ (9:6) Kwa njia hii Mungu alimtoa mmoja yule aliyekuwa na nguvu za kushinda dhambi. Mwana wa Mungu, kwa hivyo ikafanya hali ya kutofanya dhambi kuwezekana lakini sio lazima. Kwa hivyo Mungu atakuwa mwokozi wa Binadamu na utukufu na sifa zote zitakuwa zake.
Wanawake waaminifu wa Israeli walijua kwamba Messia âangezaliwa na mwanamkeâ na walitamani kuchaguliwa kwa heshima hii. Gabrieli alimtokea Mariamu pekee na kumwamkua, Salamu, ewe uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe: umebarikiwa kuliko wanawake woteâ (Mst.28) Mariamu alifadahika na kuwaza ni kwa jinsi gani alikuwa amebarikiwa kuliko wanawake wote. Alipowaza haya, malaika akamwelezea âUsiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kutoka kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba, na kuzaa mtoto wa kiume, nawe utaitwa Yesuâ.
Ili kubainisha zaidi heshima yake kama âmtumishi wa Bwanaâ (Mst.38) na mama ya Masiya, Gabrieli alimfunulia huduma ya baadaye ya mwanawe. Angekuwa mwana wa Mungu na Mwana wa Daudi na angetawala juu ya makabila ya Yakobo kutoka Yerusalemu (Mst. 32-33) Haya yalikuwa maneno ya kawaida na yaliweka wazi kwamba atakuwa mama wa Masiya. Lakini hakuelewa kwa njia gani hili lingetendeka, kwani hakuwa mwanamke aliyeolewa. Hakutambua kwa njia gani Masiya angekuwa âMwana wa aliye Mkuu zaidiâ. Gabrieli alimwelezea kwamba nguvu za kipekee za Mungu, Roho Mtakatifu, zingeshuka kwake, na kwa njia ya miujiza atapata mimba na hivyo mtoto mtakatifu atakuwa Mwana wa Mungu (Mst.35).
Ebu tafakari jinsi fikra za Mariamu zilivyozunguka akijaribu kufahamu ukuu wa neema hii. Unabii ulipita akilini mwake jinsi alikuwa anatambua kwamba angekuwa na jukumu muhimu katika nia ya Kimungu. Ili kumpa sababu ya kuamini, Gabrieli alimkumbusha kushika mimba kwa Elisabethi katika umri wake mzee na kisha akatangaza kwamba â hakuna kisichowezekana kwa Munguâ (Mst.37) Maneno haya yalikuwa ya muhimu kwani yalinenwa kwa mara ya kwanza na malaika kwa Sara wakati alipotia shaka kwamba atapata mimba kulingana na ahadi (Mwa 18:14). Mariamu akajibu, "Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosemaâ. Kauli hii ya kukubali, kufuatia malelezo ya malaika kwamba mtoto atazaliwa nje ya ndoa, inaonyesha kwamba alikuwa amekubali kubeba kauli ya kutokuwa mwaminifu.
Gabrieli alimwacha peke yake akiwa na mawazo mengi ya kutatanisha. Jinsi alivyopata ufahamu wa neema na jukumu alilopewa alipata tamaa ya kujiweka katika mikono ya Mungu. Hii pia iliamsha tamaa ya kutafuta tumaini kwa moyo wa kuelewa. Ni kwa nani angeeda? Elisabethi, binamu yake mkubwa, alikuwa anafurahia matarajio ya kupata mwana. Hivyo Mariamu akaondoka kwa haraka akielekea mlima wa nchi ya Yudea na kule wanawake hawa wawili waliobarikiwa walizungumzia juu ya nguvu za Mungu, na kutafakari kuhusu kazi kuu ambayo Mungu alikuwa tayari kutenda kupitia mjumbe na Mwokozi(Mst.39-55). Baada ya miezi mitatu mariamu akarudi nyumbani. Yosefu alikabiliwa na changamoto ya hali hii. Alichanganyikiwa kati ya heshima yake kwani hangekubali kuvumilia uhusiano huo, na mapenzi yake kwake; na akaamua kumficha mbali ili kuepuka aibu ya umma (Mt.1:19). Usingizi wake ulio na wasiwasi ulitembelewa na mgeni kutoka mbiguni: âYosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa maana Mimba yake ni ya Roho Mtakatifuâ. Ujumbe wa Mungu ungetenda zaidi ya kurudisha umoja na upendo, ungeleta heshima kubwa kwa Yosefu pamoja na jukumu la mwanaume kumsaidia na kumlinda katika nyakati ngumu zilizokuwa mbele yao.
JINA NA HUDUMA(Mathayo 1:21).
Yosefu pia aliambiwa kwamba jina la mtoto litakuwa â Yesu, kwani atawaokoa watu kutoka kwenye dhambi zaoâ. Yesu anahusishwa na maneno mawili, âBwanaâ na âWokovuâ. "Yesu" ni sawa jina la Kigiriki "Yoshua" (linganisha na Mdo 7:45; Ebr. 4: 8.), Au "Jehoshua" (Hes. 13:16.). Hivyo alikuwa awe na jina la Mwisraeli mashuhuri, ambaye huduma yake ilifanana na yake. Yoshua alisababisha watu kuridhi nchi. Vile vile, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akamwezesha kuharibu adui wa dhambi. Hivyo njia ya uridhi wa milele katika Bwana umefunguliwa kwa wale wanaomwamini (Isa 49:. 6; 2 Kor. 5:. 19-21; Mdo 2:38).
MWOKOZI ANAZALIWA (Luka 2:1-7).
Amri ya Kaisari Agostino kwamba sensa ifanyike katika Israeli kwa lengo la kutoza watu kodi katika siku za usoni ilikuwa ifanyike nchi nzima. Amri ilihaji kila mtu kwenda hadi mahali alipozaliwa kujisajilisha. Hivyo Yosefu na Mariamu walipatwa na safari ndefu na yenye hatari katika wakati huu muhimu.Mariamu bila shaka angejua, kama vile waandishi walijua, kwamba Masiya alikuwa amezaliwa Bethlehemu (Mik. 5: 2., Yn. 07:42.). Jinsi gani unabii huu ungetimia? Maelezo yalikuja kwa njia ya ajabu- lazima angeenda Bethlehemu katika wakati sahihi na ule alipaswa kujifungua mwanawe kwa kufuata kile kilichoonekana kama matakwa ya kisheria ya kibinadamu. Njia za Mungu ni za kushangaza. Kwa kweli anatawala ufalme wa binadamu. Neno lake ni la uhakika.
Safari ilikuwa ngumu na ndefu na walisafiri polepole. Mariamu alikuwa na ufahamu wa jinsi tukio kubwa lilivyokaribia na hili lilikuwa limemjaa mawazoni mwake na sala zake katika miezi iliopita. Lakini, ole wao walipowasili Bethlehemu hawakuweza kupata mahali pa malazi na wakati wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Hakukuwa na chumba katika nyumba ya wageni. Hali ya Mariamu ilikuwa wazi kwa wakazi wengi wa Bethlehemu. Hata hivyo hakukuwa na hata mmoja aliyetoa chumba cha kumpokea. Ilikuwa ishara ya ujio wa Masihi ambaye âAlikuja kwa watu wake na watu wake hawakumpokeaâ (Yn. 1:11).kile walichopata ni zizi la ngombe lililojaa harufu. Pale Mariamu alijifungua mtoto wake wa Kwanza.
Pale kwenye kiza cha usiku kilio kidogo cha mtoto kilichochanganyika na sauti za punda na ngamia kilisikika. Katika mji ambao Mungu alikuwa amemchangua na kumteua Daudi kama Mfalme wa Isaeli, Mwana Mkuu wa Daudi alizaliwa.
Mariamu akamlaza horini. Hapa kuna mazingira ya unyenyekevu , zizi katili, Yesu anapewa sifa na kutukuzwa, akaanza maisha yake- â yeye.....amewatukuza wale wa kiwango cha chiniâ (Lk 1:52.). "Mungu amechagua mambo yaliyo dhaifu ili awaibishe wale wenye nguvu, na vitu vilivyo chini vya dunia, na mambo yaliyodharauliwa, ili avibatilishe vile vyenye nguvuâ (1 Kor. 1:27). Hata hivyo, leo, Ukweli na wale wanaofuata, wamedharauliwa. Lakini siku itakuja hivi karibuni wakati watatukuzwa! "Ni nani anayedharau siku ya mambo madogo?" (Zek. 4:10). Hili ni somo pale horini.
WACHUNGAJI MALISHONI (Luka 2:8-20).
Usiku huo malaika wa Mungu akatokea kwa utukufu kwa wachungaji wakiwa malishoni karibuni. Hofu yao haikuwa inafaa, hasa katika habari za furaha kwa wanadamu ambazo malaika alikuwa amekuja kutangaza. Malaika akasema, âUsiogope, kwa maana, nawaletea habari njema za furaha kuu, ambayo itakuwa kwa watu wote. Kwa maani kwenu nyinyi katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi, ambaye ni Kristo Bwana." (mst. 10-11). Katika maneno haya kuna kiini cha baadhi ya unabii muhimu wa Kimasihi.
- Neno "amezaliwa" limetoka Isaiya 9: 6.
- "Mwokozi" anatimiza maazimio ya Mungu ya nia yake ya kutoa wokovu kupitia kwa mtumishi wake (Isa.45: 21; 49: 6; 53: 11-12).
- "Ambaye ni Kristo" au Masihi inaonekana kuandikwa katika Zab. 2: 2-7, ambapo Mungu anasema kwamba Mwana wake atakuwa Mteuliwa.
- "Bwana" anasikika katika Zab. 110: 1, ambayo Daudi anakubali kwamba mwanawe pia ni Bwana wake.
Baadaye, kufuatia ufufuo ya Bwana, Petro alikusanya kutoka kwa Zaburi jina jipya la wokovu ambapo kila binadamu lazima abatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi - Bwana Yesu Kristo (Mdo 2: 34-38).
Kama ishara ya ukweli wa maneno yake, malaika aliwaambia wachungaji kwamba watampata mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini. Ilikuwa ni wakati huo ambapo mbigu ilingaa kwa utukufu wa malaika na sifa kwa Mungu. Umuhimu wa kuzaliwa kwa mwana wa aliye mkuu umeelezewa kwa maneno haya âUtukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa ukarimu kwa watu". Katika maneno haya kuna maelezo. Binadamu lazima kwanza atukuze Mungu, kama atataka kupokea âamani na ukarimu". Mungu anatukuzwa wakati sisi tunafanya kulingana na mapenzi yake katika toba, kukiri na ubatizo. Kisha anatupa amani na furaha, katika ondoleo la dhambi (Rum 4:20; 5: 1.). Wachungaji walienda Bethlehemu na wakakuta kila kitu hasa kama vile malaika alivyosema. Walirudia maneno ya malaika na kuwashangaza wote waliokuweko na wakarudi kwa mifugo wao wakiwa wamejaa sifa za Mungu vinywani mwao.
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Maandiko ya Unabii wa ujio wa kwanza wa Kristo yalitimizwa yote, na hivyo tunaweza amini unabii unaohusiana na ujio wake wa pili.
- Mungu alimchagua Mariamu kwa heshima ya kuwa mama wa Mwana wake. Tangu ujana wake alikuwa na upendo wa Mungu na maendeleo ya imani ambayo yalimwezesha kumwongoza mtoto wake katika kila njia za Mungu.
- Kwa udhibiti wa ajabu wa taasisi ya juu ya binadamu Mungu aliwezesha unabii wa Mika kuhusu kuzaliwa kwa Masihi katika Bethlehem kutimizwa.
- Yesu, mkuu zaidi, alizaliwa katika mazingira nyenyekevu. Somo kwa ajili yetu ni kwamba njia za kifahari za mwili hazina maana yoyote. Kama sisi tutajinyenyekeza, Mungu atakuwa radhi kwa kutuonyesha huruma.
MAKTABA YA KUREJELEA
"Life of Jesus" (M. Purkis)â Sura 1
"Nazareth Revisited" (R. Roberts)â Sura 6, 7, 8
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol. 8, Nam. 1, 2
MASWALI YA AYA:
- Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa mazingira ya kuzaliwa kwa Yesu?
- Nini kilisemwa na malaika kwa wachungaji wakati Yesu alizaliwa?
- Ni nini maana ya maneno haya?
- Ni nini maana ya jina, "Bwana Yesu Kristo"?
- Mika alitangaza kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu. Jinsi gani unabii huu wa ajabu ulitimia?
- Majibu ya Mariamu yalikuwa yapi kwa manenoo ya Gabrieli.
MASWALI YA INSHA:
- Kwa njia gani kuzaliwa kwa Yesu kulithibitisha Agano la Kale?
- Kwa kifupi toa muhtasari wa matukio yanayozunguka kuzaliwa kwa Yesu.
- Andika insha juu ya wahusika, Mariamu na Yusufu kama ilivyobainishwa hadi kuzaliwa kwa Yesu.
KIELEZO
|
KITABU |
UFUPISHO |
|
AGANO LA KALE |
|
|
MWANZO |
Mwa. |
|
KUTOKA |
Kut. |
|
MAMBO YA WALAWI |
Law. |
|
HESABU |
Hes. |
|
KUMBUKUMBU LA TORATI |
Kum. |
|
WAAMUZI |
Amu. |
|
YOSHUA |
Yos. |
|
HOSEA |
Hos. |
|
SAMWELI |
Sam. |
|
AYUB |
Ayu. |
|
ISAYA |
Isa. |
|
WAFALME |
Fal. |
|
MAMBO YA NYAKATI |
Nya. |
|
NEHEMIA |
Neh. |
|
ZABURI |
Zab. |
|
DANIELI |
Dan. |
|
YOELI |
Yoe. |
|
MITHALI |
Mit. |
|
MHUBIRI |
Mhu. |
|
MIKA |
Mik. |
|
YEREMIA |
Yer. |
|
EZEKIELI |
Eze. |
|
HAGAI |
Hag. |
|
MALAKI |
Mal. |
|
AGANO JIPYA |
|
|
MATHAYO |
Mt. |
|
MARKO |
Mk. |
|
LUKA |
Lk. |
|
YOHANA |
Yn. |
|
MATENDO YA MITUME |
Mdo. |
|
WARUMI |
Rum. |
|
WAKORINTHO |
Kor. |
|
WAEFESO |
Efe. |
|
WAFILIPI |
Flp. |
|
WATHESALONIKE |
Thes. |
|
TIMOTHEO |
Tim. |
|
WAEBRANIA |
Ebr. |
|
FILEMONI |
Fil. |
|
YAKOBO |
Yak. |
|
PETRO |
Pet. |
|
UFUNUO WA YOHANA |
Ufu. |
MAELEZO ZAIDI
|
NENO |
UFUPISHO |
|
MSTARI |
Mst. |
|
TOLEO |
Tol. |
|
KURASA |
Kur. |
|
NAMBARI |
Nam. |